Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 683
- 124
Wakuu nimeona nije na hii issue kwa sababu naona hili ni tatizo kubwa kuliko wengi wetu tunavyoliona. Sasa hivi kumezuka wimbi la biashara ya vyuma chakavu ambavyo vinasafirishwa kwenda Kenya. Biashara ni nzuri lakini ukiangalia hasara ya hii biashara kwa taifa letu ni kubwa sana. Nikizungumzia tuu kwa kifupi:
1.Sasa hivi mifuniko ya maji taka mjini huwezi kuiona kwa sababu watu wanaiba na kuuza kama vyuma chakavu. Hii ni hatari sana kwa watumiaji wa bara bara na pia huliingizia shirika hasara kubwa sana km kuziba kwa mitaro nk.
2. Nyaya za simu na umeme zinaibiwa kila siku na kusababidhia taifa hasara kubwa sana.
3. Vyuma vya madaraja vinaibiwa na kusababisha hasara ya maisha ya watu na mali zao.
4. Vyuma vya reli vinaibiwa na hii ni hatari sana kama huko Mbeya jamaa waling'oa reli ya TAZARA ili wapate vyuma vya kuuza.
5. Nakumbuka hapo nyuma kidogo kuliwahi kutoke mlipuko kwenye maghala ya kuhifadhi hivi nyuma na kusababisha upotevu wa maisha na mali.
Kuna mambo mengi sana kuhusu hii biashara ila wakuu mimi mwenyewe naona kama hatua za haraka sana hazitachukuliwa hii kitu itasababisha hasara kubwa sana kwa taifa.
WITO: Naiomba serikali na mamlaka zote zinazohusika kuanzia serikali za mitaa kupia marufuku hii biashara.