Mwanza inaelekea kuwa kama bukoba. In short imetengwa kiaina na serikali. Sherehe kubwa kama hizi wasukuma na wakuria kuzigeuza gulio LA uchinga ni kosa kubwa.
Kadri siku zinavyoenda mwanza inakosa mvuto na ubunifu.
Ujenzi holela bila mpangilio,
Uchafu kila kona
Joto Kali na mama ntilie kila kona vinaikosesha mwanza heshima.
Kiukweli mamlaka ya jiji hili ni pasua kichwa, kuna uzembe wa ajabu si katika kukusanya mapato tu bali hata kusimamia miradi,
kutatua kero za wananchi ikiwemo uchafu hivi sasa maeneo ya katikati ya jiji hususani pale Nyerere square/round about muda wote mitaro inatoa harufu kali ya vinyesi na taka ngumu zimezagaa si mjini hadi mitaani hamna anayejali,
Suala la ubunifu ni kizungumkuti serikalini na hata usimamizi wa mambo madogo madogo kama haya ya maonyesho bado ni shida,
Sasa nini kinakuzuia kama serikali kuja na utaratibu wa kuhamasisha wadau muhimu kujitokeza katika maonesho ya namna hii nchini na kama ikibidi unawawekea na conditions kabisa kuwa kama unaleta baa/hoteli yako kwa nia ya kuuza tu bidhaa zako katika maonyesho haya hakikisha pia unakuwa na banda lako pembeni (katika eneo la mabanda) ambalo litakupa fursa ya kunadi biashara yako,kutoa taarifa kwa wateja na kujifunza,
Vivyo hivyo ifanyike kwa makampuni, taasisi na mashirika ambayo kwa namna moja au nyingine yanahitajika kuwa serious na kuja na marketing strategies nzuri katika mabanda na ushiriki wao ili kunogesha na kuleta dhima nzima ya maonesho na siyo gulio la mitumba na samani za ndani.
Pili serikali ya mkoa inashindwa nini kuja hata na mpango wa kuzungushia eneo lote kwa uzio wa senyenge ambao utawaruhusu wao kuwa na geti la forodha kwa ajili ya kutoza viingilio kwa wanaohudhuria maonesho hayo hata ikiwa ni sh.200 kwa kila mtu, mwisho wa siku kibaba hiki kinaweza kutatua kero za wakazi wa kishiri ambao hawana barabara, Kangae au kahama huko ambako pengine hawafikiwi na huduma ya maji.