Maonesho ya NANE NANE yasiyo NANENANE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maonesho ya NANE NANE yasiyo NANENANE

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mwanawao, Aug 8, 2012.

 1. mwanawao

  mwanawao JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 1,982
  Likes Received: 1,639
  Trophy Points: 280
  Dhumuni kubwa la Maonesho ya nane nane kwa kadri miaka inavyozidi kusonga mbele ndivyo yanavyozidi kupoteza uhalisia wake. Maonesho haya kwa siku nyingi yamekuwa yakijulikana kama maonesho ya wakulima. Uhalisia huu wa kuwahamasisha wakulima kuja kuona jinsi watakavyoweza kufanya kilimo kwa ufanisi zaidi umezidi kupotea jinsi siku zinavyo kwenda.

  Watu mbalimbali wanaoenda kuangalia maonesho haya wengi tunategemea kukutana na mambo yatakayohamasisha ukuaji wa kilimo ndani ya nchi yetu. Lakini siku hizi cha kushangaza unapofika kwenye maonesho haya zaidi 50% utakutana na watu wakiuza bidhaa mbalimbali kutoka china, na nchi nyinginezo za Asia. Ukulima wetu hapa upo wapi? Je, maonesho ya nane nane yamegeuka kuwa maonesho ya kichina?

  Utakutana na mabenki kibao yakiwa yanajitangaza. Sikatai wajitangaze. Je, katika kujitangaza kwao, ni benki ngapi kati ya hizo zinamjali na kumsaidia mkulima?

  Je, kwenye maonesho haya kuna products za kilimo kweli ambazo zinaweza kumhamasisha mkulima kusonga mbele na kumuinua kiuchumi?

  Wadau tuchangie ni namna gani tunaweza kuboresha maonesho haya yaweze kuwa tija kwa Taifa letu.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kwanza maonyesho yawe yanazunguka toka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine kwa kila kanda. Pili tuweke utaratibu wa nini kiingie ktk maonyesho hayo, na kipi kiingie ku-support maonyesho yenyewe.
   
 3. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,330
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  nakubaliana nawewe kwamba yanapoteza maana mbaya zaidi wakulima wengi maskini wanashindwa kuingia uwanjani kwa ajili ya gharama za kiingilio,usafiri na chakula.
  ni vyema serikali ikafanya maonyesho haya angalau siku ya nanenane kuwe hakuna kiingilio inaweza kuwasaidia watu pia.
  lakini wakulima pia ambao wengi ni maskini wanahitaji kujifunza kitu pia kwani wengi wanaogopa kufika madukani kuulizia vitu vya kichina wanavyovipenda na kuviona ghali hivyo tuahitaji pia wabangaizaji wawepo japo wasiwe wengi.
  kingine cha msingi ni vyema killa bara bara au mitaa ya ndani ikaboreshwa kwa kueleza maeneo hayo kunamabanda ya aina gani kuliko kuzunguka uwanja mzima unatafuta banda moja (ikiwezekana lamani na vipeperushu vikatolewa.
  wisho hebu wekeni rami basi kwenye hizo barabara ndani kuondoa vumbi humo uwanjani
   
 4. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Bila kusahau benki za wakulima za kanda zinaweza kuwaokoa wakulima wadogo wasio na mitaji na pembejeo.
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Maonyesho ya NANE NANE YAKO KISIASA ZAIDI KULOKO KIUHALISIA, Sioni logic ya kufanyia maonyesho ya kilimo Dodoma, huku mikoa yenye kuongoza kwa kulima ikiiachwa, N yale maonyesho yako kisiasa na ni moja ya maeneo ya VIONGOZI WA SERIKALI HASA HALIMASHAURI KUJA KUTAFUNIA POSHO, Halimashauri nyingu unakuta hazina cha kuonyesha na matokeo yake unakuta wamekusanya WAFUMA VITAMBAA, SHANGA, VINYAGO, NA KAZALIKA NDO WAMEPELEKWA KWENYE MAONYESHO YA KILIMO,

  Na TASO wako kimasilahi zaidi, Cheki mfano wa Maonyesho ya kimimo ya Arusha, na HUWA YANAKUSANYA WATU WENGI KULIKO HATA HAYO YA KITAIFA HUKO DODOMA, Ila Maonyesho yenyewe yamejaa, vitu vya utalii, vyumbo kutoka china, MAKAMPUNI YA SIMU, Kila KAMPUNI YA SIMU INAZAIDI YA MABANDA MANNE NDANI YA UWANJA WA MAONYESHO,

  Na maonyesho hurudia vitu vile vile kila mwaka no any IMPROVEMENTS
   
Loading...