Habari za asubuhi ndugu zangu wa JF
Leo asubuhi tarehe 29/03 ni siku ya furaha kwangu kwa sababu kuu mbili. Kwanza kabisa ni siku ya kuzaliwa mke wangu mpendwa, ametimiza miaka 29
. Namtakia kheri ya kuzaliwa na ningependa kusheherekea nanyi ndugu zangu. .
Pili, Leo hii tuko hospital magomeni hapa. Mda huu amepangiwa c section (kujifungua kwa operation). Huyu akiwa mtoto wetu wa pili. Hivi navyoandika hapa yuko chumba cha upasuaji (Theatre) na mimi niko nje nasubiri.
Ndugu zangu huu ni mwezi wa Kwaresma na pia ni mwezi wa Ramadhani. Tuwe pamoja na kheri njema ya maombi yenu. .
Ndugu yenu
Gily . .