Maombi yenu, ili niitwe kazini

Maombi yenu, ili niitwe kazini

Genesis og

New Member
Joined
Nov 18, 2021
Posts
2
Reaction score
6
Habari wadau last week niliitwa kwenye usaili utumishi position ya commercial manager Kibaigwa water supply and sanitation tulikuwa watu watano wanaume wanne na mdada moja tukapewa assignment ya swali then tuandae power point baada ya hapo tukaitwa kufanya presentation ya kile tulichoandika kwenye assignment waliyotupa kwa kweli kulikuwa na watu kama kumi kutoka idara mbali mbali za maji nilifanya kwa uwezo wangu Wakatuambia watatupigia simu maombi yenu wadau niitwe kwenye hii kazi🙏
 
Tuombe
Baba katika jina la Yesu Kristo.
Naliweka mikononi mwako jina la kijana huyu ili aweze kupata hii kazi ya ndoto zake,najua ushindani ni mkubwa sana,lakini Baba tazama kijana huyu yuko tayari kuwatumikia ndugu zake watanzania kwa moyo na nguvu zake zote.Mungu Baba kapate kumfanyia muujiza kijana huyu ili naye akapate kuwa daraja kwa vijana wenzake ambao kwa muda mrefu wamekaa bila kuwa na ajira.Eeh Mungu kapate kumfungulia milango ya baraka kijana huyu mchapakazi ili nae akapate kuonekana mtu miongoni mwa watu kwa kumpatia kazi hii ambayo itafanya maisha yake kuwa mazuri.
Ni katika jina lako tukufu Baba Mungu tunakuomba na kukushukuru.
Amen 🙏.
 
Back
Top Bottom