Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,199
- 7,562
Kutokana na Ongezeko la Vyuo vikuu nchini na kutokana na serikali kufanya jitihada za kutoa mikopo kwa vijana wanaojiunga vyuo vikuu, sasa hivi Tanzania tuna wahitimu wa vyuo vikuu maelfu kwa malaki. Haya ni maendeleo na ni jambo zuri tu.
Hata hivyo maendeleo haya yamekuja na changamoto kubwa inayowaumiza wengi. Asilimia kubwa ya Graduates hao, hawapati ajira kokote na kwa sababu mbali mbali wanashindwa kujiajiri vile vile na hivyo kujikuta wanabaki wakitangatanga. Aidha , kwa kuwa wanakuwa hawapati kazi , sio tu kwamba elimu wanayokuwa wamepata inakuwa haiwasaidii lakini pia wanashindwa kurudisha mikopo.
Katika kipindi kimoja cha televisheni, nimemsikia ndugu Polepole akieleza kuwa kwa mwaka huu, serikali imeongeza maradufu, kiwango cha mikopo kwa vijana wanaojiunga na vyuo vikuu.
Maombi yangu ni kwamba; ikiwa itaonekana inafaa, basi fedha za mikopo badala ya kutolewa kwa ajili ya elimu ya juu tuu, fedha hizo zigawanywe mafungu mawili. Fungi moja wapewe baadhi waende Chuo kikuu na fungu lingine wakopeshwe wengine wakaanzishe miradi midogo midogo. Hii itasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, itasaidia vijana kuweza kurudisha mikopo na itasaidia kukuwa kwa uchumi.
Aidha, ifanyike kampeni ya kuwajengea uelewa vijana na kuwahamasisha kuwa sio lazima watu wote wasome vyuo vikuu ndio wafanikiwe na waeleweshwe kuhusu changamoto za ajira zilizopo mbele yao ili wafanye maamuzi sahihi mapema.
Hilo ndilo ombi langu ambalo naamini litawasaidia vijana wengi ambao Mara nyingi hujikuta kwenye utata mkubwa.
Bethlehem.