Maombi yangu kwa Mh. Rais Magufuli

Maombi yangu kwa Mh. Rais Magufuli

serikali pia ibadili sera, badala ya kujaza watoto wa kitanzania kwenye kambi za jeshi, iwapeleke watoto hao veta na iwe sheria na kigezo cha kujiunga na elimu ya juu.
Mkuu, tatizo ni watu wote kusoma /kupita kwenye mkondo mmoja. Hata zamani wakati kukiwa na graduates wachache hapakuwa na tatizo kubwa la graduates wasio na cha kufanya ila changamoto kubwa imejitokeza baada ya vyuo vingi kufanywa kuwa vyuo vikuu na hivyo kila mtu kuhamasishwa/ kuhamasika kuwa na degree. kwa hiyo hata watu wote wakilazimishwa kwenda VETA, tatizo litarudi pale pale. Suala ni kuwa na mgawanjiko, wengine waende huko wengine kule. Haitakiwi watu wote kupita kwenye njia moja maana wanapokwama wanakwama karibu wote.
 
Ila mkuu hata Dar wako wahanga wengi wa ajira; kwa mantiki hiyo suala hili lina adhari kote, mijini na vijijini.

Ni sawa lakini wengi wa wasio na ajira hapo Dar wamekimbia huko mikoani kwa kushindwa kuwezeshwa. Iwapo watawezeshwa huko mikoani wengi watarudi na kuwa wazilishaji zaidi. Wachache watakaobaki wataenda kufanya kazi kwenye hivyo viwanda 3,000+ hapo Pwani kama ni kweli kunajengwa viwanda.
 
Nijuacho mimi ili mti akue kiuchumi ni soma shule huku ukisoma maisha ya mtaani,ili mwisho wa siku upambane hata kivingine nje na elimu yako,nahakika kwamba vyuo vyote vikitoa vijana ktk mwaka mmoja wa kumaliza masomo ni vijana wengi wanakua uraiyani na ukweli ni kwamba Serikali nyingi za Africa na hata huko ulaya hapawezi kua na maofisi au ajira za kuwatosha watu wanaotoka masomoni,sema tu kwa ushauli labda Serikali ingejikita ktk kuboresha kilimo kwa watu wote nchini kwa kupeleka nguvu nchini ya kupandisha maji toka Ziwani,Baharini,mito na kuchimba mabwawa,tulime na tuuze nje ya nchi maana ardhi tunayo bado.kilimo ni njia pekee ya kujikwamua kitaifa japo vijana wengi hasa mlioenda chuo hamtaki kukubali,mafanikio siyo lelemama na serikali haiwezi hudumia wote.jaribuni kutazama kwamba kule South Africa ni nchi inayotegemea viwanda kiuchumi,kuna viwanda chungu mzima lakini tatizo la ajira liko kubwa tu.ajira nyingi za kule ni za viwandani kitu ambacho wala watu hawakuhitaji kwenda hata chuo kikuu badala ya vyuo vya ufundi na usindikaji wa chakula.so wasomi wa kiTanzania changamkeni kuivamia mitaa na ardhi kwa akili mliyotoa vyuoni,pambanueni vichwa vyenu mtafanya nini ili kukuza uchumi wenu na taifa kwa ujumla.serikali haiwezi kuona vijana wako serious na wanajituma alafu wakatazama tu bila kutoa msaada.tatizo liko kwa sisi wananchi pia,unamkuta mtu kapewa mkopo wa biashara au kilimo lakini mkopo huo anaanza nao baa kupiga mvinyo iliyo chachwa.tubadilike,wenye elimu ni wengi lakini ajira hazitoshi.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Jambo muhimu ambalo linatakiwa kutiliwa manani ni kwamba si lazima kila Mtu awe na degree has a katika kipindi hiki ambacho kuna changamoto kubwa ya ajira rasmi kote duniani. Kwa mantiki hivyo, vijana wanapaswa kueleweshwa kuwa hawapaswi kusoma kama fasheni Bali kwa malengo maalum. Wanatakiwa kuelewenza fursa na changamoto zilizo mbele yao punde tu baada ya kumaliza kidato cha sita. Kwa kufanya hivyo serikali itakuwa inapunguza uwezekano wa fedha kupotea, inawasaidia vijana kuweza kujitegemea na inachochea maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
Kwahiyo sababu hakuna ajira wengine wasisome? Wasipate haki ya elimu? Kwanini isiwe kubadilisha elimu yetu iwe inaweza kumtegemeza mtu baada ya kumaliza elimu yake
 
Naungana na wewe kwamba Kwa sasa serikali ibuni mfuko maalumu wa mikopo kwa wahitimu wa vyuo vikuu.

Mabilioni ya kikwete yakienda pasipoeleweka...sasa ni vyema kwa mfano zile milioni 50 kwa kila kijiji zikapelekwa kwa wahitimu ambao watatakiwa kujiajiri na kuwaajiri wanakijiji.

Kwa sasa ziko fedha zinazotolewa kwa vikundi vya kina mama na vijana ingawa ukiangalia walengwa wengi sio watu wenye elimu.

Sisemi tusitishe mikopo hii midogo ya hawa kina mama na vijana wasio soma bali ni muda muafaka wa kuwafikiria graduates wetu wasio na ajira.

Wako graduates kutoka SUA waliostruggle kupata mikopo ya gharama kubwa na kuanza kufanya kilimo cha kisasa na wakaweza kujiajiri na kuajiri ...sasa tuchukue mfano huo na kuwawezesha graduates wetu.

Fedha itatoka wapi?hii ni changamoto inayohitaji ubunifu.

Mfano tunaweza kuamua kuitumia bodi ya mikopo ya elimu ya juu na kuweka bonus package ya kuendelea kupata mkopo kwa kipindi cha mwaka au miaka miwili hivi au labda itolewe lumpsum ya mkopo wa miaka miwili kwa graduate na baada ya miaka miwili aanze marejesho ya mkopo na ka riba kiasi flani.Mkopo huu ulenge maandiko ya miradi katika final year at University.

Pia tunaweza kuchagua graduates wachache waliofanya vyema katika masomo yao na kuwapa mikopo ya kuanzisha miradi ambayo itaendana na tafiti.

Benki kama ya Kilimo inaweza kupewa sharti la kutoa mikopo yake let say kwa asilimia hamsini iwalenge graduates wa maswala ya kilimo na ufugaji.na hakika wanafunzi wa kilimo watajaa kuliko kawaida.

Benki ya biashara kwa muktadha huo huo ikapewa sharti la kuwakopesha vijana mahiri waliomaliza vyuo vya biashara let say kwa asilimia 20 ya wateja wake.

Tunaweza kuweka sharti la kwamba vikundi vya ujasiliamali hivi vidogo vidogo au so called saccoss ni lazima viajiri graduates wetu japo wawili kama waelekezaji washauri.

Kwangu mimi sio sahihi kupeleka sh 10,000 kwa familia masikini hapo ukiwa unetumia mifedha kibao ya kufuatilia na kufundisha n.k ...ni heri mfuko huo wa TASAF Ukawakopesha wahitimu let say wa VETA kutoka huko huko vijijini ili waweze kujiajiri na kuajiri.

Fedha za mifuko ya jimbo ni dubwana jingine linalotafuna fedha za umma kwa manufaa ya wabunge ili waendelee kujizolea sifa wasizostahili.

Tunaweza kuzifuta kabisa ama la ziwekewe sharti la kuwakopesha vijana graduates watakaorudi na miradi au projects za kusaidia majimbo.

Iko hii kitu inaitwa corporate social respinsibility ya makampuni mbalimbali...sasa ifike wakati waachane na usanii wa kugawa mchele na sabuni nyakati za sikukuu na badala yake wapewe program maalumu za kuwawezesha graduates katika field zinazoendana na biashara zao.
Kampuni ya madini inatakiwa imuwezeshe graduate wa madini kuwa mchimbaji mdogo au wa kati na sio kutujengea choo na kurusha ITV na kuiita social reponsibility.

Yapo mengi ya kuelezana au kuishinikiza serikali kama vijana espcially graduates na tukaacha ushabiki wa udaku au uhanaharakati usio na makengo ya kuwakomboa kiukwelikweli.

JINGALAO!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Pambana na hali yako naona ushaanza kufulia..ngoja akili zitakurudi tu
 
Kwahiyo sababu hakuna ajira wengine wasisome? Wasipate haki ya elimu?
Mkuu hatujasema wasisiome, tumesema wasome vitu vinavyoweza kuwasaidia kuboresha maisha yao na kuiletea nchi mandeleo na sio kusoma kwa kuwa watu husoma au kwa mazoea. Kwa mantiki hiyo, sio lazima kila mtu kusoma, form 4, kisha 6, kisha chuo kisha alichokisoma hakina uhitaji kwenye soko.

halafu kuhusu suala la haki; hili suala watu wengi hulitizama ndivyo sivyo. Si lazima kila haki uitumie au uipate. Kwa mfano ni haki yako kuoa au kuolewa ila si lazima uoe.Utaoa au kuolewa ikiwa tu inafaa kufanya hivyo kulingana na mazingira. Una haki ya kuwa tajiri ila si lazima uwe tajiri. Una haki ya kuwa kiongozi lakini si kila mtu anaweza kuwa kiongozi.
 
Pambana na hali yako naona ushaanza kufulia..ngoja akili zitakurudi tu
Ukiona unashungulikia masuala yanayokunufaisha wewe tu na maisha yanaenda vizuri; ujue kuna watu wako mahali wanashungulikia masuala yao, yako na ya wengine. Kama kila mtu akisema ajiangalie yeye tu; hakuna mtu atakayebaki duniani.
 
Kwa mfano kitu gani hakina uhitaji kwenye soko? Usiangalie tu kuajiriwa ndio maana tunataka misingi ya elimu ibadilike
 
Pambana na hali yako naona ushaanza kufulia..ngoja akili zitakurudi tu
Usitake kuharibu mada usiipeleke mada hii katika mantiki za kisiasa au kishabiki.Tutaiharibu kama tukianza kuingiza ufuasi.
 
Ukiona unashungulikia masuala yanayokunufaisha wewe tu na maisha yanaenda vizuri; ujue kuna watu wako mahali wanashungulikia masuala yao, yako na ya wengine. Kama kila mtu akisema ajiangalie yeye tu; hakuna mtu atakayebaki duniani.
Tatizo la msingi hamligusi mnazunguka zunguka tu imagine bombardier moja ingenunua matrekta mangapi, kivuko kibovu kingejenga mabwawa mangapi ya samaki vijana wajiajiri, mwenge umgewekwa store ni wamachinga wangapi wangepata mahali pa biashara.
Hivi kuhamia dodoma na kunyanyua wananchi kimapato kipi ni cha msingi? Marekani, uingereza ufaransa urusi china japan korea wapi umeona wamelazimisha shughuli zote kuwa katikati ya nchi. Sahivi tuko karne nyingine mambo yote kwa mtandao sasa unaenda kujenga kwa kutumia hela nyingi halafu vijana wanaugua umaskini mtaani. Tatizo kubwa ni kuplan na kusimamia plans. Watu wa chato wanahitaji airport wakati chakula tu ni shida!!
 
Usitake kuharibu mada usiipeleke mada hii katika mantiki za kisiasa au kishabiki.Tutaiharibu kama tukianza kuingiza ufuasi.
We nimfuasi wa wanaofundisha ujinga tatizo hamtaki kuusema ukweli mil 50 hamjatoa 10% kila halmashauri hamjatoa, viwanda hakuna, biashara zinafungwa vijana wanazidi mtaani lakini wewe ndo wa kwanza kuimba kuwa tunanyooshwa.
 
Wewe utakuwa mfuasi wa propaganda na uongo wa wanasiasa na ni lazima unichukie kwa kuwa sijawahi kutetea walaghai au mafisadi au wanasiasa wasanii wanaosimama kwa ajili ya matumbo yao.

Kuhusu milioni hamsini hiyo ni ahadi na mkataba kati ya CCM na wananchi kwa hiyo tusubiri...kinachotakiwa kukijadili ni pamoja na utaratibu mzuri wa kuzitoa ili zifike kwa walengwa sahihi na kuleta tija tarajiwa.

Unaposema viwanda hakuna na biashara zinafungwa unatumia takwimu gani au unarefer kwenye magazeti ya udaku?

Unaweza kunionesha sehemu yoyote niliyotoka povu kwamba tunanyooshwa?kwangu mimi Serikali inaturejesha kwenye nidhamu ya kutafuta kihalali na kutumia kihalali kwa faida ya nchi.

Rudi kwenye topiki ambayo lengo ni kuhakikisha vijana hasa graduates wanaomaliza wanawezeshwaje kuhakikisha wanajiajiri na kuajiri kwa faida ya nchi?

Kumbuk kundi kubwa la hawa vijana ambao ni graduates wameshindwa kujenga hoja ya jinsi gani serikali iwatatulie tatizo hilo la kujiajiri.

Usiturudishe kwenye malalamiko njoo na solution.
 
Solution yangu ni 10% ya halmashauri itekelezeke na serikali iachekujiingiza kwenye miradi isiyo na impact kwa taifa, kingine mwenge uzimwe uwekwe store kama mnauona wa muhimu uzunguke mara moja kwa miaka mitano.
 
Usitake kuharibu mada usiipeleke mada hii katika mantiki za kisiasa au kishabiki.Tutaiharibu kama tukianza kuingiza ufuasi.

Unalalamika japo ww mwenyewe ndio tabia yako.
 
Solution yangu ni 10% ya halmashauri itekelezeke na serikali iachekujiingiza kwenye miradi isiyo na impact kwa taifa, kingine mwenge uzimwe uwekwe store kama mnauona wa muhimu uzunguke mara moja kwa miaka mitano.
10% ya halmashauri kwa mara ya kwanza toka ianzishwe ndio inatekelezwa vilivyo...nenda kwa vijana na kina mama huko halmashauri utaliona hili tofauti na miaka kadhaa nyuma.

Je Mwenge unatumia kiasi gani kwa mwaka ?
Na je unahamasisha miradi ya kiasi gani kwa mwaka?Kama una data zinazoonesha mwenge hauna faida na unaleta hasara zimwage hapa.
 
Kwani mimi sio kijana au? Haitekelezeki nipe mfano wa halmashauri walizotekeleza
 
10% ya halmashauri kwa mara ya kwanza toka ianzishwe ndio inatekelezwa vilivyo...nenda kwa vijana na kina mama huko halmashauri utaliona hili tofauti na miaka kadhaa nyuma.

Je Mwenge unatumia kiasi gani kwa mwaka ?
Na je unahamasisha miradi ya kiasi gani kwa mwaka?Kama una data zinazoonesha mwenge hauna faida na unaleta hasara zimwage hapa.
Mwenge unahasisha vipi miradi? Hata kama ni milioni mia 2 ni nyingi sana ukisave
 
Back
Top Bottom