Maombi ya msaada kutoka baba mwupe ila binadamu kama weusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maombi ya msaada kutoka baba mwupe ila binadamu kama weusi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by simbamweupe, May 25, 2012.

 1. s

  simbamweupe Member

  #1
  May 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari zenu?
  Naitwa Giuseppe Zingaro, raia wa Italia, nimezaliwa Ragusa – Italia, tarehe 26/11/1960.
  Mwezi wa 4 mwaka 2004 pamoja na mchumba wangu wa enzi ile, Edna Boimanda (kwanzia sasa Boimanda) raia wa Tanzania, tulifungua kampuni chini ya jina la ITANZA ENTERPRISES LIMITED.
  Katika kampuni hii, mimi nilikuwa na asilimia 80 na Boimanda asilimia 20
  Sehemu ya kazi ya kampuni ilikuwa Tanga - Tanzania .
  Baada ya kuwekeza, niliomba na nilipewa “RESIDENT PERMIT Class A” ya kutengeneza npya kila miaka miwili.
  Mwaka 2008, tarehe 29 mwezi wa nane, alizaliwa Nelson G. Zingaro, mtoto wangu na wa Boimanda.
  Maelewano ya mapenzi, lakini, kati ya mimi na Boimanda, yalianza kuwa sio mazuri, kwasababu ya utofauti wa tabia, hadi yaliaribika kabisa (wiwu wake ulikuwa too much, hadi nilikuwa nakosa hewa).
  Hivyo basi, mwanzoni mwa mwaka 2010 niliamua kuacha nyumba, na nilienda kuishi peke yangu.
  Baada ya hapo, nilimkuta msichana na anaitwa Elizabeth Mustafa Kimaro, pia yeye raia wa Tanzania, na huyu mwanamke, tulipendana na tuliamua kuishi pamoja.
  Boimanda, hajakubali matokeo hayo.
  Katika muda wote alijaribu kila aina ya machukizi, sana sana na Elizabeth.
  Huyu msichana lakini hajakubali ugomvi na kila mara alimwacha Boimanda aendelee peke yake katika machukizi yake.
  Mwezi wa 11 2010, Resident Permit yangu, ilikuwa inaexpire, kwa hiyo nilikuwa najandaa kuirenew.
  Boimanda, wakati nilirudi Italia kwa kipindi cha miezi 6, alikuwa amekuwa rafiki sana na Mkuu wa Mkoa wa kipindi kile Said Said Kalembo,
  Wakati hule, Tanga nzima watu walikuwa wanadai kwamba Boimanda na Kalembo wanatembea pamoja kimapenzi.
  Mwenyewe, niliipata habari hiyo, kutoka mkuu wa immigration Danny Msuya (alihamishwa mwezi wa 2 kwa kuwa ofisa mbovu kabisa, tamko la Waziri mwenyewe).
  Boimanda mwenyewe anakubali kwamba ni kweli watu walikuwa wanasema hivyo.
  Niliporudi Tanzania, nilikuwa bize kwa kuandaa documents zote zilikuwa zinatakiwa na ofisi ya uhamiaji ili nitengeneze Resident Permit npya.
  Maelewano na Boimanda, yalikuwa haiwezekani hata kuongea, maana mara kwa mara uwivu wake ulikuwa unatokea na ugomvi na matusi.
  Katika hali hii, imekuwa ngumu, kila siku zaidi, kumwona na kukaa karibu na mwanangu Nelson.
  Siku moja, mwezi wa 11 mwishoni, nilipewa simu kutoka na mkurugenzi wa ofisi ya uhamiaji Mkoa wa Tanga, alisema niende haraka ofisini ya Mkuu wa Mkoa Kalembo.
  Ilikuwa saa ya chakula cha mchana, na mimi nilikuwa namaliza chakula changu, nilimwambia, kwamba sielewi maana ya mkutano huu, halafu saa ile.
  Mkurugenzi wa ofisi ya uhamiaji, aliniambia niende haraka bila kupoteza muda wala kuuliza chochote.
  Nakumbuka, nilikuwa napanda ngazi za ofisi ya Mkuu wa Mkoa, nilipopata simu ya pili, alikuwa tena mkurugenzi wa uhamiaji Mkoa wa Tanga, alikuwa ananiharakisha.
  Nilipofika mbele ya mlango ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, nimeshangaa kumwona pamoja na mkurugenzi wa uhamiaji, pia Boimanda.
  Baadaye kidogo tulipoingia, nilielewa kitachoendelea: Mkuu wa Mkoa bila kunipa nafasi ya kujitetea, hata kidogo, alisema kwamba mimi sina kazi maalum Tanzania, kwa hiyo nilikuwa sina maana ya kubaki nchini, bali alisema, itabidi niondoke mapema inawezekanavyo.
  Najiuliza na pia nawauliza ni mimi naona Kalembo alivunja kifungu cha 12 cha Tamko la Kimataifa la haki za binadamu, wakati aliingia ndani ya matatizo yangu ya familia?
  Tarehe 10 desemba 2010 katika gazeti la kila siku “Tanzania Daima”, Kalembo alitoa kauli, kwamba ataomba msaada wa polisi, ili wakamatwe wazungu, ambao hawana sababu ya kubaki nchini.
  Alitaja majina matatu, moja kati yao lilikuwa langu.
  Muhimu kuzingatiya kwamba wale wavili wengine bado wanaishi Tanga bila usumbufu wowote.
  Zaidi, katika gazeti lile, ili afanikiwe maslahi yake, yaani nifukuzwe nchi, Kalembo alimshitaki na alimwogopesha pia mkurugenzi wa uhamiaji wa Mkoa wa Tanga, Danny Msuya.
  Kalembo alisema, Msuya anakula rushwa.
  Baada ya mkutano ule, ofisi ya uhamiaji Tanga, ilikataa kuirenew Resident Permit yangu, hivyo basi, katika siku chache, nilikuwa lazima niondoke, baada ya kuishi nchini, kikazi kwa miaka karibu 7.
  Desemba 2010 nilipewa barua kutoka ofisi ya uhamiaji Tanga.
  Katika ile barua sijapewa sababu ya kukatazwa kuirenew Resident Permit yangu.
  Hakuna maelezo kabisa, kukataa tu!
  Nafikiri msingi ya haki (ya kujua sababu ya maamuzi) yasili ya tatu, umevunjiwa!
  Niliomba na nilipewa, tarehe 15 desemba 2010, special pass ya miezi miwili, ili niweze kupanga vizuri ondokeo.
  Niliambiwa, kwamba sitaweza kufanya kazi yoyote au biashara tena wala kuwa na mali Tanzania.
  Wakati ule, nilikuwa nahisi nachanganyikiwa, unyonge na pia kutishwa.
  Najiuliza na pia nawauliza, je labda kifungu cha 17 cha Tamko la Kimataifa la haki za binadamu kimevunjiwa?
  Tarehe 17 desemba 2010 tulifanya mkutano wa bodi ya kampuni.
  Katika mkutano ule niliamua hisa zangu za kampuni ziende kwa mtoto wangu Nelson G. Zingaro.
  Boimanda alienda Dar es Salaam peke yake, maana amekataa kwenda wote, kushugulikia uamisho wa hisa zangu za kampuni.
  Aliporudi Tanga, mwanzoni februari 2010, aliniambia haiwezekani kuamisha hisa zangu, moja kwa moja kwenda Nelson, maana bado mdogo.
  Boimanda alidai kwamba azipewe yeye, alafu, Nelson atakapokuwa wa umri wa mtu mzima atazipewa kutoka kwake Boimanda.
  Nilikuwa na wasiwasi, lakini nilikubali.
  Nilikuwa sina muda wa kufatilia kama kweli mtoto alikuwa hawezi kuzipata hisa zangu.
  Baada ya siku chache nilikuwa lazima niondoke nje ya nchi.
  Tarehe 14 februari 2011 ilikuwa siku ya mwisho kukaa nchini.
  Nilikuwa bado chini ya tishio la Mkuu wa Mkoa.
  Tarehe 13 februari 2011, niliamua kuondoka, lakini sijaenda Italy.
  Nilifikiri, niende Kenya kwa muda, alafu nitarudi Tanzania kama mtalii, maana hata kama Mkuu wa Mkoa alikuwa amenitishia, vilevile, sijafukuzwa nchi, sijafanya ubaya wala natafutwa na polisi.
  Hivyo nilifikiri nitakuwa na muda wa kumwangalia mtoto wangu, hata kama kwa shida, na pia kuhakikisha kama utaratibu wa kuamisha hisa zangu, utakamilika vizuri.
  Boimanda, alikuwa anajua kwamba, nilienda Kenya na pia alikuwa anafahamu nia yangu ya kurudi, kwa hiyo alimwambia Kalembo, afanikiwe ili nitakaporudi Tanzania kupitia Horohoro - Tanga, nikatazwe kuingia nchini.
  Na kwa kweli tarehe 18 februari 2011, bila sababu, bila maelezo ya maneno au ya maandishi, nilikatazwa kuingia Tanzania.
  Tena msingi ya haki (ya kujua sababu ya maamuzi) yasili ya tatu, umevunjiwa!
  Nilisimdikizwa tena Lungalunga - Kenya na kutoka pale, ndiyo nilirudi Italy.
  Pasipoti yangu (naunganisha attachment) iligongwa muhuri na maandishi R.E. (refused entry).
  Siku, wiki, na miezi zilikuwa zinaenda, na mimi nilikuwa nashindwa kukubali, nisimwone tena mtoto wangu, kwa hiyo, najua nilifanya kosa, nilibandika juu ya muhuri wa kukataliwa (R. E.), sticker ya kodi ya pasipoti ya serikali ya Italy, ili kuficha R. E.
  Baada ya miezi 7, yaani tarehe 18 septemba 2011, nimerudi Tanzania.
  Nilipewa visitors visa ya miezi mitatu.
  Nilipofika Tanga, nimegundua, kwamba kukaa karibu na mtoto wangu, itakuwa ngumu sana.
  Boimanda, ambaye alishtuka alipojua nimerudi, aliweka vikwazo vingi, ili nishindwe kukanae mtoto karibu.
  Boimanda, alikuwa anataka mimi niende kumwona mtoto nyumbani kwake, bila kuweza kutokanae hata kwa kula ice cream, au kuogelea beach au kutembea mjini.
  Ila maelewano kati ya mimi na Boimanda yamekuwa mabaya kiasi kwamba siwezi kwenda nyumbani kwake.
  Niliuliza pia kuviona vitabu vya kampuni, ili nielewe na nihakikishe kama hisa zangu zilienda kwa Nelson.
  Boimanda alikataa, tena na ujeuri.
  Nimejaribu kuelewananae katika ofisi ya ustawi na jamii ya Tanga, lakini bila mafanikio yoyote, maana Boimanda alikataa kwa njia zote.
  Tarehe 19 octoba 2011 ofisa wa ofisi ya ustawi na jamii Tanga, Mr. Tekwa, alinipa barua ya kuipeleka kwa hakimu wa Mahakama ya mwanzo, ili nifungue kesi.
  Siku ya kwanza kesi ilitajia, tarehe 26 octoba, Boimanda alikata rufaa, maana alikuwa anahitaji huduma ya wakili.
  Baada ya siku chache, yaani tarehe 3 novemba, nilikamatwa na polisi kwa kuwa nilimpiga picha na kumpiga na kumtukana mpenzi wake mpya Boimanda.
  Nilikaa ndani usiku moja, alafu nimetoka.
  Kesi ile hijafika mahakamani, maana katika uchunguzi wa polisi, umekuwa wazi kwamba hakuna picha, simu nilirudishiwa baada ya kutokuwa na picha (maandishi katika kitabu cha polisi Chumbageni Tanga tarehe 5), wala mapigiano na matusi.
  Ila tarehe 4 asubuhi, nilikuwa nasikia kutapika, maana chumbani cha ulinzi pale Chumbageni hewa ilikuwa nzito sana, kuna kazi zilikuwa zinafanyika na chumba cha muda kilikuwa hamna choo, lilikwepo dumu na wengi walikuwa wanakojoa nje kwa hiyo hewa ilikuwa nbaya sana kweli.
  Niliomba askari wa kaunta, nitoke dakika 5 tu, ili nipate pumzi, yule askari alikubali, ila nilipotoka alinipeleka pembeni kabisa, akasema,”LETE CHAI NYEKUNDU 2” nilipoelewa alikuwa anataka TSH 20,000, nimekataa na hapo hapo akanifunga tena ndani kwa hasira kwani alikuwa amekosa hela.
  Tarehe 28 novemba 2011, mahakama ya wilaya alikubali rufaa.
  Kwa hiyo nilichukua hatua ya kufungua kesi Mahakama ya Wilaya Tanga (naunganisha plaints)

  1. kwa kuwa na uwezo wa kukanae mtoto na uhuru na kutokanae, pia nje ya nyumba yake, kama sheria ya Tanzania inavyokubali,
  2. kwa kuwa nilivyoona hisa zangu za kampuni, zilienda moja kwa moja kwa Boimanda ambaye anazisimamia kwa maslahi yake badala ya mtoto, naiomba mahakama ifute makubaliano ya tarehe 17 desemba 2010.
  Mkrugenzi wa uhamiaji Mkoa wa Tanga, alikiri, mbele ya mashaidi, kwamba alianza kupewa mashinikizo, kutoka Mkuu wa Wilaya, na pia ya RAS ambaye alianza kazi yake Tanga, wakati wa uongozi wa Kalembo, ili nifukuzwe nchi.
  Tena kifungu cha 12 cha Tamko la Kimataifa la haki za binadamu kilivunjiwa!
  Boimanda siku ile ile alipewa summons ya kesi zangu, alienda polisi kunishitaki, alidai namtishia maisha, baada ya kuniambia “UTANITAMBUA, NITAKUONYESHA MIMI NI NANI”.
  Nilienda polisi mkoani kutoa ripoti ya maneno haya, niliongea na ofisa Mr Mwajaliwa, ambaye alinishauri nifanye hivyo pia kituo cha polisi Chumbageni.
  Nilipofika pale tulikuwa tunafika wote na Boimanda
  Bahati nbaya kaunta siku ile, askari polisi wa zamu, yaani tarehe 2 desemba, alikuwa yule yule wa “CHAI NYEKUNDU 2”.
  Aliponiona alichukua nafasi ya kunifunga na raha zote, na pia alinishitaki kwa kumtukana.
  Jina lake askari ni Lugano.
  Nilifungwa siku 2 kituo cha polisi Chumbageni - Tanga, na siku 2 Maweni, kwa kukosa ukamilifu wa dhamana.
  Nilitoka baada ya dhamana kukamilika tarehe 7 desemba.
  RAS, siku nilikamatwa alikuwa Dar es Salaam, akampigia simu mkurugenzi wa uhamiaji, pale Tanga; kauli ya Msuya mwenyewe mbele ya mashaidi, ili amjulishe kuhusu ukamataji wangu (najiuliza alifahamishwa na nani RAS, wakati alikuwa Dar es Salaam?), na aliendelea na mashinikizo yake kuhusu mimi.
  Tarehe 14 desemba Mahakama ya Wilaya Tanga, ilitaja kwa wakati wa kwanza kesi zangu kuhusu mtoto na kampuni.
  Tarehe 16 desemba ilitaja kwa mara ya pili kesi ya vitisho, na tayari, ilieleweka kwamba Boimanda alinishitaki kwa makusudi.
  Nilikuwa ningependa kesi iendelee hadi mwisho ili niweze kuthibitisha kwamba sijamtishia maisha, wala sijafanya vurugu, ila nilizuiliwa.
  Pia kesi ya askari Lugano ilitajia kwa mara ya pili tarehe 16 na pia hapo, mahakamani alibanwa sana na wasaidizi wa hakimu hadi ametoa jasho nyingi baada ya kuja ameleva vibaya.
  Alibanwa kwasababu alikuwa hakumbuki mashitaka yangu, na pia kwa sababu niliifahamisha mahakama kuhusu sababu ya mashitaka yake, yaani kutaka hela yangu kinyume cha sheria.
  Mashaidi walikwepo, na walikuwa tayari kutoa ushaidi wao kwa kuwa sijamtukana, ila nilimwambia “umenifunga kwasababu nimekataa kukupa pesa”.
  Hata kesi hii nilizuiliwa kuendelea hadi mwisho.
  Tarehe 16, yaani siku ile ile, ofisi ya uhamiaji, alinituma mahakamani kwa ajili ya kuibandika sticker juu ya muhuri R. E.
  Mashitaka yalikuwa mawili: ya kwanza kwasababu nimetoa maelezo si kweli wakati niliingia nchini, ya pili kwasababu nilisababisha ofisa wa uhamiaji NIA airport Dar, asifanye kazi yake vizuri, kwa kuibandika sticker juu ya muhuri ya tarehe 18 februari 2010.
  Tarehe 22 desemba 2011 saa 8 mchana, hakimu aliniachia huru kwa ajili ya shitaka la kwanza, na kwa shitaka la pili alinipa adhabu ya kulipia fine ya TSH 20,000, maana alisema katika hukumu yake, sijaingia nchini, kinyume cha sheria, maana ile R. E. ilikuwa inanizuia kuingia nchini kwa miezi 6, na mimi nilirudi Tanzania baada ya miezi 7 (hukumu inapatikana mahakama ya wilaya Tanga).
  Licha ya hii, joni ya siku hiyo hiyo, yaani tarehe 22 desemba 2011, mkurugenzi wa uhamiaji, bila hata kusoma hukumu, alichukua hatua ya kunipa P. I.
  Nilipewa kasoro ya masaa 48 kuondoka nchini.
  Hiyo P. I. inaelewesha kwamba sitaweza kurudi tena Tanzania.
  Kwa ufupi, nilizuiliwa kukamilisha kesi zangu zote.
  Nilizuiliwa kuthibitisha kwamba Boimanda na Lugano na mashitaka yao walinidhalilisha na walivunja heshima ya vyombo vya sheria kwa kuwa walivitumia vibaya, kwa maslahi yao binafsi.
  Sitaweza tena kumwona mtoto wangu Nelson na sitaweza kumwona yule mtoto ambaye atazaliwa mwezi agosti ujayo, ndiyo kwasababu Elizabeth anabeba mimba yangu.
  Nchi za ustarabu zinazilinda haki za binadamu, na kuwatengana wazazi na watoto wao, ni kukunyaga na miguu michafu haki hizo.
  Kinachonishangaza ni kwamba hakuna kiongozi hata mmoja hajawahi kufikiri, je kunahutu kutengana yule baba na mtoto wake?
  Kunahutu kuaribu kisaikolojia cha mtoto mchanga kwa kuwa kumweka mbali na baba yake?
  Mimi nawaomba kujaribu kuifuta hiyo P. I.
  Vinginevyo, itakuwa wametengana daima, baba mzazi na watoto wake.
  Pia nachukua nafasi hii kwa kuwahoji viongozi wote,
  Ndugu Viongozi, je mnawatoto nyinyi?
  Mmoja, wawili, watatu, wangapi?
  Mtasikiaje, mtafikiriaje, mtafanyaje, siku mtatenganwa na watoto wenu?
  Mtaona mambo ya kawaida?
  Ingekuwa vizuri sana kulipewa jibu lao Mh. Viongozi
  Nawaomba msamaa kwa ajili ya kiswahili kibovu changu.
  Hata hivyo nimejitaidi kuwaelewesha kuhusu matatizo yangu.
  Ninaimani mtanisaidia pamoja na watoto wangu, yule ambaye yupo tayari na ananipenda sana, na pia yule ambaye bado hayupo lakini atakuwa atalihitaji penzi la baba yake.
  Nawashukuru kwa kusoma ujumbe wangu, na pia kwa vyote mtaamua kufanya kwa kunisaidia.
  Nawatakia kila la heri.
  Giuseppe Zingaro
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Loh. . .pole sana Simbamweupe.

  Kumuona Nelson ni wewe tu utafute namna ya kuelewana na mama yake. Ila mtoto wa Elizabeth waweza kumuona kirahisi tu, mkaribishe kwenu Italy wawe wanakutembelea.
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  pole ..lakini kuna watu wana bahati za kuwapatia wanaume waliowaacha revenge za ukweli eeeh..
  i wish aisee ...
  kweli Edna Boimanda ana bahati....
  pole mkuu
  msubiri Mr Rocky aje..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  @lizzy umeona hiyo heading kwanza....
   
 5. s

  simbamweupe Member

  #5
  May 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  jAMANI, MIMI NILIJARIBU NJIA ZOTE KWA KUELEWANANAE, ILA AMEKATAA KILA AINA YA MAELEWANO. SASA NA ELIZABETH, HAMNA SHIDA KABISA, TAYARI NIMESHANDAA DOCUMETS ZOTE ILI AFIKE ITALY KWA KUISHI PAMOJA. JE NELSON LAKINI? SASA MIMI NAWAOMBA KAMA UNAWAFAHAMU NJIA YA KUNISAIDIA KWA KUIONDOA HIYO P.I.
   
 6. N

  Ntu JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 564
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 60
  Duh inauma sana, na pole sana mkuu! Ngoja wanasheria wa humu ndani wapange vifungu vya sheria viendane na maelezo yako ili waje kukupa suluhu. Kitu Kidogo + Ngono + Kujuana = Magamba Government.
   
 7. s

  simbamweupe Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Samahani, labda sijawaelewesha vizuri kuhusu maana yake P.I. (prohibited immigrant) yaani, nilifikuzwa nchi kwa sababu nilivikanyaga miguu viongozi vyenu katika yule mama mjinga ambaye hana akili hata kidogo. Nawaomba mniamini, ninachokisumbua kichwa sana ni kwamba yule mtoto, ambaye hana makosa yoyote, ambaye hausiki na matatizo kati ya mimi na mama yake, alipoteza nafasi ya kulipewa penzi la baba yake mzazi. Nasikitika sana, kwasababu, najua itafika siku atakuwa anasikia huzuni na unyonge kwa kuwa baba yake hayupo karibu nae. Nawaomba tena kama kuna mtu mwenye roho safi anipe ushauri na msaada wake. Email yangu: peppezingaro@hotmail.com
  Nawategemea!!!
  Ahsanteni sana
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe Mtaliano huwajui mafia? watumie.

  Boimanda hajui kuwa damu ya Kiroma huwa haiwachwi kupotea.

  Jamani ndugu zangu Watanzania, msihini huyu Boimanda na Kalembo wake, Wataliano huwa hawachezewi kwa damu yao. Hii aliyoandika hapa huyu Mtaliano ni warning kali sana kama hamuwajui hawa watu, huwa wana justify revenge kabla ya kuifanya. Huyu hata ipite miaka 100, kama si yeye basi nduguye au mwanae au mtu yeyote wa ukoo wake atalipiza kisasi.

  Nakupa pole boimanda na kalembo na koo zenu wote wawili in advance.
   
 9. s

  simbamweupe Member

  #9
  May 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Acheni na mafia, mafia ni kitu kibaya sana, na pia sitaki kuitumia njia mbaia, mimi nataka niwe na haki za binadamu.

  Haki ya kukaa karibu na mtoto wangu, sawa sawa na wengine ambao walitengana lakini wanajali sana mazingira masafi kwa watoto wao.

  Mnaona, mimi sijawahi kusema nataka mtoto aishe na mimi. Hapana, ninachotaka ni haki ya kuwa karibu nae hata kama ataishi na mama yake, ila sasa wakati siwezi kurudi nchini, nitafanyaje?
  Mtoto wangu atafanyaje kwa kuwa na haki ya kuwa karibu na baba yake.
  Nye hamwezi kujua, yule mtoto ananipenda kiasi kikubwa sana. alipokuwa na mimi alikuwa anafurahi.
  Yaani nasikia huzuni mno.
   
 10. s

  simbamweupe Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
 11. mka

  mka JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu pole, hilo la uhamiaji ulipaswa kulichukulia hatua za kisheria mapema sana. Ila hujachelewa kwa sasa tafuta wakili atakusaidia kuomba custody au kumuona mtoto, umiliki wa kampuni yako na pia hilo la kunyimwa visa ya makazi kwa shinikizo unaweza omba mahakamani 'judicial review' on ground that Immigration Department was dictated and abdicated by the RC contrary to the principles of Administrative law'. Hapo mahakama itayapitia upya maamuzi ya Idara ya Uhamiaji na kutoa uamuzi wa kuyafuta na kuamuru Uhamiaji wafuate sheria. Mwishowe wapaswa kumfungulia Said Kalembo kesi ya kuchafuliwa jina (defamation).
   
 12. s

  simbamweupe Member

  #12
  May 31, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ahsante sana, rafiki yangu Mka, pia mimi nilikuwa tangu mwanzo nataka kumfungulia kesi na Kalembo, kwa jinsi, alinichafua jina langu, tena kwa uwongo, maana mimi nilikuwa na kampuni yangu kabisa yenye usajili BRELA.
  Pia nakushukuru sana kwa ushauri kuhusu mto.
  Sasa nakuomba cha mwisho, huyu wakili, afungue kesi wapi? Yaani, Tanga, Dar es Salaam au mahakama nyingine?
  Maana,unajua, nikiwa mbali hivyo sio raisi kuwa makini sana, ndiyo maana, niliamua kuuomba msaada wenu
   
 13. congobe

  congobe JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 499
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  pole sana Dada mi nakushauri ni vyema pia ukawasiliana na ubalozi wa Italiy hapa Tanzania kisha upate msaada wa kisheria itakuwa ni rahisi kwa maana una mtu wa kiserikali wa kwenu
   
 14. mka

  mka JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 318
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu kuhusu kupitia maamuzi ya uhamiaji ni mahakama kuu-Tanga, maana ndio huko tukio lilikotokea. Ila sasa ufanye haraka kufungua kesi hiyo na kutoa sababu kwa nini ombi likubaliwe kwa maana upo nje ya muda kisheria. Maombi ya kupitiwa uamuzi wa utawala (judicial review) ni miezi sita baada ya tukio kutokea. Hilo la defamation unaweza fungua kesi Tanga tukio lilipotokea au mahali alipo mdaiwa, Kalembo.

  Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
   
 15. s

  simbamweupe Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ahsante, ila mimi ni Baba, sio mama, kwa hiyo mwanaume
   
 16. s

  simbamweupe Member

  #16
  Dec 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari zenu mabwana na mabibi?
  Napenda kuwasilisha kwamba, hatimaye, nimeshinda kusuluhisha matatizo yangu.[
  Balozi wa Italia, alikutana na Mhe Waziri Nchimbi, na baada ya kujadili mambo, Waziri tarehe 21 mwezi huu ameifuta P.I. didhi yangu.
  Sasa narudi, na nitaiomba mahakam tuendelee na kesi zangu, ya kwanza kesi ambayo mimi ndiyo mshtakiwa na Edna Boimanda mshtaki.
  Maana hakuna kosa nililofanya, na ilikuwa imeshaeleweka, baada ya hiyo kesi, ndiyo itakuja "revenge".
  Sina uhakika kama Edna Boimaanda ana bahati kweli.
  Nawatakia heri ya Mwaka Mpya kwa wote.
  Ahsanteni sana
  P.S. Kama mnakumbuka, Elizabeth alikuwa mimba.
  Tarehe 6 mwezi wa 9 2012 amezaliwa Dayana G. Zingaro.
  Naenda kumfahamu mtoto wangu mwingine
  QUOTE=zomba;3934261]Wewe Mtaliano huwajui mafia? watumie.

  Boimanda hajui kuwa damu ya Kiroma huwa haiwachwi kupotea.

  Jamani ndugu zangu Watanzania, msihini huyu Boimanda na Kalembo wake, Wataliano huwa hawachezewi kwa damu yao. Hii aliyoandika hapa huyu Mtaliano ni warning kali sana kama hamuwajui hawa watu, huwa wana justify revenge kabla ya kuifanya. Huyu hata ipite miaka 100, kama si yeye basi nduguye au mwanae au mtu yeyote wa ukoo wake atalipiza kisasi.

  Nakupa pole boimanda na kalembo na koo zenu wote wawili in advance.[/QUOTE]
   
 17. Kamanda Kazi

  Kamanda Kazi JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2012
  Joined: Dec 15, 2012
  Messages: 2,622
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  hujachelewa...chukua hatua kupitia ubalozi wenu hapa Tanzania. au pitia ubalozi wa Tanzania nchini Italy! ukipitia katika ofisi za balozi ishu huwa zinakuwa so sensitive.
   
Loading...