Maofisa TRA wazungumzia sababu ya makontena kulundikana bandarini

Mkuu wangu Njowepo wafanyabiashara wa k.koo walikuwa wanamlipa HSC kuanzia mil.8-14 pesa za ushuru yeye alikuwa anajua kucheza na watumishi wa TRA na TBS wafanyabiashara wanepelekewa mzigo warehouse bila hata doc.
NA AM SURE HAKUNA MTU TRA wa kura sahani moja na HSC mtaishia kukomaa na Dagaaa tuu
 
Hongereni Vijana Wa Mwakyembe
Wekeni Uzi huo huo kuhakikisha bandari siyo shamba ya bibi
John, jabiri, Shayo, Jaffer, Kawishe Uzi huo huo
Ujasiri wenu ni kipi tosha Cha kusema Vijana mnaelewa kazi
 
Wengi nliowaona ni CDMA,Kila leo mara Magamba sasa mko wapi? Mkianza WIZI mapema hivi mkipewa nchi mtaibugia
Kama nguluwe warifanya mikutano ya kumnyanyanya hms kazi ya mizigo waliposhindwa wakachoma bila kujua wanakata mti wakiwa wamekalia tawi sasa wacha wavunjike migongo
 
Naona watu wengi wanachangia vizuri lakini kwa kusikia maelezo kati ya wafanyabiashara na TRA,mimi sio mfanyabiashara ila siku kama 6 zilizopita nilitoa mzigo wangu ambao ulikuwa na vifaa vya kutumia, ningeweza ku attach makisio ya TRA ningefanya hivyo lakini nimeshindwa,mngeona makisio yao yalivyo fake na ya ovyo ovyo,kwa mfano kulikuwa na baiskeli ya mtoto wa miaka 3 ambayo niliinunua kwa dola 100 wao katika makisio yao wakaweka $300 yaani sikuamini!!!Tax yote ikaja 6.5ml wakati kwa ule mzigo na kwa vile ninatuma mara kwa mara makisio yangu ilikuwa 3.5ml.Tra wana uplift sana,makisio yao fake hayaendani kabisa na thamani ya vitu wanavyothaminisha..Hii ndiyo nilimjibu Lara 1 katika uzi wake wa mambo ya biashara kuwa Tanzania haina mazingira mazuri kwa biashara maana system yetu ya kodi haipostable ata kidogo..Nigeria wana system nzuri sana ya kodi kwa wazawa ndio maana ukitembelea miji ya kibiashara duniani utakutana nao sana hii stability of taxation system imesaidia sana ajira kwa vijana wa Nigeria,leo hii nchi zote za afrika magharibi kama cameroon,Guinea,Chad,senegal nk vijana wao hawaendi dubai/china kununua bidhaa wanakwenda Lagos Nigeria..Sisi pia tungekuwa na system nzuri ya kodi vijana wa Rwanda,Burundi,Zambia,Malawi nk wasingeenda Dubai/China wangekuja Tz kununua bidhaa,lakini sasa ni tofauti sisi wenye bandari tunakwenda kusiko na bandari(Rwanda,Uganda)nk kununua bidhaa.Wanatoa sababu eti wafanyabiashara wanaandika kwenye container kuna viatu wakati kuna magari!!!pale bandarini kuna T scanner ambayo ata ukificha sindano kwenye container itaonekana..Tunatakiwa tubadilishe system yetu ya kodi tuache mambo ya kukisiakisia,ndio maana mpaka leo simu iliyopitwa na wakati kama samsung S3 zinauzwa bei ya juu wakati hapo dubai ni tsh 480000/na less than 350000/kwa bei ya jumla../ mzigo wangu haukuwa wa biashara naona huruma kwa wafanyabiashara waliochukua mikopo kusafirisha tu container la futi 20 toka dubai is almost $2000 na kodi na storage za pale bandarini sijui mtarudisha vipi mikopo
 
Majanga haya kasababisha HOME SHOPING CENTRE container la nguo yeye anaandika Net

Huo ulikuwa mradi wa baadhi ya wazito wa TRA na waserikali wengine,HSC akawa ndiye Clearing agent wa bei RAHISI,mzigo wa kodi ya 50m yeye alikuwa anachukua 20m ambazo alikuwa anagawana na maofisa wa TRA na Viongozi wengine huku makontena ya nguo,matv,vipuri vya magari Nk.Nk.NK yakitolewa kama shehena ya Viandarua bila kulipiwa hata senti tano.
Hivyo wafanyabiashara wanaposema kwamba kodi imepandishwa hadi 100 au 200% ni kwamba sasa hivi kodi inatakiwa iende TRA na sio kwa wale majambaZI WA HSC NA GENGE LAO LA UHARIFU. Limebumburuka wakuu kazeni buti toeni mizigo
 
Mimi nadhani asilimia kubwa wafanya biashara wamekuwa wakikwepa kodi ili hali wafanyakazi hawakwepi kodi. sasa wanakaguliwa wanaona tabu. Mimi nadhani wachukuliwe hatu za kisheria kama hawalipi kodi stahili. lakini pia nawahasa TRA wahakikishe na wakubwa hawakwepi hizo kodi. Isiwe ni wadogo tu
 
[QUO

ndgu yangu hizo container zilikuwa 700 ktk icds mbalimbali ktk hizo container waliandika kwenye nyaraka zao kuwa wamebeba mosquito nets kumbe ni wax sasa huoni huu ni wizi tena wa wazi kabisa?? na hii biashara imefanyika kwa mialka zaidi ya sita sasa hapo tr analaumiwaje?


TE=Njowepo;6462368]Huu ni mradi mwingine wa TRA kupiga ela
Ivi hawa TRA wamekuwa miungu mpaka tuwaamini kiasi iko?Kila kona watu wanapiga including hao TRA kama vinala wa kuwaambikia watu KODI.
Ivi unafanya physical verification kwa container 400 how long willit take.
Ivi kuwa serious mlianza lini TRA?TRA hiii hiii ya Tanzania au ya UK
Mizigo mngi inapita bila kulipa kodi apo leo mumeamua kukomaa na wafanyabiashara kuna kitu apo sio bure![/QUOTE]
 
Hii issue sasa ndo nimeielewa baada ya kusoma thread kama 3 tofauti tofauti.
Iyo koadi muilipe tuu mambo ya kusema kontena lina tooth pick kumbe lina WAX
Kamua TRA ili tuwe tunakusanya 1 trillion plus
Ila Kitilya ana bahati ningekuwa bosi wake kila mwezi nampa Malengo ukiferi miezi 3 kazi basi
Kwa kuanzia ningeanza na 1trillion ili kwa mwaka tuwe na 12trillion apo tunaweza kuwa na bajeti ndogo tegemezi
 
Tuwe wakweli walipa kodi wakubwa katika Taifa letu ni wafanya kazi walio kwenye ajira, hao si rahisi kukwepa kulipa kodi, kodi inakatwa kwenye mshahara wao moja kwa moja.

Binafsi naona mawakara wa kutoa mizigo bandarini walikuwa wanashirikiana na baadhi ya viongozi/wafanyakazi wa TPA na TRA yenyewe katika kufanikisha ukwepaji mkubwa wa kulipa kodi, si rahisi mfanya bihashara kujua jinsi ya ku-grease chain nzima ya walaji katika vitengo husika - mawakara ndio wana-deal na chain hiyo kila siku na kusema kweli wame nemeheka sana kutokana na tabia hiyo chafu; TRA haiwezi kukwepa lawama nayo inahusika katika kashfa hii- baadhi ya wafanya kazi wao wanahusika sana, na wala wasije kutudanganya kwamba walikuwa hawajui kilicho kuwa kinaendelea behid the scene, na si hajabu sakata hilo limekuja kuwa exposed baada ya aidha wafanya kazi wa TRA wenyewe au wafanya bihashara kuchomeana UTAMBI.

Katika nchi zilizo endelea Raia au Rais anaweza kuteleza kidogo akapewa onyo, lakini kama ikidhihilika kwamba Rais au Kiongozi fulani Serikalini aliwahi kukwepa kulipa kodi na ikathibitika, basi utiwa pingu na kuishia gerezani - hawana utani na masuala ya ukwepaji wa kulipa kodi - hapa kwetu ni tofauti kabisa, ndio maana maghorofa Kariakoo yanahota kama uyoga sababu wafanya bihashara wanapata hyperprofit kutokana na ukwepaji mkubwa wa kulipa kodi!

Wanakwepa kodi huku wanauza kwa bei kubwa as if wamelipa kodi.
TRA wana haki zote za kukagua mizigo kwa namna yoyote waki,utilia shaka. Naunga kabisa na TRA kuwataka wafanyabiashara walioagiza mizigo walipe kodi stahiki bila kukosa. Kiasi walivyodanganya huko nyuma sasa wamekamatwa no way na wakileta ujuaji wajue imekula kwao.
 
NA AM SURE HAKUNA MTU TRA wa kura sahani moja na HSC mtaishia kukomaa na Dagaaa tuu

wakomae nae mara ngapi??haya makontena ya wafanyabiashara wa kariakoo yanakuja kama ya HSC na wafanyabiashara hawa wanachukua warehouse za HSC bila documents coz docs zote wanazo HSC.....sasa yamezuiwa mpaka walipe ushuru unaostahili......
 
Tufike mahali tujitendee haki sisi wenyewe......kukwepa kodi ni wizi......Vyombo vya dola na TRA fanyeni kazi yenu......mapato yakiongezeka na ndio uwezo wa serikali unakuwepo wa kuwapa nyongeza na marupu rupu....

...mkiruhusu mambo ya ujanjaujanja kuendelea wezi wataendeleza wizi, wala rushwa wataendelea na rushwa.....na mlio wengi mtakosa nyongeza/marupurupu.......it is as simple as that!.......Ninawapongeza TRA kwa hatua yao........Ninawaomba pia wafanye hivyo hivyo kwa mizigo ya Vigogo na ya Foreigners wote.......sio wengine wapite bila kuchekiwa huku wananchi tunaangalia.........
 
Niliwahi kileta mzigo wa thamani ya $1000 na huo mzigo umekuja na risiti yake ndani ya box kutoka Dubai.
Kilichonishangaza TRA kuthaminisha lile box kwa $5000 na ile risiti nimeambiwa kuwa ni feki.iliniuma sana kwasababu ulikuwa ni mzigo wangu binafsi sio wa biashara.

So kwa mtazamo wangu TRA ndo inatufundisha Wizi,wanakwekea vikwazo ili ulipe kodi kubwa au utozwe rushwa.hawana uhakika na valuation yao so lazma system ita corrupt.
Ukienda airport cargo terminal ndo vichekesho alie kuwa mamantilie nae anakutolea mzigo
 
Niliwahi kileta mzigo wa thamani ya $1000 na huo mzigo umekuja na risiti yake ndani ya box kutoka Dubai.
Kilichonishangaza TRA kuthaminisha lile box kwa $5000 na ile risiti nimeambiwa kuwa ni feki.iliniuma sana kwasababu ulikuwa ni mzigo wangu binafsi sio wa biashara.

So kwa mtazamo wangu TRA ndo inatufundisha Wizi,wanakwekea vikwazo ili ulipe kodi kubwa au utozwe rushwa.hawana uhakika na valuation yao so lazma system ita corrupt.
Ukienda airport cargo terminal ndo vichekesho alie kuwa mamantilie nae anakutolea mzigo

Mkuu...hili jambo mimi nimekumbana nalo mara kwa mara.........sijui ni mfumo gani utumike ili TRA waamini risiti unazowaonyesha ni halali......hii ya kuachiwa afisa fulani aamue.......au mambo ya kuanza kushitakiana mahakamni.......si sahihi na si haki kabisa......kwa watu waliojidundulizia vihela vyao na kurudi nyumbani na vitu vyao binafsi kulipishwa mikodi ya ajabu ajabu.......

Ifike mahala mtu unatakiwa kujisikia ni haki na ni sahihi kulipa kodi STAHIKI na kwenye mfumo makini.......
 
Huo ulikuwa mradi wa baadhi ya wazito wa TRA na waserikali wengine,HSC akawa ndiye Clearing agent wa bei RAHISI,mzigo wa kodi ya 50m yeye alikuwa anachukua 20m ambazo alikuwa anagawana na maofisa wa TRA na Viongozi wengine huku makontena ya nguo,matv,vipuri vya magari Nk.Nk.NK yakitolewa kama shehena ya Viandarua bila kulipiwa hata senti tano.
Hivyo wafanyabiashara wanaposema kwamba kodi imepandishwa hadi 100 au 200% ni kwamba sasa hivi kodi inatakiwa iende TRA na sio kwa wale majambaZI WA HSC NA GENGE LAO LA UHARIFU. Limebumburuka wakuu kazeni buti toeni mizigo


Tena hawa jamaa wa Home Shopping ni wabaya sana maana nimeckia kwamba wanahusishwa hata na kuivuruga system ya TRA maana watu wamekuwa wakilalamika kwenye ma ICD kwamba kuna wakati unakuta mnaambiwa system iko down lkn utashangaa mizigo ya HSC inatoka,tena mbaya zaidi inasemekana jamaa hata realese anazifyetua mwenyewe kwa kuhack system ya TRA.
 
Huo ulikuwa mradi wa baadhi ya wazito wa TRA na waserikali wengine,HSC akawa ndiye Clearing agent wa bei RAHISI,mzigo wa kodi ya 50m yeye alikuwa anachukua 20m ambazo alikuwa anagawana na maofisa wa TRA na Viongozi wengine huku makontena ya nguo,matv,vipuri vya magari Nk.Nk.NK yakitolewa kama shehena ya Viandarua bila kulipiwa hata senti tano.
Hivyo wafanyabiashara wanaposema kwamba kodi imepandishwa hadi 100 au 200% ni kwamba sasa hivi kodi inatakiwa iende TRA na sio kwa wale majambaZI WA HSC NA GENGE LAO LA UHARIFU. Limebumburuka wakuu kazeni buti toeni mizigo

Sijui huu mpango wa kukata ulaji wa watu wachache TRA utakuwa endelevu
 
Dah huo utaratibu wa scanning ni bora ukaendelea ila kwa huo wa kufumua makontena na kuchungulia kuna nini naona umepitiliza mipaka...sijui sheria za kimataifa za kibiashara zinasema nini juu ya hili.......

Kwani cha ajabu ni nini hapo? Mbona kabla ya kuleta hizo scanner macontainer yalikuwa yanafunguliwa na custom officers wanahakiki kilichomo? Tatizo hapo ni kwamba hao individual customs officers wanatakao kuwa wanafanya hiyo kazi, utajiri ni nje nje!!!!!


Tiba
 
Niliwahi kileta mzigo wa thamani ya $1000 na huo mzigo umekuja na risiti yake ndani ya box kutoka Dubai. Kilichonishangaza TRA kuthaminisha lile box kwa $5000 na ile risiti nimeambiwa kuwa ni feki.iliniuma sana kwasababu ulikuwa ni mzigo wangu binafsi sio wa biashara. So kwa mtazamo wangu TRA ndo inatufundisha Wizi,wanakwekea vikwazo ili ulipe kodi kubwa au utozwe rushwa.hawana uhakika na valuation yao so lazma system ita corrupt. Ukienda airport cargo terminal ndo vichekesho alie kuwa mamantilie nae anakutolea mzigo


Mkuu hata mimi yalisha wahi nikuta hayo! Baadhi ya wafanyakazi TRA wana viburi sana, mzigo nilinunua mwenyewe nilipo kuwa nje ya nchi na risiti ilikuwa ni halali sio fake au nini - lakini 4 some reason jamaa alikuwa anatafuta kila njia ili nishindwe kabisa kutoa mzigo wangu ali-inflate charges zaidi ya mara sita!! Nilijaribu kumuelewesha bila mafanikio, alipo nichosha na mizengwe yake nikahamua kumuona Kamishena nikamsimlia kila kitu na kumuonyesha documents husika, kwa bahati Afisa huyo alikuwa ni mtu muelewa i.e alijua kilicho kuwa kinaendelea, akafanya tathimini iliyo sahihi na kunambia niende kulipia. Nataka nikili kwamba bila kamishna huyo kuingilia kati mzigo ungenishinda kutoa, sasa matukio kama haya wakati mwingine unaweza kuchangia katika watu kuwasilisha documents za uongo-hapa nazungumzia mtu wa kawaida aliye nunua luninga moja say, sio mfanya biashara.

Tukija kwenye system zao, hapo ndio utachoka - masaa yote wanasingizia kwamba hiko down, lakini ukweli wa mambo wanataka wafanye manually ili waweze ku-doctor figures, wakati mwingine unaweza kufikili labda hawana uelewa mkubwa wa kutumia baadhi ya applications kwenye system zao, waliwahi kuwa na system mahili inayo julikana kama ASYCUDO (kama sikosei spelling) system hii bado inatumika kwa ufanisi mkubwa sana huko makao makuu ya COMESA nchini Zambia (Lusaka), waswahili wa hapa wakishirikiana na makampuni ambayo wamiliki wao wengi ni Watanzania wenye asili ya ASIA (siyasemi haya kwa nia mbaya,Taifa likubali kuna wizi mkubwa katika nyanja ya ku-supply vifaa na software za takohama, na kibaya zaidi watu wa kawaida si rahisi kuligundua hilo), basi waswahili wakarubuniwa na jamaa hawa wajanja mpaka wakafikia hatua ya kuitupilia mbali system ya ASYCUDO!!!

Jaribu kuangalia kila mwaka utaona TRA inatoa tenda za mabillion kununulia system zile zile, na si TRA peke yake karibu mashirika makubwa ya Serikali yana tatizo hili, yaani mtu unashindwa kuelewa ulazima wa kununua system hizo hizo kila mwaka, kwa nini hawa upgrade apps programs kama kuna ulazima na wala huitaji mfanya bihashara ukufanyie hilo, hiyo ni kazi ya System Admin na Director/Manager wa ICT kufanikisha hilo, mimi huwa na shangaa! Hivi hawa ma Manager na ma Directors wa ICT kwenye mashirika Makubwa ya Serikali kazi zao ni zipi HASA!!! Kusema ukweli Serikali inapaswa kuangalia upya mbinu zinazo tumika katika kutangaza TENDA za uongo na kweli za takohama kwenye mashirika yake TANZU, kuna wizi mkubwa sana - tofauti yake na mambo ya Richmond ni mdogo SANA, narudia kuna Makampuni yaliyo kubuhu katika wizi huo wakishirikiana na ma Directors/Managers wa ICT tatizo hili linapaswa kuwa addressed na Serikali yetu kikamilifu kwa madhumini ya ku-plug loopholes zote zinazotumika katika kufanikisha njama hizo; kumbuka tatizo ni kubwa SANA.
 
HSC,,,,,, ni mabingwa wa kubadilisha ma clearing agent,mara EAGLE,LONE ,RED WAYS. NAWN ENGINE KIBAO
 
wakomae nae mara ngapi??haya makontena ya wafanyabiashara wa kariakoo yanakuja kama ya HSC na wafanyabiashara hawa wanachukua warehouse za HSC bila documents coz docs zote wanazo HSC.....sasa yamezuiwa mpaka walipe ushuru unaostahili......
Bado sina imani kwa serikali hii ya TZ mwenye updates atupe imeishaje hii issue
 
Back
Top Bottom