Maofisa TRA wazungumzia sababu ya makontena kulundikana bandarini

TCleverly

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
1,921
866
wafanyabiashara wa kariakoo wamelalamika kwamba makontena yao yamekwama bandarini kwa zaidi ya mwezi mmoja na nusu sasa. wafanyabiashara hao wamedai kuwa tra wamepandisha ushuru ghafla kwa zaidi ya 100-200%.
leo maofisa wa tra wanahojiwa na clouds fm na wamesema kuwa kilichosababisha makontena hayo kukwama bandarini ni udanganyifu uliokuwa unafanywa na wafanyabiashara hao lkwa muda mrefu.wafanyabiashara hao walikuwa wanaorodhosha mizigo aidha tofauti au idadi ndogo na ukweli uliopo ndani ya kontena.baada ya kugundua hilo tra wakasitisha kutumia scanner na kufungua kila kontena.walichogundua ni bidhaa tofauti na zilizoandikwa.

kwa mujibu wa tra na sheria za nchi ukidanganya bidhaa uliyoleta unatakiwa upewe adhabu lakni tra waliamua kufuta adhabu na kuwapa wafanyabiashara hao siku 21 walete viuelelezo vingine vilivyo sahihi.
wafanyabiashara hao baada ya kuleta vielelezo wameishia kulalamika mitaani na kwenye vyombo vya habari.tra wanasisitiza ili makontena hayo yatoke ICD ni juu ya wafanyabiashara walete vielelezo nini kimo kwenye makontena hayo,kwa idadi gani na thamani gani la sivyo zikipita siku 21 tra wana mamlaka ya kunadi bidhaa hizo.

pia tra wanasisitiza kukagua mizigo physically badala ya scanning sio kubadili utaratibu ni uamuzi tu wa kuamua kufanyakazi,wafanyabiashara wameabuse utaratibu wa scanning ndio maana tra wameamua kufungua makontena.
tra inasisitiza wafanyabiashara walete nyaraka lakini hadi leo wamekimbia wanalalamika kwa vyombo vya habari,wafanyabiashara pia wanashauriwa walete malalamiko yao ni ofisa gani wa tra anawasumbua na watoe taarifa nini hasa anawasumbua.

kauli ya tra ni kwamba:wafanyabiashara waje watoe vielelezo,walipe kodi inayostahili wachukue mali zao
 
Customs wako sahihi kabisa, ni lazima wahakikishe kila mzigo unaoingia bandarini umefuata sheria za forodha na kukidhi viwango vya kodi.
Lakini customs wanajua toka mwanzo kabisa aliyesababisha dhahama ili ni nani ushahidi walipewa wiki iliyopita kwenye kikao cha waziri na makontena yake yote wameishayakamata.

Sasa kigugumizi cha kumshughurikia huyo mtu aliyekuwa anawaghiribu wafanyabiashara wasilipe kodi kinatoka wapi? Kwanini wasimshughulikie ili watoe mwanya wa michakato mingine ya kutoa mizigo kuendelea badala ya kulazimika kukagua makontena yote na hivyo kupunguza ufanisi wa bandari na mzigo kwa wafanyabiashara wasafi.
 
Huyo nae afisa wa TRA aliyekabidhiwa kuhakiki bidhaa physical atakua bilionea sasa hivi!

yaani una akili nyingi sana kumzidi dhaifu.waswahili tunasema zali la mentali.ashindwe yeye tu.nchi hii ndipo tulipofikia,kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.ni ubinafsi tu umetawala.
 
Dah huo utaratibu wa scanning ni bora ukaendelea ila kwa huo wa kufumua makontena na kuchungulia kuna nini naona umepitiliza mipaka...sijui sheria za kimataifa za kibiashara zinasema nini juu ya hili.......
 
Customs wako sahihi kabisa, ni lazima wahakikishe kila mzigo unaoingia bandarini umefuata sheria za forodha na kukidhi viwango vya kodi.
Lakini customs wanajua toka mwanzo kabisa aliyesababisha dhahama ili ni nani ushahidi walipewa wiki iliyopita kwenye kikao cha waziri na makontena yake yote wameishayakamata.

Sasa kigugumizi cha kumshughurikia huyo mtu aliyekuwa anawaghiribu wafanyabiashara wasilipe kodi kinatoka wapi? Kwanini wasimshughulikie ili watoe mwanya wa michakato mingine ya kutoa mizigo kuendelea badala ya kulazimika kukagua makontena yote na hivyo kupunguza ufanisi wa bandari na mzigo kwa wafanyabiashara wasafi.

Mkuu na wewe mtaje basi huyo mfanya biashara bado unaleta kigugumizi?
 
Dah huo utaratibu wa scanning ni bora ukaendelea ila kwa huo wa kufumua makontena na kuchungulia kuna nini naona umepitiliza mipaka...sijui sheria za kimataifa za kibiashara zinasema nini juu ya hili.......

Mkuu hakuna sheria ya kimataifa ina guide kuhusu kufungua au kutofungua kontena na kuchungulia ndani. Hayo mambo ya scanner yaliwekwa tu ili kufacilitate trade na kupunguza delay kwa wafanya biashara. Na kwa kuwa wanafanya false declarations tra haina budi kufanya physical verification Sio kosa.
 
Lakini kuna uhakika gani kuwa hakuna wizi utakao kuwa unatokea kwenye hayo makontena??

Kama mtu kaagiza say vito vya thamani na vimo ndani ya kontena TRA wana uhakika gani hawatapata malalamiko ya udokozi hasa ukizingatia wapiga deal wamejaa sana pale TRA??
 
Wizi unatokeaje sasa na wakati wa ukaguzi agent lazima awepo au atakuibia agent wako?
 
Customs wako sahihi kabisa, ni lazima wahakikishe kila mzigo unaoingia bandarini umefuata sheria za forodha na kukidhi viwango vya kodi.
Lakini customs wanajua toka mwanzo kabisa aliyesababisha dhahama ili ni nani ushahidi walipewa wiki iliyopita kwenye kikao cha waziri na makontena yake yote wameishayakamata.

Sasa kigugumizi cha kumshughurikia huyo mtu aliyekuwa anawaghiribu wafanyabiashara wasilipe kodi kinatoka wapi? Kwanini wasimshughulikie ili watoe mwanya wa michakato mingine ya kutoa mizigo kuendelea badala ya kulazimika kukagua makontena yote na hivyo kupunguza ufanisi wa bandari na mzigo kwa wafanyabiashara wasafi.

huyo mtu atashughulikiwa.....lakini kontena hazitatoka hadi zilipiwe kodi inayostahili....
 
Huyo nae afisa wa TRA aliyekabidhiwa kuhakiki bidhaa physical atakua bilionea sasa hivi!

kukagua bidhaa physically haijaanza recently,ndio utaratibu wa zamani...ila wakaleta scanner ili irahisishe ukaguzi wa vitu straight foward lakini wafanyabiashara(labda kwa kushirikiana na watu wachache tra) wameabuse hii system...sasa wanakagua kwa naked eyes....wakwepa kodi wanalialia....
 
Huu ni mradi mwingine wa TRA kupiga ela
Ivi hawa TRA wamekuwa miungu mpaka tuwaamini kiasi iko?Kila kona watu wanapiga including hao TRA kama vinala wa kuwaambikia watu KODI.
Ivi unafanya physical verification kwa container 400 how long willit take.
Ivi kuwa serious mlianza lini TRA?TRA hiii hiii ya Tanzania au ya UK
Mizigo mngi inapita bila kulipa kodi apo leo mumeamua kukomaa na wafanyabiashara kuna kitu apo sio bure!
 
Majanga haya kasababisha HOME SHOPING CENTRE container la nguo yeye anaandika Net
 
Huu ni mradi mwingine wa TRA kupiga ela
Ivi hawa TRA wamekuwa miungu mpaka tuwaamini kiasi iko?Kila kona watu wanapiga including hao TRA kama vinala wa kuwaambikia watu KODI.
Ivi unafanya physical verification kwa container 400 how long willit take.
Ivi kuwa serious mlianza lini TRA?TRA hiii hiii ya Tanzania au ya UK
Mizigo mngi inapita bila kulipa kodi apo leo mumeamua kukomaa na wafanyabiashara kuna kitu apo sio bure!

two wrongs dont make a right.....kama wengine walipita huko nyum kwa kutumia mianya fulani wewe ukinaswa leo usilalamike....just paythe right amount of tax off u go.......
 
Hiyo scanner huwa haioni vizuri,au kuna tofauti gani na kufungua container?
 
huyo mtu atashughulikiwa.....lakini kontena hazitatoka hadi zilipiwe kodi inayostahili....

Bila kusahau TBS nao wanakula nae HSC haingii akilini container la TV liandikwe used computer ambazo hazilipiwi kodi.
 
Back
Top Bottom