Maofisa BoT kutaja vigogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maofisa BoT kutaja vigogo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Sep 3, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Maofisa BoT kutaja vigogo

  Mwandishi Wetu Septemba 3, 2008
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  Ni walioshinikiza kupitishwa kwa nyaraka feki

  MAOFISA wa Benki Kuu (BoT) ambao wanatajwa kuhusika katika mchakato wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika benki hiyo, sasa wanaelezwa kujiandaa kupasua bomu kwa kuwataja vigogo halisi waliohusika na wizi huo.

  Habari zinaeleza kwamba, baada ya mchakato wa kuwachukulia hatua za kisheria kuanza, maofisa hao wakiungwa mkono na watumishi wengi wa BoT, wametishia kumwaga hadharani yote wanayoyafahamu kuhusu wizi huo ulioligharimu taifa Sh bilioni 133.

  "Wamesema wao walijua kuwa iko siku watatolewa kafara, hivyo walikusanya ushahidi wote na walikuwa makini katika kupitisha kila dokezo lililohusu upitishaji wa fedha hizo na sehemu zote walitekeleza maelekezo ya mkubwa wao wa kazi na kwa kupitia idara ya sheria ya BoT," anasema ofisa mmoja wa BoT aliye karibu na maofisa hao.

  Akitoa mfano wa nyaraka zote zilizopitisha takriban shilingi bilioni 40 zilizochotwa na kampuni moja tu ya Kagoda Agricultural Limited, maofisa hao walitaka uhakiki wa wanasheria wa BoT, kabla ya kutaka tena baraka za aliyekuwa Gavana, Dk. Daudi Ballali, ambaye naye anaelezwa kufanya hivyo kwa maelekezo ama shinikizo kutoka kwa wanasiasa.

  RAIA MWEMA imeona baadhi ya nyaraka hizo za mawasiliano ambazo moja kwa moja zinaonyesha jinsi maofisa hao walivyotaka ushauri kwa wanasheria na idhini ya Gavana kabla ya wao kutoa maelekezo kwa watekelezaji wengine.

  Mfano katika moja ya nyaraka za kupitisha malipo ya Kagoda Agricultural Limited za mtajwa mmoja, Imani Mwakosya, ambaye alikuwa akikaimu kitengo cha mikopo, alimtaka mkuu wa idara ya sheria kuhakiki kwanza nyaraka za idhini ya kununua deni (Deed of Assigment) za kampuni hiyo kabla ya kuendelea na mchakato wa malipo na kabla ya kuwasilisha kwa Gavana kwa uidhinishaji.

  "Tafadhali thibitisha uhalali wa nyaraka husika kabla ya kupeleka maombi haya kwa Gavana kwa uhakiki wake na uidhinishaji," anaeleza Mwakosya katika dokezo lake la Oktoba 21, 2005 kwa Katibu wa Bodi ambaye naye siku hiyo hiyo aliandika kwa kusema;

  "Ninathibitisha kwamba nyaraka zilizoambataniswa ni halali na zinakidhi matakwa ya kisheria. Nyaraka hizi zinaweza kutumika na BoT kuidhinisha malipo husika."

  Baada ya mwanasheria kuandika dokezo hilo, siku hiyo hiyo (Oktoba 21, 2005) Mkurugenzi wa Fedha za Nje, alimuandikia Gavana kwa ufupi akisema, "ukiamua unaweza kuidhinisha malipo haya," na Gavana Ballali siku tatu baadaye kuidhinisha kwa neno moja tu, "approved" (imepitishwa).

  Habari za awali kutoka kwa BoT zinaeleza kwamba, dokezo hilo lilichelewa kwa siku tatu kutoka Oktoba 21, 2005 hadi Oktoba 24, 2005 kwa Gavana Daudi Ballali (Marehemu) kutokana na kusita kwake kupitisha malipo hayo hadi alipokutana na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, akiwa na mwanasiasa mmoja na Ofisa Mwandamizi wa Serikali na kuagizwa kuidhinisha.

  "Hata Mkurugenzi wetu (wa Fedha za Nje) alisita na alimwelezea Gavana wasiwasi wake kuhusu malipo hayo na ndio maana katika dokezo lake alimwambia wazi mkubwa wake kwamba kama akiamua anaweza kuidhinisha badala ya kumwambia ni halali idhinisha," kinaeleza chanzo chetu ndani ya BoT.

  RAIA MWEMA limeona dokezo ambalo Mkurugenzi wa Fedha za Nje alilofikia hatua hata ya kuandika neno, ‘what is this?' (nini hichi?) akihoji maelezo kutoka kwa maofisa wa chini yake kuhusiana na malipo ya Kagoda Agricultural ambayo yalikosewa kwa kuandikwa wakaandika Euros badala ya fedha za Ujerumani (Deutch Marks) ambazo ndizo zilizopo katika nyaraka za madai.

  Makosa hayo yalihojiwa pia na wakaguzi wa kampuni ya Ernst &Young ambao walishangazwa mno na jinsi mabadiliko hayo yalivyofanyika kwa haraka kwa wakurugenzi wanaoishi Ujerumani kuwasiliana kwa siku chache na wenzao wa Tanzania na kurekebisha makosa hayo na baadaye kurudisha nchini nyaraka husika. Makosa hayo yalisaidia kugundulika kuwa zilikua nyaraka za kughushi.

  Pamoja na taarifa za wanaochukuliwa hatua kuelezwa kuwagusa maofisa wasiozidi watano, habari za ndani ya BoT zinaeleza kwamba wanaotajwa kuhusika katika mchakato huo ni wengi zaidi na ambao waliorodheshwa moja kwa moja katika ripoti ya wakaguzi iliyowasilishwa serikalini.

  Wanaotajwa kwa nyadhifa zao baada ya Gavana aliyevuliwa madaraka na Rais ni Mkurugenzi wa Fedha na Katibu wa Bodi ambao walikuwa maofisa wawili walioshika nafasi hiyo katika kipindi ambacho fedha za EPA zilichotwa kutoka BoT (2005/2006) akiwamo mmoja aliyekaimu nafasi hiyo.

  Wengine wanaotajwa ni maofisa wawili waliongoza kitengo cha sera katika kipindi cha 2005/2006; Naibu Mkurugenzi Idara ya Madeni ambao nao wanatajwa kuwa wawili katika kipindi hicho; Mkuu wa kitengo cha madeni makubwa na ya kibiashara; Kaimu Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki aliyekuwapo.

  Maofisa wanaoonekana katika nyaraka nyingi za EPA ni pamoja na Imani Mwakosya, Esther Komu, Kimela, A.A.Chaula na M. Nderimo ambao kwa kiasi kikubwa wanaelezwa na maofisa wa BoT kwamba walifanya kazi kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zao akiwamo Marehemu Ballali ambaye naye alishinikizwa na viongozi wa juu na wanasiasa.

  Wiki hii imeripotiwa kwamba maofisa wanne kati ya watano waliosimamishwa kazi BoT wamefukuzwa kwa madai kwamba walizembea kuzuia upotevu huo mkubwa unaoendelea kuizonga serikali ya Rais Kikwete.

  Taarifa za kufukuzwa kwa maofisa hao ndio imeibua sasa hoja ya kutaka kuwataja wahusika wote waliohusika na walioshinikiza kuchotwa kwa fedha za EPA na kwamba sasa wameelezwa kutumia hata vyombo vya sheria kutimiza azma yao hiyo.

  Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba suala la wafanyakazi hao linashughulikiwa kwa kuzingatia mfumo wa kiutawala na kwa uangalifu zaidi kuepuka athari za kisheria kwa serikali na benki.

  Hatua ya kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua wafanyakazi hao, ilikuwa miongoni mwa hatua zilizoanishwa na wakaguzi na kukubaliwa na Rais Kikwete ambaye naye aliagiza zitekelezwe na kusisitiza katika hotuba yake bungeni wiki iliyopita.

  Katika hotuba yake kwa Bunge, Rais Kikwete alisema alikwisha kuiagiza Bodi ya Benki Kuu ichukue hatua za kinidhamu kwa maafisa wote wa Benki Kuu waliotuhumiwa na Mkaguzi ambao wapo chini ya Mamlaka ya Bodi.

  Mbali ya kuchukuliwa hatua kwa maofisa hao, Bodi ya BoT ilivunjwa na wengine wapya wakateuliwa, lakini baadhi ya wajumbe walirejea katika nafasi zao kwa nyadhifa zao akiwamo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.

  Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema, "Naelewa hoja ya wajumbe wanaoingia kwenye Bodi kwa nyadhifa zao, kuendelea kuwa Wabunge hata pale Bodi inapovunjwa kwa mapungufu au wale Wajumbe wa Bodi waliopungukiwa sifa mnawaondoa kwa kuivunja lakini mmoja ambaye anaingia pale kwa wadhifa wake anaendelea kuwepo.

  "Sasa hili tunalitafakari maana kama sheria imekwishamtaja atakuwepo fulani tutampeleka nani badala yake ukaonekana umetekeleza sheria, ni huyo huyo. Kwa hiyo, kama huridhiki nalo hilo fuata taratibu za utawala bora. Tusipokwenda na taratibu hizo nchi hii tutaingiza kwenye mess kubwa na wale wenye mamlaka kama mimi utakuwa unaonea watu kweli. Nikisema kwamba mkamateni fulani, atakamatwa tu."

  Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema uchunguzi kuhusu kampuni 13 yaliyochota Sh bilioni 90 umekamilika, wakati makampuni tisa yaliyochota shilingi bilioni 42, unalazimika kuhusisha washirika wa mataifa mengine ya nje na hivyo ametoa muda hadi Oktoba 31 kwa kamati aliyoiunda chini ya Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika kukamilisha kazi hiyo.

  Rais alisema wamekamata mali za watuhumiwa wote na kwamba "wale watu ambao kwa kweli walikuwa wanaonekana ni matajiri sana wapo katika hali ngumu sana. Wenyewe wanajijua hali zao zilivyokuwa ngumu sana."

  Alisema kwa sasa zimekusanywa shilingi 53,738,835,392/= na akaagiza fedha hizo kuingizwa katika mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo zikichanganywa na nyingine zinazotarajiwa kufikia shilingi 64,844,770,688/= .

  "Kamati imeomba idhini kuwa madeni hayo yanayoendelea kulipwa yaendelee kulipwa mpaka tarehe hiyo, maombi yao hayo nimeyakubali. Lakini tumekubaliana kwamba itakapofika tarehe 31 Oktoba,2008 mwisho ambaye hakulipa mpaka tarehe 1 Novemba, 2008 awe amefikishwa mahakamani ili Mahakama itusaidie kupata fedha za watu, hatuko tayari kulipa deni la marubeni India, Japan na mtu amekula hela yupo pale Dar es Salaam, hapana," alisema Kikwete.

  Hata hivyo, kumekua na hoja kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo wananchi wa kawaida ambao wamesisitiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wote wanaohusika hata ikiwa watalipa fedha walizopata isivyo halali vinginevyo nchi itagawanyika kwa wenye fedha kutochukuliwa hatua za kisheria na walalahoi kujazana magerezani.
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Patamu hapo sijui wataanza na Mkapa... yangu macho
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,194
  Trophy Points: 280
  Halafu Punda alidai kwamba wimbo wa EPA unaboa!!!!
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Punda ndio nani?
   
 5. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  While I applaud any effort to name names, this by no means exonerates the BOT officials. Unless they are saying they were clueless as to what was going on - which, first of all, with the admission of the preparations of wads of documents in anticipation of something big can hardly hold water - let alone the fact that admitting that would be synonymous with saying they were not qualified for their positions, simply forwarding a fraudulent document and accepting a superior's rubber stamp of approval without any further action makes these people accomplices in the grand corruption.

  If one is convinced some dishonorable ways are used to circumvent the checks and balances designed to act as a robust block against fraud, one should raise that as an issue internally or if the outcome is deemed as unsurmountable, one should promptly resign and blow the whistle.

  It is quite possible that, had just one junior BOT employeed acted in the manner outlined above, today the saga may not even have happenned.

  Inaction does not exonerate, part of the responsibility is theirs just the same.
   
 6. D

  Dotori JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2008
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jinamizi la EPA halitakwisha mpaka haki itendeke.
   
 7. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Wana ubavu wa kuwataja vigogo?
   
 8. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Intriguing
   
 9. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndio maana Mkapa amelikalia kimya suala hili, maana hawezi kukubali ukweli kua alihusika moja kwa moja na wizi huu mkubwa, na vilevile hawezi kukataa kwamba alikuwa hahusiki kwa sababu anafahamu kuna documents za ku-support kwamba yeye anahusika moja kwa moja.

  The only way ya ku-find out the truth about this matter is to take him to court. Muungwana anaregarega kwenye hili, ila we know Mkapa na Muungwana watakuwa hai for the next 10 years. Hivyo, lazima atatokea mtawala mwenye kujali maslahi ya nchi hii ambaye atawafikisha wote wawili into task... Mkapa kwa wizi akiwa Ikulu, na Muungwana kwa kumlinda mwizi ingawa alikuwa na vithibitisho vyote. Tusubiri tu, iko siku sauti ya wasiosikilizwa leo itakuwa ndio sauti ya kuwaangamiza wanaotuhujumu sasa hivi... Kwani Polisi Zombe alitegemea kuna siku atakuwa katika hot soup kama alivyo leo hii? Evidence zipo, na tutazitumia siku moja........... IKO SIKU!!!!!
   
 10. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Really now?
   
 11. Nikifufukammekwisha

  Nikifufukammekwisha JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 260
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa sala na nyimbo mzee... Inabidi kuwaombea kwenye sehemu za ibada ili wasife mpaka wapate kulipa maovu waliyotutendea wadanganyika.
   
 12. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #12
  Sep 4, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nilikuwa najiuliza nini maana ya kula kiapo kwa rais kwamba atailinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, tena kwa msahafu mbele ya watanzania. Kurudi kwenye hoja ya msingi, mimi naona kama rais kikwete amevunja hata hiyo katiba kwa kubaka kazi za mahakama ( rule of law and separation of power) kwani justice must be seen to be done na si vinginevyo. Nchi yetu sasa imekamatwa na kikundi cha watu, yani Ufisadipolitsm ( naufananisha na "Corporatism" in latin america). Rais akaye akijua kwamba Latin American nguvu ya umma ilibadilisha na kuua huo mfumo wa makampuni ya wajanja.

  Inakuwaje mwizi akabembelezwa na mkuu wa nchi ? Rais is not above the law na amesigina katiba kwa kutofuata mfumo wa utawala kama ilivyoelezewa kwenye katiba. Suala wezi wa EPA waligushi na kuiba. Mtuhumiwa wa wizi anatakiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria na kushtakiwa. Rais kwa kutumia ujanja ujanja anaamua kusoma "risala" kwa masaa matatu kujaribu kutetea watuhumiwa. Kuna double standard Tanzania. Nasema haya kwa uchungu. Mfumo mzima wa utawala umebakwa na ufisadipolitism kwa sababu it is an order the day that if you want to get reach quickly enter into politics business, hii si siri.

  Umefika muda sisi wadau kuanza mpango mbadala wa kuinusulu nchi hii. Tunatakiwa kuakikisha tunakuja na katiba mbadala na kuweka popular presure to the exisiting regime. Katiba iliyopo does not reflect the will of the Tanzania.Mfano kunatakiwa si tu suala la mihili ya utawala kutajwa katika katib, Kinachotakiwa ni spreading the power kwenye hizo nguzo 3 za uongozi.

  Bunge letu kama lilivyo ni extension ya chief executive( President). Investigatory power should be vested to the people through the legislature na si kwa mtu mmoja yahani Rais.

  Shime watanganyika na wazanzibari, kuakikisha 2010, majority of the mps watoke upinzani.

  Naomba kuuliza, article of the union ni public document , manake hapo ndo chimbuko la Tanzania. Document hii ni muhumu katika kutafsiri sheria ya nchi hii. Kwa nini document hii imefichwa?

  Mwisho, Kikwete ameseti precedent kwamba Penal Code ni ya walalahoi. Wanachama wa mfumo wa Ufisadipolitism wanalindwa na kusafishwa na chombo chao kiitwacho PCCB ambacho badala ya kuwajibika kwa bunge, kimeelekezwa kwa mtu mmoja aiwatye rais.

  NASEMA Constitulism in Tanzania is a "sham philosophy" ambayo inaestablish Emperial Presidentialism.

  God Bless Tanganyika & Zanzibar
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Nguzo zote za CCM zimevunjika, mahali pake wamesimika Fedha.
  Tangu lini Fedha inaleta umoja wa kitaifa wa chama na serikali yake??
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hawa Dagaa walicho haribu kutishia kuwa watataja vigogo wote waliohusika ilitakiwa wachune kwanza kisha wawataje mahakamani wanako taka kwenda hapo tayari mafisadi wamesha wapiga mkwala na hawawezi kuwataja tena labda muwashauri wawataje hapa JF....
  65465654 BOT.jpg
  Hawa wamekosea sana kutangaza hadhalani namna hii mafisadi watawamaliza na wataishiwa nguvu kabisa.
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,610
  Trophy Points: 280
  Naogopa sana wasije wakawatishia maisha yao maana najuaa watakuwa wameharibu deal zima.....najuaa watawatishia maisha yao.....
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kama hata presidoo analeta usanii kwenye ishu hii, kilichobaki si sinema tuu!!!!!!!!!!!
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,106
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesoma makala ya Samson Mwigamba kwenye Tanzania Daima ya Sept 3? exactly kama unavyosema, Serikali ya awamu ya nne ni kama filamu vile. Ni bora ingekuwa maigizo kwani maigizo hulenga vituko halisi vinavyotokea maishani sasa hii ya CCM ni sinema mpya.
   
 18. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama sala na nyimbo zingekuwa zinafanya kazi basi mapapa, wafalme na marais wasingekufa.

  As Marx nailed it, religiosity is the opium of the lumpen proletariat.

  As for the EPA pigs, suspend the rule of law for a milisecond and use that to sign summary executions in the name of national security.Like an ancient kingom afflicted with famine, our country could use the right kind of sacrifical blood.Acase can be built that what they accomplished to kill with their gluttony can never be repaid with their lives.
   
 19. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Wala haihitaji kutaja kwani wako wazi katika docs zote na office records na transactions sasa sidhani kama base ni kutajwa. Base ni kushughulikiwa. Lakini na nani ikiwa hawa jamaa ni fraudulent vile vile. Kesi ya kondoo ukipelekea fisi of-course ni kilio tu. Mifano ni mingi; jamaa kauwa kwa bastola ikaonekana ni bahati mbaya sijui nk. Jameni wananchi siku si nyingi watataka nchi yao kwani kama wameweza kuishi miaka yote bila kuona intervention ya serikali kiuchumi na kila mtu amekula na kulala kwa jasho lake ana kulipa kodi obviously wataweza kuishi bila interventions za kifisadi kwa raha zaidi. Au mwasemaje wana JF
   
 20. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hakuna jipya kabisa hapa. Hawa wafanyakazi wa BOT walijua wizi wote huu. Hizo barua walikuwa wanaandika tu kama kutimiza wajibu.

  Wameona sasa Ballali kapotea, basi kila kitu kitapelekwa kwake. Wnajuaje mazungumzo ya Ballali na Mkapa yalikuwa juu ya hilo suala?

  Hao wafanyakazi wa BOT ndio mahali pa kuanzia ili kupata ukweli wote. Haitoshi kufukuzwa kazi, inabidi wakaseme yote mahakamani na huko ndio wataje vigogo wote ambao wamehusika.

  Ukiangalia sehemu kubwa ya hizi pesa zimeenda kwa wajanja mjini, hii ni ishara tosha kwamba huenda baadhi ya wafanyakazi wa BOT baada ya kuona wanasiasa wanachota na wenyewe wakaanza kuchota zao kidogo kidogo kwa kutumia wafanyabiashara wa kati.

  Pesa kama za Kagoda inaonyesha ni wanasiasa, lakini kuna pesa zingine inaonekana ni deal ya wafanyakazi wa BOT.

  Nashangaa hata hao watu wa dini na jumuia zingine wanaoendelea kumkumbatia Mkapa. Jamaa inatakiwa apuzwe na Watanzania wote. Aoombee afe haraka, ikija serikali nyingine anaweza kuja kupandishwa kizimbani.
   
Loading...