Manzese kimenuka asubuhi ya leo.

Manzese kimenuka asubuhi ya leo.

Kiroroma

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2009
Posts
370
Reaction score
117
Kumekucha na sura tofauti katika mji wetu mdogo Manispaa ya Manzese!!Kuna askari kila kona pale Manzese kati wanapofurika wafanya biashara wa kila aina,Ni siku chache tu Mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya Morogoro STRABAG aliamua kusimama kujenga eneo hili maarufu la Manzese kwa sababu za kiusalama. Kwani wafanyabiashara walivamia eneo lote la ujenzi na kukata vizuizi vilivyowekwa.Ili hali wakijua hakuna wa kuwachukulia hatua. Mahindi yanachomwa katikati ya barabara nk Nadhani Dola ikaona haina haja ya kusukumana nao kwa kutumia nguvu.Leo kunako majira ya saa 11 alfajiri askari wamemwagwa eneo hilo na magari ya deraya yakiranda randa kwenye viunga vya mitaa hiyo. La kufurahisha kila mfanyabiashara akifika anajibebea frame yake na kuanza zake kusikojulikana. Kumbe basi Jiji letu linaweza kuwekwa katika mazingiora yanayostahili kwa kufuata mfumo huu.:kev:
 
salaleeeee,jiografia ya darasa la 4
 
Sisi wakaazi wa kwa Mfuga Mbwa na Uwanja wa Fisi tunatambua himaya yetu kama Manispaa!!Kama ni hizo elimu zenu za Kata basi karibuni kwenye Manispaa yetu yenye bei tofauti na ujuavyo,Supu hata ya shilingi Mia unakunywa na kushiba.Dukani sukari robo kilo na vijiko ni kawaida yetu.Dada poa wote huripoti hapa ndipo waende huko viungani kwenu.Nani kakwmbia hapa siyo Manispaa,dini vyama vya siasa au mwenye nchi mwenyewe!Panaogopwa na kila Mtanzania kutoka kona zote za nchi.Panajulikanika kuliko huko kwenu Oysterbay.Karibu Manzese Municipality!
 
yeah, manispaa ya manzese mpeshe maendeleo yaje, serikali ya ccm inawafanyia mambo eti!!!
 
nakumbuka manzese darajani niliwai kupigwa kabari la nguvu muda wa saa kumi na mbili nikaporwa laptop nikiwa nakatiza kwenda sinza though naona sasa hivi kama vibaka wamepungua.
 
Chonde chonde wawe wapore wana Manzese, la sivyo watavunjwa mbavu maana kichaa kapewa rungu na Waziri Mkuu amempa madaraka ya kupiga!
 
FFU wanahamu na maagizo ya Waziri mkuu aka mtoto wa Mkulima..
 
Tumeshasema tutawa PIGA tu, maana ameshaturuhusu mkubwa kuPIGA..
 
Hili ni tatizo kubwa kuliko tunavylidhania! hasa tatizo letu ni kukosa utaratibu katika majiji na miji yetu. watu wanahamia kila siku kutoka vijijini wengine wamezaliwa humu humu mijini na wamekua hakuna utaratibu mtu anaamua kuanzisha shughuli za kumuendeshea maisha popote iwe barabarani serikali haijali, alafu wanakurupuka siku moja eti wanataka kuweka utaratibu hii inasababisha machafuko, inazalisha vibaka na mengine maana kumzibia riziki mtu atafanya lolote ili aishi. mipango miji fanyeni kazi kubainisha maeneo ya biashara, maeneo ya makazi na shughuli nyingine na manispaa wayasimamie haya
 
Ubungo wamesharudi hao wamachinga! wenzetu uongozi hawauwezi!
 
Hili ni tatizo kubwa kuliko tunavylidhania! hasa tatizo letu ni kukosa utaratibu katika majiji na miji yetu. watu wanahamia kila siku kutoka vijijini wengine wamezaliwa humu humu mijini na wamekua hakuna utaratibu mtu anaamua kuanzisha shughuli za kumuendeshea maisha popote iwe barabarani serikali haijali, alafu wanakurupuka siku moja eti wanataka kuweka utaratibu hii inasababisha machafuko, inazalisha vibaka na mengine maana kumzibia riziki mtu atafanya lolote ili aishi. mipango miji fanyeni kazi kubainisha maeneo ya biashara, maeneo ya makazi na shughuli nyingine na manispaa wayasimamie haya

Wameambiwa waende bunju
 
Wabongo hamwendi bila KIPIGO, Pinda kula tano wacharaze mpaka wapate akili.
 
Back
Top Bottom