Manyanyaso ya askari wa barabarani, wananchi tususie kuendesha magari..

Polisi wanatumika vibaya na serikali ,ni njaa zinasumbua wanabambikia makosa ,mimi jana Goba kanisimamisha eti tairi chafu sijaosha kaniandikia faini 30000, anaitwa INNOCENCIA huyo dada ... kwenye mkeka eti tairi mbovu wakati zipo vizuri
Ati???
 
faini ni ndogo sana bora wafanye laki moja kila kosa' hakuna kosa dogo fuata utaratibu ulio wekwa kisheria acheni kulalamika
 
Nilishangaa hadi Siku ya x mass pale jirani na kituo chao salender bridge walikua wanakamata tena niliwaona kwenye SAA 12.15 hivi jioni kagiza kanaanza nikashangaa sana!
 
Dawa yao ni kuwa na kila kitu maana wanaweza ulizia hata screw driver
Kusubiri kote kule juani lazima ukisimama inatafutwa sababu yeyote,kumbuka hali imekua ngumu sana ya maisha kwa kila mtz kila MTU anatafuta ada na kodi siku hizi
 
Mkuu nafikiri jamaa hana gari.
Kweli kabisa mkuu jamaa ana Gari huyo. Inafikia kipindi mtu anakuja na Gari mpaka Kimara mwisho anaacha pale kwenye parking kimara mwisho kuogopa askari auto inabidi aamke asubuhi na mapema awawai askari kabla ya wao kufika barabarani
 
Wanajamvi salamu kwa wote.

Natumaini kama ni mmiliki wa chombo cha moto hususani hapa Dar e's salaam utakuwa umeisha kutana na kadhia hii.

Siku hizi askari wa barabarani wamekuwa kero kwa kuwalipisha faini kwa makosa hata madogo ambayo kama wangezingatia weledi hakuna haja ya kumlipisha dereva faini.

Hivi kwa umoja wetu hatuwezi siku moja madereva wote kususia kuendesha magari na tutembee kwa miguu ili kufikisha ujumbe kwa mamlaka husika?

Tukiendelea kukaa kimya hakika tutakufa.

Naomba kuwakilisha.
Hìi ni hatari sana kuna gari yangu moja baada ya traffic police kukosa kosa la kiusalama barabarani alipiga faini eti kiti cha dereva nyuzi zimeachia kidogo!sasa wanajamvi munisaidie kosa kama hilo linauhusiano gani na usalama barabarani???
 
Back
Top Bottom