miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,821
- 48,973
Mkuu kuwa komoa ni kufuata sheria wanachukia kichizi
Na bado yatashuka sababu tunafuata sheriaTatizo wamekuwa sehemu ya kukusanya mapato wacha watukamue si umeona mapato yameshuka mwezi uliopita
huna gari wewewatanzania bila kupigwa fini....huwa tunakuwa wagumu kuelewa...lkn tukipigwa mikeka minne kwa mwezi ya faini...automatically tutafata sheria
Sheria ni sheria siku hizi hata ukipita service road opposite site unachukua cheti nafikiri kosa kama hili ni kukuelimisha dereva asitumie service road ya opposite side. Na kama ni mstaarabu basi polisi anaweza mrudisha dereva aliko toka kama adhabu!!Hakuna kosa dogo barabarani. Mutuka inaweza badilisha jina la mtu ndani ya sekunde.
Fuata sheria tu ndg yangu
Nikweli sina gari lakini siwezi tetea uvunjwaji sheria wa makusudi wa wenye magari kisa tu eti hili ni kosa dogo upewe onyo.Wewe huna gari.
hao ni sehemu ya TRA........... izoee hali hiyo,Wanajamvi salamu kwa wote.
Natumaini kama ni mmiliki wa chombo cha moto hususani hapa Dar e's salaam utakuwa umeisha kutana na kadhia hii.
Siku hizi askari wa barabarani wamekuwa kero kwa kuwalipisha faini kwa makosa hata madogo ambayo kama wangezingatia weledi hakuna haja ya kumlipisha dereva faini.
Hivi kwa umoja wetu hatuwezi siku moja madereva wote kususia kuendesha magari na tutembee kwa miguu ili kufikisha ujumbe kwa mamlaka husika?
Tukiendelea kukaa kimya hakika tutakufa.
Naomba kuwakilisha.