KERO Manyanyaso tunayopitia Wauguzi Watarajali Manyara

KERO Manyanyaso tunayopitia Wauguzi Watarajali Manyara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa wauguzi watarajali (Intern Nurses) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, kuna changamoto kubwa tunazopitia kutoka kwa msimamizi wa mafunzo wa hospitali yetu. Tumejaribu kuwasilisha malalamiko yetu bila kupata msaada wowote katika Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC).

Tumekuwa tukinyanyaswa kwa maneno na vitendo, kupewa adhabu zisizo za kitaaluma (mtu anapata ugonjwa anapewa adhabu ya zaidi ya wiki baada ya kukosekana kwa siku moja), pamoja na kutumika kama nguvu kazi badala ya kupata mafunzo stahiki (tunaenda kujifunza lakini wao wanataka tukamilishe kazi zao).

Pia kuna mabadiliko yasiyo rasmi ya rotations na wakati mwingine tunatamkiwa maneno ya kudhalilisha kama “punda wa hospitali.”


Tunaomba suala hili liangaziwe ili wahusika Wizara ya Afya wapate kusikia na kusaidia kuboresha mazingira ya mafunzo na kulinda haki za watarajali.
 
Pole sana Muuguzi. Nenda kwa mkuu wa mkoa hapo jirani tu. Huku wanaweza wasione kilio chako.
 
Back
Top Bottom