Manufaa ya mkojo na kinyesi cha sungura

Dany Mrushi

Member
Feb 10, 2016
7
20
Jamani ndugu habarini,aam nilikuwa napenda kufahamishwa kwa kisayansi manufaa ya mkojo na kinyesi cha wanyama wa kufuga aina ya sungura.

======

Sungura ana sifa kadhaa zinazompambanua kama mnyama ikiwamo sifa ya ujanja. Hii ndiyo sifa ijulikanayo na watu wengi ndio maana wamekuwa wakimuita kwa jina la ‘sungura mjanja’

Hata hivyo, mnyama huyu ana sifa nyingine. Umejaribu kuonja nyama yake ikiwa imeandaliwa na mpishi mahiri? Jihimu kuitafuta nyama yake ugundue utamu wa nyama ya sungura?

Mkojo wa sungura

Sambamba na utamu wa nyama yake, sungura pia ana thamani ya ziada kwa binadamu hasa wakulima. Taarifa ni kwamba mkojo wake una uwezo wa kufanya maajabu shambani.

Waliowahi kuutumia akiwamo Suzan Mushi, wanasema mkojo wa sungura unaweza kutumika kama mbolea ya maji na kiuatilifu kwa ajili ya kudhibiti wadudu.

Suzan anayeendesha shughuli za kilimo cha mapapai katika kijiji cha Sanya Juu mkoani Kilimanjaro anasema pamoja na kufuga sungura awali hakujua kama wana faida katika shughuli za kilimo.

‘’Nilikuwa nafuga sungura wawili lakini sikujua kama mkojo wake unaweza kuwa mbolea shambani kwangu hivyo baada ya kubaini hilo nikaanza kuwekeza katika ufugaji huo,” anasema na kuongeza kuwa alibaini hilo baada ya kutembelewa shambani na mtaalamu wa kilimo mwaka 2013.

“Alipokuja nikawa namtembeza shambani kuangalia mazao lakini pia katika mabanda ya mifugo yangu alivyowaona sungura wangu wawli akasema kwanini nisiwekeze katika wanyama hao, akaniuliza kwani hujui kama mkojo wao ni mbolea?,”anaelezea.

Anasema mtaalamu huyo alimueleza kuwa mkojo wa sungura unauwezo wa kustawisha mazao yake bila kujali ni yaaina gani, lakini pia kufukuza wadudu waharibifu.

Anasema baada ya kupata ushauri huo aliufuata na baada ya hapo alianza kuongeza idadi ya mifugo hiyo kutoka watatu hadi sita na baadaye 15.

“Sasa hivi ninao sungura 15, na natarajia kuongeza wengine kwani mbali na matumizi yangu binafsi ya shambani lakini pia nataka kuwa mfanyabiashara wa mkojo wa sungura kwani lita moja hivi sasa huuzwa kwa Sh 10,000,”anasema.

Jinsi ya kuvuna mkojo huo.

Anasema baada ya kuongeza idadi ya sungura aliboresha na mazingira kwa kutengeneza banda ambalo ni rahisi kuvuna mkojo kama iliyo katika uvunaji wa maji ya mvua

“Uvunaji wake hauna tabu ni kama vile mtu anayevuna maji ya mvua lakini tofauti na maji ya mvua mkojo wa sungura zile kata zinazungushwa chini kisha naweka ndoo,”anasema.

Kutokana na idadi ya sungura anasema kwa siku anakinga si chini ya lita tano hadi sita.

Mkojo kama mbolea

Suzan anasema mkojo wa sungura ni mkali sana hivyo hautakiwi kuweka mwingi kwenye mmea kwani mmea unaweza kuungua.

“Mkulima anatakiwa kuchanganya lita moja ya mkojo wa sungura kwenye maji ya ujazo wa lita tano na wakati wa kumwagilia kama ni mipapai mkulima mwagilie lita moja yenye mchanganyiko huo wa maji na mkojo.

Udhibiti wa wadudu

Anasema kabla ya kupata ushauri wa kutumia mbolea hiyo mazao yake yalishambuliwa na wadudu na hata mavuno alipata kidogo kuliko nguvu alizotumia kuwekeza.

“Nilipoamua kufanya kilimo cha papai kwa ajili ya biashara nilinunua mbegu za kisasa ambazo matunda yake ni makubwa kuliko mbegu niliyokuwa naitumia awali, lakini nilishindwa kufikia malengo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwamo wadudu,” anasema.

Lakini anasema baada ya kupata ushauri kuhusu kutumia mbolea ya mkojo huo na kuzifuata kama alivyoelekezwa na mtaalamu wa kilimo alianza kukiona kilimo hicho kuwa na faida lukuki.

Anasema mkojo wa sungura unastawisha mazao lakini pia hata wadudu wasumbufu wanaoshambulia maua hawawezi kuharibu mimea.

Tahadhari

Pamoja na uzuri wa mkojo wa sungura, kunahitajika maarifa ya kutosha hasa kutoka kwa wataalamu wa kilimo ili yasije kukukuta yaliyompata Ramadhan Shaban,mkulima wa mihogo na migomba mkoani Pwani.

Anasema aliposikia kuhusu mkojo wa sungura unavyoweza kutumika kama mbolea, aliamua kuutumia bila ya kumshauri mtaalamu. Haya ndiyo yaliyomtokea;

”Nilisikia tu kuwa mbali na kutumia kinyesi chake bali hata mkojo wa sungura ni mbolea nzuri kwa kufukuza wadudu waharibifu, nilienda tu kununua nikatumia miche kadhaa ilikauka,”

Anasema baada ya kupewa maelekezo mazao yake hayakukauka tena na badala yake yalistawi na kupata mavuno mengi.

”Manufaa ya huu mkojo siyo kwa ajili ya kustawisha mimea bali hata wale wadudu ambao huharibu maua au kushambulia mimea wanapotea kabisa. Mimi tangu nimeanza kutumia hii mbolea hakuna mdudu yeyote aliyetoboa majani au kushambulia maua,”anasema

Mtaalamu auzungumzia mkojo wa sungura

Mtaalamu wa kilimo, Abdul Mkono anasema mkojo wa sungura unasifika kwa kuwa na uwezo wa kuongeza virutubisho kwa mimea na kuondoa wadudu hatari kama vile wadudu mafuta, inzi weupe na utitiri.

Mbali ya hayo, mkojo wa sungura pia anasema unaweza wa kukabiliana na magonja ya bakteria na fangasi.

Mkono anasema mkojo ukishapatikana mkulima atauchuja ili kuondoa uchafu kisha atauweka katika solo kwa ajili ya kupulizia kwenye mimea.

‘’Mkulima atamwagilia maji asubuhi, kisha kuanzia saa tatu asubuhi atauchukua mkojo huo kwa ajili ya kupulizia kwenye mimea. Atapulizia katika maeneo yaliyoathirika au katika majani ya mmea husika, shina la mmea na pia kwenye udongo,’’ anasema.
 
baba frances

Member
Dec 18, 2016
39
125
Nilisikia sehemu kuwa mkojo unauzika ila usichanganyike na uchafuu wowote sasa matumizi yake hapo mi mgeni, kwani unawafunga?
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,665
2,000
Kinyesi cha sungura hutumika kama mbolea kama ilivyo kwa vinyesi vya wanyama wengine.
Mkojo wa sungura pia hutumika kama mbolea na pia kama kiwatilifu kwa ajili ya kupambana fangasi kwenye mimea na wadudu kama utitiri mabuibui. Kenya wanatumia sana.
 
ni ngumu

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
3,370

very true
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,205
2,000

Biashara/ ufugaji wa sungura sio kitu kibaya, ni kitu chema sana, ila wafugaji wasidanganywe, waelezwe ukweli Kuwa bei ya sokoni ni 20,000/-.
Namaingo wanawadanganya watu kuwa sungura ni TZS.60,000/- kitu ambacho hakiwezekani kwa kipato cha Mtanzania wa Magufuli
 
Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
3,318
2,000
Sungura ana sifa kadhaa zinazompambanua kama mnyama ikiwamo sifa ya ujanja. Hii ndiyo sifa ijulikanayo na watu wengi ndio maana wamekuwa wakimuita kwa jina la ‘sungura mjanja’

Hata hivyo, mnyama huyu ana sifa nyingine. Umejaribu kuonja nyama yake ikiwa imeandaliwa na mpishi mahiri? Jihimu kuitafuta nyama yake ugundue utamu wa nyama ya sungura?

Mkojo wa sungura

Sambamba na utamu wa nyama yake, sungura pia ana thamani ya ziada kwa binadamu hasa wakulima. Taarifa ni kwamba mkojo wake una uwezo wa kufanya maajabu shambani.

Waliowahi kuutumia akiwamo Suzan Mushi, wanasema mkojo wa sungura unaweza kutumika kama mbolea ya maji na kiuatilifu kwa ajili ya kudhibiti wadudu.

Suzan anayeendesha shughuli za kilimo cha mapapai katika kijiji cha Sanya Juu mkoani Kilimanjaro anasema pamoja na kufuga sungura awali hakujua kama wana faida katika shughuli za kilimo.

‘’Nilikuwa nafuga sungura wawili lakini sikujua kama mkojo wake unaweza kuwa mbolea shambani kwangu hivyo baada ya kubaini hilo nikaanza kuwekeza katika ufugaji huo,” anasema na kuongeza kuwa alibaini hilo baada ya kutembelewa shambani na mtaalamu wa kilimo mwaka 2013.

“Alipokuja nikawa namtembeza shambani kuangalia mazao lakini pia katika mabanda ya mifugo yangu alivyowaona sungura wangu wawli akasema kwanini nisiwekeze katika wanyama hao, akaniuliza kwani hujui kama mkojo wao ni mbolea?,”anaelezea.

Anasema mtaalamu huyo alimueleza kuwa mkojo wa sungura unauwezo wa kustawisha mazao yake bila kujali ni yaaina gani, lakini pia kufukuza wadudu waharibifu.

Anasema baada ya kupata ushauri huo aliufuata na baada ya hapo alianza kuongeza idadi ya mifugo hiyo kutoka watatu hadi sita na baadaye 15.

“Sasa hivi ninao sungura 15, na natarajia kuongeza wengine kwani mbali na matumizi yangu binafsi ya shambani lakini pia nataka kuwa mfanyabiashara wa mkojo wa sungura kwani lita moja hivi sasa huuzwa kwa Sh 10,000,”anasema.

Jinsi ya kuvuna mkojo huo.

Anasema baada ya kuongeza idadi ya sungura aliboresha na mazingira kwa kutengeneza banda ambalo ni rahisi kuvuna mkojo kama iliyo katika uvunaji wa maji ya mvua

“Uvunaji wake hauna tabu ni kama vile mtu anayevuna maji ya mvua lakini tofauti na maji ya mvua mkojo wa sungura zile kata zinazungushwa chini kisha naweka ndoo,”anasema.

Kutokana na idadi ya sungura anasema kwa siku anakinga si chini ya lita tano hadi sita.

Mkojo kama mbolea

Suzan anasema mkojo wa sungura ni mkali sana hivyo hautakiwi kuweka mwingi kwenye mmea kwani mmea unaweza kuungua.

“Mkulima anatakiwa kuchanganya lita moja ya mkojo wa sungura kwenye maji ya ujazo wa lita tano na wakati wa kumwagilia kama ni mipapai mkulima mwagilie lita moja yenye mchanganyiko huo wa maji na mkojo.

Udhibiti wa wadudu

Anasema kabla ya kupata ushauri wa kutumia mbolea hiyo mazao yake yalishambuliwa na wadudu na hata mavuno alipata kidogo kuliko nguvu alizotumia kuwekeza.

“Nilipoamua kufanya kilimo cha papai kwa ajili ya biashara nilinunua mbegu za kisasa ambazo matunda yake ni makubwa kuliko mbegu niliyokuwa naitumia awali, lakini nilishindwa kufikia malengo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwamo wadudu,” anasema.

Lakini anasema baada ya kupata ushauri kuhusu kutumia mbolea ya mkojo huo na kuzifuata kama alivyoelekezwa na mtaalamu wa kilimo alianza kukiona kilimo hicho kuwa na faida lukuki.

Anasema mkojo wa sungura unastawisha mazao lakini pia hata wadudu wasumbufu wanaoshambulia maua hawawezi kuharibu mimea.

Tahadhari

Pamoja na uzuri wa mkojo wa sungura, kunahitajika maarifa ya kutosha hasa kutoka kwa wataalamu wa kilimo ili yasije kukukuta yaliyompata Ramadhan Shaban,mkulima wa mihogo na migomba mkoani Pwani.

Anasema aliposikia kuhusu mkojo wa sungura unavyoweza kutumika kama mbolea, aliamua kuutumia bila ya kumshauri mtaalamu. Haya ndiyo yaliyomtokea;

”Nilisikia tu kuwa mbali na kutumia kinyesi chake bali hata mkojo wa sungura ni mbolea nzuri kwa kufukuza wadudu waharibifu, nilienda tu kununua nikatumia miche kadhaa ilikauka,”

Anasema baada ya kupewa maelekezo mazao yake hayakukauka tena na badala yake yalistawi na kupata mavuno mengi.

”Manufaa ya huu mkojo siyo kwa ajili ya kustawisha mimea bali hata wale wadudu ambao huharibu maua au kushambulia mimea wanapotea kabisa. Mimi tangu nimeanza kutumia hii mbolea hakuna mdudu yeyote aliyetoboa majani au kushambulia maua,”anasema

Mtaalamu auzungumzia mkojo wa sungura

Mtaalamu wa kilimo, Abdul Mkono anasema mkojo wa sungura unasifika kwa kuwa na uwezo wa kuongeza virutubisho kwa mimea na kuondoa wadudu hatari kama vile wadudu mafuta, inzi weupe na utitiri.

Mbali ya hayo, mkojo wa sungura pia anasema unaweza wa kukabiliana na magonja ya bakteria na fangasi.

Mkono anasema mkojo ukishapatikana mkulima atauchuja ili kuondoa uchafu kisha atauweka katika solo kwa ajili ya kupulizia kwenye mimea.

‘’Mkulima atamwagilia maji asubuhi, kisha kuanzia saa tatu asubuhi atauchukua mkojo huo kwa ajili ya kupulizia kwenye mimea. Atapulizia katika maeneo yaliyoathirika au katika majani ya mmea husika, shina la mmea na pia kwenye udongo,’’ anasema.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom