Manufaa ya mkojo na kinyesi cha sungura

Mkojo wa sungura unakazi gani please naombeni nami nijue
Mkojo wa sungura huweza kutumika kama mbolea, ingawa mkojo wa sungura ni mkali sana hivyo hautakiwi kuweka mwingi kwenye mmea kwani mmea unaweza kuungua.
Mkulima anatakiwa kuchanganya lita moja ya mkojo wa sungura kwenye maji ya ujazo wa lita tano. Na wakati wa kumwagilia kama ni mipapai, mkulima amwagilie lita moja yenye mchanganyiko huo wa maji na mkojo.
 
Back
Top Bottom