Kama CUF Walishasema Hawatashiriki Uchaguzi Huo Wa Marudio, Coz Hakuna SHERIA Yoyote Inatoa Nafasi Ya ZEC Kufuta Matokeo Ya Uchaguzi Na Kutangaza Kurudia Tena (Achana Na Kutokuwepo Na Sababu Za Msingi, Hata Kama Zingekuwepo) !! Sasa Kama CCM Wamepewa Nafasi Ya Kufanya Uchaguzi Wao (Kumuhidhinisha Dkt Shein) Bila Ya Kubughudhiwa Na Chama Hicho (CUF) Sasa Kwanini Kila Siku Mnawakamata Viongozi Na Wanachama Wao!! Si Mjipange Tu Kugawana MADARAKA Yenu!!!
MAMLAKA YA JECHA KUUFUTA UCHAGUZI.
Siku Jecha anafuta matokeo yale ya Uraisi pomoja na kutaja sababu nyingi za kuufuta Mimi nitaelezea moja tu kikatiba.
Jecha alidai kuwa ndani ya tume kuna watu waliokuwa wakipigana , hiki ni kiashiria tosha kuwa wajumbe wa tume wamejiunga na vyama vya siasa.
Ibara ya 14 katika sura ya pili ya katiba yetu inakataza wajumbe wa tume kujiunga na chama chochote japokuwa wana ruhusa ya kupiga kura. Kwa maana hiyo Jecha Alikuwa sahihi kuufuta uchaguzi ule.
UHALALI WA UCHAGUZI HATA KAMA BAADHI WATAJITOA.
Chama cha wananchi Cuf wanasema hawatashiriki uchaguzi wa marudio japokuwa Tume ya uchaguzi Zanzibar wanadai wapo nje ya sheria kwenye kujitoa.
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar sura ya nne sehemu ya kwanza Ibara ya 2 inafafanua kuwa:-
Litokeapo jambo lolote lililotajwa katika katiba na kulazimu uchaguzi wa raisi kufanyika, kila chama cha siasa kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa raisi kitawasilisha kwa tume yabuchaguzi ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria jina la mwanachama wake mmoja atakayesimama kama mgombea uraisi.
Hapa hawakutaja kuwa ni lazma vyama vyote vishiriki bali katiba inadai kuwa chama kinachotaka kushiriki. Cuf kujitoa huku vyama vingine vikikubali kushiriki bado uchaguzi unabaki kuwa halali kabisa.
Si lazma Cuf washiriki ndio uchaguzi uwe halali.Mpaka hapa bado Cuf katika mazingira yoyote yale wapunguze jazba na waombe busara itumike zaidi kuliko sheria.
Na ni vigumu sana kuendesha nchi kwa kufuata busara badala ya kanuni na sheria tulizojiwekea.
BAADHI YA VYAMA VYA UPINZANI KUNUFAIKA NA CUF. KUTOKUSHIRIKI.
Hadi sasa kuna watu wanaowinda nafasi ya Umakamu wa kwanza wa Raisi wa Zanzibar ambapo katiba ya Zanzibar inajipambanua wazi kuwa chama kitakachofuatia kwa kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu nyuma ya chama kitakachoshinda ndicho kitakachotoa makamu wa kwanza wa raisi.
Wakati Cuf wakinekana kama kitanzi kwao kwa kipengele hiki kuwaweka njia panda ya kushiriki uchaguzi au kuacha kwa upande wa Hamad Rashid yeye kipengele hiki anakitazama kwa umuhimu mkubwa zaidi na anatamani kunyakua nafasi hiyo nyeti kabisa kwenye serikali ya SUKI.
KATIBA YA ZANZIBAR INASEMAJE KUHUSU MAKAMU WA KWANZA WA RASI??.
Ibara ya 39 (3) ya katiba ya Zanzibar inampa mamlaka Rais aliyechaguliwa kuteua nani awe makamu wa kwanza wa rais ambapo mamlaka hayo atayapata endepo tu :-
i) Kama chama kilichofuata kwa wingi wa kura nyuma ya chama kilichoshinda kitakuwa kimepata kura chini ya asilimia 10 ya kura zote zilizopigwa. Katika hali hiyo katiba inampa uhuru raisi mteule kumteua mtu yoyote anayeona anafaa.
ii) Kama Raisi hakuwa na mpinzani basi chama cha upinzani kilichofuatia kwa wingi wa viti kwenye baraza la wawkilishi kitatoa makamu wa kwanza wa raisi.
Kwa Maelezo zaidi soma:-