Mansour aswekwa rumande

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,206
Wakati wananchi wa Tumbatu wakidai kuchoshwa na madhila wanayofanyiwa na vyombo vya ulinzi na kusababisha baadhi yao kuondoka kwenye nyumba zao kama alivyobainisha Bw. Chambu Ahmad Makame huku Mjini nako jioni hii Mshauri wa Maalim Seif, Mansoor Yussuf Himid anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mara nyengine tena, Mansoor aliitwa na polisi leo hii kwa ajili ya mahojiano akiambatana na Wakili Karume Haji Mrisho ambaye amesema Mansoor ameshutumiwa kwa mambo mbali mbali ikiwemo suala la kulipuliwa Kisonge hata hivyo wamekataa kumpa dhamana hivyo ataendelea kuwepo polisi.

Mwenyeenzi Mungu atuvushe na balaa katika nchi yetu Orodha ya viongozi wa CUF wanaoshikiliwa na polisi Zanzibar kwa mujibu wa Naibu katibu mkuu wa CUF Magdalena Sakaya, hadi sasa viongozi waliokamatwa ni pamoja na, Eddy Liamy mwanamikakati ya ushindi CUF; Nassoro Mazrui, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar; Mahomoud Mahinda, Katibu Mtendaji JUVICUF; Abeid Hamis Bakari, Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi na Hamad Masoud, Mkurugenzi wa Habari CUF.

(Salma Said & Mwanahalisi)
======================
Jeshi la Polisi linamshikilia mwanasiasa Mansoor Yussuf Himid kwa mahojiano kuhusiana na kulipuliwa kwa maskani ya CCM, Kisonge Michenzani mjini Unguja.

Mansoor, ambaye ni mshauri wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad alipigiwa simu jana jioni na polisi kwa ajili ya mahojiano katika kituo cha Madema.

Kukamatwa kwa Mansoor kumekuja siku chache baada ya Jeshi hilo kuwakamata wafuasi wengine 42 akiwamo Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Hamad Masoud akituhumiwa kutoa taarifa kwamba kuna watu wamekimbilia porini na wengine wamekwenda Mombasa.

Wafuasi hao 42 ambao bado wanashikiliwa ni kutokana na kuhusishwa na tukio la kulipuliwa nyumba ya Kamishina wa Polisi, Hamdan Omar Makame.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam jana alithibitisha kukamatwa kwa Mansoor na kwamba ni kutokana na hali ya matukio ya milipuko na mambo mengine, hivyo wanahitaji kupata maelezo ya kina kabla ya kumwachia.

Alisema lengo la kumshikilia Mansoor si kumkomoa bali ni kupata ufafanuzi na maelezo kwani hivi sasa kutokana na hali na matamshi ambayo huwa yanatolewa katika mitandao ya kijamii, Jeshi la Polisi linayafuatilia kwa kina kuyachunguza.

“Kwa hivyo tunataka maelezo na tukishapata maelezo yake tutaamua kama ni kumwachia au la, lakini kwa sasa tunamhitaji kwa kuisaidia polisi kwenye upelelezi,” alisema Mkadam.

Tukio hilo limekuja saa chache baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya kulalamikia dalili za wazi za uvunjifu wa haki za binadamu Zanzibar zinazofanywa na vyombo vya dola dhidi ya wafuasi wao kwa kivuli cha utunzaji wa amani.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Sakaya aliisihi Serikali ya Rais John Magufuli kuingilia kati kwani wananchi wanaweza kuchoshwa na vitendo hivyo na kuleta uvunjifu zaidi wa amani.

Sakaya alisema kuwa wanaamini mambo yote hayo yanatokea kutokana na msimamo wao wa kutokubali kushiriki uchaguzi wa marudio unaofanyika Jumapili hii.

Uchaguzi huo wa marudio unafanyika baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana kufutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kutokana na kile alichodai kukithiri kwa ukiukwaji wa taratibu na sheria za uchaguzi.

Sakaya alisema kuwa kuna vitendo vingi wanafanyiwa wafuasi wa CUF visiwani humo vikiwamo vya kupigwa na vikundi vya uhalifu vinavyoitwa ‘mazombi’, kuchomewa nyumba na kutiwa ndani kwa viongozi wa chama hicho kwa visingizio vya kushiriki uhalifu.


Chanzo: Mpekuzi
 
Magufuli alishasema mtu akileta fyoko fyoko iwe pemba,unguja ,mwanza au popote pale ata tandikwa!

Hivyo ukileta choko choko usitegemee kuachwa hivi hivi hata Maalim seif akileta fyoko fyoko akiwa bara lazima adhibitiwe...

Tuache jeshi letu liwadhibiti waleta fyoko fyoko...
 
Ukiona giza limekua kubwa basi ujue kunakaribia kupambazuka.

Eh Mungu waondoe hawa madhalimu huko visiwani.
Siku zote Utawala wa Mabavu haufanikiwi milele , hata Sadam Hussein alishindwa sembuse hao wa Tamganyika .
 
Hata somali walikua na serikali imara tu chini ya Siad Bare..lakini yalianza hivi hivi .nguvu ndidi ya raia wasio na hatia kwa kisingizio cha fyoko fyoko..leo somali miaka 30 wanatafuta amani imekua mtihani...sasa fyoko fyoko ya maalim ni kusema hashiriki uchaguzi kwa sababu hakuna sababu na uchaguzi wenyewe ulokusudiwa ndio huu tunao uona ..moja kwa moja walikua na sababu ya kususia..
Na wazi wamewambia wafuasi wao wake kimya watulivu wasifanya fujo wala kuandamana . Maalim ametumia uongozi kuwambia wafuasi wake tulieni na wakatulia...
Na pia amewataka siku ya kura wakae majumbani ili isipatikane sababu ya kusingiziwa...na huo ndio msimamo wao cuf..
Sasa vipigo na falso flag hizi za nini ?

Lengo nini ? Kupendwa zaidi nz wazanzibari ? Ukiangalia kwa undani haya ya sasa hayawasaidii ccm znz kupata wapenxi zaidi wanaonekana ni wayu hatari kwa uroho wa madaraka wanaweza kufanya lolote baya hata wakizurika wote basi haizuru...
Hii nchi yetu sote historia itufunze huwezi kila siku binadamu umgeuze ngoma ya kupigia na akabaki tu hivo hivo
Kinachofanyika Zanzibar Kwa Sasa ni CCMkuchoma moto Ofisi zake kurusha mabomu na vurugu zote kisha kuwasingizia CUF ili wapate sababu ya kuwakamata na kuwapiga . Huo ni Ukolon 100% Pemba wadai Uhuru toka Tanganyika mapema kabla hawajakaliwa kimabavu Kama ilivyokuwa Afrika kusini Enzi ya Ubaguzi wa rangi
 
Magufuli alishasema mtu akileta fyoko fyoko iwe pemba,unguja ,mwanza au popote pale ata tandikwa!

Hivyo ukileta choko choko usitegemee kuachwa hivi hivi hata Maalim seif akileta fyoko fyoko akiwa bara lazima adhibitiwe...

Tuache jeshi letu liwadhibiti waleta fyoko fyoko...
Hivi si mmeshaambiwa kuwa CUF hawashiriki uchaguzi na nendeni mkapige kura peke yenu? tunatakiwa tuipende Tanzania kwanza ndo vyama vyetu. sasa mmeachiwa goli wazi mfunge magoli mtakavyo kinachowafanya mpeleke majeshi huko pemba kwenda kuua/kuumiza raia wasio na hatia ni nini?
 
mimi ninachompendea Magufuli akisema anatenda maana alishasema yeyote akileta fyoko moto utamshukia kwahiyo wahuni wote wanaoleta fyoko lazima wachapwe tu.
 
Kuna wababe hapa Afrika walikuwa na tabia na mwenendo kama huu wa kuwasweka wapinzani rumande lakini walikuja kushindwa vibaya kwenye masuala ya kutawala nchi zao. Wababe hao ni Mobuto Seseseko wa Congo DR (zamani Zaire), Muamar Gadafi wa Libya na Hosni Mubarak wa Misri ambaye aliwaua waandamanaji zaidi ya 1000 pale kwenye viwanja vya Tahriri. CCM watambue kwamba hakuna utawala uliotumia mabavu ukasalimika. Watafurushwa kirahisi sana kule visiwani.
 
Back
Top Bottom