Manny Pacquiao V/S Floyd Maywether Jr | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Manny Pacquiao V/S Floyd Maywether Jr

Discussion in 'Sports' started by SHERRIF ARPAIO, Aug 29, 2011.

 1. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,819
  Trophy Points: 280
  Kwa muda mrefu ndondi esp. za heavy weight division zimekosa ule utamu wa boxers wa miaka ya akina enzi za watu kama akina Mike Tyson, Evander holyfield, Lennox Lewis, John Ruiz, Larry Holmes, Riddick Bowie etc.
  Kwa muda mrefu watu tumekuwa tukitegemea hili pambano kati ya hawa dogo wawili, yule mfilipino Pacquiao na huyu mmarekani Floyd Maywether Jr.ambao wamekuwa wakitambiana kila kukicha kutokana na boxing records zinazovutia sana.
  Maywether Jr. hajapigwa hata pambano moja. Pacman ameweka record ya kuwa bingwa wa pound for pound kwa uzito wa aina mbalimbali na speed ya punches zake sio ya kawaida inatisha.
  I can't wait kwa hawa jamaa wakizipiga kwani imesemwa kuwa itakuwa is one of the mega fights of the century. Kuna wanaosema Mayweather anamwogopa mfilipino. I hope watamaliza ubishi sooner than later
   
 2. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mayweather anamwogopa Pacman huo ndio ukweli. Mara kadhaa ameombwa wazipigi na kila saa anakuja na visingizio, mara ooh apimwe damu.
   
 3. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  ``Record ya kuwa bingwa wa pound for pound`` !

  Alimpiga nani, lini, kushinda ``rekodi ya kuwa bingwa wa pound for pound``
  ?
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Litakuwa lini pambano la masumbwi aka ndonga aka ndondi aka ....,?
   
 5. P

  Pazi JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 2,918
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
  Floyd money Mayweather namkubali ila tatizo lina kuja pia na mie kidogo natia wasiwasi sababu za Floyd zinakuwa kama anamuogopa Pacman..

  Sema hapo hapo naweza kumtetea Floyd kwanini Pacman hataki kupima damu???????? Pacman kitu gani kinamfanya agome? ingekuwa watu weusi wanagoma wangeshaambiwa wanatumia madawa ya nguvu... Pacman naye anamuogopa Floyd hawa watu wanaogopana..


  Kuna Dogo anaitwa Amir Khan ni mkali ila naye bado sijamuona kuzichapa na watu kama Floyd ndio tutajuwa ukali wake. Pacman na Floyd waache kutafutiana sababu wazipige..

  UFC ndio nachotizama sikuhizi mie kuna Mbrazil Silva jamaa anachapa kama Bruce Lee.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Aug 29, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Anderson Silva si binadamu yule.

  Mwanzoni Fedor Emelianemko alionekana kama si binadamu lakini hivi karibuni kashindwa mipambano mitatu mfululizo.

  Ila Silva bado hajashindwa kabisa. Kuna moja alishindwa kwa disqualification dhidi ya Yushin Okami lakini kalipiza Jumamosi kwa kumpa kisago cha ukweli.

  Kwenye daraja lake la kati (185 lbs) Silva hana mpinzani. Labda aende kwenye lightheavyweight lakini huko anaweza akakwaa kisiki kwa Jon Jones manake huyu naye ni moto wa kuotea mbali.
   
 7. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa naona tunafananisha dagaa na Sangara..., huyu dogo baada ya kushinda Gold Medal Olympic wamekuwa wakimpambanisha na vilaza ili kwanza atengeneze Jina..., kumuweka kwenye kundi la kina Floyd nadhani ni mapema sana.... tumpe muda...
   
 8. P

  Pazi JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 2,918
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
  Kweli Mkuu ... Amir Khan si mbaya ila mie nataka akutane na watu wanaotandika vibaya sana kama wa Mexico tuone atahimili vishindo sababu shingo yake kidogo Khan inaonekana akipigwa ile ya kuyumba sizani kama anauwezo wa kuendelea pambano, kuna watu wanapigwa wana yumba ila wanarudi strong.. Khan ashukuru pia ana trainer mzuri.
   
 9. P

  Pazi JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 2,918
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
   
 10. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #10
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Binafsi namkubali sana Mayweather japo pacman nae rekodi yake sio ya kudharau hata kidogo.
  Khan ana safari ndefu sana kufikia levels za hawa jamaa.
   
 11. senator

  senator JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mpaka sasa mpambano wao haujawa confirmed na nakumbuka pacman alisema angetaraji kustaafu october 2011 si unajua kwa sasa pia ni mbunge nchini kwake!.
  Kwa kifupi Folyd anamuogopa Manny mana kile kichapo alichopewa Cotto kilikuwa fundisho kwake..Pacman yupo juu
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Angalia pacman/marquez....halafu angalia mayweater/marquez.
   
 13. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama watapigana.
   
Loading...