Manji, Sanga wachukua fomu kuwania uongozi Yanga

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,985
Yusuph Manji ambae ni mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Leo amejitokeza kuwania nafasi hiyo baada ya muda wa kuongoza kuelekea tamati. Manji amechukua fomu pamoja na makamu mwenyekiti wa sasa, Clement Sanga.

Pamoja na TFF kutangaza uchaguzi "wake" wa Yanga, Uchaguzi wa Yanga chini ya klabu ya Yanga umepangwa kufanyika Juni 11 na ratiba kamili imetolewa.

Tarehe 1/6/2016. Kutangaza mchakato wa uchaguzi wa Yanga, nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo.Mhusika/ Katibu Mkuu.

Tarehe 2-3/6/2016. Kuanza kuchukua fomu za ugommbea. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi. Mhusika/ wagombea wote

Tarehe 4/6/2016. Kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali na kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea.

Mhusika/ Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na Sekretarieti.
Tarehe 5/6/2016. Kipindi cha kupokea na kuweka mapingamizi kwa mgombea. Mhusika/ Kamati ya uchaguzi ya Yanga na Sekretarieti.

Tarehe 6-7/6/2016 Kupitia pingamizi zote na kufanya usaili wa awali, kupeleka majina TFF ilikuhakikiwa, kusikilizwa na kutolea maamuzi ya masuala ya maadili na kukata rufaa kwa maamuzi yaliotolewa, Kusikilizwa rufaa na kutoa maamuzi ya rufaa na kisha kutangaza majina ya wagombea. Mhusika /TFF.

Tarehe a7-10/6/2016 Kipindi cha Kampeni kwa wagombea. Mhusika/ Wagombea.

Tarehe 11/6/2016 Uchaguzi wa Yanga. Mhusika/ Wanachama

Tarehe 12/6/2016 Kutangaza matokeo. Mhusika/ Wote.
 
Attachments

  • MANJI+NA+SANGA.JPG
    MANJI+NA+SANGA.JPG
    29.5 KB · Views: 87
Nasikia wameishachukua tayari

Ni ukweli ulio wazi kuwa Manji bado anahitajika Yanga sana tu
 
View attachment 352898
Baada ya ukimya, sasa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji na makamu wake, Clement Sanga wanachukua fomu za kugombea nafasi hizo, leo.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinasema, Manji na Sanga watachukua fomu za kugombea tena nafasi hizo, kesho saa sita mchana.

“Ni kweli tuna taarifa hizo, maana siku ni moja tu na Manji na Sanga watajitokeza (kesho)leo ,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Pamoja na TFF kutangaza uchaguzi "wake" wa Yanga, Uchaguzi wa Yanga chini ya klabu ya Yanga umepangwa kufanyika Juni 11 na ratiba kamili iko hivi.
Tarehe 1/6/2016. Kutangaza mchakato wa uchaguzi wa Yanga, nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo.Mhusika/ Katibu Mkuu.

Tarehe 2-3/6/2016. Kuanza kuchukua fomu za ugommbea. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi. Mhusika/ wagombea wote

Tarehe 4/6/2016. Kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali na kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea.

Mhusika/ Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na Sekretarieti.
Tarehe 5/6/2016. Kipindi cha kupokea na kuweka mapingamizi kwa mgombea. Mhusika/ Kamati ya uchaguzi ya Yanga na Sekretarieti.

Tarehe 6-7/6/2016 Kupitia pingamizi zote na kufanya usaili wa awali, kupeleka majina TFF ilikuhakikiwa, kusikilizwa na kutolea maamuzi ya masuala ya maadili na kukata rufaa kwa maamuzi yaliotolewa, Kusikilizwa rufaa na kutoa maamuzi ya rufaa na kisha kutangaza majina ya wagombea. Mhusika /TFF.

Tarehe a7-10/6/2016 Kipindi cha Kampeni kwa wagombea. Mhusika/ Wagombea.

Tarehe 11/6/2016 Uchaguzi wa Yanga. Mhusika/ Wanachama

Tarehe 12/6/2016 Kutangaza matokeo. Mhusika/ Wote.

Hivi TFF Inaingiliaje mambo ya uchaguzi wa Yanga?,
Yanga imesajiliwa kama Sports club, (YOUNG AFRICAN SPORTS CLUB) na wala sio YOUNG AFRICAN FOOTBALL CLUB, Uchaguzi wa Yanga unapaswa kuwa chini ya BMT

TFF inapaswa kusimamia uchaguzi wa timu kama Azam nk, zilizosajiliwa kama Ffotball Club
 
Uchaguzi wa Yanga unapaswa kuwa chini ya BMT

TFF inapaswa kusimamia uchaguzi wa timu kama Azam nk, zilizosajiliwa kama Ffotball Club
Bahati mbaya BMT sio mwanachama wa FIFA so haina template ya mifumo ya katiba ya FIFA. Lakini pia Yanga inaweza ikajitoa uanachama wa TFF kama inaona shughuli zake hazipaswi kuwa chini ya TFF, ijiunge na CHANETA na CHABATA au boxing zilizo chini ya BMT
 
Nadhani haujapata logic, Yanga haichagui viongozi wa Soka bali wa Club ya Michezo, so hiyo footbal ni sehemu tu ya Yanga, wanachofanya TFF ndani ya Yanga, hata Channeta, Boxing, wanaweza nao kuja kusimamia uchaguzi wa Yanga

BMT PEKEE NDIO WANAWEZA KUSIMAIA UCHAGUZI WA YANGA
 
TFF hawakutaka uongozi wa manji, sasa imekula kwao wana yanga wanaangali fedha timu inafanya vizuri kwa kuwa haina njaa, wanafiki wataumbuka tu.
 
Nasikia wameishachukua tayari

Ni ukweli ulio wazi kuwa Manji bado anahitajika Yanga sana tu

MANJI ni kweli anahitajika mno YANGA...Mimi binafsi naomba YANGA isipatwe na tatizo na kumlazimisha MANJI kuondoka...Hata hivyo hofu ipo kauli za MANJI ni hatari kwa mustakabali wa uhai wa YANGA...hii figisufigisu na TFF na BMT ni hatari...hili la kusema kuna mpepelezi wa kimataifa alikodishwa kuwarekodi watu ni hatari...hili la kusema namsimamisha huyu uanachama ni hatari...Inaelekea MANJI hana watu makini wa kumwambia ni mambo gani ya kusema na kwa wakati gani...Baadhi tunaifahamu YANGA vizuri, na tunaifahamu SOKA ya Tanzania..Tunaifahamu Tanzania hii...Hii ni hofu ya kweli, and for one thing, MANJI hawezi kuongoza YANGA milele...nawaomba YANGA wajipange...hivi itakuwaje MANJI akiondoka leo, hivi kutakuwa na YANGA pale?...Tusubiri tuone, ila baadhi yetu tunaoipenda YANGA lakini hatutaki kuingilia mambo ya uongozi tuna hofu...
 
Naona mezani wapo na maji Kilimanjaro huku baadae wakimpiga vita yule mangi kwenye magazeti yake dah. Au ndo wameyanunua ili wayamwage.....
 
Naona mezani wapo na maji Kilimanjaro huku baadae wakimpiga vita yule mangi kwenye magazeti yake dah. Au ndo wameyanunua ili wayamwage.....
Hawakuongelea bidhaa za IPP kwa ujumla wake, so you better wake up wa mchangani!
 
TFF wanataka kuingiza watani zetu kwenye migogoro tunachopata sisi huku sitaki kabisa watani zetu wafike huku kuna asilimia 200 huyu malinzi hawatakii mema watani zetu aiseee
 
Back
Top Bottom