Hivi kuna vitendo vingapi vya uhujumu uchumi ambavyo amevifanya na amejaribu kufanya?! Yeye haithamini nchi yake.
Sio unaropoka tu umeona tangazo au? Nenda kaangalie tangazo halafu urudi hapa home manji kapewa tuzo kama nani,@Elli ndiyo Tanzania ni nchi yake kwani ana uraia wa nchi nyingine? Kuna tatizo la watu kuwaza kwamba wahindi siyo watanzania. Ni bahati mbaya sana!!
Ni kweli anaweza kuhama nchi ila tujue tu atahama na ajira za watu kibao ambao mpaka sasa serikali bado haijajipanga kuwapa ajira wala kuwawezesha kujiajiri.Ahame inchi,namjua kama mpigaji na mdhulumati ukifuatilia apeech ya mengi JPM hawezi muonea ivi ivi tuu kuna rafu apo.
Maana utajiri wote alionao ukiuliza kodi alipayo sasa ndo unaweza zimia
manji ni mwekezaji bepari, tena mlanguzi. mtindo wake wa kuwaza ni wa kibepari. sio kama bepari hana faida na maendeleo ya nchi ila mukimuendekeza atawanyonya hadi kubakia mifupa. bepari lazima kumdhibiti ili mwananchi aweze kufaidika na uwekezaji wake.Kuna tangazo linarushwa Clouds, Manji Diwani wa Magala kuu ameonekana akilalamika sana juu moja ya kampuni yake kuhusu uendelezaji wa ufukwe Coco Beach. Ameeleza mengi mpaka swala la Magomeni.
Ameeleza mafanikio yake kupitia kampuni yake ya Quality Plaza na dunia inavyomthamini. ila amesema nchi yake haimthamini.. Sijajua nini maana ya Manji kusema nchi haimthamini, anakusudia nini? Maana nchi ni watu na viumbe..
Anasemaje sisi watanzania hatumthamini wakati tumempa udiwani Mbagala na tumempa uenyekiti Yanga? Naomba Manji atupe ufafanuzi ni nchi haimthamini au viongozi ndio hawamthamini?
Atueleze vizuri..
magufuli anamchukia sana Manji, sijui alimfanyia nini...manji amesaidia watu wengi sana mpaka club yetu ya Yanga