Manji Mwenyekiti Mpya Yanga!

Mkuu Azam FC na Yanga na Simba ni vitu viwili tofauti. Azam ni ya mtu na hizi Simba na Yanga ni za wanachama.
Hakuna kinachoshindikana na manji kaja yanga kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuifanya yanga ijitegemee na sio kumtegemea yeye kwa kuwa yeye ni binadamu lolote linaweza kutokea akawa hayupo,na amekuwa akisema wazi kwamba hapendi kuiona yanga ikitoweka atakapotoweka yeye au mfadhili yeyote,anataka kusimamia mabadiliko makubwa ya katiba ya yanga ambayo aliowaamini na kuwapigia debe waingie yanga ili wasaidie kuleta mapinduzi yanga wamemuangusha hasa imani maugila wa madega
 
Duh Radio One ya Mengi kiboko. Haitaki kumtaja Manji hata kidogo. Inataja kuanzia MAkamo Mwenyekiti na wajumbe; Manji no! Mengi na Manji wana bifu na mmoja anamdai mwingine Shilingi moja (Tsh. 1/=).
 
Hakuna kinachoshindikana na manji kaja yanga kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kuifanya yanga ijitegemee na sio kumtegemea yeye kwa kuwa yeye ni binadamu lolote linaweza kutokea akawa hayupo,na amekuwa akisema wazi kwamba hapendi kuiona yanga ikitoweka atakapotoweka yeye au mfadhili yeyote,anataka kusimamia mabadiliko makubwa ya katiba ya yanga ambayo aliowaamini na kuwapigia debe waingie yanga ili wasaidie kuleta mapinduzi yanga wamemuangusha hasa imani maugila wa madega

Mkuu maono ya Manji ni kuinunua Yanga na kuimilki. Akishaimiliki basi anaweza kuifanya kama Tp Mazembe ama hata Azam. Lakini katika hali hii ya Makomandoo na watu wanaoitwa Watu wa Mpira hapa TZ Manji ataishia kuondoka Yanga kwa aibu. Unakumbuka Mengi kuna wakati alitia guu yanga; nini kilimpata: Anajua mwenyewe! Manji anawajua makomandoo kwani wakati ule aliponunua mechi ya Yanga kule Mwanza kwa shilingi millioni mia moja ilibidi awape Makomandoo nauli ya kurudia Dar. Walikosa nauli kwa kuwa hawakukaa magetini kusaidia kukusanya mapato! Hao ndio watu wa mpira ambao hawataki kuona mabadiliko ya uendeshaji wa wa timu hizi kubwa. Chezea makomandoo na watu wa mpira hapa TZ. Hao ndio aanawaweka hata viongozi wa TFF!
 
Umenikumbusha usemi wa "NYANI HAONI KUNDULE" . Inaonekana jamaa hawajui kwamba mwenyekiti wao ni mtanzania mwenye asili ya KISOMALI

Mkuu kwa Simba siyo issue kuongozwa na Msomali, Mhindi ama Mwarabu. Kwa asili Simba ni yao. Ila Young Aftican Sports Club ni ya Wamatumbi na ilikuwa na uhusiano na vyama vya TAA na ZAA. Hii kitu ina ujumbe mzito sana bahati mbaya hatujui. Kinachotokea yangu kinaonyesha kwamba Yanga si Club ya wanyonge tena; si club ya wananchi. Ukijumlisha moja na mbili utagundua kuwa hii kitu ina bearing kwenye siasa za nchi yetu.
 
ok manji be like abramovic...

Mkuu nngu007 mbona Abromovich yeye anaimiliki Chelsea na si kiongozi ila Manji si mmiliki bali mwanachama sawa na mzee Mzimba ama Akilimali na amegombea na kufanikiwa kuwa Mwenyekiti. Kuna tofauti kubwa. Au Manji ndio anataka kuinunua Yanga na kuimiliki kama Chelsea ama TP Mazembe?
 
Last edited by a moderator:

Si ndio Anataka kuifanya Yanga Kampuni na kuuza HISA? na Yeye atakuwa na HISA kubwa...
 
Hahah huyu bwana mkubwa ndio alifanya mikia fc ubingwa wausikie kwenye redio RTD kwa miaka mitano mfululizo.
 
Back
Top Bottom