Rasmi: Manji 'OUT' Yanga, Watano Wajitosa Kumrithi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wanachama na mashabiki wa Yanga sasa wanapaswa kujiandaa kisaikolojia kuishi maisha bila Yusuf Manji baada ya jina la mwenyekiti huyo kutokuwapo miongoni mwa wagombea 27 waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa klabu hiyo utakaofanyika Janauri 13, 2019.

Tofauti na ilivyotarajiwa Manji hajachukua wala kuchukuliwa fomu kama ambavyo kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilitaka Yanga wafanye endapo watahitaji kumrejesha mwenyekiti huyo, badala yake wanachama wanne wamejitokeza kuwania nafasi hiyo.

Mwanasheria wa TFF, Herman Kidifu aliwataja wagombea waliojitosa kuwania nafasi ya Mwenyekiti ni Dk Jonas Tiboroha, Yono Kevela, Mbaraka Igangula na Erick Ninga.

Wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti ni Titus Osoro, Salum Magege Chota na Kevela wakati wajumbe ni Hamad Ally Islamu, Benjamin Jackson Mwakasonda, Sylvester Haule, Salim Seif, Musa Katabaro, Shftu Amri na Said Baraka.

Wengine ni Pindu Luhoyo, Dominick Francis, Seko Jihadhari, Ally Omary Msigwa, Arafat Ally Haji, Geofrey Boniphace Mwita, Frank Kalokola, Ramadhan Said, Leonard Marango, Bernard Faustin Mabula, Christopha Kashiririka, Athanas Peter Kazige na Faustin Peter Bisangwa.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wakili Ally Mchungahela alisema mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu umefungwa rasmi na keshokutwa Ijumaa utafanyika mchujo kwa wagombea wote.

“Uchaguzi uko palepale kwa wagombea waliochukua fomu, baada ya mchujo wa Ijumaa kutakuwa na usaili na baadaye wagombea wataingia kwenye kampeni kuelekea katika uchaguzi,” alisema Mchungahela.

Mchungahela alitoa onyo kwa mtu yeyote atakayejaribu kujipenyeza kuvuruga mchakato wa uchaguzi kwa kuanzisha vurugu, kuwa vyombo vya dola vitafanya kazi yake.
 
Na kesho wanaaanza mechi za mikoani huku wachezaji wanadai mishahara lazima wapigweeeeee
 
Kwani lazima Manji awe kiongozi ndani ya Yanga ndipo aweze kufadhili klabu?
Mbona sikuwahi kumsikua MO akigombea uongozi Simba lakini ameweza kuwa mwanahisa mkuu wa klabu?
Sifa nyingine wajameni mmmh!!!
 
Cjaona Jina LA mzee #akimali
Au bado anafikilia wito
 
Vipi kupiga magoti hakujasaidia? Kutegemea mtu ni upumbavu wa hali ya juu.
Halafu unakuta hao hao wanatoa kasoro mambo ya watu wengine. Na kuwaita majina.
 
Timu za Tanzania zimeshindwa kuwekeza nje ya soka sasa kila leo wanawaza kudanga tu.

Pumbavu kweli.
Timu inawekeza vipi nje ya soka
Mapato ya timu za soka duniani kote yanatokana na vitu vifuatavyo
1.Viingilio(hiyo ndo namba moja)
2.Wadhamini
3.Matangazo ya TV
4.Mauzo ya jezi
5.Mauzo ya wachezaji
 
Kwani lazima Manji awe kiongozi ndani ya Yanga ndipo aweze kufadhili klabu?
Mbona sikuwahi kumsikua MO akigombea uongozi Simba lakini ameweza kuwa mwanahisa mkuu wa klabu?
Sifa nyingine wajameni mmmh!!!

Mo siyo mwana hisa mkuu Simba, hamna hata sehem moja inayomtambua Mo kama mmiliki wa Simba zaidi ya ushabiki wa mtaani na magazetini! Anajitolea tu kuwalisha lisha basi ila kwenye hisa Simba haijafika huko
 
Timu inawekeza vipi nje ya soka
Mapato ya timu za soka duniani kote yanatokana na vitu vifuatavyo
1.Viingilio(hiyo ndo namba moja)
2.Wadhamini
3.Matangazo ya TV
4.Mauzo ya jezi
5.Mauzo ya wachezaji

No viingilio siyo no moja mkuu ! Viingilio ni hela ndogo sana Kwa club nyingi kulinganisha na mapato yatokanayo na tv & broadcasting
 
Mo siyo mwana hisa mkuu Simba, hamna hata sehem moja inayomtambua Mo kama mmiliki wa Simba zaidi ya ushabiki wa mtaani na magazetini! Anajitolea tu kuwalisha lisha basi ila kwenye hisa Simba haijafika huko
Katika mabadiliko ya Simba Mo atamiliki hisa 49% na wanachama 51%.
 
Naomba Unijibu Hayo mabadiliko yatakuwa lini ?

Ukweli ni kwamba hamna muwekezaji aweke hela kubwa vile alafu asichukue timu .yan kwamba yeye aweke hela let’s say bil 20 alafu akae pembeni kama mwanachama tu . Hapa tunajidanganya, ile ni biashara tena kubwa Kwa hiyo ili Mo achukue timu lazima Simba wakubali kumuuzia ziadi ya hisa 51% ili aichukue aweke management yake timu iendeshwe kibiashara, na yeye Faida yake irudi , ki ufupi yeye ndo a control ile hela vinginevyo hiyo 49% haitakaa itokee. Tuangalie mambo Kwa mapana zaidi Mo hawezi weka hela kisa anaipenda Simba , yule ni entrepreneur..
 
Back
Top Bottom