Manji kujitoa Yanga?

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
126
Kuna habari kuwa anaejiita mfadhili wa Yanga Yusuf Manji ambae pia ni mkurugenzi mtendaji wa Quality Group maji yamemfika shingoni na sasa anautema "ufadhili" wa klabu hiyo kongwa yenye historia ya migogoro isiyo kwisha.

Chanzo chetu ndani klabu hiyo kinatuhabarisha kuwa "mfadhili" amechoshwa na mwenendo wa kusua sua wa Yanga ktk ligi ya Vodacom sanjari na kunitumia mamilioni kununua wachezaji wanaoitwa wa kulipwa na kulipa mishahara minono kwa makocha na wachezaji.

Manji ambaye aliingia kwa mbwembwe na kuahidi kuifanya yanga kuwa "Arsenal" ya Tanzania anajiunga na mlolongo wa watu maarufu walijitahidi kutatua migogoro ya Yanga akiwemo Reginald Mengi,Yusuf Makamba ( akiwa mkuu wa mkoa Dar Es Salaam ) Sulemain Kuchaya ( aliyekuwa mshauri wa Rais Mkapa) Mbunge Azan Zungu nk.

Yanga ambayo imenyang'anywa ubingwa na yule Mnyama mkali Simba imeshafungwa mechi 3 ktk ligi inayoendelea. Na kutia chumvi ktk kidonda aliye kuwa kocha wao mkuu Razak Siwa amekiri mwenyewe kuwa yeye ni m-babaishaji na haiwezi kazi na kupelekea kurejeshwa Jack Chamangwana ambaye alikuwa akizurura mitaani Dar kama machinga bila kazi yeyote ya maana. Bado haijafahamika mara moja kama Jack ana mkataba wowote (let alone work permit kutoka immigration) au ni day worker mpaka atakapo kuja huyo mlima maparachichi kutoka Poland.

Tunachokuwa nafasi hii kuwakumbusha watani kuwa ile ni Yanga Sports Club neno Sports linajumuisha pia netball labda wajaribu bahati yao huko
 

Yusufu Manji asitisha kuendelea kuidhamini Yanga
Na Clara Alphonce


YUSUF Manji, ambaye kampuni yake ya Quality Group, inaidhamini klabu ya Yanga, jana alitangaza kujiengua rasmi kuidhamini klabu hiyo kongwe baada ya kipindi cha takriban miezi 16, akidai kuwa uongozi ulimuahidi makubwa, lakini haujatekeleza.


Manji alitangaza udhamini huo ofisini kwake jana, ikiwa ni siku sita kabla ya kocha mpya kutoka Poland kuwasili nchini kuinoa klabu hiyo, huku timu ikiwa inasuasua kwenye Ligi Kuu licha ya kusajili wachezaji wageni nyota kutoka nchi jirani.


"Unajua nimekuwa nikitoa pesa nyingi sana ili Yanga ifanye vuzuri, lakini hali imekuwa kinyume na nilivyotegemea na nilishawaita viongozi nikaongea nao na wachezaji pia na wote waliniaidi kufanya vizuri lakini imekuwa sivyo," alisema Manji.


"Sasa nimefikia uamuzi kwamba sitaendelea na mkataba mwingine na Yanga na nimefikia uamuzi huu mzito baada ya kushauriana kwa kina na familia na marafiki zangu. Najua uamuzi huu utazua maswali mengi, lakini lakini nimefanya hivyo kwa sababu ya maadili yangu na familia yangu pamoja na sababu zangu binafsi.


"Kama uongozi wa Yanga unahitaji muda ili kujipanga na (kutafuta) vyanzo mbadala vya mapato, niko tayari kulipa mishahara yote ya mwezi huu, ila nawasihi watumie muda huu vizuri."


Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, lakini katika siku za karibuni kumekuwepo na mgogoro unaoendelea chini chini kwenye klabu hiyo kutokana na uongozi kusita kuikabidhi timu kwa kampuni.


Inasemekana kuwa Manji amekuwa akishinikiza timu ikabidhiwe kwa kampuni ili iiendeshe, lakini Madega na viongozi wenzake wamekuwa wakisita kutokana na kutokamilika kwa zoezi la usajili wa kampuni na zoezi la uchaguzi wa viongozi wa kampuni.


Manji alifanikiwa kurejesha umoja kwenye klabu hiyo baada ya makundi ya Yanga Asili na Kampuni kupambana kwa karibu miaka minne, na aliingiza fedha nyingi wakati klabu hiyo ikishiriki Ligi ya Mabingwa wa Afrika na baadaye Kombe la Shirikisho.


Hivi karibuni aliwaita viongozi na wachezaji ofisini kwake na kuwakaripia kuhusu mwenendo mbovu wa timu kwenye Ligi Kuu, baada ya Yanga kupoteza mechi tatu na kushinda mbili.


Katika taarifa yake, Manji anamshukuru rais wa zamani wa Yanga, Francis Kifukwe, kiongozi wa kundi la Yanga Asili, Yusuf Mzimba, wajumbe wa kamati ya rasimu, na mwenyekiti wa kamati ya ushindi, Jamal Malinzi.


Source Mwananchi

Haya wana Kandambili tuliwa tabiria hili sana limewakuta...

Only on JF heh hey!
 
hilo ndo tatizo la soka letu lililolaaniwa la bongo...hasa hizi club zetu mbili kubwa..simba na yanga..yaaani kwa migogoro hazina wapinzani halafu kichekesho zaidi ni pale zinapopokezana migogoro...mwaka huu ikiwa ni wana msimbazi basi kwa jangwani kuna tulia likilipuka la jangwani basi msimbazi kwatulia...yaani sijui mpira utaendelea lini..halafu cha ajabu watu wengine wamezeeeka wanatakiwa kuwa wanawasimulia vitukuu na vilembwe vyao hadithi za miaka yao ya 47..lakini bado tuu wanangangania uongozi na madaraka without aibu...dohhh
 
yanga tuliwaambia kuwa lengo la manji halikuwa mpira..kwanza manji ni simba[na alipotaka kujiingiza kwenye mpira alitaka kuingilia simba,washauri wakamuambia kwa kuwa simba walikuwa ni kina MO..NI BORA ANGEINGILIA YANGA AMBAO kwa wakati ule walikuwa na shida na vile vile azingatie histororia ya yanga]..lengo lake kuu lilikuwa ni PUBLIC IMAGE BUILDING CAMPAGNE..especially hasa alivyokuwa akikabiliwa na kashfa mbalimbali....sasa kwa kuwa hisia za wananchi na magazeti hawaongelei tena kashfa za manji..hana haja tena na sabuni YANGA...

Poleni sana................
 
Tumeshapoa! I try 2 imagine sijui hata itakuwaje..... yaani hadi naogopa
 
ahaaaaaaaaaa
yaani mie sijui itakuwaje,kwani mkataba wake ulikwisha lini?
na vipi mishahara atawalipa nani?
na Simba wanacheza lini?
 
eeeeeeeee
tunaweza kupata iyo barua ya aliyoandika Manji kwa vyombo vya habari?na Mwenyekiti Madega anasemaje?
 
Timu zilizokuwa na msimamo Tanzania, zilikuwa timu za makampuni....
1) Pamba 2) Ushirika 3) Ndovu 4) RTC (mwanza, kigoma, kagera) 5) Mecco etc........yaani tangu mashirika hayo yaachane na michezo ligi ya bongo chovu tu.
Hao Simba/Yanga majina makubwa ila utumbo mtupu....kila siku kufarakana tuuu aaah, wanaboa.

Hivi kombe la taifa liliishia wapi? Linaloshirikisha kombaini za mikoa....Mzizima United, Kagera Eagles, Mwanza Heroes etc....labda hiyo itachangamsha mpira kidogo hapo nyumbani.

whatteva happened?
 
Back
Top Bottom