Quality plaza ni mali ya Manji au PSPF?
kwani Ni kipi hujakielewa mkuu?
Jamani, hawa vibosile kinachowashinda kulipa kodi ni nini!!
MODS PLS RESERVE THIS THREAD.
Leo kulikuwa na mkutano wa kampeni wa
mgombea ubunge jimbo la Mbeya mjini Shambwee
Shitambala. Mkutano huu pia ulihutubiwa na Mh.
Mwigulu Nchemba ambaye alishuka kwa chopa
kwenye saa 12 kamili na akapewa nafasi ya
kuhutubia kwa taribani robo saa hadi saa 12:17
jioni ambapo ndipo mkutano ulifungwa.
Sitagusia mkutano wenyewe ulivyokuwa ila nahitaji
kuandika kidogo tu kuhusu mambo kadha
aliyosema Mwigulu Nchemba. Kwenye hotuba yake,
muda mwingi aliutumia kutaja ugonjwa na udhaifu
wa Ugonjwa wa mgombea Urais wa UKAWA kupitia
CHADEMA Ndg. Edward Lowassa. Kauli alizotoa ni
kama:
1. Hawezi shika mike anatetemeka
2. Hana uwezo wa kuuwakilisha nchi kimataifa
kwani ugonjwa wake unamfanya ahutubie dakika
tatu tu.
3. Anatembea huku anajikojolea
4. Akisimama sana betri inakuwa low hivyo
kupoteza network.
5. Hata jina la mke wake( Mama Regina Lowassa)
huwa analisahau.
6. Tukimchagua Lowassa hatutakuwa tumeitendea
nchi yetu haki kwani tutakuwa tumemchagua
mgonjwa ambaye hawezi kufanya kazi.
Mimi siwezi kupinga kauli zako kwani uliyezisema
ni wewe mkuu. Nilitaka tu kwa faida ya wote humu
tutafakari sisi ni akina nani na nafasi yetu ni ipi
katika kuwahukumu au kuwatakia mabaya wale
tusiowapenda.
Tukumbuke kuwa sisi sote ni ndugu, kuna maisha
baada ya uchaguzi na Mungu wetu ni mmoja na
ndiye aliyetuumba na sisi sote tuko sawa mbele
zake. Mimi ni mkiristo na katika kukamilisha kile
ninzchotaka kusema nitatumia nukuu chache toka
Biblia takatifu kama ifuatavyo:
1. ZABURI 139:14 : " Nitakushukuru kwa kuwa
nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha,
Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua
sana".
2. MATHAYO 7:1,2 : " Msihukumu, msije
mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile
mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo
kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa".
3. 1 Wakorintho 4:5 :" Basi ninyi msihukumu neno
kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye
atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na
kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu
atakapoipata sifa yake kwa Mungu".
4. Wagalatia 6:7,8 :" Msidanganyike, Mungu
hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu,
ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa
mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu;
bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna
uzima wa milele".
5. Jeremiah 32:27 :" Tazama, mimi ni BWANA,
Mungu wa wote wenye mwili; Je! Kuna neno gumu
lo lote nisiloliweza?".
Baada ya nukuu hizo chache naomba kusema
kuwa nimesikitika sana kuona Mtanzania
mwenzetu na mtu ambaye amewahi kuwa kiongozi
wa ngazi ya Waziri Mkuu kutukanwa na
kudhalilishwa kwa kiwango hiki cha sasa. Jamani
ndugu zangu Watanzania, mbona tunakuwa na
uadui wa namna hii??? Hivi tunapofungua vinywa
vyetu kuwatukana ndugu zetu kwa kiwango cha
kutisha namna hii, je sisi tuna guarantee na
maisha yetu??? Je, sisi tuna mkataba na Mungu
wetu ambaye ndiye alituumba na mwenye
mamlaka ya uhai na uzima tulio nao???
Katika mojawapo maadili wanayojifunza Madaktari
ni pamoja na kutotoa siri za ugonjwa wa mgonjwa
kwa mtu yeyote isipokuwa kwa mgonjwa tu na
baada ya hapo mgonjwa mwenyewe anaweza
kumwambia atayeona inafaa. Lakini pia hata kama
Madaktari wanaona kuwa mgonjwa anaenda kufa
bila kujali nini kitafanyika, hawaruhusiwi kuacha
kumhudumia mgojnwa hadi dakika ya mwisho na
pia hawatakiwi kumdhihaki kwa namna yoyote ile
hata kama anakufa kwa ugonjwa wa kujitakia. Sasa
sisi ambao hatujawahi kumpima Lowassa ili kujua
kama kweli ni mgonjwa ni kitu gani kinamsumbua,
inakuwaje tunajitwalia mamlaka ya Uungu na
Uumbaji na kuanza kutoa hukumu kiasi hiki???
Lowassa ana miaka 62 sasa na hivyo ni mzee. Na
hivyo bila shaka tunajua kuwa mtu akishafika umri
wa uzeeni kinga ya mwili na nguvu vinapungua
hivyo kumpelekea mtu kupata matatizo mbali mbali
ya kiafya. Hakuna mtu na hata hawa
wanaomtukana Lowassa ambaye kama Mwenyezi
Mungu atamjalia Maisha marefu hatapitia umri wa
uzee na kuona tabu zake.
Jamani bila kujali itikadi zetu za kisiasa,
tusimdhihaki Mungu. Tusicheze na Mungu ambaye
ni muumbaji wetu. Sote tuliumbwa kwa kwa
namna inayo fanana hivyo tulinde sana mioyo yetu
na ndimi zetu. Mungu huyo huyo aliyetupa uzima
na afya ndiye huyo huyo aliyeruhusu Lowassa
kuumwa ugonjwa wa kupoteza nguvu, kumbu
kumbu na kujikojolea kama wanavyomtukana watu
wakiwamo Mh. Mwigulu Nchemba.
Mi leo baada ya kusikia Mh. Lowassa
akiporomoshewa matusi kana kwamba alichagua
kuwa vile, imebidi nitafakari sana upya juu ya
uhusiano wangu na Mungu wangu ambaye ndiye
kanipa uzima hadi dakika hii na wakati uo huo
karuhusu wengine walale usingizi wa mauti. Mungu
wangu ninakushukuru na nitazidi kukushukuru na
kulitukuza jina lako kwa kuniumba kwa namna
nilivyo. Amen.
Mwisho kabisa naombeni sana Watanzania
wenzangu tupendane. Siasa zisitufanye tukapoteza
utu na kujiona kuwa sisi ni bora kuliko wengine.
Uchaguzi utapita na maisha yataendelea.
AFRIKA NI MOJA, SOTE NI NDUGU.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
na MUNGU WABARIKI WATANZANIA.
WASALAM.