Manji apewa saa 48 Kuhama Quality Plaza

sasa kama ni mgonjwa watu wasiseme,,,eti itakuwa tunamhukumu?.....
yaani tuchague mtu baada ya wiki awe wa kukagua gwaride akiwa kalala kwenye machela?,watu waogope kusema eti unaweza ugua na ukaondoka kabla yake,itdoesnt matter,,,ukweli lazima tu usemwe,,ili kama mnachagua kitu muwe mmefanya uamuzi mkiwa well informed,,ili baadae msilete kelele tena za kulalamika

Hatumchagui mtu kwa nguvu zake bali akili na hekima zake.
 
Maccm midomo inawasha kwani magufuli dawa anakunywa za nini? Moyo wake mdogo Na yule Wa kebby' s anaumwa sana
 
Kwa jinsi nchi yetu ilivyo asemayo Fareed yanaweza kuwa kweli.
Magazeti yafanye basi utafiti watuletee ukweli wote.
 
sasa kama ni mgonjwa watu wasiseme,,,eti itakuwa tunamhukumu?.....
yaani tuchague mtu baada ya wiki awe wa kukagua gwaride akiwa kalala kwenye machela?,watu waogope kusema eti unaweza ugua na ukaondoka kabla yake,itdoesnt matter,,,ukweli lazima tu usemwe,,ili kama mnachagua kitu muwe mmefanya uamuzi mkiwa well informed,,ili baadae msilete kelele tena za kulalamika

Tunataka tupate kuona raisi akiwa mgonjwa anaendeshaje nchi, kwa maana wote waliopita walikua wazima
 
Mkuu usihangaike, watu wa CCM wapo juu sio tu kwa watanzania bali pia wapo juu hata kwa Mungu. Wanajua mambo ya leo, ya kesho na ya milele. Hakuna cha kuwatisha. Hawamuogopi mungu wala nani yake...

Wanajua hata atakayekufa hata kama ni wa chama chao
 
Hii nchi kweli mwenyenacho huongezewa...unadaiwa kodi miaka mitatu, wakati wengine tunalipa ndio tunakaa.

Mwenye ujuzi anijuze baada ya hayo masaa 48 akiondoka watamdai?

Natabiri ataondoka halafu wakija mdai atagoma kulipa watampeleka mahakaman halafu manji atashinda kesi kws kosa la kuondoshwa kinyume na sheria fidia yake itakuwa sawa na manj kuuziwa jengo lote.
 
hivi kumbe Quality Plaza ya PSPF? mbona waliliita Quality plaza? Jamaa akisema lake itakuwaje? Jengo la Shirika la Umma kulipa jina la kampuni ya Fisad nao ni ufisadi..menejimenti ya PSPF nayo ichunguzwe, kuna harufu ya ufisadi hapo.!

Nijuavyo mimi pspf ina umiliki wa 30%
 
Ukweli lazima usemwe na uongo ukemewe kwani ukawa mnataka Tanzania ya watu waongo waaminiwe zaidi. Tumekataa tabia hii ya hovyo kabisa.
 
Kwenye kipindi cha mahojiano Chanel Ten Manji amesema atakuwa anaongea na wanambagala kwa njia ya " Vedio Conference" Hana muda wa kuonana nao physically. Na wengine watakuwa wanaeleza shida zao kwa secrtaries wake watano waliopo ofisini kwake. Sababu kubwa amesema ni kuwa diwani halipwi mshahara na kuwa hana muda wa kumsaidia mtu mmoja mmoja shida zake. Pia anatakiwa aendelee na biashara zake ili aweze kulinda ustawi wa familia yake. Wanambagala kuu watakuwa wamekosea sana kumchagua huyu kuwa mwakilishi wao. Manji kama anataka kusaidia jamii angefanya kama Azam sio kujificha kwenye siasa ili kulinda maslahi yake
 
Hii nchi kweli mwenyenacho huongezewa...unadaiwa kodi miaka mitatu, wakati wengine tunalipa ndio tunakaa.

Mwenye ujuzi anijuze baada ya hayo masaa 48 akiondoka watamdai?

Natabiri ataondoka halafu wakija mdai atagoma kulipa watampeleka mahakaman halafu manji atashinda kesi kws kosa la kuondoshwa kinyume na sheria fidia yake itakuwa sawa na manj kuuziwa jengo lote.

Angalia vizur hiyo thread ni ya mwaka gani kwanza
 
Hehe, Manji ndiye aliwauzia PSPF hili jengo la Quality Plaza kwa bei kubwa sana (nadhani kati ya 30-40 bn/-). Alipowauzia, aliwahakikishia kuwa kutakuwa na 100% occupancy kwenye jengo hilo hivyo watarudisha pesa zao fasta. Manji na makampuni yake lukuki wakachukua karibu nusu ya jengo wakakodi wao ili jengo lijae. Wakawa hawalipi kodi. Sasa yamefikia haya.

Cha kusikitisha ni kuwa, PSPF hawana hati ya ardhi ya jengo hilo la Quality Plaza. Kuna utapeli mkubwa Yusuf Manji wa Quality Group aliwafanyia alipowauzia jengo at a grossly inflated price tag.

Sawa, wamemfukuza Manji kwenye jengo "lao" kama mpangaji, lakini Manji aliwauzia jengo hilo kwa thamani iliyo mara 10 ya bei halisi. Halafu pia PSPF hawana hati ya ardhi ya jengo hilo. Nani mjanja (fisadi Manji), nani kaliwa (sisi Watanzania).

hao walionunua kwa niaba ya pspf walikuwa hawajui sheria?hawana mwanasheria?au walishirikiana na huyo muuzaji kufanya huo utapeli?au ndiyo ule usemi WA tumbo langu kwanza maadili na uzalendo baadae.
 
Kwenye kipindi cha mahojiano Chanel Ten Manji amesema atakuwa anaongea na wanambagala kwa njia ya " Vedio Conference" Hana muda wa kuonana nao physically. Na wengine watakuwa wanaeleza shida zao kwa secrtaries wake watano waliopo ofisini kwake. Sababu kubwa amesema ni kuwa diwani halipwi mshahara na kuwa hana muda wa kumsaidia mtu mmoja mmoja shida zake. Pia anatakiwa aendelee na biashara zake ili aweze kulinda ustawi wa familia yake. Wanambagala kuu watakuwa wamekosea sana kumchagua huyu kuwa mwakilishi wao. Manji kama anataka kusaidia jamii angefanya kama Azam sio kujificha kwenye siasa ili kulinda maslahi yake
Nilimsikiliza,jamaa huyu hafai kabisa anataka kutumia mwanya huo kumilikishwa plots kubwa kwa kisingizio cha kuendeleza Mbagala,maendeleo ya Mbagala Kuu yatafanywa/letwa na Manispaa siyo ujanja janja wa Yusuf Manji kutumia viwanja kuchukulia mikopo halafu anafanyia vitu vingine tofauti kabisa - kwa nini hagombei Ubunge kama ana ubavu,hawezi anajua jina lake haliwezi kupitishwa 4 a good reason ndio maana kakimbilia kwenye Udiwani anafikiri anaweza kuzuga watu kwa mipango yake lukuki ambayo si rahisi kutekelezeka!!
 
Hawa ndio madiwani wetu watarajiwa wanaowaza na umeya.......Handbill ya sera zake imejaa "umimi" na ndoto za alinacha

1445402316378.jpg

1445402331058.jpg
 
Kiongozi atakaye ingia madarakani atapaswa kupitia upya michezo michafu baina ya mashirika ya mifuko ya jamii na Yusuf Manji,jamaa huyu kaichezea sana mifuko hii akishirikiana na Wafanyakazi walio pewa dhamana ya kusimamia mifuko husika,si rahisi Manji kama Manji kuchota fedha za wavuja jasho na kukarabati/jenga majengo ambayo mengi ni prefabricated gharama za ujenzi ni ndogo sana anacho fanya ni kuweka urembo na vioo basi,kwa mtu ambae hajui mambo haya anaweza kufikiri yamejengwa kwa gharama kubwa wakati si kweli!

Kinacho shangaza zaidi Manji anawahuzia majengo hayo hayo kwa mifuko ya jamii iliyo mpatia mikopo, bei inakuwa mara kumi ya mkopo - huu kama sio utapeli uliyo pitiliza mipaka ni nini? Binafsi ningependekeza wahusika wote wa utapeli huu wachukuliwe hatua kali ili liwe fundisho kwa Wakurugenzi wengine wa mifuko ya jamii hata kama wamestaafu wakamatwe tu na kufungwa.
 
ndg zangu kabla hamjatiana vodole machonu kwa kutokubaliana,zingatieni hili "13:33 22nd December 2010".
 
Kwa nini asipewe masaa 48 ya kuondoka nchini -- arudi kwao India? hasa yeye na wale wengine watatu -- RA, Subhash na Tanil. Ikitokea hivyo Watanzania tutaishi kwa amani.
Usiwe mshamba wewe tembea uone ulimwengu, sio unakaa bila kutembea na kujielimisha kuona au kujua ulimwengu wa karne hii ulivyo, ubaguzi umepitwa na wakati mtu hahukumiwi kwa rangi, kabila, jinsia au dini, anamhukumu kwa kosa alilofanya.Tembea ulimwengu uone nchi zina raia wa kila asili na kabila, wote wana haki sawa kama raia wengine. Haya yalioyotokea yanahosiana na biashara sisi hatuyajui, yanahusiana nini na kupewa masaa 48 kuondoka nchini kurudishwa India, tuache chuki na wivu wa kijinga, tuwe na wivu wa maendeleo tujiendeleze.
 
Kwenye kipindi cha mahojiano Chanel Ten Manji amesema atakuwa anaongea na wanambagala kwa njia ya " Vedio Conference" Hana muda wa kuonana nao physically. Na wengine watakuwa wanaeleza shida zao kwa secrtaries wake watano waliopo ofisini kwake. Sababu kubwa amesema ni kuwa diwani halipwi mshahara na kuwa hana muda wa kumsaidia mtu mmoja mmoja shida zake. Pia anatakiwa aendelee na biashara zake ili aweze kulinda ustawi wa familia yake. Wanambagala kuu watakuwa wamekosea sana kumchagua huyu kuwa mwakilishi wao. Manji kama anataka kusaidia jamii angefanya kama Azam sio kujificha kwenye siasa ili kulinda maslahi yake
Hii ni karne ya Technologia sioni vibaya ikiwa utaweka centre au sehemu ukaongea na watu kwa Video, mbona jambo la kawaida siku hizi kuna hata tiba zinatolewa kwa njia ya Video (Telemedicine)na mahakama kuna wakati wanatumia video.Usimhukumu kabla ya kuujua au kuuona utendaji aliyo uzungumzia ataufanya vipi. Kuhusu utoaji msaada au kusaidia, hata dini inasema unapoamua kumsaidia mtu unatakiwa utoe kwa mkono wa kulia hata wa kushoto usione, kwahiyo utaratibu wa kuweka watu foleni toka asubuhi wanangojea nje ya ofisi yako uje utoe msaada, huko ni kudhalilisha watu na kutaka jionyesha hata Mungu hapendi.
 
Oh! Kumbe! Mimi nilijua quality centre ni ya Manji.
Manji apewa saa 48 kuhama Quality Plaza

na Bakari Kimwanga

amka2.gif

MFANYABIASHA maarufu nchini Yusuf Manji, amepewa notisi ya saa 48 na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), kuhama katika jengo la Quality Plaza Complex.
Jengo hilo ambalo liko kitalu namba 182/2 barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam ni mali ya PSPF na Manji ambaye ni mpangaji anadaiwa kukiuka masharti ya mkataba wa upangishwaji kwa kushindwa kulipa kodi.
Wakili wa PSPF, Benitho Mandele, alisema katika barua yake yenye kumbukumbu namba DLA/IMAGE/2010/12 kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Quality Group Limited, Manji anadaiwa kodi ya kuanzia Aprili, 2009 hadi Desemba 2010, hivyo jumla ya deni lote ni dola 2,335,189.06 za Marekani.
“Manji, ameshindwa kuheshimu makubaliano baina ya wateja wangu ambao ni PSPF na yeye… tangu Aprili mwaka jana hadi Desemba, 2010 ameshindwa kulipa kodi.
“Tumempa masaa 48 kuanzia leo hadi kesho kutwa awe amehama katika jengo lile,” alisema wakili huyo wa PSPF.
Alisema kwa kutambua uzito wa suala hilo amemwandikia Manji barua ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake kwenda kwa Mkurugenzi wa Quality Group Limited, Gaming Management Limited, Quality Ligistics Co. Limited, International Transit Ivestment Limited na Q-Consult Limited.
Kwa mujibu wa barua hiyo, Manji amepewa nakala ya barua hiyo kama Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Quality Group Limited.
Hata hivyo, Manji alipotafutwa na gazeti hili kwa njia ya simu yake ya mkononi, alikata simu baada ya kuulizwa kama amepata barua hiyo.
Hata hivyo, baadaye gazeti hili lilipomtafuta kupitia simu yake hiyo, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni katibu mukhtasi ambaye alisema ujumbe umefika. Hadi tunakwenda mitamboni jana jioni kulikuwa hakuna majibu yoyote kutoka kwake.
Source: www.freemedia.co.tz
 
Back
Top Bottom