Manji apewa saa 48 Kuhama Quality Plaza

Manji apewa saa 48 Kuhama Quality Plaza

Gurudumu

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2008
Posts
2,349
Reaction score
264
Manji apewa saa 48 kuhama Quality Plaza

na Bakari Kimwanga

MFANYABIASHA maarufu nchini Yusuf Manji, amepewa notisi ya saa 48 na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), kuhama katika jengo la Quality Plaza Complex.

Jengo hilo ambalo liko kitalu namba 182/2 barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam ni mali ya PSPF na Manji ambaye ni mpangaji anadaiwa kukiuka masharti ya mkataba wa upangishwaji kwa kushindwa kulipa kodi.

Wakili wa PSPF, Benitho Mandele, alisema katika barua yake yenye kumbukumbu namba DLA/IMAGE/2010/12 kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa Quality Group Limited, Manji anadaiwa kodi ya kuanzia Aprili, 2009 hadi Desemba 2010, hivyo jumla ya deni lote ni dola 2,335,189.06 za Marekani.

“Manji, ameshindwa kuheshimu makubaliano baina ya wateja wangu ambao ni PSPF na yeye… tangu Aprili mwaka jana hadi Desemba, 2010 ameshindwa kulipa kodi.

“Tumempa masaa 48 kuanzia leo hadi kesho kutwa awe amehama katika jengo lile,” alisema wakili huyo wa PSPF.

Alisema kwa kutambua uzito wa suala hilo amemwandikia Manji barua ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake kwenda kwa Mkurugenzi wa Quality Group Limited, Gaming Management Limited, Quality Ligistics Co. Limited, International Transit Ivestment Limited na Q-Consult Limited.

Kwa mujibu wa barua hiyo, Manji amepewa nakala ya barua hiyo kama Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Quality Group Limited.

Hata hivyo, Manji alipotafutwa na gazeti hili kwa njia ya simu yake ya mkononi, alikata simu baada ya kuulizwa kama amepata barua hiyo.

Hata hivyo, baadaye gazeti hili lilipomtafuta kupitia simu yake hiyo, ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni katibu mukhtasi ambaye alisema ujumbe umefika. Hadi tunakwenda mitamboni jana jioni kulikuwa hakuna majibu yoyote kutoka kwake.

Source: Tanzania Daima
 
"Tumempa masaa 48 kuanzia leo hadi kesho kutwa awe amehama katika jengo lile," alisema wakili huyo wa PSPF.
Alisema kwa kutambua uzito wa suala hilo amemwandikia Manji barua ambayo Tanzania Daima inayo nakala yake kwenda kwa Mkurugenzi wa Quality Group Limited, Gaming Management Limited, Quality Ligistics Co. Limited, International Transit Ivestment Limited na Q-Consult Limited.
....Hii ni kali...wamenyimwa mgao nini?
 
...Watamalizana kiutu uzima tu.A call to someone, biashara imekwisha. Nilianza kufurahi nikidhani kuwa ni 'Manji apewa masaa 48...KUONDOKA NCHINI!". Wishful thinking....
 
Hawa mafisadi wana hela za mchezo, inamaana wanazuia magazeti yote yasiuzwe, what if wakirudia kuiandika?
 
Kwa nini asipewe masaa 48 ya kuondoka nchini -- arudi kwao India? hasa yeye na wale wengine watatu -- RA, Subhash na Tanil. Ikitokea hivyo Watanzania tutaishi kwa amani.
 
Hehe, Manji ndiye aliwauzia PSPF hili jengo la Quality Plaza kwa bei kubwa sana (nadhani kati ya 30-40 bn/-). Alipowauzia, aliwahakikishia kuwa kutakuwa na 100% occupancy kwenye jengo hilo hivyo watarudisha pesa zao fasta. Manji na makampuni yake lukuki wakachukua karibu nusu ya jengo wakakodi wao ili jengo lijae. Wakawa hawalipi kodi. Sasa yamefikia haya.

Cha kusikitisha ni kuwa, PSPF hawana hati ya ardhi ya jengo hilo la Quality Plaza. Kuna utapeli mkubwa Yusuf Manji wa Quality Group aliwafanyia alipowauzia jengo at a grossly inflated price tag.

Sawa, wamemfukuza Manji kwenye jengo "lao" kama mpangaji, lakini Manji aliwauzia jengo hilo kwa thamani iliyo mara 10 ya bei halisi. Halafu pia PSPF hawana hati ya ardhi ya jengo hilo. Nani mjanja (fisadi Manji), nani kaliwa (sisi Watanzania).
 
Du hivi lawyers wa PSPF wapo kweli? they must be insane! if they wa RANGI HIYO think they have a lot of money to bride every one,wapo chaka we have God they can never bribe!
 
Jamani, hawa vibosile kinachowashinda kulipa kodi ni nini!!
 
Hehe, Manji ndiye aliwauzia PSPF hili jengo la Quality Plaza kwa bei kubwa sana (nadhani kati ya 30-40 bn/-). Alipowauzia, aliwahakikishia kuwa kutakuwa na 100% occupancy kwenye jengo hilo hivyo watarudisha pesa zao fasta. Manji na makampuni yake lukuki wakachukua karibu nusu ya jengo wakakodi wao ili jengo lijae. Wakawa hawalipi kodi. Sasa yamefikia haya.

Cha kusikitisha ni kuwa, PSPF hawana hati ya ardhi ya jengo hilo la Quality Plaza. Kuna utapeli mkubwa Yusuf Manji wa Quality Group aliwafanyia alipowauzia jengo at a grossly inflated price tag.

Sawa, wamemfukuza Manji kwenye jengo "lao" kama mpangaji, lakini Manji aliwauzia jengo hilo kwa thamani iliyo mara 10 ya bei halisi. Halafu pia PSPF hawana hati ya ardhi ya jengo hilo. Nani mjanja (fisadi Manji), nani kaliwa (sisi Watanzania).

Hivi vitu kweli vinatokea Tanzania hasa kwa organisation kubwa kama PSPF I am shocked!!!!
 
he is a drug user.. amesizi.. katumia fedha nyingi kubadilisha damu kwani Unga na Virus vinamnyong':teeth😱nyesha
 
Wakuu hilo linawezekana ni bonge la changa la macho,,kwani huyo mdosi halikopa pesa za wabongo akafatua Quality Plaza (Low Quality Plaza),then akalitumia akawauzia hao wamiliki wa mapesa ya wabongo hao hao washkji there after akajifanya mpangaji......then faida ya hilo jengo anafyatua another Quality low Quality Plaza mita elfu kadhaa kutoka hiyo ya awali.Hivyo hata kama wangempa nusu saa Imeshakula kwetu sana tu.
 
Back
Top Bottom