Manji amuokoa Komba, anunua shule zake

Manji amuokoa Komba, anunua shule zake

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
26,021
Reaction score
25,423
Sakata la mali za John Komba kupigwa mnada kufuatia deni la Tsh bilion 1.2 analodaiwa na benki ya CRDB limefikia tamati baada ya mfanyabiashara nguli na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Bw Yusuf Manji, kununua shule zake pamoja na baadhi ya mali zake ambazo zilikuwa zipigwe mnada.

Komba alikuwa anakabiliwa na uwezekano wa shule na mali zake kupigwa mnada (na kufungwa jela) ili kufidia deni hilo alilokopa CRDB miaka 5 iliyopita.

Source: Mwananchi.

MAONI YANGU
Komba amshukuru sana Manji kwa kumuokoa kwenda jela na mali zake kupigwa mnada. Sipati picha kama Komba angefungwa jela kile kitambi chake angekificha wapi. Lazima kingenywea kama puto lililotoboka. Hivi alidhani kuendesha shule ni lelemama au ni sawa na kuimba kwaya na kusimamia bendi? Chezea mikopo wewe!
 
Daaaaaaaaa Vitega uchumi vya komba ndio vinaondoka hivyo.
 
Sakata mali za John Komba kupigwa mnada kufuatia deni la Tsh bilion 1.2 analodaiwa na benki la CRDB limefikia tamati baada ya mfanyabiashara nguli na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Bw Yusuf Manji, kununua shule zake pamoja na baadhi ya mali zake ambazo zilikuwe zipigwe mnada.

Komba alikuwa anakabiliwa na uwezekano wa shule na mali zake kupigwa mnada (na kufungwa jela) ili kufidia deni hilo alilokopa CRDB miaka 5 iliyopita.

Source: Mwananchi.

MAONI YANGU
Komba amshukuru sana Manji kwa kumuokoa kwenda jela na mali zake kupigwa mnada. Sipati picha kama Komba angefungwa jela kile kitambi chake angekificha wapi. Lazima kingenywea kama puto lililotoboka. Hivi alidhani kuendesha shule ni lelemama au ni sawa na kuimba kwaya na kusimamia bendi? Chezea madeni wewe!
Nijuavyo mimi, ukikopa na kushindwa kulipa, sio kosa la jinai la kumpeleka mtu jela!, ni kosa la madai ambapo ukiisha filisiwa kwa mali kupigwa mnada that is the end!.

Hakuna hukumu ya kifungo cha jela kwa kudaiwa!.

Pasco
 
Daaaaaaaaa Vitega uchumi vya komba ndio vinaondoka hivyo.
No sidhani kama zimeondoka!, kilichofanyika ni bail out tuu, kwa Manji kumlipia deni ili mali zisiuzwe na benki, out of that bail out, inawezekana Komba akaachia baadhi ya mali hizo preferably land kuifidia hiyo bail, out!.
Pasco.
 
Nijuavyo mimi, ukikopa na kushindwa kulipa, sio kosa la jinai la kumpeleka mtu jela!, ni kosa la madai ambapo ukiisha filisiwa kwa mali kupigwa mnada that is the end!.

Hakuna hukumu ya kifungo cha jela kwa kudaiwa!.

Pasco

nijuavyo mimi ni kwamba ikiwa thamani ya mali zako ni ndogo kuliko deni, utasweka ndani sawia.
 
Tarehe ya mnada ilikuwa haijafika au???!!!

tarehe ilifika Komba akaruka kiunzi, mahakama yalikuwa yamemtega--hakuwa na uwezo wa kukwepa kitanzi hiki, ndio maana ameamua kujisalimisha kwa Manji.
 
No sidhani kama zimeondoka!, kilichofanyika ni bail out tuu, kwa Manji kumlipia deni ili mali zisiuzwe na benki, out of that bail out, inawezekana Komba akaachia baadhi ya mali hizo preferably land kuifidia hiyo bail, out!.
Pasco.

mkuu, hata akiuza mali zake zote hazifiki 1.2 bilion. labda ajiuze yeye, mkewe na watoto ndipo hesabu itatimia.
 
Nimejifunza biashara na ulevi wa totoz ni kama ccm na cdm

ni ujuha kukopa fedha benki na kuzitumia fedha hizo kujivinjali na totoz! hili ni fundisho kwa wanaCCM wengine wenye tabia kama za Komba.
 
Komba kumbe ametoka msituni kuchimba dawa..kaja kupiga mnada mali zake, labda ameona bank wakipiga mnada itakuwa aibu akapiga mwenyewe..
mantiki si ni ile ile..
ikipigwa mnada inanunuliwa na akiuza mwenyewe pia inanunuliwa.
 
Back
Top Bottom