Yusuf Manji akamatwa kutokana na malimbikizo ya kodi Tsh 300 milioni, ofisi zake zafungwa


Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,647
Likes
51,682
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,647 51,682 280
Kampuni ya Udalali ya Yono (Yono Auction Mart) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Tawi la Temeke leo Oktoba 27 wamemkamata mfanyabiashara Yusuf Manji kutokana na kutolipa malimbikizo ya kodi anayodaiwa zaidi ya Tsh 300 milioni.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Yono, Scolastica Kivera alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo amesema kwamba mbali na kumkamata Manji, pia wamefunga nyumba ya kuhifadhia mali (godown) pamoja na Ofisi yake iliyopo kando ya barabara ya Nyerere ili alipe kodi anayodaiwa na Serikali.

Yono ambao ni wakala wa ukusanyaji wa madeni ya Serikali kupitia TRA, wamesema kwamba wanamshauri Manji alipe deni analodaiwa ili waweze kufungua majengo yake wanayoyashikilia kwani kinyume na hapo watapiga mnada mali zilizopo ndani ya majengo kwa idhini ya TRA ili waweze kufidia deni hilo.

Kivera ameeleza kwamba, hatua ya wao kushikilia mali hizo ni kumtaka Manji alipe deni analodaiwa.
 
M

mangatara

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2012
Messages
11,745
Likes
7,755
Points
280
M

mangatara

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2012
11,745 7,755 280
Amekamatwa kwa barua sio kwa pingu wakuu msihofu. Kichwa cha habari ni kukuvutia uisome thread tu. Akamatwe huku Barrick wanadaiwa matril na wakaitwa kukaa mezani na maji ya kunywa wakapewa! Utakuwa uharamia huu
 
kilambalambila

kilambalambila

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Messages
7,899
Likes
4,076
Points
280
kilambalambila

kilambalambila

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2013
7,899 4,076 280
Alipe tu yaishe
 
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Messages
8,424
Likes
13,549
Points
280
mitale na midimu

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2015
8,424 13,549 280
alipe tu kama anadaiwa. mbona aliwahi kutulipia bure kama 100M kuingia uwanjani bure, hiyo 300M sioni kama inamshinda.
 

Forum statistics

Threads 1,235,164
Members 474,353
Posts 29,213,561