Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,650
- 218,105
Pamoja na serikali ya Tanzania kutambua ugumu wa mzunguko wa biashara nchini humo kutokana na janga la Corona , na kupitia BOT imetoa maelekezo kwa benki zote kutoa nafuu ya marejesho ya madeni ya mikopo kwa wateja wake , ambapo baadhi ya benki nchini Tanzania ikiwemo Exim bank , ambayo imetoa likizo ya malipo kwa wateja wake wanaodaiwa kwa miezi mitatu kuanzia June hadi Septemba .
Lakini leo Maduka yanayozunguka stendi ya mabasi ya kusini kwenye eneo la Tandika yamefungwa na mmiliki wa jengo ambaye ni Manispaa ya Temeke , amewafungia milango wafanyabiashara ambao ni wapangaji wake kwa kuchelewa kulipa kodi kwa miezi miwili na wengine miezi mitatu , bila kujali ugumu wa biashara zao kutokana na corona , zipo pia taarifa za Manispaa hiyo kuanza kuwasaka waliochelewesha malipo ya kuhuisha leseni zao na ambao bado hawakupata leseni za biashara .
Si lengo langu kutetea wafanyabiashara wasiolipa bali ninaishangaa Manispaa kwa timing ya kichovu ya jambo lenyewe kutokana na hali halisi , wenzako wanatoa nafuu wewe unawakomesha watu wako ! haikuwa sahihi kwa sasa kuanza kuwahangaisha wajasiriamali kutokana na mambo yalivyo , Hali ni ngumu mno , na hasa kwa maeneo ya DSM ambayo baadhi ya wakazi wamekimbia na wengine wanakataa kurudi tena kwa sasa ili kujiokoa na corona .