Manispaa Sumbawanga lipeni fidia wenye mashamba viwanja mliviuza msiwalazimishe wamiliki kulipa fidia

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Mh. Waziri wa ardhi nakuomba ufuatilie mgogoro wa ardhi Kizwite manispaa ya Sumbawanga unaosababishwa na maafisa ardhi wala rushwa kwa kushirikiana na matapeli wa viwanja mimi ni mmoja wa wamiliki wa hivyo viwanja nilikinunua manispaa katika mradi wao wa upimaji viwanja.

Mwaka 2004 Manispaa iliwataa mashamba na kuwalipa fidia wahusika na ofisi ya mkuu wa wilaya ilihusishwa kusaini majedwali ya fidia kisha kupima viwanja na tukauziwa na kumilikishwa kwa hati milki ya miaka 66.

Limeibuka kundi la matapeli wanadai wazazi wao ambao eti ni marehemu hawakulipwa fidia mwaka 2004 maafisa ardhi wamekuwa wanatutaka wamiliki eti tuwalipe fidia wahusika wakati manispaa ndio iliyatwaa hayo mashamba na kutuuzia viwanja baya zaidi maafisa ardhi wanadiriki kutoa barua za kuwaruhusu hao matapeli waviendeleze hivyo viwanja huku wakijua vina wamiliki halali wenye hati tunakuomba mh.Waziri ingilia kati mgogoro huu unaochochewa na watendaji wako.
 
Hii shida ipo halmashauri ya mji makambako nina offa ya miaka 33 aridhi wanataka mimi ndo nielewane na mwenye kiwanja swali, walipima vipi kiwanja bila kufidia? Yaani ni matapeli wabobezi mimi nimepanga kumwona DC, Ikishindikana RC, ikishindikana waziri.
 
Hii shida ipo halmashauri ya mji makambako.nina offa ya miaka 33.aridhi wanataka mimi ndo nielewane na mwenye kiwanja.swali,walipima vipi kiwanja bila kufidia?yaani ni matapeli wabobezi.mimi nimepanga kumwona DC,Ikishindikana RC,ikishindikana waziri.
Ikibidi Mahakamani ndio Dawa yao
 
Back
Top Bottom