Mgogoro kati ya wamiliki Viwanja na maafisa ardhi Manispaa Sumbawanga

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Maafisa ardhi wanataka kuiingiza serikali kwenye mgogoro mkubwa na wamiliki wa viwanja wanaovimiliki kwa title deed za miaka 66 huko kizwite.

Maafisa ardhi wanashirikiana na matapeli wa ardhi wakiwadanganya kuwa mashamba ya marehemu wazazi wao hawakulipwa fidia wakati wa upimaji viwanja hivyo. Manispaa ilitwaa mashamba yao na kuwalipa fidia mwaka 2004 na majedwali ya fidia yapo ofisi ya dc wa sumbawanga.

Maafisa ardhi badala ya kujilidhisha kuwa hao wanaodai fidia ndio wamiliki sahihi kwa kutumia hayo majedwali wao wamekuwa wanawataka wamiliki halali kuviachia viwanja hivyo kwa hao matapeli kwa kisingizio cha kuwa manispaa haina fedha za kuwalipa fidia.

Ni jukumu la manispaa kutafuta fedha au viwanja mbadala ili kuwapa hao wanaodai fidia kama itakuwa imejiridhisha kupitia majedwali ya fidia ya mwaka 2004.

Kutokana na utendaji mbovu wa maafisa ardhi ni dhahiri wanashirikiana na matapeli kutaka kuwanyang'anya.

Viwanja wamiliki halali kinyume na sheria .Isitoshe kuna baadhi ya matapeli wamepewa barua za kuwaruhusu kuviendeleza viwanja hivyo huku wamiliki halali wana hati milki mikononi na wamegoma kuziachia mpaka mahakamani.
 
Mkuu wasalimie wale wa mazwi, majengo, chanji, sumbawanga wenyeji, bangwe, jangwani na kizwite.
 
Back
Top Bottom