Mangwea tangulia!

Mangwea tangulia!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Nafasi nachukua,shairi kukuandikia,
Albert Mangwea, uliyetangulia,
Asili ya Songea,mzaliwa wa Mbeya,
Mangwea tangulia!

Nilianza kukusikiliza,ili kukuelewa,
Mengi ukanifunza,hadi kunogewa,
Kwa zako stanza, zilizopangiliwa,
Mangwea tangulia!

Umeimba mambo mengi, kwa sanaa yatosha,
Tena yale ya msingi, UKIMWI kuelimisha,
MIMI ikawa shilingi, ujumbe kuufikisha,
Mangwea tangulia!

Kolabo ukafanya,na wenzako kukubali,
Wazembe ukawakanya, kwa lugha isiyo kali,
Utani ukaufanya, marafiki kila mahali,
Mangwea tangulia!

CNN na mikasi,nyimbo zako maarufu,
Zikakupatia nafasi, ya sanaa kali turufu,
Bila wasiwasi, hakuna uliyemkashifu,
Mangwea tangulia!

Kifo chako ugenini, funzo kubwa kwetu,
Ulikuwa safarini, kupigania wako utu,
Mengi sasa redioni, ulivyokutwa mfu,
Mangwea tangulia!

Pole kwa wazazi,ndugu na jamaa,
Pengo li wazi, marafiki wanashangaa,
Sasa tunayo kazi, kumpata anayefaa,
Mangwea tangulia!

Sisi tulikupenda, Mungu amekuhitaji,
Mema mengi umetenda, nje na ndani ya jiji,
‘Free-style ulipenda, kilikuwa chako kipaji,
Mangwea tangulia!

Mapungufu hukukosa, ni ubinadamu,
Hukuweza kutuasa, hatuwezi kulaumu,
Tunasamehe tangu sasa, na hilo ndilo muhimu,
Mangwea tangulia!

Lala salama Albert Mangwea! See you there my son!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Kaunga alikusikia, akashindwa kufikiria,
Umauti umekufikia, huku Smile anakulilia,
Hakuna mtu aliyezimia, ila Paloma anaugulia,
Mangwea tangulia!

WanaChitChat tunakuombea, mahali pema kuelekea,
Japo mwenzio kakufuatia, haina budi kuvumilia,
Mwanao ataangaliwa, shaka kabisa ondoa,
Mangwea tangulia.

Uchakachuzi unapoanzia

Erickb52 nakuhusia, Chocs kumsikia,
Chochote anachokuambia, ni vyema kumfanyia,
Mapochopocho kumnunulia, na upendo kumuonyeshea,
B52 nakuambia, natumaini hautomkimbia.

Mr Rocky angalia, njia unazokimbilia,
Mamndenyi anakulilia,weye wafurahi na Nivea,
Baba V anakuangalia, bila hata kukukemea,
Rocky kuwa makini, umshinde TUMAINI.

sosoliso nakuapia, Paloma kukuchukulia,
Khanga moja kunivalia, na macho hunilegezea,
Wowowo kunitingishia, na mwendo hunibadilishia,
Soso angalia, kabla sijakuingilia.

Shairi nalimaliza, japo nimewaumiza,
Mizaha nimeiendekeza, na ukweli kuwajuza,
Someni mkijiuliza, na pia kunijibiza,
Shukrani natanguliza, kumradhi kwa niliowakwaza.

Aisome Asprin, Slave, Bishanga, manoah, King'asti, Kongosho, Zamaulid, Queen Kan, kamtu33, Dark City, Safari_ni_Safari, Elli, Filipo na wengine nilioshindwa kuwataja.
 
Last edited by a moderator:

Dah saudari nimekusoma mkuu...namuombea class mate wangu alale mahala pema aisee(RIP Bro)
 
Last edited by a moderator:
Hahahaaaa fani imeingiliwa Wallah
Hata Saudari kawa mtunzi?
Wallh Mangwea pumzika kwa Amani Little Angel kuja huku
Pole zako tuzisikie,
Nawe Fidel80 unhyesho wako ut......

Mmmh kama vile nakosea sijui
Kaunga alikusikia, akashindwa kufikiria,
Umauti umekufikia, huku Smile anakulilia,
Hakuna mtu aliyezimia, ila Paloma anaugulia,
Mangwea tangulia!

WanaChitChat tunakuombea, mahali pema kuelekea,
Japo mwenzio kakufuatia, haina budi kuvumilia,
Mwanao ataangaliwa, shaka kabisa ondoa,
Mangwea tangulia.

Uchakachuzi unapoanzia

Erickb52 nakuhusia, Chocs kumsikia,
Chochote anachokuambia, ni vyema kumfanyia,
Mapochopocho kumnunulia, na upendo kumuonyeshea,
B52 nakuambia, natumaini hautomkimbia.

Mr Rocky angalia, njia unazokimbilia,
Mamndenyi anakulilia,weye wafurahi na Nivea,
Baba V anakuangalia, bila hata kukukemea,
Rocky kuwa makini, umshinde TUMAINI.

sosoliso nakuapia, Paloma kukuchukulia,
Khanga moja kunivalia, na macho hunilegezea,
Wowowo kunitingishia, na mwendo hunibadilishia,
Soso angalia, kabla sijakuingilia.

Shairi nalimaliza, japo nimewaumiza,
Mizaha nimeiendekeza, na ukweli kuwajuza,
Someni mkijiuliza, na pia kunijibiza,
Shukrani natanguliza, kumradhi kwa niliowakwaza.

Aisome Asprin, Slave, Bishanga, manoah, King'asti, Kongosho, Zamaulid, Queen Kan, kamtu33, Dark City, Safari_ni_Safari, Elli, Filipo na wengine nilioshindwa kuwataja.
 
Last edited by a moderator:
Ujumbe umetufika shaka mtimani ondoa, ngwea sio kwanza hilo twalijua, nami sio wamwisho kuiacha hii dunia, wengi watafua wala ardhi haitotosha, wimbowe wa kimya kimya,katoka tz kimya kimya, mpaka south kimya kimya, umauti umemfika kimya kimya hata rafiki yake hakujua.
 
aisee, humu ndani watu ni watoto sana,
hebu niamkie haraka sana..........
na kuanzia leo kila siku niwe nakuta umeniamkia, sawa?
Hahahaaaa
Shikamoo DADA FP !
 
Last edited by a moderator:
Kaunga alikusikia, akashindwa kufikiria,
Umauti umekufikia, huku Smile anakulilia,
Hakuna mtu aliyezimia, ila Paloma anaugulia,
Mangwea tangulia!

WanaChitChat tunakuombea, mahali pema kuelekea,
Japo mwenzio kakufuatia, haina budi kuvumilia,
Mwanao ataangaliwa, shaka kabisa ondoa,
Mangwea tangulia.

Uchakachuzi unapoanzia

Erickb52 nakuhusia, Chocs kumsikia,
Chochote anachokuambia, ni vyema kumfanyia,
Mapochopocho kumnunulia, na upendo kumuonyeshea,
B52 nakuambia, natumaini hautomkimbia.

Mr Rocky angalia, njia unazokimbilia,
Mamndenyi anakulilia,weye wafurahi na Nivea,
Baba V anakuangalia, bila hata kukukemea,
Rocky kuwa makini, umshinde TUMAINI.

sosoliso nakuapia, Paloma kukuchukulia,
Khanga moja kunivalia, na macho hunilegezea,
Wowowo kunitingishia, na mwendo hunibadilishia,
Soso angalia, kabla sijakuingilia.

Shairi nalimaliza, japo nimewaumiza,
Mizaha nimeiendekeza, na ukweli kuwajuza,
Someni mkijiuliza, na pia kunijibiza,
Shukrani natanguliza, kumradhi kwa niliowakwaza.

Aisome Asprin, Slave, Bishanga, manoah, King'asti, Kongosho, Zamaulid, Queen Kan, kamtu33, Dark City, Safari_ni_Safari, Elli, Filipo na wengine nilioshindwa kuwataja.

saudari.................utajibeua hahahaa
RIP Albert
 
Last edited by a moderator:
Umesahau kitu muhimu sana, shairi hili limetungwa . . . . na kuletwa kwenu na . . . .
 
Sio kwamba unakosea, ni wivu wanionea,
Mengi huniongelea, huku ukinisogelea,
Hata kufungwa cha Sea, serekali imemunea,
Hivyo sitaki ongezea, usije ukakolezea.
Duh heri nikae kimya... Paloma huyu jamaa kumbe ni mshairi
 
Last edited by a moderator:
Duh heri nikae kimya... Paloma huyu jamaa kumbe ni mshairi

malenga haswaaa...watu wana vipaji acha kabisa!
Hahahahaaaa!!!!! Paloma na Elli mnanifurahisha sana.
ujumbe.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom