Kaunga alikusikia, akashindwa kufikiria,
Umauti umekufikia, huku
Smile anakulilia,
Hakuna mtu aliyezimia, ila
Paloma anaugulia,
Mangwea tangulia!
WanaChitChat tunakuombea, mahali pema kuelekea,
Japo mwenzio kakufuatia, haina budi kuvumilia,
Mwanao ataangaliwa, shaka kabisa ondoa,
Mangwea tangulia.
Uchakachuzi unapoanzia
Erickb52 nakuhusia,
Chocs kumsikia,
Chochote anachokuambia, ni vyema kumfanyia,
Mapochopocho kumnunulia, na upendo kumuonyeshea,
B52 nakuambia, natumaini hautomkimbia.
Mr Rocky angalia, njia unazokimbilia,
Mamndenyi anakulilia,weye wafurahi na
Nivea,
Baba V anakuangalia, bila hata kukukemea,
Rocky kuwa makini, umshinde
TUMAINI.
sosoliso nakuapia,
Paloma kukuchukulia,
Khanga moja kunivalia, na macho hunilegezea,
Wowowo kunitingishia, na mwendo hunibadilishia,
Soso angalia, kabla sijakuingilia.
Shairi nalimaliza, japo nimewaumiza,
Mizaha nimeiendekeza, na ukweli kuwajuza,
Someni mkijiuliza, na pia kunijibiza,
Shukrani natanguliza, kumradhi kwa niliowakwaza.
Aisome
Asprin,
Slave,
Bishanga,
manoah,
King'asti,
Kongosho,
Zamaulid,
Queen Kan,
kamtu33,
Dark City,
Safari_ni_Safari,
Elli,
Filipo na wengine nilioshindwa kuwataja.