Mangula na Kinana mmejidhalilisha

Mangula na Kinana mmejidhalilisha

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Posts
3,429
Reaction score
6,393
Mzee Mangula na Kinana,

Mlifanya siasa za mkakati mkashinda chaguzi nyingi na chama chenu kikawa imara na kujipatia sifa za kutosha.

CCM ilianza kupoteza mvuto mlionekana nyie ndio tegemeo kubwa na mna uzoefu wa kutosha kuokoa jahazi lisizame.
Mkaombwa kurudi kwenye usukani wa chama mkakubali mkajiwekea mikakati ya namna ya kuendesha chama. Mkaomba mpewe timu ya ushindi mmepewa.

Swali je timu yenu ya ushindi imeshinwa kazi? Mmepokonywa kata 5, mmepata kura chache kuliko upinzani pamoja na kushinda kata nyingi.

Hii tafsiri yake chama kinazidi kuporomoka na hata vitongoji na vijiji vilivyofanya uchaguzi vingi vimeangukia upinzani.

Je hamuoni huu ni muda muafaka wa kuachia ngazi kabla mambo hayajawa mabaya zaidi?

Mnaweza kusema bado mnaweza kubadilisha hii trend kwa kufanya mabadiliko kwa kupindi kilichobakia. Kama mmeshindwa walau kunyakua hata kata moja ya CHADEMA au hata kijiji leo hii ni kitu gani kinakupa nguvu kwamba utaweza mwaka mmoja ujao?

Kumbukeni kwamba nguvu zenu(physical strength) zinapungua kila kukicha sababu ya uzee na dunia inabadilika kwa kasi sana kutokana na technologia. Na kwa umri wenu technolijia inawaacha. Je huu si muda muafaka mkawapa watu wengine wapange timu ya ushindi kuanzia sasa?

Kama mnadhani bado kuna uwezekano wa ushindi hapo mbeleni, je timu ya Mwigulu, Nape et al, unadhani itawafikisheni kwenye malengo.

Kulinda heshima yenu jiuzuluni muwape vijana ama wazee wengine waoneshe umahiri wao nyie mmbakie kuwa washauri.

Usione aibu kujiuzulu sasa maana aibu inayofuata ni kubwa kuliko ungejiuzulu sasa.
 
Tatizo kinana yupo bize muda wote kuhangaikia biashara yake ya yale ma nani hii ya wanyama wetu,huku maskini mangula akishindwa kujua aanzie wapi kutokana na aliyokuja kuyakuta aliporudi kutoka shambani alikokuwa akilima nyanya,mwigulu amejivisha u kapteni huku akiwaacha kina Nape bila kazi yoyote,kinana na mangula hawakubaliani kabisa na aina ya siasa anayoifanya mwigulu,ila pia hawana mtu mwingine wa kumtegemea kama mwenezi baada ya nape kuamua kukaa pembeni na kumwachia mwigulu aendeshe siasa zake za mauaji,mwigulu ni janga kwa ccm.
 
Kumbe ccm hawajajua nani adui yao! mbona CDM wanajua kuwa msingi wa ushindi wao wa kuongeza kata kutoka 5 hadi 10 ni uzezeta wa mpiga debe wa ccm MWIGULU! anapanga kuua kumbe ndio anapaisha umaarufu wa CHADEMA.Ni sawa kumpiga teke chura ukidhani umemkomoa kumbe umemwongezea hatua. kata tano siyo mchezo.Wenye akili wote ndani ya chama cha mapinduzi wameamua kukaa kimyaa waone mwisho wa MWIGULU anayejifanya kuwa yeye ni katibu mkuu, mwenyekiti na chochote unacho weza kudhani ndani ya chama cha ccm.hakuna line ya operation.
 
ccm wana matatizo mengi lakini ukiangalia mfano, mwenyekiti alishauriana na nani kumpata naibu katibu mkuu? alishauriana na nani kumpata katibu mwenezi? ni nani alimshauri mwenyekiti kuwakaribisha kwa mbwembwe wale vijana waliotoka cdm pale dodoma wakati wako vijana waliosotea chama kwa moyo wao wote miaka nenda rudi!
Tutaishia kusema kuwa mwenyekiti anashauriwa vibaya lakini hapa ndipo tatizo lilipo ndugu zangu. Watu wanahubiri chuki za kikabila, kidini na ukanda huku wakichekewa tu!
 
Wakuu kwa hali ilivyo sasa Nchini CCM hata iongozwe na nani hakuna jipya zaidi ya kupoteza kata kila panapotokea uchaguzi,wazee wamestuka,wamama wameanzakuona thamani ya kura dhidi ya khanga feki,vijana ndio usipimime.......CCM hawana pa kushika,muda si mrefu jeshi la polisi nalo litastuka na hapo ndio utakuwa mwisho wa kiazi kikuu CCM.
 
CCM majembe wewe! wanaendelea kutupa kata majimbo mwisho nchi kwa chadema.
 
Tatizo kinana yupo bize muda wote kuhangaikia biashara yake ya yale ma nani hii ya wanyama wetu,huku maskini mangula akishindwa kujua aanzie wapi kutokana na aliyokuja kuyakuta aliporudi kutoka shambani alikokuwa akilima nyanya,mwigulu amejivisha u kapteni huku akiwaacha kina Nape bila kazi yoyote,kinana na mangula hawakubaliani kabisa na aina ya siasa anayoifanya mwigulu,ila pia hawana mtu mwingine wa kumtegemea kama mwenezi baada ya nape kuamua kukaa pembeni na kumwachia mwigulu aendeshe siasa zake za mauaji,mwigulu ni janga kwa ccm.

How about Shonza and Mtela? Nao hawawezi kuokoa jahazi?
 
Tukubali Mwigula,Nape;Wasila;na waziri mkuu Pinda kauli zao zinaporomosha CCm kwa haraka sana wajue uonevu wao kwa wananchi watu hubaki na hasira na huruka ya binamu huegemea kea yule anayeonewa ndivyo ilivyo kwa Cuf Pemba ndicho kilicho tokea Arusha
 
Ccm inakoelekea siko, na sisi tunaiombea ife kifo cha mende bila kuleta vita katika nchi hii, hao wazee wamekuja kujidhalilisha, kinana alijifanya kastaafu siasa kumbe alikuwa anataka abembelezwe kwa kacheo ili arudi.mangula angekuwa mtu wa aibu wala asingekubali hiyo nafasi, alidhalilishwa vibaya sana pale iringa mjini baada ya kupigwa chini uenyekiti wa mkoa, na kama vile haitoshi baada ya kupewa madaraka aliyonayo sasa nape akaanza kupita kila kona na kudai eti wao wana demokrasia kwa kuwa wampa cheo mkulima aliyechoka kabisa kutoka njombe yaani mangula.
 
tatizo kinana yupo bize muda wote kuhangaikia biashara yake ya yale ma nani hii ya wanyama wetu,huku maskini mangula akishindwa kujua aanzie wapi kutokana na aliyokuja kuyakuta aliporudi kutoka shambani alikokuwa akilima nyanya,mwigulu amejivisha u kapteni huku akiwaacha kina nape bila kazi yoyote,kinana na mangula hawakubaliani kabisa na aina ya siasa anayoifanya mwigulu,ila pia hawana mtu mwingine wa kumtegemea kama mwenezi baada ya nape kuamua kukaa pembeni na kumwachia mwigulu aendeshe siasa zake za mauaji,mwigulu ni janga kwa ccm.
inaniuma roho ninposoma haya na kukumbuka kuwa mwigulu ni mbunge kule nilkozaliwa lah!
 
Hali ndani ya CCM ilipofikia ni kwa wao kukubali kwamba muda WA kuwa wapinzani umefika,waachie madaraka kwa wengine kwa amani ili wajipange taratibu. Makundi humo ndani ni mwiba na hakuna aliye tayari kukubali kushindwa na hili ndo tatizo hata utekelezaji WA ilani yake ni WA kusuasua,wanahujumiana wao kwa wao lakini mwishoni inatuumiza watu WA chini kwani miradi mingi haitekelezwi na hela inapotea kusikojulikana.
 
Tatizo kinana yupo bize muda wote kuhangaikia biashara yake ya yale ma nani hii ya wanyama wetu,huku maskini mangula akishindwa kujua aanzie wapi kutokana na aliyokuja kuyakuta aliporudi kutoka shambani alikokuwa akilima nyanya,mwigulu amejivisha u kapteni huku akiwaacha kina Nape bila kazi yoyote,kinana na mangula hawakubaliani kabisa na aina ya siasa anayoifanya mwigulu,ila pia hawana mtu mwingine wa kumtegemea kama mwenezi baada ya nape kuamua kukaa pembeni na kumwachia mwigulu aendeshe siasa zake za mauaji,mwigulu ni janga kwa ccm.

jk anamkubali sana mwigulu nchamba.alifurahi sana alipoichanachana bajeti ya chadema bungeni.lakini wasomi wanaomfuatilia nchamba wanasema huyu ni "MAJANGA"!KUJENGA USHAHIDI FEKI WA KUKIONYESHA CDM KUWA CHAMA CHA KIGAIDI UTAMTOKEA PUANI.KWELI CDM NI CHAMA CHA KIGAIDI????????????????????????????????????????????????HATA MTOTO WA SHULE YA MSINGI HATAKUBALIANA NA HOJA HII.!!!!
 
Wana jf

CCM chini ya Mzee wa pembe za ndovu imepanga mipango mikali sana jamaa wa ndani sana amenitonya kama ifuatavyo:
1. Wanasema kuwa lazima CHADEMA ife kabla ya zoezi la kuteu wagombea wa uraisi na ubunge kutoka vyama kwa uchaguzi 2015 halijafika wala kukaribia, kwa kuwa eti ikifikiwa wakati huo na CDM kikiwa na nguvu iliyonayo sasa hivi, eti
CCM itasambaratika yenyewe na ndio itakuwa mwisho wake.Hii wanasema ni kutokana na mgawanyiko uliopo sasa hivi,Kwa mtazamo huo jamaa kaniambia wamekuja na plan A na B. Plan A ni kuwabambika kesi viongozi wote wa CHADEMA ili wawe wanahangaika na kesi na fedha zote ziishie kwenye kesi wakose muda wa kufanya mikutano ya kushawishi wananchi,kuongea na wamiliki wa vyombo vya habari kupunguza kabisa kuandika habari ya CDM na kuanzisha vipindi kwenye redio wakati wa asubuhi na jioni vyenye lengo ya kuzunguzia amani kwa lengo la mlango wa nyuma wa kuiponda CHADEMA. Kuwatumia baadhi ya viongozi wa upinzani kuiponda chadema hasa class mate wangu pale UDSM Mbatia. Jamaa akaniambia kama plan A itashindikana plan B watadili na Dr Slaa moja kwa moja watadili naye vipi hakunitonya. Tafakari chukua hatua.
 
Kwa hiyo kwa Mbatia kuipinga Red Brigade ina maana ameanza kutekeleza mkakati huo?
 
Back
Top Bottom