Mangula, Dr. Slaa na Changamoto za Ufisadi Tanzania

JingalaFalsafa,

Ni kweli tuna utamaduni wa kuja na maazimio mengi lakini yasiyokuwa na utekelezaji; Kwa mtazamo wako, katika suala la formation of our own state tuanzie wapi? Kwa mfano, mimi sina woga wa kujulikana jina langu halisi na sura yangu halisi licha ya vitisho na matusi ya hapa na pale; Sasa kwa wale ambao bado waoga, inabidi watoke huko, hasa ikiwa nia ni kukosoa na kujenga hoja kwa kuweka taifa mbele, siasa nyuma, na maslahi binafsi nyuma zaidi; Kwa vile mimi tayari nipo wazi, unanishauri nifanyeje zaidi?

Wapo wanaosema mabadiliko ya kweli ni lazima yapiganiwe nje ya CCM; Kuna ukweli kwa kiasi gani ndani ya hoja hii lakini the truth is not absolute but relative; huko kwingine, je baada ya harakati za mabadiliko kufanikiwa, kuna guarantee gani kwamba sauti na mawazo yetu yataendelea kusikilizwa? Tatizo langu lipo hapo tu
 
Last edited by a moderator:
Kobello amekazania sana kuuliza swali la atafanyeje? Napenda niamini kwamba Kobello aliwahi kuwa kiongozi katika taasisi ndogo japo shule. Fanya utafiti mdogo kwa kuangalia namna ambavyo walimu na wanafunzi wanaweza kuwa na tabia zinazoendana na mkuu wa shule. Kama mkuu wa shule ataweka sheria na taratibu za uendeshaji wa shule na akazisimamia kwa kuanza kuwawajibisha watendaji wake, nakuhakikishia watendaji wake hawatamfumbia macho yeyote watakayegundua kwamba amekiuka sheria na taratibu za aina yoyote. Ndiyo maana shule inayofanya vibaya hubadilishwa mwalimu mkuu na si walimu wote.
Wrong!!!!

Analogy uliyoitumia inatia moyo lakini haina maana. Rais ni mwakilishi wa wananchi kitaifa, wabunge ni wawakilishi wa wananchi kimajimbo na pia kuna mahakimu, majaji na waendesha mashtaka. Hawa wote wana nguvu sawa na independent tofauti na shule ambazo mwalimu amepewa mamlaka ya wazazi (dictator). Wazazi, kama alivyo principal ni top down no discussion, no meeting halfway kind of order .... huwezi kuleta hiyo kwenye 40million plus democracy, it's just naive.

Ndiyo maana Mwalimu Nyerere alisema kuwawajibisha mawaziri hakutoshi, ukimzuia trafiki kupata rushwa, watahakikisha na hao mabosi wao hawapati rushwa .... tunataka mwanasiasa atayetuambia kuwa sisi watanzania tumeoza, ubongo wetu unavyofikiria ni tofauti na matarajio tunayotegemea, hakuyna mesiah atayezuia rushwa ....NAKUBALIANA ASILIMIA 100 NA MCHANGIAJI ANAYETAKA MAGEUZI YA KIFIKRA.
 
Wrong!!!!

Analogy uliyoitumia inatia moyo lakini haina maana. Rais ni mwakilishi wa wananchi kitaifa, wabunge ni wawakilishi wa wananchi kimajimbo na pia kuna mahakimu, majaji na waendesha mashtaka. Hawa wote wana nguvu sawa na independent tofauti na shule ambazo mwalimu amepewa mamlaka ya wazazi (dictator). Wazazi, kama alivyo principal ni top down no discussion, no meeting halfway kind of order .... huwezi kuleta hiyo kwenye 40million plus democracy, it's just naive.

Ndiyo maana Mwalimu Nyerere alisema kuwawajibisha mawaziri hakutoshi, ukimzuia trafiki kupata rushwa, watahakikisha na hao mabosi wao hawapati rushwa .... tunataka mwanasiasa atayetuambia kuwa sisi watanzania tumeoza, ubongo wetu unavyofikiria ni tofauti na matarajio tunayotegemea, hakuyna mesiah atayezuia rushwa ....NAKUBALIANA ASILIMIA 100 NA MCHANGIAJI ANAYETAKA MAGEUZI YA KIFIKRA.
Hata mimi naunga mkono mageuzi ya kifikira, lakini tunaanzia wapi? Nimeshakuwa kwenye researches nyingi sana zinazolenga kuwaendeleza wananchi vijjijni na kuboresha ufundishaji mashuleni. Nime-initiate project nyingi ambazo baada ya muda fulani huwa nazifanyia evaluation (sustainability study/impact study).

Wengi wa walimu na wanavijiji huwa hawa-implement hizo new innovations. Na sababu kubwa kabisa ambayo wananchi/walimu wanaitoa ni kutowajibika kwa uongozi. Hawa watu wa chini wanawasilikiliza sana viongozi wao ndugu zangu, naomba mfahamu hilo. Ni kujidanganya kabisa, kuendelea kuamini kwamba wananchi from no where watabadili fikra na kudhani kwamba sasa wanatakiwa kuikataa rushwa kama viongozi wao hawatalisema na kulionyesha kwa vitendo jambo hilo. There must be some initiatives, and those initiatives cannot be broght by just a mere person like me. Ni lazima awe ni mtu mwenye mamlaka na anayeaminiwa na kuheshimiwa. Viongozi wawaelekeze wananchi rushwa ni nini? Ni vitu gani na mazingira gani yanaweza kusababisha rushwa wakiona hayo wafanye nini, na waelezwe matokeo ya kutoa rushwa au kupokea ni nini?

Mchambuzi ameongelea suala la wananchi kupoteza imani kwa serikali yao. Hapo ndo pana shida. Kama wananchi wangekuwa na imani na serikali yao, isingekuwa shida kwa wananchi kuikataa rushwa. Sidhani kama wengi wetu tunaipenda, but kwa kuwa hatuoni anayeonyesha nia ya dhati kuikataa, na kwakuwa tunaamini kwamba hata tukiirepoti hakuna atakayeishughulikia, basi tunaamua kunyamaza au na sisi kuamua kucheza ngoma wanayocheza wenzetu. Based on this explanations, idea ya mabadiliko ya kifikira mnayosema itokane na wananchi is as well a naive idea. Kwa kuwa mabadiliko hayawezi tu kuibuka from no where. Ni lazima awepo initiator, that is why mimi bado naamini katika maamuzi na msimamo wa kiongozi wa juu wa serikali.

Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania utawala wa kidemokrasia siyo effective sana, hasa pale linapokuja suala zima la kubadilisha na ku-implement some policies ambazo tayari zipo kwenye damu za watu.

Umetoa mfano wa trafic polisi kwamba akizuiwa kuchukua rushwa basi hata wakubwa wake wataacha. You are wrong! The reverse is true! kama wakubwa wa trafic wakiacha kuchukua rushwa basi wataweza kummonitor huyu mdogo kuhakikisha hachukui rushwa. The same applies kwa wakuu wa idara, taasisi hadi mawaziri. Kama mkuu wa idara hachukui rushwa, katu hatakubali mfanyakazi ndani ya idara yake achukue rushwa halafu amfumbie macho.

Nilichojifunza mimi kutoka kwenu ni kwamba we are in a two antagonistic types of schools of thoughts. While I believe in top-down leadership approach, you believe in bottom-up leadership approach ambayo for years now it has not worked. Hayo mabadiliko ya fikra yalikuwa wapi kutokea tangu miaka ya 90 rushwa ilipoanza kushamiri nchini, na hadi leo hali yake imekuwa mbaya zaidi, na bado tunataka tuendelee kujiaminisha kwamba hiki kizazi cha nyoka siku moja kitakuja kiwe na mabadiliko ya kifikra. This will never work my brothers!

You are talking about the legislatures: rais, mbunge, mahakama etc. Labda kwa katiba ijayo, tunaweza kuwa na kitu cha tofauti. Lakini kwa katiba ya sasa, na utendaji wa sasa, Rais yupo above all the other legislative bodies. Mara ngapi bunge limemwagiza Rais kutekeleza baadhi ya mambo na hakufanya hivyo? Bunge lilishamwagiza Rais amfukuze kazi Mwanyika, Hosea, Luhanjo etc ni wapi alitekeleza? Na mambo yalibaki kama yalivyo. Mara ngapi mahakama imepindisha sheria na taratibu kutokana na maagizo ya mamlaka za juu? Mara ngapi mahakama imetoa hukumu na Rais akatoa msamaha kwa wafungwa? Rais is above all, huo ndiyo uhalisia wa mambo.

Ndiyo maana nasema rais ambaye yupo serious, anaweza kulipunguza kama si kulimaliza kabisa tatizo la rushwa. Mbona Mkapa miaka miwili ya mwanzo alifanikiwa sana kuipunguza rushwa ile iliyokuwa imeshamiri wakati wa utawala wa Mwinyi? Ninachosema inapothibitika mtu amekula rushwa, bila kujali cheo chake; asiwepo wa kufumbiwa macho hata kama ni waziri aliyepo madarakani amekula rushwa, avuliwe uwaziri siku hiyohiyo na kuwekwa rumande kusubiri kesi yake. Unafikiri kama ikitokea japo waziri mmoja tu akafanyiwa hivyo, ni nani huko chini atakayefanya utani?
 
Lukolo,

Thank you for sharing your experience kuhusu hali halisi ilivyo huko kwenye jamii per your visitation kama mtafiti na mambo kama hayo; Tunahitaji sana kusikia uzoefu wa namna hii; Pia nimependa hoja yako kwamba kinachoendelea baina yetu ni utofauti wa mtazamo, hasa schools of thought, kwa upande mmoja wewe na naamini wengine wapo, mkiamini juu wa umuhimu wa top - down approach katika kupata ufumbuzi wa tatizo la rushwa, huku mimi na wengine tukiamini katika bottom - up approach kufanikisha hilo;

Kimsingi, mimi mtazamo wangu ni kwamba people should be put at the centre, not be treated from the periphery; Muhimu zaidi ni kwamba, naamini real change comes from the grass roots, not from above; It has to be initiated at the bottom it has to be well understood at the bottom, and it has to be implemented in the bottom - kwani key and primary stake holders wa mchakato huu ni the WATU wenyewe; Kwa kifupi, any fight against corruption needs grassroots support ili ifanikiwe; muhimu hapa ni kwamba there has to be a sense of ownership of the policies miongoni mwa jamii; to me thats the bottom line;
 
JingalaFalsafa,

Ni kweli tuna utamaduni wa kuja na maazimio mengi lakini yasiyokuwa na utekelezaji; Kwa mtazamo wako, katika suala la formation of our own state tuanzie wapi? Kwa mfano, mimi sina woga wa kujulikana jina langu halisi na sura yangu halisi licha ya vitisho na matusi ya hapa na pale; Sasa kwa wale ambao bado waoga, inabidi watoke huko, hasa ikiwa nia ni kukosoa na kujenga hoja kwa kuweka taifa mbele, siasa nyuma, na maslahi binafsi nyuma zaidi; Kwa vile mimi tayari nipo wazi, unanishauri nifanyeje zaidi?

Wapo wanaosema mabadiliko ya kweli ni lazima yapiganiwe nje ya CCM; Kuna ukweli kwa kiasi gani ndani ya hoja hii lakini the truth is not absolute but relative; huko kwingine, je baada ya harakati za mabadiliko kufanikiwa, kuna guarantee gani kwamba sauti na mawazo yetu yataendelea kusikilizwa? Tatizo langu lipo hapo tu
Nakupongeza kwa hilo, ingawa sijui moyo huo unaupata wapi? ... Kama wote tungekuwa na nia ya kuwaweka madarakani viongozi wasiopenda rushwa, ninaamini viongozi karibu asilimia 99 waliopo leo wasingekuwa hata kwenye political game ya Tanzania.
Kuhusu mabadiliko ya ukweli kupiganiwa nje ya CCM, nakubali asilimia 100, ila pia yapiganiwe nje ya vyama vya siasa. Kama kasheshe anayoipata Morsi ingeweza kuletwa Tanzania ... basi hawa viongozi wangeshika adabu zao.
Hakuna mtu atayetuletea hili, uongozi wa nchi unareflect wananchi. Huwezi kuwa dictator Marekani au England. Huwezi kutawala miaka 20 Tanzania au kenya ila Rwanda na Uganda unaweza. Simply because the people are cool with it, if they were not, Museveni asingekuwa madarakani ... angeua as many as possible but at the end of the day watu wangepata chao.

Rushwa imekithiri Tanzania, kupewa fomu ya mirathi tu ni elfu hamsini mpaka laki ... ukiwatishia kuwa najuana na jaji fulani basi wanakwambia tuna foleni kubwa ... wakati wenzetu unajaza online, unapewa confirmation number na date ya kukutana na jaji..... we're just so corrupted, it stinks.
 
JingalaFalsafa

Let me agree with you kwamba vyama vya upinzani havina fikra mpya. Wala hakuna taasisi yenye uwezo wa kuleta fikra mpya. Then tell us where will these new thoughts come from? What will be the source, who is going to pioneer them?

Sio Upinzani tu, bali ni Taasisi zote! Namaanisha kuwa, FIKRA MPYA zile ambazo si za Ki-azimio la Zanzibar, kama zipo basi zipo kwa mtu mmoja mmoja, hazijafikia ngazi ya Taasisi! Kwani leo hii karibia Taasisi zote zinaongozwa na kufungwa na Sera na Kanuni za AZ, namaanisha hivi, sera, kanuni, itikadi, desturi, falsafa, tamaduni, n.k za taasisi zetu za leo, zimezaliwa kutoka AZ. Si chama tawala wala pinzani, vyote ni zao la AZ. Sasa, niulize labda...ni lini mzoga wa uvundo ukatoa kimfaacho mtu kutia kinywani mwake? UMIZA KICHWA, MAMBO SIO RAHISI TUZANIAVYO!
Tuachane na HULKA zetu, tugeukie MANTIKI ya mambo tutajenga FIKRA MPYA. Kichwa chako na changu ndimo zinakopatikana fikra hizo! Tukishazipata sisi wenyewe ndio tutakaozipigania, si mwingine ila ni wewe mwenyewe!
FUNGUA FIKRA ZAKO, jiweke katikati ya mstari, pasi kuegemea upande wowote, si wa dini ama siasa, wala utamaduni na mazoea, HOJI kile ulichosikia, ulichohisi, ulichoona, au kuki-experience katika maisha yako ya kila siku, pima ufaida na uhasara wake, na hiyo ndio MANTIKI. Ikuongoze sasa ufanye nini au usifanye.
Mungu wetu anaita!
 
Last edited by a moderator:
Lukolo,

Thank you for sharing your experience kuhusu hali halisi ilivyo huko kwenye jamii per your visitation kama mtafiti na mambo kama hayo; Tunahitaji sana kusikia uzoefu wa namna hii; Pia nimependa hoja yako kwamba kinachoendelea baina yetu ni utofauti wa mtazamo, hasa schools of thought, kwa upande mmoja wewe na naamini wengine wapo, mkiamini juu wa umuhimu wa top - down approach katika kupata ufumbuzi wa tatizo la rushwa, huku mimi na wengine tukiamini katika bottom - up approach kufanikisha hilo;

Kimsingi, mimi mtazamo wangu ni kwamba people should be put at the centre, not be treated from the periphery; Muhimu zaidi ni kwamba, naamini real change comes from the grass roots, not from above; It has to be initiated at the bottom it has to be well understood at the bottom, and it has to be implemented in the bottom - kwani key and primary stake holders wa mchakato huu ni the WATU wenyewe; Kwa kifupi, any fight against corruption needs grassroots support ili ifanikiwe; muhimu hapa ni kwamba there has to be a sense of ownership of the policies miongoni mwa jamii; to me thats the bottom line;
I completely agree with you in this sense. Sina tatizo kabisa. Hata katika masuala ya kuibua new innovations katika jamii tunasisitiza umhimu wa community ownership ya hiyo innovation. lakini hakuna innovation inayokuja by accident. Innovations zinakuwa initiated ili kumaliza tatizo fulani. Na hicho ndicho ambacho ninakisimamia toka mwanzo. Ni nani anayetakiwa kuinitiate hizo new ideas? Nafikiri swali hili pia linamhusu JingalaFalsafa. Idealy, naamini kwamba ni lazima awepo kiongozi wa kuanzisha mjadala. Na kiongozi huyo hawezi kuwa wewe au mimi kwa kuwa hatuna influence kwa jamii. No body will listern to us, na pia mimi na wewe hatuwezi kusimama na ku-initiate mikakati ya kupambana na rushwa ilihali Rais wa nchi anaimendea hiyo rushwa. You cant survive!
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa,

Nakubaliana na hoja yako juu ya umuhimu wa FIKRA MPYA; Nilijadili kidogo hili awali lakini umeliweka vizuri zaidi, hasa kwa kuliweka katika muktadha wa FIKRA;

Kwa kweli moja ya sababu kubwa kwanini watanzania maskini ni kutokana na UMASKINI WA FIKRA; Umaskini wa fikra ni tatizo la kiakili, haina tofauti kubwa sana na hali ya kukubali kuishi kama mtumwa; Mwathirika ana perceive maisha kama ni hopelessness, yamefungwa, na ni beyond recovery; Kwake yeye, umaskini ni suala la kawaida katika maisha na mara nyingine, umaskini unaweza kuwa kitu cha kuvutia kwani kinamjengea maisha ya kuhurumiwa na kusaidiwa na wengine;

Watu wenye ugonjwa huu ni mabingwa wa kulaumu wengine kwa miseries zao, hawana inward orientation kuhusu umaskini bali outward orientation, kwa mfano, umaskini wake unatokana na kulelewa na mzazi mmoja au kulelewa vibaya, au unatokana na ushirikina, au unatokana na nguvu za waliofanikiwa kimaisha zaidi yake;

Watu wa namna hii pia ni jadi kwao kuwalaumu wanasiasa kwa kila jambo, hata mvua zikichelewa kunyesha, sio kitu cha ajabu kuilaumu serikali; Wakitokea nzige au mafuriko, pia lawama kwenda kwa serikali sio kitu cha ajabu; kwa watu wa namna hii, external environment ndio yenye majibu kwa kila madhaifu yao, hasa serikali au wanasiasa;

Sababu zinazopelekea Umaskini wa Fikra ni Zipi?

Ni vingi lakini muhimu kwanza ni malezi; wagonjwa wa namna hii mara nyingi wamerithi ugonjwa huu kutoka kwa wazazi wao ambao waliwalelea katika mazingira ya kukubali maisha kama yalivyo, kwamba mungu ndio mweza wa yote, aliyekunyima wewe, amenipa mimi, na imani za namna hiyo; Wagonjwa hawa, wengi wao wakiwa watoto huwa wanafundishwa na wazazi wao hata ikibidi to exaggerate umaskini wao ili iwe rahisi kwa wao kuonewa hurumu na wenye uwezo na kupata misaada mbalimbali;

Sababu ya pili ni political factors, na hii inahusiana sana na mjadala ulio mbele yetu; Jamii kama ya Tanzania kwa mfano, zipo sehemu ambazo tangia uhuru hawajui maana ya uraia ni nini, au taasisi za kiraia ni zipi; Wao wanajua tu kwamba Kabila lao ni Kabila fulani, mipaka ya maeneo yao tangia enzi za mababu ni ipi, kwa mfano mashamba yao – na hawana habari kwamba shamba lao linapakana na mkoa tofauti kiutawala au hata nchi nyingine; Wengi wa watu katika jamii hii will never become official citizens wa Tanzania kwani baada ya uhuru, tulirithi colonial state, na kuanza state consolidation bila kwanza ya kuwafanya watanganyika wale kuwa raia rasmi wa Tanzania; badala yake walikusanywa kusanywa tu ovyo ovyo kama jamii vijijini na kuanza kupewa somo la itikadi ya chama, huku wakipewa huduma za kijamii bure, and in return, wakawa wanalisha urban elites kwa mazao yao na pia kulima for exports za kuendesha bureaucracy na kuweka law and order mijini;

Jamii za namna hii hazikutendewa haki na serikali baada ya uhuru kwani nyingi, hadi leo hazijui Maendeleo ni kitu gani, na hawana habari kwamba kwamba Maendeleo ni haki yao ya kikatiba; wanachoona wao ni kodi zinakatwa kwenye mazao yao, na wanaheshimu tu kwani hata machifu walifanya hilo; Hata hiyo katiba hawajui ni kitu gani, na ndio maana sio kitu cha ajabu kusikia kwamba wengine wanakuja na maoni kwamba kwenye katiba mpya, iwepo sala maalum ndani ya katiba ya kuombea taifa lipate mvua; Jamii za namna hii ni waathirika wa ufisadi wa miaka nenda, miaka rudi ambao umechangia sana umaskini wao kwa miaka zaidi ya hamsini, hivyo kizazi hadi kizazi to perceive kwamba umaskini ni suala la kawaida, kwani mungu ndiye mweza wa yote;

Sababu nyingine zinazochangia umaskini wa fikra ni pamoja na lack of exposure, illiteracy n.k;

Mwalimu Nyerere alijitahidi kubadilisha hali hii, hasa pale alipo declare kwamba Umaskini, maradhi na Ujinga ni Maadui watatu wa Maendeleo; lakini kwa bahati mbaya, jitihada zake hizi hazikufanikiwa sana kwa sababu mbalimbali ambazo kwa ujumla wake, wengi wetu tunazitambua;

Kama mtakubaliana nami katika hayo hapo juu, nadhani pia mtakubaliana nami kwamba poverty eradication MUST begin with the Mind; Pia, kama inakubalika kwamba Maadui watatu wa Maendeleo ni Umaskini, Maradhi na Ujinga, basi UJINGA ndiye Shetani mkubwa kuliko wengine; Hii ni kwa sababu, Ujinga ndio unapelekea matatizo mengine kama umaskini na maradhi kushamiri; Tukitatua ujinga, haya mengine yatajitatua yenyewe; Kwa mfano:

Ignorance/ujinga, unapelekea baadhi ya watanzania kuendelea kuishi katika maeneo yaliyojaliwa makaa ya mawe, upepo wa kasi, maporomoko ya maji, na vitu kama hivi, lakini kwa wao kuishi bila umeme au kukosa ajira ambayo ingetokana na viwanda vinavyotegemea umeme, kwao, ukosefu wa umeme ni suala la kawaida tu na hawaoni sababu yoyote ya kuanza ku-protest; lakini pia hawaoni tatizo kwa maeneo yao kuzalisha Umeme ambao unasafirishwa moja kwa moja kwenda mijini, huku wao wakiendelea kuishi katika kiza; Kwa vile ni wajinga, hilo kwao sio tatizo;

Pia ujinga unapelekea baadhi ya watanzania wanaoishi katika maeneo yenye rasilimali nyingi kama vile Tanzanite, Dhahabu n.k, kuona ni sawa kuishi maisha ya kimaskini wakati wageni wanaendelea kunufaika na kujitajirisha kwa wingi huku wakiwawekea wanasiasa fedha za asante kwa kuchakachua wenyeji, kwenye mabenki ya uswisi; Kwa wenyeji hawa, kuambulia vibara bara vya vumbi ambavyo mvua zikinyesha havipitiki, wakijengewa kisima cha maji, wakijengewa kishule cha ovyo ovyo kisochokuwa na vitabu, madawati na Walimu, kwa vile wao ni wajinga, Munga awape nini zaidi;

Ujinga pia unapelekea baadhi ya watanzania kudhoofika kiafya kutokana na kukosa madawa huku mapori yao yakimilikishwa kwa wageni, tena kwa patents za miaka hata hamsini, hivyo kuzuia hati miliki kwa watanzania, huku madawa haya yakifaidisha mataifa ya nje na pia watanzania wachache wenye uwezo huko mijini; Lakini kwa vile wao ni wajinga wa kupindukia, hili ni sawa tu, kwani mungu ndiye mweza wa yote, ndugu au jamaa akifariki, Bwana Alitoa, na Bwana akatwaa;

Wajinga kazi yao kubwa ni kulaumu wanasiasa kwa yote, lakini ni wajinga hawa hawa ambao wanasahau shida zao za kudumu kwa vijizawadi vya muda mfupi kama khanga, pombe, fulana n.k, wakati wa chaguzi za siasa i.e. short term gain at the expense of long term loss; kwa wajinga hawa, vijizawadi hivi ndio haki yao ya msingi kwani kwa wao, rewards are supposed to be immediate, ngoja ngoja uhumiza matumba, na pia uhai wa kesho anaujua mungu pekee; Kwa wajinga hawa, ufisadi ni njia sahihi tu ya kusaidia wanasiasa ili na wao wawasaidie kwa vijizawadi, badala ya fedha za umma kutumika kuwekeza in economic growth katika maeneo yao; iwapo unagombea siasa katika maeneo ya wajinga hawa, Watakuona wewe ni mwendawazimu wa kupindukia iwapo utaenda na Vipeperushi juu ya jinsi gani utaenda kupigania maslahi yao bungeni, hasa kodi zao kwa manufaa yao, badala ya kuja na Vipeperushwa na kumaliza mchezo;

Hakika tunahitaji FIKRA MPYA, kwani Wajinga ndio Waliwao;
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wangu Mchambuzi:

Naomba ni kujibu hivi....
1. Juu ya wapi pa kuanzia katika Re-formation of our own state. Ilishasemwa bila kujitambua wenyewe kwanza ni kazi bure, bila kubainisha tulivyo na tupaswavyo kuwa mbeleni ni kazi bure! Binafsi sitaacha kuamini kuwa tunahitaji kupata FALSAFA/ITIKADI YA TAIFA kwanza, huo ndio utakuwa msingi na imani yetu ya kwanza tutakayotakiwa kuifuata, aidha kwa lazima au laa!

Itapaswa kutuambia sisi ni nani? Tupo wapi? Na tunataka kwenda wapi? Na kiaje tutafikia huko? FALSAFA YA TAIFA ndiyo ya kutuongoza katika mabadiliko yoyote yale tuyatakayo, iwe ya kitamaduni, kiuchumi au kisiasa! Leo hii hilo halipo, tupo tu kusikiliza NGURUWE WEUPE wanatuambiaje nasi tutekeleze, kwa madai Eti ndio Reality of The World! Pumbavu! Inauma sana! Leo wajinga 80 wana nguvu ya maamuzi dhidi ya werevu 79, ni ULIMBUKENI!

Pia naamini FALSAFA SAHIHI YA TAIFA, itatokana na FIKRA SAHIHI za kupanga tuishije kwa kuzingatia mambo makuu matatu (3)
1. MAZINGIRA YETU HALISI, yaani kama eneo ni kame Fikra hzo zisiruhusu kulima mahindi ila mtama.
2. NYAKATI ZETU HALISI, yaani mahusiano yetu halisi, yaliyomo katika Mazingira yetu. Mila, desturi, itikadi, imani, nk.
3. MANTIKI, yaani UUWIANO SAHIHI kati ya NYAKATI na MAZINGIRA. Yaani, ni kusema kwanini tamaduni hii inafaa au haifai kwa mazingira haya na yale. Mimi naita UTU!

Tukikaa chini, na kuamua kujitoa...HATUSHINDWI.

*Naamini pia katika nyanja kuu tatu katika kuisimika imani hiyo kwa raia, ni kupitia Nyanja ya HABARI, SANAA na ELIMU. Pandikiza chochote huko baada ya miaka 5 angalia matokeo yake, kama ulitaka kujenga utakuwa umewajenga kama kubomoa utakuwa umewaharibu kabisaaa! Kupata hiyo falsafa haitaji watu kubebwa na taasisi fulani, hata mkiwa watu watano inatosha kuipigania iingizwe tu katika nyanja hzo 3, Habari, Sanaa na Elimu! Ni lazima TUKOKOTOE NA KUTEGA HESABU KALI WAKUU WANGU!

2. Kuhusu wewe ufanye nini zaidi! Nachoweza kukujibu ni hiki... Binafsi kwanza naamini u miongoni mwa Kizazi kipya cha Fikra. Sasa pima nguvu yako ya kila kitu, na ushawishi, itumie yote ipasavyo, usiache hata japo kapunje kadogo ila tu kama kuna MANTIKI. Mwanaharakati ni tofauti na mwanasiasa wa leo, Mwanasiasa atapigania KWELI lakini atafungwa na Sera na Kanuni za Mfumo wa siasa uliopo, tofauti na Mwanaharakati hatofungwa na kitu chochote katika kupigania KWELI ila MANTIKI tu!

Naamini mpo wengi mnaoweza kutafakari kwa kina mambo, nguvu ni UMOJA na KUTHUBUTU.

3. Hakika, mabadiliko ya kweli ni lazima yapiganiwe nje ya CCM. Ila tusiishie hapo tu, haitoshi. Mabadiliko ya kweli ni lazima yapiganiwe nje ya Siasa zetu za leo, kwa maana ya nje ya vyama vyote na wajiitao wanaharakati wa siasa hizi za leo, iwe cuf au chadema, ni bure. Wanasiasa wa leo wanafungwa na Sera na Kanuni za mfumo MFU wa Siasa, hivyo ni Buree! Sijasema usiwe na chama, waweza kuwa nacho ila Strategically kama MANTIKI inaruhusu. Chama sio Vazi ama kadi, chama ni FALSAFA, ndizo hizo MFU.

4. Mkuu wangu Mchambuzi, nikuhakikishie tu kuwa KAMWE HATA SIKU MOJA MANTIKI HAIWEZI KUFA, NA HUJIPIGANIA YENYEWE. Huna haja ya kuhofia hatima ya FIKRA ZAKO, zitaishi na huko ndio kutakuwa kuishi kwako hata baada ya kifo chako. TUKIPATA FIKRA SAHIHI, ZITASIMIKA VIONGOZI SAHIHI, WATAKAOANDAA KIZAZI SAHIHI. Mimi nimesema!

TUSIJIFIKIRIE SISI ILA WATOTO WETU. Mito ya machozi ya FURAHA kutoka machoni mwa watoto wetu italowesha mifupa yetu aridhini, gharama ya Upendo wetu kwao.

UBUNIFU HAUNA KIKOMO.

Mungu wetu yuko mbele yetu kutupigania.
Anaita sasa.
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa,

Kimsingi naunga mkono hoja kwenye bandiko lako namba 49 hapo juu; Nimependa falsafa yako kwamba "MANTIKI HAIWEZI KUFA"; Hii inanikumbusha falsafa ya mwalimu nyerere kuhusu ukweli, ambapo katika kitabu chake cha TUJISAHIHISHE (1962) anasema kwamba:

["Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake, watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwa."]
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Bongolander # 24, umesema maneno haya ''the whole thing is very complicate''. Maneno hayo yanashadidiwa na Mchambuzi pale aliposema tatizo la rushwa ni ka kimfumo zaidi kuliko individual.

Nakubaliana kabisa na hoja hizo na pia kumuunga mkono Lukolo ya kuwa watu wanaonekana kukata tamaa katika suala linalowezekana kabisa.

Siafiki hoja ya kuwa mapambano ya rushwa yaanzie bottom-up.

Kwa vile ni mfumo tena madhubuti mwananchi hawezi kuudhibiti kwa sababu sheria zinazomruhusu kufanya hivyo zinamilikiwa na mfumo wenyewe na mwananchi ataadhibiwa kwa sheria hizo kugeuzwa kama kutumia maneno, tunachunguza, tunafanyia kazi na uvunjifu wa amani na utulivu.

Nitoe mfano, katika grand corruptions zote zilizotokea katika miaka ya karibuni na ambazo chimbuko lake ni wananchi kutoa taarifa zisizo na shaka na zilizothibitika, ni nini kimefanyika ili kutoa funzo kuwa rushwa haivumiliki?

Mathalani, ununuzi wa rada tunajua ni grand corruption, nani anajua pesa zilitoka wapi na nani alitoa!

Jibu ni hapana kwasababu mfumo mzima umelinda suala zima. Tumebaki kuambiwa vitabu vitanunuliwa kana kwamba hilo ndilo tatizo. Hata pale walipojitokeza watu kuhoji kulikoni, mfumo mzima umeeingiliwa kiasi kwamba watu wanaweka maisha rehani.

Hapa tulipo kwa sasa si rushwa ya kawaida ni ile ya Mafiosa ambayo inahusisha kumweka kiongozi madarakani, na kuwaondoa ''take out'' wale wanaotaka kuharibu utaratibu. Sumu na ajali za kupanga sasa ni norms.

Madai mazito kama ya Zitto Kabwe mbunge yamekingiwa kifua na serikali kwa kupitia bunge na Takukuru kutumika kuhalalaisha. Mfumo huo unahusu pia vyombo vya usalama wa nchi kama Polisi, DCI, DPP na TISS.

Kwa vile ni mfumo unaojitosheleza hakuna jinsi mwananchi anaweza kupambana nao kuanzia bottom up.

Ili kupambana na rushwa, kuna fursa moja ambayo huenda tumeikosa. Fursa ilikuwa ya katiba inayotokana na wananchi itakayomwajibisha kila mmoja wetu kwa nafasi yake kuanzia mkulima hadi Rais.

Ukitazama nchi ambazo zimefanikiwa sana kupunguza tatizo hili, utaona ya kuwa wananchi walitumia silaha yao ya katiba kuhakikisha kuwa kila mmoja ana wajibika na kwamba hakuna mfumo uliojijenga ''intertwine''.

Tungeweza kuondoa kama si kupunguza rushwa kwa kuweka utaratibu wa kumwajibisha kiongozi wa nchi. Kwamba rais awe mtumishi wa umma asiyekuwa na mamlaka zaidi ya katiba.

Hata kama atapatikana kwa njia za rushwa huko kwenye vyama atakapoingia Ikulu basi afahamu kuwa uwepo wake si tiketi ya uhalifu bali kamba itayaoweza kutumika kumnyonga wakati wowote ukibidi. Sio suala la huo ni upepeo bali la maisha yake ksiasa na kibinadamu.

Pili, tuwe na vyombo huru visivyowajibika kimoja kwa kingine. Mfano, Takukuru isiye chini ya Rais bali Bunge. Wakuu wa vyombo vya usalama kama TISS, DPP na Polisi wapatikane kwa utaratibu usiomhusisha Rais na wala wasiwajibike kwake. Mfumo wa sheria ujitegemee bila kumtegemea rais katika uteuzi wa viongozi wake

Bunge liwekewe utaratibu utakaohakikisha kuwa linafanya kazi na si sehemu ya kulindana kichama, kupindisha sheria za nchi, kanuni zake zenyewe au kichaka cha uhalifu. Halafu tuwaambie wananchi wawajibishe wabunge wao.

Ninasema hayo kwvile mfumo huu unaonekana complicated ni kwasababu upo intertwined. Ili tuweze kuuvunja ni lazima kuwepo na mistrust kati ya washiriki.

Rais asimwamini DPP, DPP asimwamini IGP.Mkuu wa TISS wasiaminiane mkuu wa PCCB na wala Bunge lisiwaamini hawa wala lenyewe kuaminiwa nao.Nguvu za bunge ziwe kisheria na kusiwepo na muingiliano wa Bunge na taasisi zingine. Kwa meneno mengine kila mmoja awe askari wa mwenzake.

Mfumo ukishavunjwa automitically huko kwenye vyama rushwa itaondoka. Rushwa iliyopo katika vyama kwasasa hivi ni ya kutaka kuingia katika mfumo rushwa uliopo. Tusidhani rushwa ya vyama ni kitu cha bahati mbaya, la hasha! ni mbinu muhimu sana ya ku-penetrate an ku-infiltrate system.

Ukishakuwa mjumbe wa NEC, Mbunge au Mwenyekiti wa mkoa tayari una link zote za system na unaweza ku-manipulate system kadri utakavyo, hilo ndilo chimbuko la rushwa huko katika vyama na hatimaye serikalini.

Watu wakishagundua kuwa sysytem kule juu ipo ''disorganized'' kwamba kila chombo kinawajibika kivyake na hao wakubwa hawaaminiani, nani atahonga ndani ya chama? Ili iweje baada ya hapo.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi hii ni bonge ya ujumbena chujio lenye lengo ni kuonyesha Watanzania, Tanzania BORA na Watu BORA wenye SIHA na akili Timamu wapotayari kulijenga TAIFA.

Katika chaguzi kuu, Wagombea wa nafasi kama vile ubunge na udiwani, wanaweza jaribu kusema THE RIGHT THINGS kuhusu THEIR HONEST OPINION kuhusu MASUALA mbalimbali ya KISERA kwa manufaa ya TAIFA, lakini wanajua fika kwamba kwa wananchi - ‘WHAT THEY SAY' has much less importance than ‘WHAT THEY DO' to demonstrate that they Care about them or they have a FOLLOWING/Wafuasi/wanakubalika; In order to make a ‘gain' therefore, they have to invest katika kutembeza viloba vya pesa na aina nyingine za ‘tangible rewards' to prospective supporters/voters;
KIlichotoke!!!!
Mchambuzi hapa ndio tatizo uanzia,mara baada ya Mwalimu kungatuka na vision yake ya Ujamaa wa kiafrika na kwa kuwa alikuwa yeye ndio oversee wa kila kilochokuwa ndani ya serikali basi ukosefu wa taasisi hakikishi na ng'amuzi za kikatiba kwenye mfumo ombwe likazaliwa.Mwalimu alijitahidi sana kujenga ujamaa wa kiafrika,lakini kama binadamu akapungukiwa kutengeneza economical, financial and national security heathly watchdogs and monitors.Hapa nguvu nyingi zake akaziweka kwenye ujenzi wa wananchi wajisikie kutumikiwa na serikali yao na si wao pia kuitumikia serikali yao kwa uaminifu na kwa kujivuna kwa uzalendo.

Mapungufu yetu ambayo yametokana na toka mwanzo kwa sisi, kutokuwa na taasisi zilizoundwa kwa nguvu ya usimamizi wa kikatiba katiba,yani Constitutionalise Institutions, hasa kwenye sekta ya uchumi, usalama, fedha, na mengineyo mambo muhimu kama governmental and all citizen constitutional norms.

Nikupitia aina hiyo ya uelewa wa chaguzi wananchi wanapokea wasichotaka na wanasiasa wanatoa wasiyoyamini.

Kifanyike nini!!!
Kupitia ujio wa katiba mpya taasisi za usimamizi, utekelezaji, hakikishi na ungamuzi ziwepo kama nguzo mama kupitia kwenye katiba majukumu yake yatambulike kikatiba dhidi ya sekta nyeti na muhim kama uchumi,Afya,elimu, Huduma za Umma, uchumi, fedha na maliasili.Vipewe jicho la kikatiba kwa miaka hamsini ijayo mbele toka sasa!!Mpaka pale kizazi kilichopo sasa chenye umri wa miaka 15 kitapokuwa na umri wa miaka 65 kinaweza kufanya marekebisho kuondoa baadhi ya articles ili kukidhi muongo huo wa nusu karne kutosha kupitia mabadilko ya kitamaduni, kisiasa na uchumi.Vinginevyo pale patakapo kuwepo wito wa dharula ya Taifa ufanye mabadiliko ya kifungu kwa mujibu wa lazimiko la ridhaa ya umma.

Mchambuzi said:
ya kujadili kwa kina dhana ya ECONOMY OF AFFECTION na jinsi gani inachochea rushwa, ningependa kusema tu kwamba – katika Tanzania, rushwa inachangiwa sana pia na FAMILY TIES; Family pressures are so pervasive; Juu kabisa kwenye pyramid of the patronage wapo Mawaziri na Maafisa waandamizi wa Serikali ambao maofisini na majumbani kwao, kutwa kuna mistari mirefu ya relatives, acquaintances, voters n.k, ambao wanaenda to air their complaints or seek material/economic support; Viongozi wengi wanakuwa hawana jinsi bali kutumia vibaya madaraka yao na kujilimbikizia mali ili kukidhi such irrational demands;

Viongozi wanafanya haya kwa sababu – source of their respect, wealth, prestige and social status inatokana na Loyalty yao katika taasisi za communities husika, sio civic institutions; mifano ni mingi – mawaziri, wabunge, na sasa wameongezwa wajumbe wa NEC; Viongozi husika ni lazima wawe loyal to their communities kwani ndio njia pekee ya kuungwa mkono na kuwika kama viongozi katika ngazi ya TAIFA; Ndio maana kwa viongozi wa namna hii, kwa vile loyalty ipo zaidi kwenye local communities and culture kuliko the STATE, wengi hutumia the STATE as a PREY (kama sehemu ya kuchuma) and milk it in order to feed their communities, na hali hi itaendelea bila ya kujalisha chama gani kipo Ikulu; Na hoja hii inatuingiza kwenye mjadala wa kina juu ya ECONOMY OF AFFECTION;

Hapa nakili kuwa ili ndilo gonjwa kubwa pia kwa jamii,yani ngazi ya familia ambayo ndio nchi namba moja, imezalisha uovu mbaya wa kifikra kwa wanajamii wake, kiasi kuwa mwenye uwezo kwenye familia yani anae jiweza kimapato [Hasa Ukwasi] basi mwanafamilia huyo atapewa heshima kubwa sana na wanafamilia kupita ata anaemzidi umri ndani ya familia husika.

Imefikia hatua wazazi wanawatoto kadha ndani linapotokea jambo la muhimu la familia kama Msiba au Harusi za kifamilia, aliye kwenye uwezo kimaisha kwa misingi ya kipato kikubwa japo aweza kuwa ana umri mdogo kupita wenzie basi familia husika mwenyekipato ndie atakuwa wa kwanza kutaarifiwa tukio husika na kisha yeye kuwa na jukumu la kuwajulisha wengine.Na kama ikitokea akawa na mahusiano yasiyo mazuri na wenzie basi wenzi wake hao hawatapata nafasi ya kujua kinacho endelea kwenye familia yao zaidi ya kusikia kutoka kwa wanajamii wengine yaliyojili.

Hivyo tabia na mwenendo uliozalishwa na jamii uku baadhi ya kabila zikiwa na tamaduni za kuthamin mali [materilism] na hivyo kuambukiza jamii za makabila mengine kupitia mahusiano ya kuona zimezaliwa tabia ambazo kwa serikali uenda zinaonekana kama ni tabia binafsi lakini ukweli zina madhara sana kwenye familia na hatimae Taifa zima kwa ujumla.

Wakoloni walijifunza sana tabia za makabila yetu mengi hivyo kufikia hatua ya kujua kabila gani litumike wapi kwa wingi kwenye eneo lipi. Japo ilikuwa ni kwa faida ya serikali ya kikoloni lakini kuna sehemu zilileta matunda mazuri,ukiondoa ile ya kuwagawa watu kwa nia ya kutawala.Inaeleweka sana wakurya wanaufanisi sana katika kazi za ulinzi, wasukuma ni wachapa kazi n.k.

Llakini sijui na sina ushahidi kwa ili kama kweli serikali yetu inajua ina Taifa [National stereo type] la watu wenye aina gani za tabia,ukizingatia mwingilino wa tabia za makabila tofauti tofauti [50/50] kwa sasa kutokana na kuona.Kama familia hapo zamani zilioana kwa kuangalia mambo ya msingi toka familia moja kwenda nyingine kama UKOMA,UCHAWI,WIZI,UONGO nk.Sembuse Serikali kuangalia watu wake na watendaji wake kwenye msingi hiyo ya kuhakiki tabia za wanajamii zake ambao kwa ujumla wake uzaa Tabia za TAIFA ambazo ndio uzalisha jumuisho la picha ya jamii ilivyo.Tukiwaona omba omba mitaani ni zao la tabia zetu ambazo zimezalisha matatizo hayo na mzigo ule wa omba omba umebaki kuwa kuwa omba omba ni ishara ya tatizo la familia husika,lakini mwisho wa yote inakuja kuwa ni mzigo wa serikali,ambayo nayo haitaki kutambua na kushiriki kama mlezi number moja kabla ya familia.Kwa mfano mdogo wa omba omba tulio nao mitaani ukijiuliza tumefikaje hapo walipo na nani anajukumu nao!!!wakija wageni wanatupima pia kupitia omba omba hao.

Uwa nasikia kichefu chefu sana pale ikitokea mwanasiasa au mtendaji wa serikali akabanwa na jambo kama la kuulizwa kuhusu ombaomba anaweza kukwambia mbona sie tunao wachache uko marekani au uk wako wengi zaidi sana!!!ni aibu kwamba uchache wa omba omba kwetu ni reference kwa wengine,why not sisi tusiwe wa kwanza kuonyeshewa kidole kuwa watanzania hawana omba omba duniani,kama tunavyooshewa kidole kuwa ni nchi pekee yenye tanzanite, na baraka za madini tele kama almas, dhahabu, ruby n.k.

Uwa naumia sana sana,pale nipona jamii kulazimisha kwamba swala la MAADILI ya Jamii kuwa ni swala la FAMILIA,HAKIKA KUTOKA MOYONI MWANGU,NAAMINI KWA DHATI KABISA KUWA TAIFA LIMEFIKA HAPA LILIPOFIKA BAADA YA SERIKALI KUJITOA KWENYE KUSIMAMIA MAADILI YA TAIFA NA MAADILI YA SERIKALI NA VIONGOZI WAKE.

Zamani jamii ngazi ya mtaa walikuwa na uwezo wa kuwa na wazee wakiwa na kamati maalum ya watendaji mtaani wenye busara zinazokubalika na watendaji wakuu wa serikali, kamati hiyo ndogo ngazi ya mtaa walikuwa na uwezo wa kumuonya na kutoa amri ambayo ingefuatwa na watendaji wa serikali dhidi ya kijana, mtoto au mwanajamii yoyote ambae matendo yake yana athari kwa jamii husika mtaani.Lakini leo thubutu!!!!!!!!!!!!!!.

Picha inayopatikana hapo ni TAIFA KUTOKUWA NA MAADILI na maendeleo yake maadili yanayozalishwa ugeuka kuwa tabia na kama jamii ina maadili ya kiovu na hakuna wa kuyasimamia basi jamii itegemee kupokea ushenzi wa maadili hayo iliyochagua.

Nini Kifanyike!!
Serikali kupitia ujio wa katiba mpya kujiandaa na institutional zitakazo kuwa na kazi ya kujenga maadili ya FAMILIA yani KAYA UMMA yani JAMII, MAADILI YA VIONGOZI yani Watendaji wa SERIKALI na Watendaji wa Vyama vya Siasa na Mashrika ya Umma na yasiyo ya Umma,MAADILI YA SEKTA BINAFSI, na MWISHO UZALENDO WA KULIFIA TAIFA.Leo hii popote pale mmarekani alipo anajua haki yake na yuko proud kulitangaza TAIFA lake.

Kuna wakati nilipata kusikia mahojiano ya kingereza ya sauti ya BBC,ilikuwa ikiwahoji raia wa kinajelia Nchini mwao,swali la mtangaji wa BBC lilikuwa "ARE YOU READY TO DIE FOR NIGERIA?". Kati ya walio hojiwa hakuna aliyesema YES!!!Ndio kusema walikofika wao kiupeo kwao HAKUNA MOTHERLAND bali mimi binafsi naona kama wapitaji.Kupitia accent yao kila mmoja aliekuwa anaohojiwa alikua anajibu "WHY SHALL I DIE FOR NIGERIA YOOOO, WHAT AS IT DONE FOR ME YOOOOO?] yani mtangazaji aliishia kuulizwa swali huku alikusudia kujibiwa swali.Tusifike huko ambako eti jukumu la kuifia nchi linabakizwa mikononi mwa wanajeshi [JWTZ] na kumbe wale ni walinzi wa AMANI TU lakini mlinzi wa NCHI ni MWANAWANCHI.

Ndio maana na wewe Mchambuzi unakuja na swali je rushwa ya Tanzania aka UFISADI tiba yake itatolewa na watu wawili MANGULA na KINANA?Kumbe wawili hawa si lolote lile bali ni tone dogo sana ndani ya bahari kubwa sana.Itakuwa na nguvu ya soda kwa kuwa kwa kutegemea watu hao wawili kuimaliza RUSHWA au UFISADI umetamalaki, nao watapita na uenda wakawa mark,kama ilivyodesturi yetu kwenye misemo ya kiswahili ya kuwa wewe nani walikuwepo kina fulani walishindwa sembuse wewe wa juzi juzi.Hivi hatuwezi kusema jambo na tukatenda kama tulivyosema.Siko hata kuwapigia dege magufuri na mwakyembe,hawa jamaa wamepewa nafasi za kimaamuzi kwa kiasi wameonyesha kuwa wanaweza.Hivi kiukweli toka moyoni mawaziri wote wakawa na sura ya MAGUMWAKYE hakika tutakuwa na miaka mitatu watanzania watasupport Taifa lao na Nchi itaamia eneo tofauti sana kimuonekano na hata siha na akili ya wananchi.

Taaluma za watu hawa wawili muhandisi na mwanasheria ni moja ya vigezo ambavyo pia vimechangia kwa ukweli jamaa hawa kudeliver kwenye misingi isiyo na hofu.Kwa watu waliopita shule wanajua hili, mtu yoyote aliyepata elimu yake kimagumashi na hata siku akipewa nafasi pia utendaji wake utakuwa ni wakimagumashi pia hivyo tuna dhohofisha jamii.

Kuna pia swala la UAFRIKA hapa hakika serikali yapaswa kukaa na wazee, wanajadi na viongozi wa dini zote na kupata kikosi kazi [TASK FORCE] ya kulivusha TAIFA toka kwenye hili,manake ili nalo limekuwa ni tatizo ambalo NCHI imefika hapa sababu ya mashindano yaliyokosa watu wa kuomba BUSARA na NGUVU ya KIMUNGU. Na kwa upande mwingine kwa wale watu wa zamani kuomba ruksa ya wazee [Ancestors] yani kana kwamba baadhi ya wanajami wamekosa mwongozo wa wazee wa jadi na kila mmoja amekuwa akijamulia kutenda yake na kudhuru wengine na hakuna wa kumemea.Kwa walio na jadi inaeleweka kuwa kuna wazee wanaongoza misingi mizima kwenye eneo hilo na kuzuia na hata kumuazibu yoyote au chochote kinachotendwa na mwanajamii kinyume na wanajamii wenzie.Zamani wanajadi waliongozwa na machifu wakishrikina na wazee!! Machifu bado wapo kwa kushirikiana na serikali huku nao wakipewa heshima kama viongozi wa kijamii wenye nafasi basi jamii italekebishwa kwa kupitia kabila husika chini ya miongozo ya machifu na wazee wa jadi husika na kama mhusika akionekana kuzidi nguvu ya kabila au jamaa yake basi vyema kupata msaada wa wazee wa jaai na machifu wa jamii nzingine za karibu.

Leo hii tunao waona mafisadi kwenye jamii,wakiitwa mbele ya viongozi wa dini wakaambiwa kutubu,sijui lakini kwa maono yangu wengi wataitikia usoni lakini ndani ya dhamila zao ni wachache sana watakubali kuwa ZAKAYO mtozo ushuru.Ila hao hao wakisikia wanaitwa na viongozi wao wa kikabila watu kama machifu na wazee wengine muhimu kwenye kabila husika basi kitakacho jili yatakuwa maajabu kwa watu kuona aliyekuwa FISADI amegeuka kuwa MPINGA ufisadi mpaka anaingia kaburini.UAFRICANIZATION bado unachukua nafasi kubwa sana kwenye jamii yetu,ndio maana Nyerere na ukubwa wake kama Rais lakini nae alikuwa akifika Butyama anakuta kuna kiongozi wake kwenye kabila lake.

Vivyo hivyo Serikali ikisisitiza na kuimarisha mifumo ya elimu za kifamilia na kusoma mazingira ya familia za kitanzania ambavyo zinaishi na kutumia mfumo ule kukuza na kujenga elimu ya kueneza kwa jamii,na hakika utakuta kuwa, kila familia ina kiongozi wake ambae pia nao kwa kujua wana nafasi kwenye jamii basi serikali ikatengeneza forum ambazo zinatoa nafasi kwa viongozi wa familia kuhudhuria na kutoa mafundisho kwa viongozi hao ambao nao uenda kuzitoa kwa wale wanaowangoza kutoka katika kaya wanazoziwakilisha kwenye familia za makabila husika.

Kuna famila moja siku za karibuni walifikishana mahakamani kupinga uamuzi wa baadhi ya wanafamilia kumchagua mwenzao ambae alionekana kupingwa na upande mweingine.Kupitia aina hiyo ya muonekano wa kiongozi wa familia kupingwa mahakamani basi serikali yaweza kuona ni muhimu kiasi gani hawa wadau kwenye sekta ya MAADILI walivyo muhimu.


Mchambuzi said:
Jamii yetu ya Tanzania inaendeshwa chini ya mfumo wa Economy of Affection. Maana yake ni: People make personal investments in reciprocal relations with other individuals as a means of achieving goals that are seen otherwise impossible to attain – such as prestige, social status, wealth n.k; katika mfumo huu, informal institutions ni muhimu kuliko formal institutions, na hata resources allocation hufanyika under the mechanism of informal institutions; Kuna kanuni kadhaa za mfumo wa Economy of Affection lakini muhimu ni tatu:


  • Kwanza – Whom You Know is More Crucial Than What You Know;
  • Pili - Sharing Personal Wealth is More Crucial Than Investing in Economic Growth;
  • Na Tatu - A helping Hand Today Generates Returns Tomorrow;
Familia zetu nyingi zimejengwa na walioathrika na swala hilo wamejikuta waanga.Waliobezwa kwenye ngazi ya familia kama Baba aliyekuwa hana kitu mbele ya ndugu zake,akajitahidi kusomesha watoto wake,na watoto waliolelewa na Baba aliyenyanyapaliwa na ndugu zake wenye uwezo wanakuwa na kilema cha kuamini ili uwe bora na kuthaminika kwenye jamii ni lazima uwe na kitu/mali [Materiliasm] basi kwa liwalo liwe kwa halali na haramu watoto wale wataangaika ili walipize/compasate maonezi ya kisaikolojia aliyopitia mzazi wao.

Kwa picha hiyo ya ngazi ya familia,mtoto huyo uenda alijibiidisha kusoma na kufanikiwa kupata elimu nzuri iliyomfikisha kupewa dhamana ya ofisi au taasisi.Basi madhara ya kilema chake kilichotokana na mateso ya kisaikolojia ya baba yao basi watalipiza kwa kujilimbikizia saana kwanza kulipiza kwa watesi wao, pili kwa ajili ya self defense kuwaandalia watoto wao wasije wakambuna na aibu.Na wanasahau MUNGU pia anamakusidio yake kwa watoto wao pia.Vilema hivyo vingi vingi na tofauti toka toka familia na makabila mengi mengi tofauti ndio vimejaa na kuzalisha JAMII UBINAFSI.Manake RUSHWA kwa lugha nyepesi ni UBINAFSI yani kilichopaswa kipatikane kwa wengi kwa misingi ya usawa, atakipata mmoja kwa misingi ya umaalumu [Privilege].


Mchambuzi said:
unachochewa sana na mfumo huu; Hii ni pamoja na ukweli kwamba, mambo ambayo wananchi wengi (hasa vijijini) wana hitaji au wanathamini katika maisha yao ya kila siku - kwa mfano goods, services, information, etc, kwa mtazamo wa wengi, all these can only be obtained from others; Ni jadi kwa watanzania kutegemeana for such valued resources na wanapeana haya kupitia informal process of exchanges ambazo ndio zinazoendesha community institutions; Exchanges muhimu hapa ni pamoja na Rewards (e.g., Cheo, Status, Power) Or Punishments (e.g., Kura ya Hapana kwa mgombea nafasi ya uongozi), na hii inategemea iwapo upande husika delivered the promise or didn't deliver;

Kwa mfano, voters may deny political patrons kwa sababu they did not deliver their immediate promises of rewards, hence they punish the patrons kwa kura ya Hapana; Kwa upande mwingine, pia Political patrons wanaweza punish voters iwapo hawatapiga kura kwa kiasi kilichotarajiwa, na adhabu inaweza kuwa pamoja na serikali husika kutopelekea huduma za kijamii katika maeneo fulani n.k; Kuna utafiti mmoja uliofanywa na Chuo cha UCLA na unaonyesha jinsi gani Wilaya fulani fulani zilipewa adhabu hii na CCM katika kipindi cha 1997 – 2007 (see Laura Weinstein: The Politics of Government Expenditures in Tanzania: 1997 - 2007);

Watanzania wengi (hasa wa vijijini) are not rational when it comes to decision making; na ni inachangiwa sana na Weakness of the State in the hinterland i.e. absence of Civic Institutions to play a prominent, leading and legitimate role over and above community institutions; Katika nchi za wenzetu zilizoendelea zaidi in terms of Strong & Consolidated States, kwa mfano, classical microeconomic theory inatoa mwongozo wa kimaamuzi ndani ya jamii husika, ambapo kwa mfano - hakuna long term relations between economic exchange partners; hii ni tofauti na Tanzania ambapo social and economic exchanges zinapendelea partners wa muda mrefu, hasa kwa kutegemeana na Rewards vis a vis punishments, katika mazingira ya Economy of Affection;

Ni kwa picha hii pia jamii kwa utambuka wake umetumia kipato cha mgombea kujipatia manufaa binafsi.Kuna Mheshimiwa mmoja ambae ni marehemu [R.I.P] alikwenda nyumbani kwao kugombea,akitokea Dar es Salaam,lakini kabla siku za nyuma akiwa mtendaji wa umma nae ni mwenyeji wa kutoka moja ya makabila yanayoheshimu undugu sana,baadhi ya ndugu zake walipokuwa wakifunga safari kuja Dar es salaam toka nyumbani kwao Mheshimiwa huyo,wakifika kwake wanakutana na mama mwenye nyumba ambae ni mwenyeji wa mikoa ya kaskazini, basi kwa haiba ya upande wa pili ya kutopenda mlundikano wa watu nyumbani akawa anawaludishia mlangoni.Basi wanajamii wale toka kanda ya ziwa magharibi walipokuwa wanatimuliwa na wanafungasha mizigp kuludi zao kijijini na kuja kumshtaki jamaa yao kwa wanajamii wao.

Siku ya siku muhusika nae ukafika wakati akapata fursa ya kuiingia kwenye siasa na kuona aende kwao kwa kuwa nyumbani ni nyumbani hata kama ni pangoni [Home Sweet Home].Kafika nyumbani wakampokea, akwaambia wanajamii wake ambao kwa hakika walimsikiliza na mwisho wa yote mpaka anatoka duniani hawakumpa tketi yao ya kuwawakilisha kwenye Bunge, pamoja na kuwa na vigezo marudufu kuzidi wapinzani wake lakini kamwe hawakumpa wakimuathibu kwa tendo la mkewe kuwaludishia mlangoni wakti kwa jadi yao ukibalikiwa kuwa na familia wageni wa jamii yako ni sehemu ya maisha yako.

Mchambuzi said:
mwingine ni kwamba, wakati classical microeconomic theory assumes kwamba actors engage in set of independent transactions that are aggregated into markets, katika Tanzania, exchanges are built on premises that actors engage in recurring interdependent exchanges with partners with specific pertners over time and they remain partners as long as they fulfill their promises in the context of the Economy of Affection;

Hapa Mkuu umepigilia msumali kama nilivyosema awali Mwalimu alipungukiwa ufahamu na ili silioni kwake kama kosa bali ndio uwezo wake kwa zama zile mtoto mchumgambuzi aliyesoma na kuja kuwa Rais lakini akatenda yale yaliyo ndani ya uwezo wake.
Mwalimu anaingia kwenye ofisi anakuta kuna sekta ya uchumi, fedha, mataifa, Afya, Elimu, biashara n,k.Yote hayo yanaitaji uyapambanue kwa kiwango chako ili utapopewa report nawe uamue kwa jinsi unavyoona inafaha basi haikuwa kazi nyepesi hata kidogo.Wahindi na waarabu waliokuwa na kulelewa toka watoto wakipokea change na kutoa change kwenye madirisha ya maduka ya baba zao wakiwa watoto,leo wanakuja kupimana na mtoto wakati wao wanapokea fedha dukani yeye anachunga mbuzi.Unaweza kuona uzoefu na ufahamu katika sekta ya biashara na uchumi.Japo wataalamu wanasema watoto uchukua asilimia 80% kwa kulithi akili za wazazi na asilia 20% inatokana na kuadapt mazingira wanayoishi.Hivyo akuweza kuwa genius kuweza kujua namna gani anaweza kujenga na kusimamia sera za uchumi wakati kipawa cha familia yake inherit ni kutawala jamii kwa amani.Wazanaki kwa asilia walikuwa ni watawala wazuri waliopenda majadiliano zaidi kuliko malumbano.Leo hii ukiwa Rais wa marekani wataalmu ufuatilia kwa umakini familia ya mgombea toka vizazi na vizazi.

Hakika tulilithi aina hiyo ya mfumo wa kibiashara watanzania wenye asili ya kiasia [Waarabu na Wahinid] matokeo yake tumefika hapo tulipofika.

Tunaitaji mabadiliko yatakayo ratibiwa na Serikali,wakati mwingine Serikali kutoa Tender za Seriakli kwa makusudi zenye sura ya joint venture kati ya ethnics hizi za Wahindi, Waarabu na Waswahili,Yani kama kuna muhindi au Mwarabu au Mswahili wanajiweza kwenye Tender tajwa wanapewa hiyo Join venture kuondoa hizo tofauti za kimitizamo.Sio siri sekta ya biashara kubwa zimemezwa na makundi machache ya aina fulani ya watu kabila hasa wahindi na waarabu.Ila sehemu ambayo mimi mwenyewe nakili kuwa Mwalimu akuangalia kwa jicho la umakini ni swala la BIASHARA, FEDHA na UCHUMI na MAHUSIANO haswa kwa hawa ndugu zetu wenye asilia ya kiasia [Wahindi na Waarabu] aliwakumbatia sana na hakuwa na shaka na ushriki wao kwenye sekta tajwa.


Mchambuzi said:
Ni muhimu kwa vyama hivi viwili kuja na consensus juu ya suala hili la rushwa badala ya kila upande kulitumia kama a political asset vis a vis political liability kuelekea 2015, huku equilibrium to wananchi walio wengi, kutokana na mchakato husika, ikiwa haina mwelekeo; It is about time sasa tuanze kushughulikia tatizo la Ufisadi kwa kuendeleza Formation and consolidation of the state of Tanzania kwani bado kazi haijaisha (e.g. kuna maeneo wananchi hawajui serikali ni nini, civics ni kitu gani, au economic, political and social justice vitu gani), kwani kwa kufanya hivyo, tutaweza kufanikiwa kuanza kuishi collectively in a modern state kama taifa na kuondokana na duality ya hivi sasa ambayo ipo dominated zaidi na community institutions and their informalities kama tulivyo jadili;

Nami nakumbuka kusema siku zilizopita huko nyuma mara kadha wa kadha TUFIKE POINT TAIFA liunde TANZANIA UFISADI RECONCILIATION COMMITTE [TURC] .Lengo litakuwa ni kuondoa SINTOFAHAMU, LETE USHAIDI, HUNA MORAL AUTHORITY, MBONA NI MIMI NA SIO YULE, na mengineyo mengi.
Ndani ya TURC wanakamati amabayo itakuwa na mandate kisheria yatakayobainika humu ndani kwa kipindi cha miaka miwili yatoe hitimisho kuhusu corruption and fisaidim ndani ya Taifa.Ushauri wangu wanakamati wawe viongozi wa dini, viongozi wa jadi, wanasheria, wanadiplomasia makini.

Na toka kwenye TRUC Taifa lije na Taasisi za KiKATIBA [Constutional Institutions] zitakazo kidhi mahitaji ya kukomesha rushwa kama si kumaliza kabisa rushwa.Mfano Mkurugenzi wa TAKUKURU na UWT wateuliwe na Rais na kupigiwa kura na BUNGE.Na taasisi zao ziwajibike kwa BUNGE na kuwe na kamati maaalumu zisizo za kibunge zenye dhamana muhimu kama watchdog wa taasisi husika ambazo ziko tayari kuwajibika bungeni na kujibu maendeleo ya TAASISI husika wakishirikiana na Mkurugenzi husika.Hakika tumechelewa lakin tunaweza kuiwai treni PUGU na safari yetu kwenda mkoani bara ikawa ya heri..Tatizo kuna foleni [Traffic Jam] tunaitaji dereva mtundu, anaejua chocholo, anaejua lugha ya kuongea na trafiki wampe green right tupite kwa haraka atakae weza kuikwepa foleni hiyo na kuakisha kuwa tunafika PUGU kabla treni aijachukua kasi kuelekea Morogoro ,tusije anza tena kasi ya kuitafuta Morogoro kwa nia ya kuiwai huko.Tunaitaji dereva anaejua njia zitakazo tufikisha kituoc sahihi ya kudandia Treni halisi.

aKSANTE mCHAMBUZI kwa uchambuzi wenye KUFIKILISHA UBONGO!!!Manake tatizo la wanaotuongoza
1: Hawataki kufikilisha Ubongo
2: Hawapendi kuwa na vya kwetu ambavyo vitafanana nasi kwa tabia na matendo
3: Hawaitaji kujifunza au kusoma na hivyo kujua ishara za kuwa kesho itakuwaje ama uenda ikafananaje!!
4: Wamaamini wanajua kuliko umma unavyojua.
5: Wameupuuza Umma na Jamii na Jadi imeeacha ijiamulie ili mladi wao wako salama.
 
Mkuu Bongolander # 24, umesema maneno haya ''the whole thing is very complicate''. Maneno hayo yanashadidiwa na Mchambuzi pale aliposema tatizo la rushwa ni ka kimfumo zaidi kuliko individual.
Nakubaliana kabisa na hoja hizo na pia kumuunga mkono Lukolo ya kuwa watu wanaonekana kukata tamaa katika suala linalowezekana kabisa.

Siafiki hoja ya kuwa mapambano ya rushwa yaanzie bottom-up.
Kwa vile ni mfumo tena madhubuti mwananchi hawezi kuudhibiti kwa sababu sheria zinazomruhusu kufanya hivyo zinamilikiwa na mfumo wenyewe na mwananchi ataadhibiwa kwa sheria hizo kugeuzwa kama kutumia maneno, tunachunguza, tunafanyia kazi na uvunjifu wa amani na utulivu.

Nitoe mfano, katika grand corruptions zote zilizotokea katika miaka ya karibuni na ambazo chimbuko lake ni wananchi kutoa taarifa zisizo na shaka na zilizothibitika, ni nini kimefanyika ili kutoa funzo kuwa rushwa haivumiliki?
Mathalani, ununuzi wa rada tunajua ni grand corruption, nani anajua pesa zilitoka wapi na nani alitoa!

Jibu ni hapana kwasababu mfumo mzima umelinda suala zima. Tumebaki kuambiwa vitabu vitanunuliwa kana kwamba hilo ndilo tatizo. Hata pale walipojitokeza watu kuhoji kulikoni, mfumo mzima umeeingiliwa kiasi kwamba watu wanaweka maisha rehani.

Hapa tulipo kwa sasa si rushwa ya kawaida ni ile ya Mafiosa ambayo inahusisha kumweka kiongozi madarakani, na kuwaondoa ''take out'' wale wanaotaka kuharibu utaratibu. Sumu na ajali za kupanga sasa ni norms

Madai mazito kama ya Zitto Kabwe mbunge yamekingiwa kifua na serikali kwa kupitia bunge na Takukuru kutumika kuhalalaisha. Mfumo huo unahusu pia vyombo vya usalama wa nchi kama Polisi, DCI, DPP na TISS.
Kwa vile ni mfumo unaojitosheleza hakuna jinsi mwananchi anaweza kupambana nao kuanzia bottom up.

Ili kupambana na rushwa, kuna fursa moja ambayo huenda tumeikosa.
Fursa ilikuwa ya katiba inayotokana na wananchi itakayomwajibisha kila mmoja wetu kwa nafasi yake kuanzia mkulima hadi Rais.

Ukitazama nchi ambazo zimefanikiwa sana kupunguza tatizo hili, utaona ya kuwa wananchi walitumia silaha yao ya katiba kuhakikisha kuwa kila mmoja ana wajibika na kwamba hakuna mfumo uliojijenga ''intertwine''.

Tungeweza kuondoa kama si kupunguza rushwa kwa kuweka utaratibu wa kumwajibisha kiongozi wa nchi.
Kwamba rais awe mtumishi wa umma asiyekuwa na mamlaka zaidi ya katiba.

Hata kama atapatikana kwa njia za rushwa huko kwenye vyama atakapoingia Ikulu basi afahamu kuwa uwepo wake si tiketi ya uhalifu bali kamba itayaoweza kutumika kumnyonga wakati wowote ukibidi. Sio suala la huo ni upepeo bali la maisha yake ksiasa na kibinadamu.

Pili, tuwe na vyombo huru visivyowajibika kimoja kwa kingine. Mfano, Takukuru isiye chini ya Rais bali Bunge.
Wakuu wa vyombo vya usalama kama TISS, DPP na Polisi wapatikane kwa utaratibu usiomhusisha Rais na wala wasiwajibike kwake. Mfumo wa sheria ujitegemee bila kumtegemea rais katika uteuzi wa viongozi wake

Bunge liwekewe utaratibu utakaohakikisha kuwa linafanya kazi na si sehemu ya kulindana kichama, kupindisha sheria za nchi, kanuni zake zenyewe au kichaka cha uhalifu. Halafu tuwaambie wananchi wawajibishe wabunge wao.

Ninasema hayo kwvile mfumo huu unaonekana complicated ni kwasababu upo intertwined.
Ili tuweze kuuvunja ni lazima kuwepo na mistrust kati ya washiriki.

Rais asimwamini DPP, DPP asimwamini IGP.Mkuu wa TISS wasiaminiane mkuu wa PCCB na wala Bunge lisiwaamini hawa wala lenyewe kuaminiwa nao.Nguvu za bunge ziwe kisheria na kusiwepo na muingiliano wa Bunge na taasisi zingine.
Kwa meneno mengine kila mmoja awe askari wa mwenzake.


Mfumo ukishavunjwa automitically huko kwenye vyama rushwa itaondoka. Rushwa iliyopo katika vyama kwasasa hivi ni ya kutaka kuingia katika mfumo rushwa uliopo.
Tusidhani rushwa ya vyama ni kitu cha bahati mbaya, la hasha! ni mbinu muhimu sana ya ku-penetrate an ku-infiltrate system.

Ukishakuwa mjumbe wa NEC, Mbunge au Mwenyekiti wa mkoa tayari una link zote za system na unaweza ku-manipulate system kadri utakavyo, hilo ndilo chimbuko la rushwa huko katika vyama na hatimaye serikalini.

Watu wakishagundua kuwa sysytem kule juu ipo ''disorganized'' kwamba kila chombo kinawajibika kivyake na hao wakubwa hawaaminiani, nani atahonga ndani ya chama? Ili iweje baada ya hapo.

Mkuu Nguruvi nakubaliana kabisa na hoja zako, nakubaliana na wewe kuwa a bottom up mode in Tanzania can not work, at least not in the near future. One of the reasons is, Stockhold syndrome is deep rooted, and education to majority of Tanzanians ni ile ya kuondoa ujinga tu, na sio kuwa critical na kuchukua hatua pale kunapokuwa na matatizo. And also CCM's divide and rule trick works so well in its favor...idara za usalama zote Tanzania zinajiona ni sehemu ya CCM na si sehemu zinazojitegemea.

Kwa sasa inakuwa vigumu kwa mwenyekiti wa CCM mkoa kumwajibisha mwenyekiti wa wilaya kwa kuwa wanajua walitumia njia moja na kila mtu ana tool ya kudeal na mwingine, kwa hoyo it has become a norm for them kusaidiana.

Bunge kama lilivyo sasa, TISS kwa sheria inayoiongoza sasa (ambayo inaonekana kuwa siri ya CCM hata watanzania, hata wabunge wetu hawaijui), Polisi, Jeshi, Mahakama hata siku moja hawawezi kubadilisha hali ya sasa.

Unajua kuna taataizo moja tulilonalo, watu tuna-bank sana kwenye opposition kutuokoa na wizi unaondelea, but wait a minute...suppose Mbowe au Zitto anakuwa rais, who will be generals, who will be makatibu wakuu, nani watakuwa makamanda wa jeshi na wa polisi, nani watakuwa TISS, je watakuwa loyal kwa wananchi, Chadema au CCM, who will be Takukurus...kwenyewe Takukuru ukianza kuangalia utaona maofisa wake ni mafisadi vilevile...kwa hiyo karibu kila kona ufisadi ufisadi ufisadi.....ina order for them to be safe and in order for them to keep on siphoning....ni lazima CCM iendelee kuwepo, otherwise ni kivumbi na jasho.

Alternatively......atokee mtu ndani ya CCM aseme sasa tunaacha ufisadi au asiyefisadi azuie ufisadi. Lakini swali who is that person, ni nani kati ya hawa tulio nao ndani ya wanaotajwa tajwa ambaye si fisadi, ni nani (kama alivyosema Nyerere) ambaye akisema atapambana na ufisadi tunaweza kumwamini kwa kumwangalia tu usoni?
 
Nguruvi3,

Asante kwa mchango wako no.51, kwa mara nyingine tena; Nimeielewa hoja yako ya msingi juu ya kwanini njia sahihi ya kupambana na rushwa ni top - bottom, na sio bottom - up; Lukolo pia yupo katika kambi hii, na ni sawa tu kwani mgongano wa mawazo, mtazamo ni kitu constructive, kikubwa ni kiambatane na ujenzi wa hoja; Pia naomba nisisitize kwamba sio kweli nimekata tamaa kwamba hatuwezi kutatua tatizo hili, nilichofanya ni kuwasilisha yote nayoamini kama ni changamoto; Vinginevyo, nikirudi kwenye hoja ya msingi, naomba ku - defend nachoamini – yani umuhimu wa bottom – up approach vis a vis top bottom approach, kwa hoja kuu mbili - tatu zifuatazo:

Kwanza, nadhani uelewa wetu juu ya dhana ya bottom – up ni tofauti; Inawezekana kwa mtazamo wenu, watu at the bottom ni watanzania maskini huko vijijini; Kikatiba, watanzania wana haki nyingi, lakini kati ya hizi, pia ipo haki ya KUCHAGUA na KUCHAGULIWA katika nafasi ya uongozi; Kama tunakubaliana katika hili, wale wote ambao waliamua kutumia haki yao ya kikatiba ya KUCHAGULIWA (badala ya kuchagua) kwa kugombea nafasi ya uongozi na wakafanikiwa, hao ni sehemu ya watu ambao wapo at the top; Na wale wote ambao wanaamua kutumia haki ya KUCHAGUA (badala ya kuchaguliwa), basi wote hawa wanakuwa sehemu ya watu at the bottom; Kwa maana hii, mimi pia ni mmoja wapo, na nadhani hata wewe, lukolo, bongolander, DSN n.k; Kama tunakubaliana hadi hapa, basi nadhani wewe kupinga kwamba bottom – up approach haiwezi kuleta mabadiliko husika, basi ni kukataa kwamba mimi, wewe, Lukolo, bongolander, na wengine ambao tumeamua kutumia haki yetu ya kikatiba kuchagua (sio kuchaguliwa) ili wengine watuongoze, hatuwezi kuleta mabadiliko husika; Hili nalikataa!!!

Pili, ni kuhusu suala la Civic Media, hii ni tofauti na centrally controlled and distributed media kama TBC, ITV, Tanzania Daima, Uhuru n.k; JamiiForums ni sehemu ya CIVIC MEDIA, na such a platform ni sehemu ya watu at the bottom; Katika mjadala huu, tayari tupo vitani challenging tuliowapa dhamana kupitia CCM, Chadema n.k; Na nadhani unakubaliana na mimi kwamba JamiiForum as CIVIC MEDIA platform imefanikiwa sana kuamsha watawala na viongozi huku juu na aidha kubadilisha tabia zao, au kufanya kazi kwa maslahi ya taifa; Kwa kifupi, JamiiForums as CIVIC MEDIA, and part of the people at the bottom, is well recognized at the top; Ni kwamba tu JamiiForums inashindwa kumalizia the last mile ambayo kwanza ni lazima ianze kwa watu kuacha kujificha sura na majina yao na kujitambulisha, kisha kusimamia hoja zao kwa maslahi ya taifa, watambulike kimakundi kutokana na itikadi, misimamo yao n.k; Hii tabia ya kujificha jificha sana sana itafanikisha kazi ya whistle blowing na mengineyo ambayo rarely lead to change;

Na tatu, nadhani unakubaliana name kwamba mamlaka ya juu kabisa ya nchi ipo mikononi mwa umma; Rais na wengine, hawa wapo kwenye nafasi zao kwa dhamana tu ya UMMA, sio vinginevyo; Njia sahihi ya umma kujiletea mabadiliko ni kwa kujihusisha na a political process aidha kupitia a political party inayoendana na aspirations zao, au a political movement, hakuna zaidi ya haya; mwisho wa siku, kama watu at the bottom wataendelea kuwa na mshikamano, loyalty, selfless, and committed, hakuna kitakachowazuia kujiletea mabadiliko, iwe sijui ni Polisi, TISS, Jeshi, Ikulu, DPP, au vyote kwa pamoja; Sidhani kama unalikataa hili; Tukiungana kupigania maslahi ya taifa, upo uwezekano kwamba wapo baadhi watapoteza maisha kwa sababu wanapambana na status quo, lakini loyalty, determination, selflessness, commitment, to the cause vikiendelea, ushindi dhidi ya rushwa utapatikana tu, again, Bottom – Up!!

Iwapo unakubaliana na hoja zangu tatu hapo juu, sina shaka kwamba kuanzia sasa utaanza kujitambua kama sehemu ya watu at the bottom, na kwamba KWA PAMOJA, TUNAWEZA KULETA MABADILIKO; Kama sehemu ya watu at the bottom, tunaweza kupigana na rushwa kwa njia mbalimbali, hasa kupitia information awareness raising, na kama unavyojua, information is power; Pia tunaweza kufanya mobilization ya wenzetu ambao tupo nao chini, lakini wao kwa sababu moja au nyingine wapo less fortunate in terms of knowledge, education, access to assets za kuweza ongeza uwezo wao wa kuelewa na kuchambua mambo n.k; Together, tunaweza kabisa kufanya kazi to advocate and support legislation zinazolenga kutatua ufisadi pamoja na taasisi zenye uwezo wa ku – expose ufisadi katika jamii;

Bottom – Up approach to tackling poverty inaweza kufanikiwa kwa kufanya haya, miongoni mwa mengine mengi:

Kwanza – ni kwa watu at the bottom kuunda kitu kama 'an anti corruption coalition' lationskuanza na petty corruption, virushwa vidogo vidogo polisi, mashuleni, mahospitalini, idara za serikali zinazotoa huduma kama vile Ardhi, TRA, RITA, BRELA n.k; Kazi kubwa hapa ni kwa wale waliopo at the bottom kama mimi na wewe, to take a lead kwa kuelimisha wenzetu tulionao chini ambao ni less fortunate (kama nilivyojadili), juu ya one's right na pia to challenge the notion kwamba rushwa katika jamii ni suala ambalo halikwepeki; Jukumu kubwa hapa ni kubadilisha mindset za watanzania wenzetu kwa kutumia silaha kuu tatu:

  • Information;
  • Education; &
  • Awareness Raising;
Ujumbe wetu from the bottom, unaweza kuwa disseminated kwa kutembelea shule za msingi na sekondari nchini, kuendesha forums mitaani na vijijini, talk shows kwenye redio, na muhimu zaidi, katika kila chaguzi, ku – endorse wagombea udiwani, ubunge na Urais ambao wanaendana na vision and mission ya our civil organization;

Pili – tunaweza ku mobilize wananchi/raia kimakundi based on Gender, Age, Occupation, n.k, na kuunda kamati za wananchi ambazo kazi zao itakuwa ni kufanya monitoring ya bajeti - matumizi na ukusanyaji wa kodi; pia tunaweza organize citizens' hearings na ku – push for greater transparency and accountability, na yote haya yatasaidia sana budget controlling, kwani tutakuwa na control system in place ambapo viongozi watakuwa held accountable and confronted for misuse of public funds, kuanzia ngazi ya chini hadi juu; hii itajenga accountability and transparency in administration at all levels;

Tatu – is to empower the civil society, ambayo sisi ni sehemu yake; Katika hiki, makundi katika jamii yanakuwa organized and trained na pia kupatia political empowerment kuanzia local, regional and national level; Key hapa ni enhancing citizens' capacity kuchambua public budgets and accounts and to draw attention to ufisadi na rushwa; Pia research institutions and journalist associations zinaweza kuwa mobilized na kuungana na civil society katika vita dhidi ya rushwa;

Mwisho, ni muhimu kwa wananchi kuwa nyuma ya wanasiasa na watumishi wa umma ambao wataamua kujitoa mhanga na kupigana dhidi ya rushwa from within; Wananchi pia ni muhimu wakashinikiza wawakilishi kuandaa legislations zinazopinga ufisadi na rushwa, au wakaziunga mkono kila mara wawakilishi wao wanapozipeleka bungeni; Whether Spika wa bunge azipokee au asizipokee, hii isiwe sababu ya wananchi kukataa tamaa kwani kuna njia kuu za aina mbili za kuleta mabadiliko – kwanza ni kupitia Chama Cha Siasa ambapo mchakato wake unapitia Bungeni, na Pili ni kupitia A Political Movement, ambapo mchakato wake hupitia kwenye jamii; Mafanikio ya TANU kwa mfano as a political movement yalipitia Jamii, Sio Bunge la Mkoloni;

Ni muhimu pia Tanzania ikaja na Watch Dog Institutions on Corruption na Pia Critical Journalism ambazo zitafanya kazi na civil society to expose and fight rushwa na ufisadi;
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi

Ahsante kwa maelezo yako ya kina sana. Kuhusu bootom-up nadhani tupo pamoja.

Mimi nimetumia mwananchi wa kawaida kwa maana hiyo hiyo uliyoikusudia.

Kuhusu hoja yako ya civic media hilo nakubaliana nawe kwasababu mabadiliko mengi nchini yamekuwa ni matokeo yake. Ni kweli kuwa nguvu ya umma ni kubwa kuliko vyombo kama Polisi n.k. Kwa bahati mbaya sana mfumo wa corruption umeingia hadi katika nguvu ya umma.

Nitakupa mifano miwili kuhusu walimu na madaktari. Iwe madai yao yalikuwa sahihi au la, mwisho wa siku tumeona kuwa mfumo wa corruption umeingia katika vyama vyao na kuwaacha wakiwa wamesambaratika. Hicho ndicho tutegemee tutakapotegemea sana nguvu ya umma.

Kuhusu hoja ya journalists,miaka ya karibuni waandishi walifanya kazi nzuri sana ya kuufahamisha umma nini kinaendelea kuhusu rushwa. Hilo likafahamika na ghafla mfumo wa rushwa kama ulivyo na matawi sehemu nyingine ukaingia katika journalism na matokeo yake ndio wakati tulio nao.

Civic society zimejaribu sana kama akina mama Ananilea Nkya kuufahamisha umma nini kinaendelea katika jamii.
Kwa bahati mbaya nguvu ya hizi society inakumbuna na nguvu kubwa sana ya mfumo wa rushwa na kuzimika.

Ninaposema bottom-up ni njia isiyoweza kuleta mabadiliko bila ghasia nina maana ya kuwa ni lazima kwanza tuvunje mfumo wa rushwa kuanzia juu ili tuweze kujenga misingi ya kuzuia rushwa kutoka chini.

Mkuu, unakumbuka kuwa kuna kesi zinazobabaishwa kwa kutumia mfumo wa rushwa uliopo. Mathalani, nimeeleza ni nani anajua suala la rada limeishaje?

Kesi ya daktari aliyepigwa na kuumizwa kilichotumika ni mfumo tu nasi wananchi wa kawaida (bottom-up) tumejikuta hatuna uwezo kwasababu mfumo mzima umetumika kulindana. Amekamatwa Mkenya na tunaambiwa kesi ipo mahakamani.

Tumeuliza pesa za Uswiss tunaambiwa majibu yatatolewa mwezi April, huku nyuma viongozi wanasema hawana la kufanya. Maana yake ni kuwa wizi ule si wa mtu mmoja ni system nzima kama ilivyokuwa kwa Marehemu Balal ambaye hatujui kama yu hai au amefariki. Vivyo hivyo kwa mambo kama EPA, KAGODA, RICHMOND n.k.

Mfumo unaotumika hapo ni Serikali kutumia Polisi, DPP, PCCB, Mahakama, Bunge n.k. kutafuta njia za kuzuia justice isifanyike. Bottom-up wamefika mahali hawana uwezo tena ndio maana tunasikia ''huo ni upepo utapita''

Pamoja na hoja zangu nakubaliana nawe kuwa bootm up ina option moja tu! kuhakikisha kuwa mfumo huo unaondoka kwa kutumia kila kinachowezekana! si kusubiri sheria kwasababu tayari mfumo wa rushwa unamiliki, ni kutumia nguvu ya umma kama kwingineko duniani.
 
DSN,

Asante sana kwa mchango wako namba 52; Kwa kweli umejadili mambo mengi na muhimu sana, na nimefurahishwa na kitendo chako cha kutoa mapendekezo juu ya nini kifanyike kutatua tatizo husika; Laiti sote tungeiga mfano huo, tungekuwa tuna jifunza mengi sana katika mijadala yetu; Kwa kweli JF ni kisima cha knowledge kubwa sana, kwa bahati mbaya sana mengi tunayojadili humu yanaishia tu kuwekwa kwenye archives, na kama upepo, yanapita;

Kuna hoja nyingi za kujibu, lakini kwa sasa naomba nijikite kwenye hoja kuu nne; Kwanza, ni kuhusu jitihada za Mwalimu kuunda taifa la Tanganyika/Tanzania, hasa kuweka misingi ambayo ililenga kutunusuru na matatizo tunayokabiliana nayo leo, hasa hili la Ufisadi; Kwa kweli Mwalimu alijitahidi lakini alishindwa kwani pamoja na uwepo wa Political Will, na pia kuonyesha kwa vitendo kabisa kwamba rushwa ni suala lisilo vumilika na kukubalika, hakuwa na timu nzuri ya kumsaidia kufanikisha vita hii; Wakati wa Mwalimu, rushwa ndani ya Serikali Kuu ilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, lakini tatizo lilikua kubwa sana kwenye Mashirika ya UMMA na Vyama Vya Ushirika; Huko Mwalimu palimshinda;

Mwalimu alishindwa kuthibiti chini ya chama kimoja, na pia chini ya mfumo wa uchumi ambao njia zote kuu za uzalishaji na usambazaji zilikuwa chini ya serikali; Tofauti ya Mwalimu na viongozi waliomfuatia ni POLITICAL WILL, hasa kwa kuonyesha kwa vitendo kwamba rushwa haikubaliki na haivumiliki, na kulikuwa na sheria kadhaa za kukabiliana na tatizo hili; Lakini tukubaliane kwamba alichofanikiwa Mwalimu ilikuwa ni kudhibiti rushwa ya aina ya kwanza kama nilivyoijadili awali - yani ile itokanayo na rogue individuals/petty corruption; Lakini rushwa ya kimfumo, hii ilimshinda, ingawa awamu zilizofuatia hali ikawa mbaya zaidi, hasa kutokana na Uchumi kuvamiwa na mabepari katika mazingira ya a weak and fragile state (of Tanzania);

Katika mchango wako, moja ya mapendekezo uliyotoa ni pamoja na umuhimu wa Katiba Mpya; Kimsingi nakubaliana na wewe, lakini je, Katiba mpya itatusaidia to strengthen our weak ‘STATE' and its Civic institutions, ili iwe/ziwe over and above Community Institutions? Je unadhani ni kitu gani kitawafanya watanzania, hasa wa vijijini waache Loyalty to their communities and institutions, jambo ambalo wamekuwa wanalifanua tangia uhuru, na badala yake, wahamishie their loyalty to the State and its civic institutions? Kwani, kwa mtazamo wangu, hiki ni kikwazo, lakini pia ni njia mojawapo ya kufanikisha vita dhidi ya rushwa, iwapo utakuwa ulinisoma vizuri awali juu ya problematic state of Tanzania na madhara yake;

Hoja yako ya pili inahusu tamaduni fulani fulani za makabila fulani fulani na jinsi gani zinachangia tatizo la ufisadi, na pia kuambukiza tamaduni nyingine; hii ni hoja nzito sana, na nategemea mjadala mzuri sana kutoka kwa wale watakaokusoma; Sina uhakika sana na maelezo yako kwamba mkoloni aligundua madhaifu haya katika makabila fulani fulani na kuyatumia kikamilifu kuimarisha ukoloni, lakini kimsingi naelewa hoja yako vizuri sana; Je una mifano ya makabila husika ambayo unaweza kutupatia, hasa yale unayodhania kwamba yamechangia sana kuenea kwa rushwa kutokana na jadi na mila zake/zao?

Hoja hii inaweza kutupatia mwanga kidogo kuhusu jinsi gani mradi wa national integration wa Mwalimu Nyerere ulipata changamoto kubwa; Vile vile ingawa tunajisifia tupo wamoja, lakini it is only to an extent; ningependa kuliacha hili kwanza hadi pale utakaponipatia majibu kwa maswali yangu hapo juu; Vinginevyo national integration ni kweli, ni suala la kikatiba, na lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa chini ya katiba ya JMT (1977), lakini sustainability yake ilipata matatizo, hasa kutokana na Chama Cha Mapinduzi baadae kuja kuwa superior to Katiba ya JMT; Na ndio maana nchi imekuwa kwenye mgogoro mkubwa sana wa Kikatiba, kwanza kule Zanzibar kuanzia miaka ya mwanzo ya themanini, na hatimaye Bara kuanzia miaka ya mwanzo ya tisini; Ingawa mgogoro wa Katiba umehusishwa zaidi na the Union Question, mimi nadhani ni zaidi ya hapo, na ndio maana Mwalimu alikuwa mkali sana na kutuonya kwamba tukiruhusu Zanzibar kujitenga, basi nchi yote itasambaratika kwa mujibu wa makabila;

Hoja yako ya tatu inahusu mfano ulioutoa kuhusu Mbunge mmoja Marehemu – jinsi gani mkewe alivyomuaribia safari yake ya siasa kutokana na Mke huyo kwenda kinyume na Kanuni za Economy of Affection; Mfano wako huu nadhani ni moja ya case studies juu ya jinsi gani mfumo huu wa uchumi ulivyokuwa na nguvu ndani ya jamii yetu; Lakini je, tutegemee katiba mpya pia kuondoa mfumo huu?

Hoja yako ya mwisho kuijadili hapa ni juu ya umuhimu wa kuunda TANZANIA UFISADI RECONCILIATION COMMITTEE [TURC]; Hoja hii ni ya msingi sana, na nilizungumzia kitu kinachofanania na hiki wakati najibu hoja ya mwenzetu mwingine nguruvi3 kwenye bandiko namba 54 ambapo nilishauri uundwaji wa Anti Corruption Coalition in Tanzania; Ingawa hauja thibitisha, kama itakuwa nimekusoma vizuri, wewe (kama ilivyo mimi), ni muumini wa kambi inayoamini kwamba tatizo la rushwa linaweza kutatuliwa na wananchi wenyewe yani bottom – up, na sio na viongozi yani top – bottom/up; Je, nipo sawa katika hili?
 
Last edited by a moderator:
Kwanza, nadhani uelewa wetu juu ya dhana ya bottom – up ni tofauti; Inawezekana kwa mtazamo wenu, watu at the bottom ni watanzania maskini huko vijijini; Kikatiba, watanzania wana haki nyingi, lakini kati ya hizi, pia ipo haki ya KUCHAGUA na KUCHAGULIWA katika nafasi ya uongozi; Kama tunakubaliana katika hili, wale wote ambao waliamua kutumia haki yao ya kikatiba ya KUCHAGULIWA (badala ya kuchagua) kwa kugombea nafasi ya uongozi na wakafanikiwa, hao ni sehemu ya watu ambao wapo at the top; Na wale wote ambao wanaamua kutumia haki ya KUCHAGUA (badala ya kuchaguliwa), basi wote hawa wanakuwa sehemu ya watu at the bottom; Kwa maana hii, mimi pia ni mmoja wapo, na nadhani hata wewe, lukolo, bongolander, DSN n.k; Kama tunakubaliana hadi hapa, basi nadhani wewe kupinga kwamba bottom – up approach haiwezi kuleta mabadiliko husika, basi ni kukataa kwamba mimi, wewe, Lukolo, bongolander, na wengine ambao tumeamua kutumia haki yetu ya kikatiba kuchagua (sio kuchaguliwa) ili wengine watuongoze, hatuwezi kuleta mabadiliko husika; Hili nalikataa!!!

Mchambuzi nami nakubaliana nawe kwa yote unayosema, ila kuna jambo la msingi ambalo linapaswa kuangaliwa kwa mapana yake nalo ni mfumo upi unatumika ndani ya TAIFA kwa jamii kupokea na kutoa mchango wao kwa TAIFA,kwenye serikali yao,tukiachana na harakati za kawaida za maisha kama mwajiliwa kwenda kazini, mkulima kwenda shambani, na mwanafunzi kwenda shule, na mama na wana jumuihiya wengine walio nyumbani kuendendela na majukumu yao ya kila siku hapo nyumbani.Ukichunguza tunavyoishi katika maisha yetu ya kila siku kwa siku tuko mbali sana kimahusiano kati ya wachaguliwa [Top bottom] na hao wachaguaji [Bottom up].

Umbali huu wa siku kwa siku uturejesha kufahamiana kwa sababu za za kufaidika ama pale bottom up anapokuwa na shida inayohusiana na shughuri muhimu za huduma zinazohusiana na serikali kama taarifa za kujaza form maalumu, mambo yanayohusu hati na nyaraka muhimu za kiserikali,ama mchaguaji anapokuwa na migongano ya kijamii inayomfikisha huyu bottom up mikononi mwa mamlaka zinazosimamiwa na top bottom na mwisho ama mwisho pale uchaguzi wa kuwaweka matop bottom kwenye mamlaka hivyo nao ututafuta wapate baraka zetu kuwaweka kwenye kilele tena ,tayari tena kwa safari nyingine.

Hivyo kwa silka hiyo na ukilinganisha na elimu na upeo wetu walio wengi,kwa walio wengi hakuna fair ya win win situation kati ya Top bottom dhidi ya Bottom up.Kwa kuwa ni dhana iliyojenga kwa wengi kuwa yule TOP BOTTOM mliyekuwa mnakunywa nae kahawa vijiweni,mnakunywa naye uji majumbani pindi anapochaguliwa toka kwenye kundi la wachaguaji mara baada ya kupata mamlaka katika ngazi yoyote ile, iwe kuanzia level ya kijiji,kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda na mpaka Taifa ghafla mchaguliwaji UGEUKA kuwa si miongoni mwetu tena bottom up bali ni miongoni mwao the Top Bottom.

Hivyo kupitia ideology hiyo isiyo lasmi, ambayo imejengwa na mfumo kupitia chama tawala na hatima vyama vya upinzani kurithi,jamii imegeuka na kukubali kuwa, kuna WAO na KUNA SISI.Jamii imekubali kuwa YOYOTE anaepata mamlaka yoyote kwenye jamii katika ngazi usika,ugeuka kuwa maraika wa eneo usika,hapa ndipo utakapo sikia kauri za kiswahili kama fulani,kaula,fulani sio mwenzetu, ameshika bingo, ametoka, na mengineyo mengi kuonyesha kuwa mteule au mchaguliwaji kwa bidii zake sio zetu kafanikiwa kwenye maisha yake.

Tumegeuza mtumishi wa umma, yani mchaguliwaji [Top Bottom] amekuwa mtumikiwaji badala ya kuwa mtumishi wa bottom Up katika kuijenga jamii.Ni kwa swala hilo hilo Top Bottom wamejikuta nao kwenye mtego wa kukubali kuwa waanga wanojikaaanga kwa mafuta yao wenyewe.Wamejipanga kuchaguliwa ili nao wakatumikiwe,wanapofika kwenye ukweli halisia wateule na wachaguliwa wanatahamaki kukuta wanageuka kuwa watumwa binafsi wa kikundi cha wawakilishi wa wanaowatumika [bottom up].Ili kukidhi maitaji na matakwa ya kikundi linachowakilisha wachaguaji, wachaguliwaji wanaingia katika uchuuzi na uuzaji wa mali ya wachaguaji ili wapate mtaji wa kuludi tena kwenye chaguzi zingine.

Waswahili wanasema mazoea ujenga tabia,tulipofika tumejenga ukuta kati ya bottom up dhidi top bottom.Bottom up wamejikuta kwenye mtego mkubwa, wakati wanatafuta mitaji ya kuwagawia kikundi cha baadhi ya wachaguaji, njia na maalifa yaliyotumika kukwapua mali ya pamoja imekuwa ni mzigo, hivyo kwa gharama yoyote ile, ni lazima siri hizo za ukwapuaji zisivuje.Hivyo top bottom wanaamua kubuni mbinu na mikakati ya kisomi, na hata wakati mwingine isiyo na sura nzuri kuahakikisha kuwa yeyote yule toka eneo la bottom up, asipaze sauti kokote kule, bila ruksa ama kibali toka kwa top bottom.Mpango huo kuna wengi wamekumbana nao mfano DK ulimboka ni moja ya matokeo ya bottom up kupaza sauti na hatimae mwisho wa sauti yake Mchambuzi umeiona.

Binafsi nina marafiki wengi ambao nimesoma na kucheza nao, tumejadiliana nao mengi na kupanuana mawazo mengi sana enzi hizo tukiwa shule, lakini leo hii, ni vijana wenye nyadhifa kubwa ndani ya serikali, na vyama lakini ajabu we dont speak the same language tena.Hatuongea tena wala kupeana mawazo kama vile tulivyokuwa shuleni na vyuoni, siku hizi sio fulani bali ni Mheshimiwa fulani.Ukitokea ukajipendekeza kwake mara mbili tatu atakwambia yuko bussy kinachofuata kwa sie wenye kuunga dot unajua huyu siyo yule fulani uliekuwa unamjua mkiwa shule au chuo.Tayari unapata picha kuwa jamii na mfumo umemshape kufunga milango ya ufahamu na kusikia kile wachache top bottom wanachotaka kusikia, anakuwa hayuko huru tena kam alivyokuwa huru.

Upofu huo wa Top bottom sio tu umekuzwa na mfumo na jamii kwa ujumla kwenye sekta ya kuchaguliwa na kuchagua bali hata kwa wasanii wetu, jana msanii aliyekuwa chini akishapata jina si msanii yule tena bali ni maraika msanii mwingine kabisa.

Binafsi naona madaraja na kuta tulizojijenga kati ya wachaguliwaji na wachaguaji. Kwa Bottom up kupaza sauti na kuanza harakati za kupingana na rushwa na mama yake ufisadi zataka kwanza wapatikane wachache kutoka kundi la Top bottom watakao kubali kuwa wasaliti wa kundi mama la Top bottom na hivyo kusimama na kuongoza kundi la bottom up kusema rushwa na ufisadi mwisho.Na woga wa kundi la baadhi ya wale walio Top bottom ambao wanavutika kuipenda Nchi kwa kungalia Taifa linakoelekea, kila wanapojalibu baadhi kusema wawaamshe bottom up kujua haki zao bottom walio wengi tumeathirika na baadhi ya namna baadhi ya mikakati ya Top bottom imejengwa kwa vitisho hivyo kuona kuwa kundi la Top bottom ni wateule toka kwa Mungu,na hapa ndipo utasikia kauri za kiswahili kama ameandikiwa, sio mwenzetu, na mengine mengi yenye sura ya vitisho na hofu hivyo bottom up pia wamekuwa wasaliti!!!!!

Pili, ni kuhusu suala la Civic Media, hii ni tofauti na centrally controlled and distributed media kama TBC, ITV, Tanzania Daima, Uhuru n.k; JamiiForums ni sehemu ya CIVIC MEDIA, na such a platform ni sehemu ya watu at the bottom; Katika mjadala huu, tayari tupo vitani challenging tuliowapa dhamana kupitia CCM, Chadema n.k; Na nadhani unakubaliana na mimi kwamba JamiiForum as CIVIC MEDIA platform imefanikiwa sana kuamsha watawala na viongozi huku juu na aidha kubadilisha tabia zao, au kufanya kazi kwa maslahi ya taifa; Kwa kifupi, JamiiForums as CIVIC MEDIA, and part of the people at the bottom, is well recognized at the top; Ni kwamba tu JamiiForums inashindwa kumalizia the last mile ambayo kwanza ni lazima ianze kwa watu kuacha kujificha sura na majina yao na kujitambulisha, kisha kusimamia hoja zao kwa maslahi ya taifa, watambulike kimakundi kutokana na itikadi, misimamo yao n.k; Hii tabia ya kujificha jificha sana sana itafanikisha kazi ya whistle blowing na mengineyo ambayo rarely lead to change;

Mkuu kuna sie wengine tunao amini kuwa kuna wakati mwingine, subira yavuta heri,ni kweli jamii forum imetoa mchango mkubwa sana kwa TAIFA,kuna watu wenye avatar na idendity ambazo kama sura zao zingewekwa wazi kwa yale waliyoyaleta humu na hakika wengi wao wangekuwa na makovu ya kuathirika na hata kupoteza maisha.Taarifa za JF zimeingia kwenye vyumba vingi sana ndani ya majengo ya serikali na nje yake.Hivyo bidii kama hizo bado ni pongezi kubwa sana kwa wana JF kwa kushirikia kujenga Taifa lao japo kwa kutumia vivuli lakini wamesikika na mengi yamefanyiwa kazi na uenda mengi tu yajayo yatatupa nafuu ya Taifa na pengine kwa mapenzi ya Mungu Tiba kabisa ya Taifa.

Kwa kuwa mfumo umeshape kudhibiti kile ambacho, kinaonekana kitaleta athari dhidi ya wachaguliwaji basi ni ngumu kuwapata washriki wa uso kwa uso zaidi ya watu walio gizani kulusha mawe kwenye paa la nyuma na kumnyima usingizi mwenye nyumba na kwenye fujo na vulugu hizo uenda mwenye nyumba akatoka nje na bastora yake lakini kama ajui kanuni za giza uenda mawe yakamdondokea kwenye giza hilo, na hivyo kutoa nafasi ya ushindi wa watu walio gizani.Moja ya faida kubwa ya gizani aliyekwenye mwanga ni ngum kumuona aliyegizani.

Na tatu, nadhani unakubaliana name kwamba mamlaka ya juu kabisa ya nchi ipo mikononi mwa umma; Rais na wengine, hawa wapo kwenye nafasi zao kwa dhamana tu ya UMMA, sio vinginevyo; Njia sahihi ya umma kujiletea mabadiliko ni kwa kujihusisha na a political process aidha kupitia a political party inayoendana na aspirations zao, au a political movement, hakuna zaidi ya haya; mwisho wa siku, kama watu at the bottom wataendelea kuwa na mshikamano, loyalty, selfless, and committed, hakuna kitakachowazuia kujiletea mabadiliko, iwe sijui ni Polisi, TISS, Jeshi, Ikulu, DPP, au vyote kwa pamoja; Sidhani kama unalikataa hili; Tukiungana kupigania maslahi ya taifa, upo uwezekano kwamba wapo baadhi watapoteza maisha kwa sababu wanapambana na status quo, lakini loyalty, determination, selflessness, commitment, to the cause vikiendelea, ushindi dhidi ya rushwa utapatikana tu, again, Bottom – Up!!

Hii nayo ina nguvu yake lakini pia,inapaswa kujijenga nje ya kuwazia kuwa ukiingia ikulu ndio mambao yote!!!Hizi movement za kutaka kuingia Ikulu,nazo uwa zinapata usiku toka kwa baadhi ya wana mfumo pale wanapokosa viashiria vya wakimbilia ikulu, kuwa dhamila kuu hasa nini?hivyo uishia kusupport kauri ya kiswahili ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili,yani ni heri ya CCM kuliko huyo wasie mjua.Rejea wimbo wa mrisho mpoto, kuwa waliopo madarakani yani CCM hatuwataki lakini wanaotaka kuingia madarakani yani CDM na CUF na wengineo HATUWAAMINI!!Kwa picha hiyo ya msanii Mrisho ambae ni kioo cha jamii unaweza kuona jins jamii inavyoviona vyama vya siasa.

Najua viongozi wa vyama vya upinzani hasa CDM wanajua kuwa kuna mfumo,je wanajijenga vipi kupata nafasi ya kukubalika na kuwaaminisha kuwa wakipewa Nchi wataifikisha huko wanakoona kunastahiki kuwapeleka Watanzania.

unakubaliana na hoja zangu tatu hapo juu, sina shaka kwamba kuanzia sasa utaanza kujitambua kama sehemu ya watu at the bottom, na kwamba KWA PAMOJA, TUNAWEZA KULETA MABADILIKO; Kama sehemu ya watu at the bottom, tunaweza kupigana na rushwa kwa njia mbalimbali, hasa kupitia information awareness raising, na kama unavyojua, information is power; Pia tunaweza kufanya mobilization ya wenzetu ambao tupo nao chini, lakini wao kwa sababu moja au nyingine wapo less fortunate in terms of knowledge, education, access to assets za kuweza ongeza uwezo wao wa kuelewa na kuchambua mambo n.k; Together, tunaweza kabisa kufanya kazi to advocate and support legislation zinazolenga kutatua ufisadi pamoja na taasisi zenye uwezo wa ku – expose ufisadi katika jamii;

Da hawa jamaa kwa bahati mbaya,jambo ambalo nimekuwa naumia nalo sana ni ile la TISS,kutotaka kuachana na kuweka mkono wake ndani ya CCM.Najua wao kama wao wanaitajika kuingia ndani ya vyama vya siasa kwa njia ya kulinda TAIFA,lakini kitendo cha kuegemea na kusupport nguvu ya CCM huku wakitumika kubomoa vyama vingine kwa mujib wa taarifa tunazozipata humu ndani ya JF na vyombo mbalimbali vya habari, wakitajwa kuhusika kwao na maonevu hayo kwangu mimi ili ni tatizo linalonikera sana.

Kuhusu polisi wao ndio imekuwa balaa,kiasi kuwa huko tunakokwenda, kama Polis hawatabadilika hakika itabidi hali iwe sio hali tena.Na kama TISS wangefanya kazi yao kwa uhakika haya yanayojili ndani ya jeshi la polisi yasingekuwapo.Na pia ujio wa katiba mpya utawatoa TISS toka mikononi mwa ofisi moja kwenda kuwa TAASISI [INSTITUTIONAL] ya KIKATIBa na hivyo wao kuwajibika kuilinda TANZANIA na sio chama cha kisiasa.

Kunawakati mwingine najiuliza TISS ya juu ni watu wenye umri mkubwa kiasi, baadhi yao wamefanya kazi enzi ya mwalimu hivyo mageuzi haya ya kuiondoa TISS kutoka kuwa taasisi yenye jicho la kuangalia watu au kitu chenye mwelekeo wa kuhujumu viongozi,bali kikusanye nguvu ya kitaasisi yenye macho makubwa ya kuangalia nani au kitu gani kinamkakati kuhujumu uchumi, fedha, afya, elimu, utamduni, maliasili na ilo la kuhujumu viongozi [yani watu personal] likawa ni sehemu ndogo kutoka katika sehemu kuu mama zenye nafsi kubwa ya kuhujumu Taifa.Watanzania walio wengi ni waoga sana juu ya taasisi hii ya TISS, kitu ambacho si sawa.


Na wao kama Taasisi sioni bidii zao za kujijenga kuwaaminisha umma kuwa wao sio tishio kwa raia mwema yeyote yule na kuwa wapo kulinda na kupambana na chochote chenye lengo la kuhujumu Taifa la Tanzania na mipaka yake.Dhana na mapokeo ya Watanzania walio wengi TISS ni kitu chenye kutisha sana.Lakini kwa mtu mwenye ufahamu TISS inapaswa kuwa na sura mbili moja ni jinsi raia wanapaswa kuiona na kujua kazi zake,mbili utendaji na upatikaji wa taarifa zake na jinsi inavoendesha shughuri zake inabaki kuwa ndio siri ya Taasisi hiyo.

Binafsi sipendezwi na jinsi umma unavywachukulia idala hiyo,japo binafsi uwa sipendi kuona inaitwa idala kwa kuwa mwenendo huo wa kuwa idala umeifanya kuwa kitengo kidogo na tafsiri hiyo imejijenga kuifanya wajanja kuichezea kupitia sheria zake zisizo na meno makali yenye kuchana na kulalua yoyote pindi akichezea katiba ambayo ndio msaafu mama, wakti kupitia wao ndiko uhai wa TAIFA ulipo lala.

Bottom – Up approach to tackling poverty inaweza kufanikiwa kwa kufanya haya, miongoni mwa mengine mengi:
Kwanza – ni kwa watu at the bottom kuunda kitu kama 'an anti corruption coalition' lationskuanza na petty corruption, virushwa vidogo vidogo polisi, mashuleni, mahospitalini, idara za serikali zinazotoa huduma kama vile Ardhi, TRA, RITA, BRELA n.k; Kazi kubwa hapa ni kwa wale waliopo at the bottom kama mimi na wewe, to take a lead kwa kuelimisha wenzetu tulionao chini ambao ni less fortunate (kama nilivyojadili), juu ya one's right na pia to challenge the notion kwamba rushwa katika jamii ni suala ambalo halikwepeki; Jukumu kubwa hapa ni kubadilisha mindset za watanzania wenzetu kwa kutumia silaha kuu tatu:


  • Information;
  • Education; &
  • Awareness Raising;

Ujumbe wetu from the bottom, unaweza kuwa disseminated kwa kutembelea shule za msingi na sekondari nchini, kuendesha forums mitaani na vijijini, talk shows kwenye redio, na muhimu zaidi, katika kila chaguzi, ku – endorse wagombea udiwani, ubunge na Urais ambao wanaendana na vision and mission ya our civil organization;
Huko mashuleni walishaanza sana haya majukwaa, lakini hao takukuru kawaulize kama wanampango/strategy ya mwaka mzima kuadovate dhidi ya rushwa.Sijaona mkakati madhubuti wa kucampain juu ya rushwa.Kama wangekuwa na mikakati wangeaanza leo kutoa matangazo ya kampeni dhidi ya rushwa za chaguzi na huduma za serikali.Ukikaribia uchaguzi utaona wanaanza kulipuka na mabango ya miezi miwili awareness.

Kama wangekuwa takukuru wako well organized kwenye swala la kampeni, na hakika hata kwa nguvu yao kwa kiwango fulani wangepunguza rushwa kwa kiwango kikubwa.Sijuai hata kama wana kitengo cha Marketing.Naamini wakijibrand na kwa kutumia wataalamu wa marketing jumbe nyingi sana zinaweza kuwafikia wanachi na kupanua elimu kwa umma juu ya mapambano ya rushwa.Yapatayo yanweza kufanywa na taasisi ya rushwa kukampeini juu ya rushwa kwenye chaguxi na rushwa kwenye jamii na ofsi za serikali.
1: Kutembelea vijijini na kuonyesha cinema na kugawa vipeperushi na posters kwenye mashule.
2: Kuwa na matangazo yenye mfumo wa vibonzo na picha za vitendo yatakayoonyeshwa kwenye TV frequently kwa muda wa miezi miwli mpaka mitatu, vikionyesha raia na wawili mpokea rushwa na mtoa rushwa wakikamatwa na kufungwa.Tangazo la sekunde 60, kama tunavyo yaona matangazo ya mashirka ya simu na mengineyo.Kwa kawaida tangazo moja likionyeshwa kwenye TV kwa muda wa wiki mbili taswila yake itamchukua miezi miwili na nusu kukaa kichwani mwa mtizamaji.Ebu pata picha umma uone tangazo la Takukuru kwa miezi mitatu hakika ufahamu huo utaibua aina nyingine ya ufahamu kuhusu rushwa.
3: Kushirikia vipinidi vya TV na kupata nafasi ya kusikiliza kero za watu hadharani,japo kwa kusikia taasisi itajifunza na kupata taarifa ambazo uenda wasingezipata.
4: Kuwa na Customer service,na hivyo kuwafanya waleta malalamiko wajikie kutoa ushirikiano,muonekano wa wasikilizaji wa customer care wanapaswa kuwa well trained na sio kuwa na sura ambao mtoa habari anajihisi yuko kitoc ha polisi na anafanyiwa mahojiano.

Yako mengi kadha wa kadha hizi taasisi zinaweza kuyafanya na vivyo hivyo taasisi zingine kama NGO's, Tume ya Uchaguzi, nk.Na hapa ikibidi TISS kuingilia kati kuahakikisha kuwa umma unapewa elimu halisi kuhusu haki zao za msingi!! na sio kuacha upotoshaji na vitisho kupokewe na wananchi.Mfano mamaneno kama ukichagua CUF, au CDM nchi itakuwa kama Rwanda.hakika kufumbia utamaduni huu, eti kwa kuwa itaifavor CCM basi ni kulimbikiza sumu ambayo mpasuko wake ni janga kwa wote na sio CCM ama CDM pekee yao.

Pili – tunaweza ku mobilize wananchi/raia kimakundi based on Gender, Age, Occupation, n.k, na kuunda kamati za wananchi ambazo kazi zao itakuwa ni kufanya monitoring ya bajeti - matumizi na ukusanyaji wa kodi; pia tunaweza organize citizens' hearings na ku – push for greater transparency and accountability, na yote haya yatasaidia sana budget controlling, kwani tutakuwa na control system in place ambapo viongozi watakuwa held accountable and confronted for misuse of public funds, kuanzia ngazi ya chini hadi juu; hii itajenga accountability and transparency in administration at all levels;
.
TISS wakijitoa kwenye hizo lalamiko la kulalalmikiwa kuwa wanatumika kuwajenga CCM, basi sehemu ambazo haki na elimu juu ya mambo ya msingi kupinga rushwa yangepata nafasi ya kutibiwa ni mobilization.Lakinii kwa jinsi ilivyo na kwa kuwa bado kuna wakubwa wanaamini kuwa ni halali TISS kuitumikia CCM basi bidii hizo uko yatakojili huko kwenye mobilizatio sipati picha!!!!!!!!!!!!!Mpaka pale ufahamu wa walinzi wa Nchi watapoweka TAIFA mbele na sio chama.

Tatu – is to empower the civil society, ambayo sisi ni sehemu yake; Katika hiki, makundi katika jamii yanakuwa organized and trained na pia kupatia political empowerment kuanzia local, regional and national level; Key hapa ni enhancing citizens' capacity kuchambua public budgets and accounts and to draw attention to ufisadi na rushwa; Pia research institutions and journalist associations zinaweza kuwa mobilized na kuungana na civil society katika vita dhidi ya rushwa;
Kwa sheria zilizopo, ni lahsi sana kubanwa,kuna sehemu nilikwenda kuomba taarifa nilichoambiwa, mimi ni nani mpaka kuomba taarifa hizo.yani naulizwa kuwa who is behind me,yani hawaamni kuwa kuna mtanzania wa kawaida kabisa anaweza kuomba taarifa za taasisi fulani kuhusu jamii fulani, bali mpaka uwe umetumwa.Fuatilia Breakifast Clouds FM Gerad na bonge wanapokuwa wanatfuta taarifa fulanitoka kwa kiongozi wa eneo husika uone mziki wake waokumbana nao.Mabadiliko ya ujio wa sheria mama za kikatiba ambazo zitampa raia wa kawaid auwezo wa kusimama mahakamni na kumshtaki mtumwenye dhamana ya Taasisi na kusiwepo na mkono wowote kupindisha hilo mpaka pale haki halisi inapopatikana kwa niaba ya taasisi au mtu husika.

Leo hii ukipigwa na polisi ukajeruhiwa ukasema uenda mahakamni haki yako ya kujeruhiwa uko utaisikia ndotoni!!!Lakini kupitia Taasisi za kikatiba ,haki ya mtu mmoja mmoja na haki za kitaasisi zitapata msimamizi kwa kuwa kila mmoja atasikilizwa sawia na hakuna atakae hujumiwa kwa kuwa kuna vyombo vingine vitakuwepo kama watchdogs kuona haki inatendeka kwa mujibu wa mahakama na faida na usalama wa jamii yani Taifa.

Mwisho, ni muhimu kwa wananchi kuwa nyuma ya wanasiasa na watumishi wa umma ambao wataamua kujitoa mhanga na kupigana dhidi ya rushwa from within; Wananchi pia ni muhimu wakashinikiza wawakilishi kuandaa legislations zinazopinga ufisadi na rushwa, au wakaziunga mkono kila mara wawakilishi wao wanapozipeleka bungeni; Whether Spika wa bunge azipokee au asizipokee, hii isiwe sababu ya wananchi kukataa tamaa kwani kuna njia kuu za aina mbili za kuleta mabadiliko – kwanza ni kupitia Chama Cha Siasa ambapo mchakato wake unapitia Bungeni, na Pili ni kupitia A Political Movement, ambapo mchakato wake hupitia kwenye jamii; Mafanikio ya TANU kwa mfano as a political movement yalipitia Jamii, Sio Bunge la Mkoloni;

Hiki neno watanzania tumekuwa wanafiki sana sana!!! wale ambao wako mstari wa mbele kupigania maslahi ya wengi mara nyingi siku hizi hawana mvuto, na wamepewa majina kibao, wabanaji, wanoko. Siku hizi ukiwa na uwezo wa kusema maovu wazi wazi,hakika utakuwa mashakani, maneno mengi sana yatakuangukia.Yani jamii imekubali kuwa watu wenye matendo ya kiovu kama wizi, dhuluma, ubabe, nk kuwa ndio wajanja,na wano heshimika kwenye jamii yani ile kanuni ya Jungle Law survival of the fittest ndio formula kwa wote walio na ubavu na wasio na ubavu wote watachungwa ndani ya zizi moja.Jamii imekuwa wapenzi na mashabiki wa watu ambao wamepata mali zao kwa njia za kiovu, utasikia maneno kama jamaa mjanja, kapatia, kibosile, don nk.

Ni muhimu pia Tanzania ikaja na Watch Dog Institutions on Corruption na Pia Critical Journalism ambazo zitafanya kazi na civil society to expose and fight rushwa na ufisadi;

Hiiiiii ndiyo TIBAAAAAAAAAAAAAAAAA Mchambuzi ya yote hayo.Yani hapo ndio when the court break become the court break haswa!! na sio The court break become the court breaker!!!.Hapa taasisi kama TISS, TAKUKURU, MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI [CIG], MWANASHERIA MKUU [AG], MAADILI YA UMMA NA UTUMISHI WA UMMA, na nyinginzo nyingi zitakapotambuliwa kikatiba basi kila mmoja anamwangalia mmoja kwa jicho la huyu anafanya nini kwa wananchi.

Ifike sehemu Askali akiua raia, kwa kukusudia TISS wanapokuwa na ushahidi kuwa askari huyu aliua wawe na uwezo kufungua mashitaka kupitia vyombao husika vya idala zake ambazo watazianzisha kuweza kumfungulia mashitaka na kufikisha mahakamani askali husika.Kuwe na ushahidi pale ambako wao walitoa ushauri kwenye taasisi fulani ya umma,kisha washauriwa wakapuuza na hatimae kuitia hasara serikali na hivyo kwa hatua hiyo wawe huru kusimama kimbani au mbele ya bunge kwa nia ya kuwajibisha kiongozi, idala, wizara, au taasisi yoyote ile.Vivyo hivyo kwa CIG na AG na DG wa Takukuru na taasisi yake.
 
Nguruvi3,

cc: Lukolo

Nimekusoma namba 55, na ninazidi kukuelewa; Ningependa kukuuliza maswali yafuatayo:

1. Je, zaidi ya wananchi kuimbiwa majukwaani, wamewahi kushirikishwa katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi? When, Who, Where and How? Nini ilikuwa matokeo?

2. Kati ya wananchi na viongozi, nani ana wakati mgumu wa kupambana na rushwa? kwanini?

3. Kati ya wananchi na viongozi, nani amemwangusha mwenzake zaidi katika vita hivi? kwanini?

4. Je imani yako kwamba top - down approach can be more effective, ina uhusiano wowote na matarajio ya katiba mpya?

5. Je nikisema kwamba - Mwalimu kwa kutumia top - down approach alifanikiwa kudhibiti petty corruption lakini sio grand corruption, utakubaliana na hoja yangu? Na iwapo utakataa au kukubali, kilichomwangusha with grand corruption ilikuwa ni watu at the top au watu at the bottom?

6. Ni kweli Civil Society imejaribu sana lakini je, as an umbrella or as individual entities? Kuna any Community Based Organization au NGO ambayo its primary purpose is to fight corruption in Tanzania? Ni ipi au zipi? Kwa uelewa wangu, zina deal na loose issue ya good governance;

7. Kuhusu suala la Uswisi, EPA, Kagoda, Richmond...unaposema tumejaribu kuulizia na kushinikiza.., tumejaribu ni kina nani, individually au as a group?

8. Na mwisho, je, bottom - up approach lazima ihusishe ghasia?

Kama nakusoma vizuri, nahisi unahusisha bottom - up approach na mapinduzi; naomba unisahihishe iwapo sipo sahihi juu ya hili; Vinginevyo, bottom-up inaweza kuchukua sura ya political movement, na jedwali hapo chini linaweza kutusaidia kujadili jinsi gani suala la ufisadi tunaweza kulitatua nje ya vyama vya siasa; Source ya Jedwali hili ni Goran Hyden:

9. Je, vita dhidi ya ufisadi, in your view vifuate orientation gani, cause or issue?

Source: Goran Hyden
VARIABLE
MOVEMENT
PARTY
OrientationCauseIssues
Level of OperationRegimeGovernment
Main Arena of OperationSocietyParliament
Method of OperationMobilizationPersuasion
Member OrientationDiffuseSpecific
Claims to ResourcesNo Formal LimitsConstrained by Rule of Law
 
Mkuu Nguruvi3 tupo pamoja sana. Nimefurahishwa sana na mifano uliyoitoa katika kukosoa bottom-up approach. Ni bahati mbaya sana kwamba mimi niliisahau. Mchambuzi, si kweli kwamba sisi tunawafikiria wakulima kama reference yetu katika bottom up approach. Tunawafikiria wananchi wote wakiwemo wafanyakazi wa Ikulu ambao ni subordinates wa Rais (wakiwemo maprofessor pia). Pamoja ya kwamba umetoa mifano ya mimi, wewe, Jingalafalsafa, bongolander na wengineo kwamba tunaweza kuwa ni wamojawapo, lakini mimi bado naona changamoto kwenye uanzaji wa hayo mapambano. Ni lazima awepo initiator mwenye influence. Lakini je atasikilizwa, ataachwa tu kuendelea kusema anayoyasema, hawatam-Ulimboka? Nguruvi amewataja wanaharakati mbalimbali ambao walisimama na kupaza sauti wakawahabarisha wananchi, wakaikemea serikali, yet hakuna kilichobadilika. Sasa huyo initiator mwingine mwenye influence kubwa kuliko za akina Dr W.Slaa waliosimama na kutaja majina ya Mafisadi hadharani na bado hawakusikilizwa atakuwa nani mwingine wa kuanzisha hii movement na ikawa na impact?

Nimependa mfano wa Nguruvi3 kuhusu kashifa mbalimbali zilizowahi kuibuliwa na watu wa chini na hazikufanyiwa kazi na mamlaka za juu. Kwa mfano ni kwa kiasi gani magazeti na vyombo vingine vya habari vimekuwa vikiandika madudu ya ofisi mbalimbali nchini na hatua hazichukuliwi? Ni kwa kiasi gani hata bunge tu limekuwa likiibua mambo kibao na kumwagiza rais ayatekeleze na hakutekeleza? Hizo kashifa za EPA, RICHMOND, RADA na nyinginezo zisizo na idadi zimeshughlikiwaje? Sasa hiyo bottom up nyingine ya kuleta mabadiliko itakuwa ipi? Somewhere Mchambuzi umeongelea suala la Watch dog institutions na critical journalists. Je hukumbuki kazi iliyofanywa na akina Jerry Muro? Huyu bwana aliamua kutenga kipindi kabisa cha kujadili rushwa, na kujaribu kuonyesha harakati za kuikabili rushwa; sasa hivi yuko wapi? Hudhani kwamba atakuwa anajutia uamuzi wake wa kujaribu kujiingiza kwenye hayo mapambano? Niambie wewe Mchambuzi unaweza kujivika ujasiri wa Jerry Muro tena, baada ya kuona yanayomsibu? Tusitiane moyo humu kwenye forum bwana.

DSN amebase sana kwenye katiba, na anadhani kwamba katiba linaweza kuwa suluhisho. Nakubaliana naye kwa kiasi fulani. Lakini bado nakwenda mbele narudi nyuma, kama hakuna commitment ya uongozi wa juu kabisa wa nchi, katiba is nothing. Kwani ni sheria na taratibu ngapi zilizowekwa na wananchi na zinakiuka? Hata katiba ya sasa ukisoma kipengere cha maadili ya utumishi wa umma inaeleza kinagaubaga kuhusu masuala ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Lakini ni nani anayejali? Hata tungeweka katiba ya namna gani kama hakuna kiongozi madhubuti wa kuisimamia, itakuwa ni kazi bure.

However, nakubaliana na hoja ya Nguruvi juu ya suala la vyombo vya kupambana na rushwa kama vile TAKUKURU viwajibike moja kwa moja bungeni. Hata kwenye tume ya kutoa maoni ya katiba nimelisema hili. Maana pale kunapoonekana kuna uzembe katika mapambano ya rushwa bunge ndiyo limfukuze kazi mkurugenzi wa TAKUKURU si kama ilivyo sasa ambapo bunge linaagiza mkurugenzi wa TAKUKURU afukuzwe, rais anaamua kujikausha. Sasa huo si ni uvunjaji mwingine wa katiba kwa Rais kutowatumikia wananchi waliomchagua. Ndiyo maana nasema hakuna njia nzuri zaidi ya kuwa na rais ambaye ana serious commitment ya kupambana na rushwa. Rais akiwa mla rushwa unategemea atawezaje kuwadhibiti wala rushwa wenzake? sanasana atakachokifanya ni kuwadhibiti vidomodomo wanaojifanya wanaipinga, kama walivyomdhibiti Jerry Muro.

Somewhere Bongolander amechallenge uwezekano wa kiongozi kutoka CHADEMA na anafikiri bado kiongozi bora anaweza kutoka CCM. I am not a fun of a chama. I am rahter a fun of a person. Anaweza kutoka CHADEMA na bado akawa mla rushwa. Lakini katu hatuwezi kupata kiongozi bora ndani ya CCM kwa kuwa mafisadi wakubwa wa nchi hii ndiyo wanaoilea na kuiongoza CCM. Kwa hali ilivyo sasa ndani ya CCM, mtu awaye yote yule atakayeweza kupita katika chujio la CC, NEC na halmashauri kuu ya CCM na kukubaliwa kugombea urais kupitia CCM, atakuwa kwa vyovyote vile ana support ya mafisadi. Maana ndani ya CCM mafisadi ndiyo wanaoamua nani awe nani na wapi na si wanachama. Kwa hiyo sina tumaini hata kidogo kutoka ndani ya CCM.

Lakini tunaweza kupata kiongozi serious kutoka upinzani, bila kujali ni chama gani. Maana yeye akiingia atakuwa na visasi dhidi ya hawa wezi wa CCM. Kwanza kwa kutumia hela za wizi watakuwa wamempa wakati mgumu sana kwenye uchaguzi, kwa hiyo akiingia atataka awakomeshe. Sifagili uongozi wa visasi, lakini hivyo ndivyo hulka ya binadamu ilivyo. Atataka kuonyesha kwa vitendo kwamba anao uwezo wa kuwashughulikia na akishaonyesha mfano huo, hatataka na kwake kuchafuke.

Tunapoifikiria Top-down approach, tujifunze kutoka jirani yetu Rwanda ambako Kagame kasimamia kidedea suala la Rushwa to an extent kwamba kila mtu ndani ya Rwanda anamwogopa mwenzie linapokuja suala zima la rushwa. Hivyo ndiyo tunavyopaswa kuwa hata huku kwetu. Tumpate kiongozi atakayetengeneza system ya watu kuogopana. Yaani hata anayetaka kukupa rushwa unamwogopa, hata rafiki yako akikuambia kuna mahali mnaweza kupata chochote, unamhofia kwamba anataka kukuingiza kwenye mtego. Hivyo ndiyo inatakiwa kuwa. Na hilo haliwezi kuanza from no where, ni lazima wenye mamlaka walianzishe na walisimamie. Tuendelee kujadili. But I am signinig out from this discussion. See you another time!
 
Back
Top Bottom