Mangula, Dr. Slaa na Changamoto za Ufisadi Tanzania

Mchambuzi,

Hoja zako ni nzito na tutazijadili kama ulivyozigawanya taratibu.

Kwa kuanzia, Wanajamvi naona kuna kutomuelewa Mchambuzi katika aya ya kwanza kabisa ya bandiko lake.

Naomba kwa hisani yake niweke sawa alichokusudia ili tujikite katika mada zaidi na si katika sintofahamu inayojitokeza.

Katika aya hiyo ya kwanza, Mchambuzi ameandika kuwa ujio wa Kinana na Mangula umeonekana kuleta tumaini miongoni mwa Watanzania. Mstari wa mwisho ameuliza kwanini Mangula na Kinana kama watu wawili waonekane kuwa na uwezo wa kupambana na tatizo la kijamii na wala siyo taasisi kubwa zinazotumia mabilioni ya fedha za walipa kodi?

Kwa maneno mengine,iweje Mangula na Kinana wawe zaidi ya taasisi kama TAKUKURU ? Kwanini watu wanaamini kuwa Mangula na Kinana wana ufunguo wa tatizo la kijamii kubwa kuliko watu wawili, kumi, mia au elfu?
Na wala hukumaanisha kuwa ujio wa wawili hao ndio tumaini la suluhu.

Katika ayaya pili, natofautiana na Mchambuzi hasa pale anaposema Mchambuzi, huko mbele katika mada yako umezungumzia kitu kinaitwa Political will. Ili kuwe na consensus ni lazima kuwe na political will.

Nadhani wapinzani kwa ujumla wao wamekuwa ''pro-consensus'' kwa bahati mbaya hawana right partner katika kutafuta suluhisho.

Taarifa zote za tatizo la rushwa zinatolewa na taasisi za serikali, vyama au kupitia wazalendo wa nchi hii wanaochukua risk kubwa sana. Taarifa zimetumika kuifikia serikali ili ichukue hatua kama sehemu ya political will, consensus and solution

Tuna mlolongo wa matukio na mengine ya karibuni tu. Badala ya chama husika chenye serikali kushirikiana na Wapinzani, imekuwa ni kinyume chake. Kwa muktadha huo, je political will ipo? na kama haipo consensus itatoka wapi? Na kwanini tuanze kuwahukumu waleta mashitaka sawa na washtakiwa?

Mimi sidhani kuwa baada ya wapinzani kukosa partner katika suala hili,wao kulieleza kwa umma hiyo ni political asset! Yes, down the road inaweza kuwa hivyo lakini kwa wakati tulio nao hiyo inabaki kuwa silaha yao pekee katika vita dhidi ya rushwa Japo kwa kuanzia tu. Sina maana ya kuwa ni suluhu ya tatizo lakini basi ni sehemu ya utambuzi wa tatizo.

Kwa vile upande mwingine umeshindwa ''ku-cross the isle'' basi hilo linabaki kuwa liability by default.

Natumaini hoja yako ni ya utaifa zaidi ya uchama nami nakubaliana nawe kabisa.
Sina nia ya kutoka nje ya mada, tuendelee na core issue

Nguruvi3,

Asante sana kwa kunisaidia kuliweka suala hili vizuri zaidi hasa kwa wachangiaji ambao wanaona hoja yangu imekaa kichama zaidi; Kuhusu suala la political will na political asset, kimsingi nakubaliana na wewe; tofauti yetu kama ipo pengine ni kwamba - kuna ishara kubwa kwamba vyama vyote vya siasa vinajaribu kutumia hoja husika kisiasa zaidi, jambo ambalo linaweza kuwa sawa tu, ili mradi mwisho wa siku, the political process inatumika kuleta mabadiliko husika - kwa vitendo, sio kila upande kujaribu ku - manipulate suala hili kwa manufaa yake; Niseme pia kwamba nadhani uchaguzi wa 1995, suala hili lilikuwa manipulated kwa kumweka mgombea urais safi huku root-cause ya rushwa na ufisadi ikibakia intact bila kuguswa; ni muhimu tusirudi kule kule; nitajadili hili la political will na political asset zaidi baadae; Asanta sana;
 
Haya maandiko yako katika vifungu hivyo hapo juu yamegusa msingi na kiini kikuu cha historia ya Tanganyikaa. Kiini ambacho mara nyingi sana huwa hakijulikani au kwa makusudi hupotoshwa/kupuuzwa. So big thank you!

Nakumbuka kumwambia mchangajia mwenzangu, CHAMA (Gongo la Mboto), kuwa siku moja tungefanya mpango kuwa na uzi mpana ambao ungetufanya tujadili kwa kina na upana wa historia ya Tanganyika na baadaye Tanzania kwa miwani ya yanayotokea leo.

Ni ktk muktadha huu, wa bahari pana ya fikra na vigezo vyenye kuthibitika; ndipo tunapoweza kuelewa chanzo/kiini cha baadhi ya matatizo ya udini na ukabila (ambayo yameingizwa kwa nguvu na hila na wanasiasa ktk miaka ya karibuni na kubebwa na watu wengine kwa kujua au kutokujua) pamoja na rushwa, siasa za nje na uchumi doro.

Mara nyingi watunga sera, wanasiasa na wasomi wetu hajajishughlisha sana kwenye kutafuta na kutoa majibu yasiyojibu kwa upana na uzito wa matatizo tuliyonayo leo. Wamekuwa hodari wa kukata matawi huku mizizi na mashina vikiendelea kustawi na kuzaa.

Binafsi ningemwomba rafiki yangu CHAMA na wengine, tujumuike hapa maana ni fursa nzuri ya kuendelea kupanua bongo zetu ktk historia hasa ya kiutawala na kiserikali wa Tanganyika/Tanzania.

Samahani wadau kama nitakuwa nimetoka nje ya mada.

Mkuu Ronal Reagan,

Haujatoka nje ya mada, umezungumza ya msingi sana; utaona umuhimu wa hoja zako nitakapomalizia sehemu za mada yangu zilizobakia ambazo nitazikamilisha baadae leo, kisha tuingie katika mjdala husika; nashukuru sana kwa mchango wako;
 
Kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako, unafikiri Tanzania kuwa Problematic State kumetokana na Wakoloni? Au kumetokana tamaduni zetu watanzania?

Mimi nafikiri, tamaduni zetu watanzania zinachangia sana kwenye tatizo la rushwa. na sijaona bado mwanasiasa wa Tanzania akiongelea suala hili. Sijawahi kumsikia mwanasiasa yeyote wa Tanzania akisema tuna utamaduni wa kutoa na kupokea rushwa.

Most politicians are "Particularists" rather than "Generalists" .... and thats a big problem.

Swali zuri mkuu kobello;

Kwa mtazamo wangu, kama ulinifuatilia vizuri, kinachochangia tuwe na a problematic state ambayo kama hatupo makini itakuja kuwa a failed state ni informal institutions kutawala civic institutions ambapo rule of law, rationality na mambo kama hayo hayapewi kipaumbele; mkoloni alikuja na dhana ya a modern state lakini jukumu la such a state was not to serve the interest of weusi bali their motherland; ndio maana aliachia sana indirect rule iendelee katika maeneo mengi ili kurahisisha utawala wake, na kwa kufanya hivyo, literally, kazi ya kujenga a public realm in Tanzania with modern and civic institutions became impaired; Communities zikaendelea kuwa na umuhimu kama alizozikuta mkoloni;

Wanasiasa wengi wapo more loyal to local community institutions and traditions (based on ukanda, udini au ukabila), kuliko civic institutions ambazo zinaondokana na sense of community na kuegemea zaidi katika sense of collectivity; kutokana na weak penetration ya capitalist system katika jamii yetu, rural areas pamoja na informal institutions zake zimebakia kuwa dominant over formal institutions, na wananchi pamoja na viongozi wao ili wasonge mbele, wana lazimika kuwa more loyal na local community and informal institutions kuliko the state; in the end, the state and its civic institutions end up being PREY for viongozi hawa kwenda kuendeleza maeneo where they are more loyal i.e. community zao rather than taifa lao in a collective manner; Making the state a PREY, ndio huzaa ufisadi;

Nitajadili swali lako zaidi kwenye sehemu yangu ya TATU na NNE ya mjadala huu;
 
Inashangaza ni kwa vipi Mangula anaweza kuwa ni tumaini kwa watanzania wote ilihali Mangula huyo huyo ndiye aliyesimamia na kusuka mikakati ya wizi wa Mabilioni ya EPA, ili kumwezesha Kikwete kushinda uchaguzi kwa kishindo mwaka 2005?

Mangula anasifiwa kwa lipi kama si ubingwa wake wa kuiba? Yeye mwenyewe ni kiongozi wa wala rushwa ndiyo maana wakati ule alishindwa kumshauri wala kumsimamia mwenyekiti wake Mkapa alipokuwa anaingia mikataba ya kishenzi kama vile meremeta, IPTL, mikataba mibovu ya madini, uuzwaji wa mabenki na viwanda nchini kwa bei ya kutupwa. Hivi mtu aliyeisababishia maumivu makubwa kiasi hicho nchi yetu, leo anawezaje kuwa tumaini kwa watanzania?

Huyu ni tumaini kwa CCM kwa kuwa ni mwizi na mla rushwa mkubwa kama CCM yenyewe. Ndiyo maana walipoona mambo yamewawia magumu wamerudisha aje aratibu wizi mwingine wa kuiwezesha CCM kushinda uchaguzi wa mwaka 2015. Huyu kamwe si tumaini kwa watanzania bali ni janga kuu, na la hatari kwa Tanzania ya sasa na ya kesho.

Mkuu nakubaliana na wewe kuwa sidhani kama kuna lolote kubwa la kutegemea kutoka kwa Mzee Mangula na Mzee Kinana katika kuondoa rushwa na ufisadi ndani ya CCM na hasa ndani Tanzania. Lakini inategemea lengo lao katika kupambana na aufisadi ni nini. Maana tunaweza kuzungumzia ufisadi ndani ya CCM, yaani viongozi na wagombea wao kwa wao kuumizana kwa rushwa, au ufisadi unaofanywa na CCM dhidi ya Tanzania na watanzania.

Mzee Mangula mwenyewe amekuwa ni victim wa rushwa ndani ya CCM na anafahamu fika jinsi inavyoenda na kuendeshwa. Labda anajua vizuri zaidi jinsi fedha za EPA zilivyogawanywa gawanywa na CCM kuwa mhimili katika issue nzima. Sasa anaposema anajaruibu kupambana nayo inawezekana anajua kabisa ni nini anachotaka kupamabana nacho, na anajua wazi kabisa kuwa anatakiwa aanze na nani na anajua kuwa hawezi kushinda.

Mzee Kinana anajua vizuri uchaguzi wa 2010 ulivyokuwa na anawafahamu vizuri kabisa mafisadi ni kina nani na wapi wamefanya ufisadi kusaidia CCM ishinde 2010. Alikuwa kampeni manager wa JK mara mbili anajua kabisa kuwa kulikuwa na rushwa, wizi na mizengwe mingi kwenye uchaguzi. Kwa hiyo the whole party machine at this moment, kuanzia ngazi ya taifa, mkoa, wilaya hadi udiwani ni rushwa na ufisadi mtindo mmoja. Lakini mafisadi wanajulikana na wametajwa wazi, lakini hakuna aliyekamatwa wala kuchukuliwa hatua za kweli. Unless that happens, the whole talk about dealing with corrpition in CCM is just a bull. There is no way that these Mzee Mangula and Kinana can wipe it out. Nawaheshimu sana hawa wazee wangu, lakini let us be realistic.

Tukiangalia tunaweza kuona kuwa tuna graft na corruption, and if you look in detail you will see grand corruption is both individualized and institutionalized. CCM ina namna nyingi za ku-bribe watu, ukiangalia idara za usalama zote, TISS, Polisi, JWTZ karibu kote watu wanakatiwa keki kubwa na CCM ili kuwafumba midomo na kuwapumbaza, kila kukicha utasikia meja huyu, kapteni huyu, ofisa huyu anateuliwa kuwa waziri, mkuu wa mkoa, mkugenzi wa tume hii au idara ile....kuna mengine mengi sana.

Lakini tukumbuke kuwa the whole thing is very complicated and very intertwined than we see. Karibu kila idaraimeingia kwenye mtandao wa ufisadi kiasi kwamba kuanza kusema unadeal na watu kwenye chama peke yake, yaani kuwaondoa wadhaifu wanaotajwa kuwa mafisadi au kuwatoa kafara wawili watatu, na kuwaacha mapapa na kuiacha infrastructure yenyewe ya ufisadi iendelee kuwa hai....sidhani kama wazee wetu Mangula na Kinana wako serious. Bado hakuna political will ya kudeal na tatizo hilo.

Pamoja na kuwa mtoa mada amezunguzia ideas za Nyerere kuhusu rushwa kuwa adui wa watu, na rushwa kuwa adui wa haki, ukianza kuangalia kwa undani kwa sasa rushwa, be it adui wa watu or adui wa haki, is very much associated with CCM and its roots have gone deeper to the extent that rooting them out is a daunting task, next to impossible. In other words, the way corruption is associated with CCM, it makes it easy to see that CCM ni aduai wa watu na adui wa haki.
 

Kwa kuanza na hoja hii, nadhani sitakosea kama nitahisi kuwa kwa maoni yako tatizo la rushwa lipo more systemic than cultural. kwa Tanzania, tatizo la rushwa lipo more cultural, nikimaanisha kuwa ni utamaduni wetu kutoa na kupokea rushwa ili tupate huduma mbalimbali.

Kwa hiyo, CCM haina uwezo, sera wala mbinu za kumaliza tatizo hili katika ngazi yeyote. Na kwa kuwa wawakilishi wa wananchi ni wabunge, basi ni jukumu la waziri au wizara husika kutatua suala la rushwa katika taasisi zilizo chini ya wizara yake.
Wananchi hawana chombo cha kuwawajibisha watendaji zaidi ya bunge, au zaidi ya kura zao kila baada ya miaka mitano.Wananchi hao hao hawana ari au moyo wa kulifuta suala hili la rushwa kwa sababu kiasili tuna tamaduni za hongo na hatuna tamaduni za kuwajibika.
hakuna chama chochote cha siasa ambacho mpaka hivi sasa kimeeleza kinagaubaga jinsi kitakavyomaliza tamaduni hii, kilichobaki ni kujitahidi kuwaaminisha wananchi kuwa wao ni wasafi kuliko waliopo. Wakati si wasafi kuliko waliopo.
Hoja ya kwamba rushwa ni utamaduni wetu naona zinaashiria dalili ya kukata tamaa na kuliona kama ni tatizo lisiloweza kutafutiwa ufumbuzi. Wakati akina Nyerere wanagombea uenyekiti wa TANU au Urais wa nchi kwa mara ya kwanza walikuwa wanatoa bei gani kwa wananchi ili wapate ushindi? Au ni kwanini wakati wa utawala wa Nyerere rushwa halikuwa ni tatizo linalohitaji mjadala wa kitaifa?

Rushwa imeasisiwa na kupaliliwa na kuwekewa mbolea na CCM wakati wa utawala wa Mwinyi ambapo ubinafsi ulitawala kuliko uzalendo. Mkapa akaihuisha na kuipaka manukato akaiita Takrima, akatumia loophole hiyo kuuza viwanda na kuingia mikataba ya hovyo kwa njia za rushwa. Viongozi wengi wakaanza kujineemesha wao binafsi kuliko nchi. Kikwete akaendelea kuilea akitumia hoja dhaifu ya kulipa fadhira kwa mafisadi waliomuwezesha yeye kuingia madarakani. kwa mtu kama Kikwete ambaye wala rushwa wakubwa nchini ndiyo waliombeba na kumpeleka Ikulu tunaweza kutegemea nini? Wafanyakazi katika idara na taasisi za umma wameendelea kutokuthaminiwa na pia kumekosekana kabisa kiongozi serious ambaye yupo tayari kusimamia utendaji kazi wa watumishi serikalini. Hospitali imekuwa bila kitu kidogo hupati huduma hata kama unaumwa kiasi gani, mahakamani haki zinanunuliwa kwa rushwa. Hata hao tunaodhani ni usalama wa Taifa hivi sasa na wenyewe wamekuwa ni ma-agenti wa utoaji na upokeaji rushwa. Mwisho wa siku rushwa imekuwa ni sehemu ya maisha. Imefika mahali Kobello na Mchambuzi wanakata tamaa na kuiita utamaduni. Nakataa kabisa kwamba huu si utamaduni, ni kitu kilichoingizwa tu katika utamaduni wetu wa ustaarabu, uaminifu na uwajibikaji.

Binafsi naamini akipatikana kiongozi mmoja tu ambaye anaichukia rushwa kwa dhati kabisa kutoka moyoni. Hasa kwa nafasi ya Rais, atakayekuwa tayari kumfunga jela hata mke wake kwa kosa la kupokea au kutoa rushwa. Nchi itashika adabu. Na huu ubadhirifu mkubwa unaotokea nchini hautaendelea. Wala huhitaji mikakati mingi kama Kobello anavyotaka kutuaminisha. Unahitaji kutoa tamko tu na kuanza kutekeleza kwa vitendo. Ninaamini idara ya usalama wa taifa ikitumiwa vizuri inaweza kufunua mianya yote ya rushwa. Na iwapo tutakuwa na rais mwenye akili asiyeweza kuvumilia rushwa ataivuruga mianya hiyo yote na kuirudisha nchi katika mstari wake.

Uongozi wa hovyo na uliooza kama wa Kikwete na CCM yake (Kinana, Mangula na Nape) haujawahi kuwa na nia hiyo. Wanatuchezea shere kwa kuwapeleka akina Mramba mahakamani halafu kesi inasikilizwa kwa mwaka wa tano sasa na hakuna kinachoendelea. Na hawa watu wapo mtaani wanadunda, ni nani atakayeiogopa rushwa katika hali hiyo. Kila mwaka CAG analeta report ya matumizi mabaya ya pesa, na hakuna anayefungwa, wala kuhojiwa juu ya hayo matumizi, ni nani atakayehofia rushwa?

Nawahikikishieni kwamba hili tatizo la rushwa linaweza kuondoka hata leo. Na linaweza kutangazwa kuwa ni historia katika nchi yetu iwapo tu atatokea Rais ambaye yupo tayari kupambana nalo na ambaye kwa hakika atachuguliwa kwa nguvu ya umma na si nguvu ya pesa. Tatizo kubwa tulilonalo hivi sasa katika nchi yetu ni kwamba tayari CCM imewajengea mazoea wananchi kwamba wakitaka kura zao basi sharti wapewe kitu kidogo. Hiki ndiyo kinachotuumiza.

Sitaki kukubali kwamba rushwa ni utamaduni wetu hata kidogo, wapo watu waadilifu na wenye nia ya dhati ya kulitumikia taifa hili kwa uaminifu, lakini wanavunjwa moyo na viongozi wao wanaopokea na kutoa rushwa. Ndiyo maana ninasisitiza Mangula na Kinana si solution ya matatizo ya rushwa ya watanzania. Kwa kuwa wao wenyewe ni waasisi wa rushwa. Na kwa ujumla wake CCM si tegemeo tena katika kupambana na rushwa na umaskini nchini kwa kuwa kila mwenye affiliation na CCM ni mla rushwa. Ninaamini lipo tumaini kutoka upinzani kwa sasa.
 
SEHEMU YA TATU

Kama nilivyo ahidi hapo awali, Sehemu ya TATU ya mjadala wangu inahusu aina kuu mbili za rushwa Tanzania – ya kwanza ikiwa ni Rushwa inayo tokana na Rogue Individuals ndani ya Jamii, na aina ya pili ikiwa ni Rushwa ya KIMFUMO; Rushwa ya Kimfumo ndio tatizo kubwa zaidi kwa maana ya kwamba ndio inayozaa UFISADI; Na rushwa ya kimfumo kwa kiasi kikubwa sana, inakubalika Tanzania, even if not formally, lakini hii haijalishi kwani nchi yetu inaendeshwa zaidi na informal institutions kuliko formal institutions; tutaona hili baadae;

Tukianza na aina ya kwanza ya Rushwa i.e. inayotokana na Rogue individuals, Rushwa ya aina hii inatokana na hali ya watu/mtu mmoja mmoja kuamua kutumia ofisi ya UMMA kujilimbikizia mali; Watu hawa huwa ni watumishi wa umma (sio official members of CCM, Chadema n.k, kwa mujibu wa sheriaza ajira) na hufanya kazi kama bureaucrats na technocrats katika bureaucracy system ya Tanzania; Such ‘State Officials' watatarajiwa na umma, kufanya shughuli zao kwa mujibu wa rules, procedures, laws and the constitution;

On the one hand, a ‘state' is FIRM/IMARA pale watumishi wake wa umma wanapo ‘act' kwa mujibu wa rules, procedures and the constitution, hence provide a measure of certainty kwa umma as to what can be expected; Rushwa katika muktadha huu maana yake kuna violation of bureaucratic procedures, organizational norms, laws and larger societal expectations for the appropriate behavior of its public officials; On the other hand, a state is SOFT/DHAIFU watumishi wanapokiuka masuala haya, na hali hii kwa kiasi kikubwa sana inachangia Utawala wa sasa wa nchi kuonekana upo DHAIFU;

Aina ya Pili ya Rushwa has less to do with ROGUE INDIVIDUALS na badala yake, ni suala la MFUMO, whereby rushwa is embedded in society; Katika hili, rushwa is institutionalized and becomes the NORM rather than the EXCEPTION;

Kama tulivyokwisha jadili awali, Nyerere alijaribu sana to build and consolidate Tanganyika as a ‘STATE' kwa kuendeleza a ‘PUBLIC REALM' aliyorithi kutoka kwa mkoloni, yenye kutumia CIVIC INSTITUTIONS kukidhi mahitaji ya wananchi ‘COLLECTIVELY' (not as COMMUNITIES); Na ndio maana in the process, akafuta mfumo wa Kichifu n.k; Pamoja na jitihada zote hizi, Nyerere hakufanikiwa sana kwani katika Tanzania ya leo, KITAASISI, bado nguvu ya nchi ipo kwenye COMMUNITIES and their Local Institutions, sio kwenye CIVIC Institutions; Ushahidi wa hili upo kwenye udini na ukabila unaoendelea chini kwa chini, ambao pia unachochewa na viongozi fulani fulani; Viongozi wanafanya haya kwa sababu – source of their respect, prestige and social status inatokana na Loyalty yao katika taasisi za communities husika, sio civic institutions; mifano ni mingi – mawaziri, wabunge, na sasa wameongezwa wajumbe wa NEC; Hii inaendana na mjadala wangu wa awali kuhusu Tanzania as a Problematic State;

Viongozi husika ulazimika kuwa LOYAL zaidi to their communities kwani ndio njia pekee ya kuungwa mkono na kuwika kama viongozi katika ngazi ya TAIFA; Viongozi hawa kwa kawaida 'talk' about Civil Society, Civil Rights lakini when it comes to their 'walk', huwa zaidi upande local communities and relevant institutions in such communities; Ndio maana kwa viongozi wa namna hii, kwa vile loyalty ipo zaidi kwenye local communities and culture kuliko the STATE and its civic institutions, ni kawaida yao Kutumia The STATE as a PREY and milk it feed their communities kama mawaziri n.k, na hili litaendelea bila ya kujalisha chama gani kipo Ikulu;

Kabla ya kuingia kwenye sehemu ya NNE ya mjadala huu, ni muhimu nikasema kwamba katika aina mbili za rushwa tulizo jadili, the Common Denominator ni "ULIMBIKIZAJI BINAFSI WA MALI";

SEHEMU YA NNE

Katika sehemu ya nne, nitajadili kwa undani zaidi kwanini nasema Ufisadi Tanzania unakubalika; nitatumia framework ya ECONOMY OF AFFECTION/Uchumi wa Mahaba katika analysis yangu; Tutajadili hili kwa undani baadae kidogo lakini kiuchumi, huu ndio mfumo mkubwa na ulio rasmi Tanzania kuliko UCHUMI Unaofuata RATIONAL BEHAVIOUR AND CHOICE; Pia katika muktadha huu, nitajadili masuala ya Social and Economic Exchanges/Mfumo wa ubadilishanaji Kiuchumi na Kijamii nchini, ambao umetawaliwa zaidi na informal processes and institutions, na jinsi gani masuala haya kwa pamoja yanachochea na ku ‘entertain' rushwa na ufisadi Tanzania;

Sehemu kubwa ya maelezo juu ya tabia hii yapo katika Cultural Forces, ambazo nitajaribu kuzijadili; Nchini Tanzania (na pengine sehemu nyingi za Afrika), STATUS & WEALTH always depends on the ability to accumulate Dependents and Followers; Kwahiyo njia kuu for individuals to Gain Status ni pamoja na kuwa na watumishi wengi na wa kila aina, Kuwa na Wake wengi, au acquisition of clients/patrons/supporters; Suala hili linaendelea kuwa sehemu muhimu ya social structuration nchini Tanzania; Ni katika mazingira, haya, spending money conspicuously ni njia muhimu for one to gain ‘STATUS' and ‘INFLUENCE';

Tukirudi kwenye mjadala juu ya local community institutions vis a vis civic institutions, katika jamii yetu Tanzania, mtanzania wa leo (hasa mwanasiasa), anakuwa na advantage zaidi iwapo anakuwa associated na anakuwa na LOYALTY zaidi kwenye local community (udini, ukabila, ukanda n.k) institutions kuliko Civic Institutions of the State (raia na Utaifa), ingawa the latter (civic institutions) ni muhimu zaidi kwa ujenzi wa Utaifa, Uzalendo, na Maendeleo ya nchi kwa ujumla; Kuna mifano mingi juu ya hili lakini mfano mmoja ni kwamba - Watanzania wengi wapo tayari kufanya ufisadi na kula rushwa ili kuwa na uwezo to spend lavishly kwenye private ceremonies ambazo hazina umuhimu kwa Maendeleo ya taifa, kama vile misiba, kitchen party, birthdays, kipa imara, wedding anniversaries, harusi n.k; Wengi hawapo kuwekeza katika civic order kama vile kulipa Kodi TRA au kuwekeza katika economic growth kama njia ya kuchangia ujenzi wa taifa leo la Tanzania; Je, ni kwa nini inakuwa hivi?

It is based on my earlier argument juu ya umuhimu wa informal and community based institutions vis a vis civic institutions; Kwahiyo kwa watanzania wengi hasa wenye nafasi zao, ni muhimu sana kujilimbikizia mali ili kuwa na uwezo wa kutumia fedha kukidhi matakwa ya community institutions; Pamoja na kwamba ni less rrelevant kwa Maendeleo ya taifa, kufanya hivyo demonstrates their commitment to local community institutions ambapo ndio source yao ya support, respect and social status (badala ya utanzania based on loyalty to civic institutions of the state), or they do so in order to earn enough respect from elders, and at times, women;

Ni vizuri tukajadili japo kidogo suala hili katika muktadha wa chaguzi zetu za ndani na nje ya vyama;

Katika chaguzi kuu, Wagombea wa nafasi kama vile ubunge na udiwani, wanaweza jaribu kusema THE RIGHT THINGS kuhusu THEIR HONEST OPINION kuhusu MASUALA mbalimbali ya KISERA kwa manufaa ya TAIFA, lakini wanajua fika kwamba kwa wananchi - ‘WHAT THEY SAY' has much less importance than ‘WHAT THEY DO' to demonstrate that they Care about them or they have a FOLLOWING/Wafuasi/wanakubalika; In order to make a ‘gain' therefore, they have to invest katika kutembeza viloba vya pesa na aina nyingine za ‘tangible rewards' to prospective supporters/voters;

Katika chaguzi mbalimbali, tumeona jinsi gani political actors katika mazingira ya uchumi wetu wa mahaba, wapo tayari kutoa perks mbalimbali kwa potential followers/voters; Hii ni tofauti na tabia ya political candidates katika nchi zilizokomaa kidemokrasia na zenye stronger STATES kama vile Ulaya na Marekani ambapo promises are ‘VERBAL'; Katika uchumi wetu wa mahaba, accountability at election time is immediate – the candidate must demonstrate personal generosity as part of the process of political campaigning; katika demokrasia zilizokomaa na zenye stronger states, suala hili huja baadae, especially only if the candidate wins and gets into political office;

Kabla ya kujadili kwa kina dhana ya ECONOMY OF AFFECTION na jinsi gani inachochea rushwa, ningependa kusema tu kwamba – katika Tanzania, rushwa inachangiwa sana pia na FAMILY TIES; Family pressures are so pervasive; Juu kabisa kwenye pyramid of the patronage wapo Mawaziri na Maafisa waandamizi wa Serikali ambao maofisini na majumbani kwao, kutwa kuna mistari mirefu ya relatives, acquaintances, voters n.k, ambao wanaenda to air their complaints or seek material/economic support; Viongozi wengi wanakuwa hawana jinsi bali kutumia vibaya madaraka yao na kujilimbikizia mali ili kukidhi such irrational demands;

Viongozi wanafanya haya kwa sababu – source of their respect, wealth, prestige and social status inatokana na Loyalty yao katika taasisi za communities husika, sio civic institutions; mifano ni mingi – mawaziri, wabunge, na sasa wameongezwa wajumbe wa NEC; Viongozi husika ni lazima wawe loyal to their communities kwani ndio njia pekee ya kuungwa mkono na kuwika kama viongozi katika ngazi ya TAIFA; Ndio maana kwa viongozi wa namna hii, kwa vile loyalty ipo zaidi kwenye local communities and culture kuliko the STATE, wengi hutumia the STATE as a PREY (kama sehemu ya kuchuma) and milk it in order to feed their communities, na hali hi itaendelea bila ya kujalisha chama gani kipo Ikulu; Na hoja hii inatuingiza kwenye mjadala wa kina juu ya ECONOMY OF AFFECTION;

Jamii yetu ya Tanzania inaendeshwa chini ya mfumo wa Economy of Affection. Maana yake ni: People make personal investments in reciprocal relations with other individuals as a means of achieving goals that are seen otherwise impossible to attain – such as prestige, social status, wealth n.k; katika mfumo huu, informal institutions ni muhimu kuliko formal institutions, na hata resources allocation hufanyika under the mechanism of informal institutions; Kuna kanuni kadhaa za mfumo wa Economy of Affection lakini muhimu ni tatu:


  • Kwanza – Whom You Know is More Crucial Than What You Know;
  • Pili - Sharing Personal Wealth is More Crucial Than Investing in Economic Growth;
  • Na Tatu - A helping Hand Today Generates Returns Tomorrow;

Ufisadi unachochewa sana na mfumo huu; Hii ni pamoja na ukweli kwamba, mambo ambayo wananchi wengi (hasa vijijini) wana hitaji au wanathamini katika maisha yao ya kila siku - kwa mfano goods, services, information, etc, kwa mtazamo wa wengi, all these can only be obtained from others; Ni jadi kwa watanzania kutegemeana for such valued resources na wanapeana haya kupitia informal process of exchanges ambazo ndio zinazoendesha community institutions; Exchanges muhimu hapa ni pamoja na Rewards (e.g., Cheo, Status, Power) Or Punishments (e.g., Kura ya Hapana kwa mgombea nafasi ya uongozi), na hii inategemea iwapo upande husika delivered the promise or didn't deliver;

Kwa mfano, voters may deny political patrons kwa sababu they did not deliver their immediate promises of rewards, hence they punish the patrons kwa kura ya Hapana; Kwa upande mwingine, pia Political patrons wanaweza punish voters iwapo hawatapiga kura kwa kiasi kilichotarajiwa, na adhabu inaweza kuwa pamoja na serikali husika kutopelekea huduma za kijamii katika maeneo fulani n.k; Kuna utafiti mmoja uliofanywa na Chuo cha UCLA na unaonyesha jinsi gani Wilaya fulani fulani zilipewa adhabu hii na CCM katika kipindi cha 1997 – 2007 (see Laura Weinstein: The Politics of Government Expenditures in Tanzania: 1997 - 2007);

Watanzania wengi (hasa wa vijijini) are not rational when it comes to decision making; na ni inachangiwa sana na Weakness of the State in the hinterland i.e. absence of Civic Institutions to play a prominent, leading and legitimate role over and above community institutions; Katika nchi za wenzetu zilizoendelea zaidi in terms of Strong & Consolidated States, kwa mfano, classical microeconomic theory inatoa mwongozo wa kimaamuzi ndani ya jamii husika, ambapo kwa mfano - hakuna long term relations between economic exchange partners; hii ni tofauti na Tanzania ambapo social and economic exchanges zinapendelea partners wa muda mrefu, hasa kwa kutegemeana na Rewards vis a vis punishments, katika mazingira ya Economy of Affection;

Mfano mwingine ni kwamba, wakati classical microeconomic theory assumes kwamba actors engage in set of independent transactions that are aggregated into markets, katika Tanzania, exchanges are built on premises that actors engage in recurring interdependent exchanges with partners with specific pertners over time and they remain partners as long as they fulfill their promises in the context of the Economy of Affection;

Haya ni baadhi ya masuala yanayochangia kwa kiasi kikubwa tatizo la rushwa ‘kimfumo', hasa ufisadi;

Katika bandiko langu namba moja la mjadala huu, nili ahidi kumalizia mjadala wangu kwa kutoa mapendekezo juu ya nini kifanyike katika kutatua changamoto hizi; Lakini kufanya hivyo nadhani itakuwa sio kuiwatendea haki wadau wengine humu kwani mawazo yenu yatakuwa ni muhimu sana katika kuhitimisha mjadala huu; Kwahiyo niseme tu kwamba hoja yangu ya msingi imekamiliika, kilichosalia ni the way forward, na hili haliwezi kutimia bila ya mchango wenu;

Vinginevyo kwa kifupi tu, ili kukidhi kiu pengine ya baadhi ya wadau humu, ningependa kuhitimisha kama ifuatavyo:

Dr. Slaa, Mangula pamoja na vyama vyao vya siasa havina uwezo wa kutatua tatizo la rushwa na ufisadi tanzania; Sana sana viongozi hawa wawili wanachofanya ni kuaminisha umma kwamba Rushwa katika jamii yetu haikubaliki na haivumiliki tena; As individuals, Dr. Slaa na Mangula, wote wawili wana moral authority kuzungumzia suala la Rushwa na ufisadi licha ya hoja za baadhi ya watu kwamba mangula hana such authority kutokana na kuwa sehemu ya chama ambacho kimeshindwa kutokomeza ufisadi; Nimejadili baadhi ya sababu kwanini vita dhidi ya ufisadi ni ngumu zaidi ya wengi wanavyodhania; CCM kulemewa na ufisadi haitokani moja kwa moja na sababu kwamba eti kuna baadhi ya watu wanaogopwa, bali ni kutokana na ukweli kwamba suala la Ufisadi na rushwa Tanzania ni la kimfumo; Hata Chadema ikifanikiwa kuingia Ikulu 2015, haitaweza kutatua tatizo la ufisadi na badala yake, inaweza kujikuta katika mazingira yanayokaribiana na CCM ya sasa; Moja ya njia sahihi za kujaribu punguza matatizo yanayotokana na makali ya ufisadi kwa vyama vyote hivi viwili ni pamoja na kulitizama tatizo hili kwa jicho kama letu ndani ya mjadala huu;

Ni muhimu kwa vyama hivi viwili kuja na consensus juu ya suala hili la rushwa badala ya kila upande kulitumia kama a political asset vis a vis political liability kuelekea 2015, huku equilibrium to wananchi walio wengi, kutokana na mchakato husika, ikiwa haina mwelekeo; It is about time sasa tuanze kushughulikia tatizo la Ufisadi kwa kuendeleza Formation and consolidation of the state of Tanzania kwani bado kazi haijaisha (e.g. kuna maeneo wananchi hawajui serikali ni nini, civics ni kitu gani, au economic, political and social justice vitu gani), kwani kwa kufanya hivyo, tutaweza kufanikiwa kuanza kuishi collectively in a modern state kama taifa na kuondokana na duality ya hivi sasa ambayo ipo dominated zaidi na community institutions and their informalities kama tulivyo jadili;

Moja ya njia effective za kuleta ufumbuzi ni kuanza kujenga Loyalty ya umma to the State and its civic institutions, na kundokana na Loyalty to local communities and their institutions kama zilivyo sasa, ambazo kama tulivyokwisha ona, zinachangia sana viongozi kuwa mafisadi; Ni muhimu tukaachana na Affective Society na tuka hamia kwenye Civil Society kwani Civic Society inatawaliwa kwa mujibu wa principles, rule of law, enhancement of citizen voice na universality unlike Affective Society;

Naomba kuwasilisha;
 
Lukolo,

una hoja ya msingi lakini naomba usome sehemu yangu ya mwisho ya mjadala wangu juu ya mada husikka i.e. rejea bandiko namba 26 hapo juu kisha tuje kwenye meza ya majadiliano kuhusu rushwa na utamaduni; ni muhimu pia ukaiangalia rushwa from demand driven and supply driven forces;
 
Binafsi naamini akipatikana kiongozi mmoja tu ambaye anaichukia rushwa kwa dhati kabisa kutoka moyoni. Hasa kwa nafasi ya Rais, atakayekuwa tayari kumfunga jela hata mke wake kwa kosa la kupokea au kutoa rushwa. Nchi itashika adabu. Na huu ubadhirifu mkubwa unaotokea nchini hautaendelea. Wala huhitaji mikakati mingi kama Kobello anavyotaka kutuaminisha. Unahitaji kutoa tamko tu na kuanza kutekeleza kwa vitendo. Ninaamini idara ya usalama wa taifa ikitumiwa vizuri inaweza kufunua mianya yote ya rushwa. Na iwapo tutakuwa na rais mwenye akili asiyeweza kuvumilia rushwa ataivuruga mianya hiyo yote na kuirudisha nchi katika mstari wake.



Nawahikikishieni kwamba hili tatizo la rushwa linaweza kuondoka hata leo. Na linaweza kutangazwa kuwa ni historia katika nchi yetu iwapo tu atatokea Rais ambaye yupo tayari kupambana nalo na ambaye kwa hakika atachuguliwa kwa nguvu ya umma na si nguvu ya pesa
. Tatizo kubwa tulilonalo hivi sasa katika nchi yetu ni kwamba tayari CCM imewajengea mazoea wananchi kwamba wakitaka kura zao basi sharti wapewe kitu kidogo. Hiki ndiyo kinachotuumiza.

Yaleyale ya kutumia cofta kutibu kifua kikuu.
Mbona hamuelezi rais atafuta rushwa nchini kivipi? How?
Inajulikana Tanzania tuna utamaduni wa rushwa, rushwa inavumiliwa sana na watanzania wa kawaida tu, Yaani mtu akimweka ndugu yake kwenye position fulani, watanzania asilimia 44 hawaoni kuwa hiyo ni rushwa.

Badala ya kujaribu kuweka hotuba za kihisia hisia, elezea ni kwa jinsi gani rais atafuta rushwa ..... mimi nasema it takes the people, not the president.
 
Lukolo,

una hoja ya msingi lakini naomba usome sehemu yangu ya mwisho ya mjadala wangu juu ya mada husikka i.e. rejea bandiko namba 26 hapo juu kisha tuje kwenye meza ya majadiliano kuhusu rushwa na utamaduni; ni muhimu pia ukaiangalia rushwa from demand driven and supply driven forces;
Mchambuzi angalau katika post yako namba 26 tunaongea kitu kinachofanana, japo mimi bado naamini kwa kuzingatia rushwa ya individuals na public (kimfumo), viongozi wa juu wakiamua kuwa serious kuikataa, hakuna atakayeiendekeza.

Kwa mfano hii rushwa ya individual, umeielezea vema kwamba inatokana na uwajibikaji mdogo, kutofuata sheria na taratibu kwa mjibu wa katiba. Je ni nani aliyeapa kuisimamia katiba? Kwanini katiba inapovunjwa hachukui hatua?

Kobello amekazania sana kuuliza swali la atafanyeje? Napenda niamini kwamba Kobello aliwahi kuwa kiongozi katika taasisi ndogo japo shule. Fanya utafiti mdogo kwa kuangalia namna ambavyo walimu na wanafunzi wanaweza kuwa na tabia zinazoendana na mkuu wa shule. Kama mkuu wa shule ataweka sheria na taratibu za uendeshaji wa shule na akazisimamia kwa kuanza kuwawajibisha watendaji wake, nakuhakikishia watendaji wake hawatamfumbia macho yeyote watakayegundua kwamba amekiuka sheria na taratibu za aina yoyote. Ndiyo maana shule inayofanya vibaya hubadilishwa mwalimu mkuu na si walimu wote.

Na ikitokea katika nchi wananchi wakaaminishwa kwamba taarifa za rushwa zinazofikishwa kwenye mamlaka husika zinakuwa investigated kwa siri na hatua stahili zinachukuliwa dhidi ya wala rushwa kwa hakika hakuna atakayelifumbia macho hilo. Niambie mtu amekwenda hospitali halafu daktari anamwambia yupo busy, akate kitu kidogo ili ahudumiwe. Hivi unafikiri huyu mwananchi hawezi kureport masuala ya kukera kama haya kama anajua kwamba uwajibikaji upo kwa kiwango cha juu? Na kwamba usimamizi ni wa kutosha? Inapotokea mtendaji mmoja katika ofisi anapokea rushwa kwa mfano, halafu mamlaka za juu zikamwajibisha huyo mtendaji pamoja na msimamizi wake (let say director wa hiyo idara), na hatua hizi zikatangazwa kwenye vyombo vya habari, unafikiri director wa idara nyingine ataruhusu hayo yatokee kwenye idara yake? Kila kiongozi wa idara ataweka strategy za kupambana na rushwa na kusimamia uwajibikaji. Lakini kama mtu anapokea rushwa mchana kweupe tena kwa wazi kabisa, halafu hakuna kinachotokea, kesi zinapelekwa takukuru halafu zinazimwa kienyeji tu, ni nani atakayehangaikia kuireport kama si na yeye kutafuta pa kupata rushwa?

Ndiyo maana nasema mtu wa kwanza kuikataa rushwa awe rais, magazeti na vyombo mbalimbali vya habari vinareport habari za rushwa kila siku. Rais makini angehakikisha intelligensia yake pamoja na Takukuru wanafuatilia kila rushwa inayoreportiwa na kuchukua hatua. Na hatua zitangazwe kwenye vyombo vya habari, kwanini masuala ya rushwa yanashughulikiwa kwa siri hata pale yanapokuwa yameshadhibitishwa? Tena mimi nafikiri ungewekwa utaratibu wa kila mtuhumiwa wa rushwa kusimamishwa kazi mara moja ili kupisha uchunguzi. Lakini utakuta Edward Hosea, Luhanjo, Mwanyika, walitajwa kuhusika na maamuzi yenye harufu ya rushwa na bunge (ambalo ndiyo wananchi) likaagiza wasimamishwe, lakini rais akajikausha, hivi utasema pana raisi anayepambana rushwa hapo? Hivi kwanini mtu wa chini na yeye asile rushwa kama wakubwa wanakula rushwa na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa. Katika mazingira hayo unadhani ni nani atamwajibisha mwenzake.

Ninaamini Rais ndiyo mamlaka ya juu zaidi yenye maamuzi ya mwisho juu ya mtu awaye yote ikiwemo maamuzi juu ya uhai wake. Sasa kama anashindwa kufanya maamuzi tu ya kumfukuzisha kazi na kumshitaki mla rushwa unategemea kuna lipi jipya linaweza kufanyika hapo. Matokeo yake ndiyo kuja na hoja nyepesi za kwamba rushwa ni utamaduni na eti haifutiki. Huko ni kukata tamaa kubaya kabisa. Ni vema tukaukubali ukweli kwamba tumekuwa na bahati mbaya kubwa sana watanzania kwamba awamu mbili za uongozi (Mkapa na Kikwete) zimeshikwa na wala rushwa na hivyo kuifanya rushwa nchini kuwa sugu, kwa kuwa wao wenye ndiyo vinara wa rushwa.

Aina ya pili uliyoizungumzia ambayo unaiona kwamba ni ya kitamaduni ni hiyo ya kimfumo au yenye public interest kwa namna nyingine. Kwamba tayari jamii imeshazoeshwa hivyo; kwamba jambo fulani haliwezi kwenda bila kupata kitu kidogo. Ninarudia tena. Tuende kwenye free and fair election hapa. Kwamba hakuna cha tshirt, wala senti tano ya kupewa mwanachama wala kiongozi wa kijiji, watu wabebe bendera za vyama vyao tu. Halafu tuone kama wananchi hawatapiga kura? Kila mtu aende kama alivyo. Tume ya uchaguzi itangaze na isimamie kwamba yeyote atakayetoa rushwa anafutwa katika wagombea. Na isimamie hilo. Siku ya kwanza mtu wa kwanza ametoa rushwa afutwe na kutangazwa kwenye vyombo vyote vya habari. Na tuwafanye wenyeviti wa mitaa na baadhi ya watendaji ambao huwa ndiyo wapokea rushwa wawe ndiyo mashushu wa TAKUKURU na tume ya uchaguzi na hatua thabiti zichukuliwe hata kama itatolewa rushwa ya shilingi 2000. Tuone kama kweli wananchi hawatafika mahali wakaelewa kwamba wanaweza kuchagua kiongozi wao kwa kuridhika na sera zake na si kiasi cha pesa wanachopewa.

Haya mambo tumeyatengeneza wenyewe na pia tunaweza kuyamaliza wenyewe. Ni kupata tu Rais asiye mla rushwa na ambaye anaichukia rushwa kwa dhati, kazi itakuwa imekwisha. Tatizo la rushwa halitahitaji mjadala tena.

Hiyo hatua ya nne, sitaizungumzia, kwa kuwa hiyo mimi sioni kama inahusika na masuala ya rushwa rather than mfumo wa maisha wenye definition ya kusaidiana na vitu kama hivyo. Lakini hizi mbili za awali kwa hakika hata mimi tu nikipewa kuwa kiongozi wa nchi nazimaliza tena in a period of a year. Hapo suala ni kufumba macho tu! Uwe tayari kwa lolote bila kujali panga hilo na wala rushwa linamfikia nani. Awe ni mwanao au mkeo wote wakikutwa na hatia ya rushwa wawajibike kwa mjibu wa sheria. Adhabu za makosa yatokanayo na rushwa ziongezwe.

Hivi kweli nchi inakuwa na rais anayeweza kuvumilia rushwa za hadi kusafirisha wanyama hai kwenda nje, kusafirisha pembe za ndovu, EPA, Sijui mabilioni ya Uswis, sijui Richmond, TANESCO na utitiri mwingine kibao, na ana usalama wa taifa, polisi, jeshi na kila aina ya majeshi. Rais kama huyu mnawezaje kumuweka katika nafasi ya watu waliojaribu kupambana na rushwa? Sipo tayari na katu sitakaa niwe tayari kuamini kwamba rushwa ni tatizo lisilotatulika. Hilo sipo tayari kabisa kulikubali kwa namna yoyote ile. Ila sipo tayari pia kukubali kwamba kuna mwanaCCM anayeweza kusimama kwa dhati kupambana na rushwa. kwa kuwa ndani ya CCM rushwa ni kama chakula, kila aliye humo ni lazima ale ili aweze kuishi. Iwe ni ndani ya chama au nje ya chama.

Lakini naamini kabisa kiongozi wa kupambana rushwa atatoka upinzani (si lazima awe Slaa au Zitto au Mbowe au Lipumba). Mtu mwingine yeyote kutoka upinzani akiamua kuwa serious kabisa kuimaliza rushwa katika nchi hii anaweza kwa kuwa yeye atakuwa bado hajawa polluted na mfumo CCM ambao unanuka rushwa kila mahali chamani na katika idara na taasisi za serikali. Lakini kiongozi wa upinzani akiingia na nia ya dhati, maamuzi yake hayatamdhuru sana kwa kuwa yeye hatabebwa na wala rushwa wakubwa nchini kama ambavyo CCM inabebwa na kuendeshwa na wala rushwa.
 
Mchambuzi angalau katika post yako namba 26 tunaongea kitu kinachofanana, japo mimi bado naamini kwa kuzingatia rushwa ya individuals na public (kimfumo), viongozi wa juu wakiamua kuwa serious kuikataa, hakuna atakayeiendekeza.

Kwa mfano hii rushwa ya individual, umeielezea vema kwamba inatokana na uwajibikaji mdogo, kutofuata sheria na taratibu kwa mjibu wa katiba. Je ni nani aliyeapa kuisimamia katiba? Kwanini katiba inapovunjwa hachukui hatua?

Mkuu Lukolo tunatakiwa tukumbuke kwanza kuwa CCM iliamua kuacha rasmi kuchukia rushwa na ufisadi baada ya kupitisha azimio la Zanzibar. Misingi yote inayozuia ufisadi na mazingira ya kupokea rushwa ilivuinjwa kwa makusudi, baada ya kuvunja azimio la Arusha. Kutokana na sababu hiyo, hata kama kiongozi wa juu wa chama tawala na nchi hatakuwa fisadi, system ya sasa imebariki ufisadi.

Kuna mahali mchambuzi alianzisha uzi mmoja akiuliza ni kwanini vijana wanagombea uongozi ndani ya CCM. Si vijana tu, walio wengi madarakani hakuna anayejali watanzania, Tanzania au CCM, wanajali maslahi yao tu. Kutokana na mazingira yaliyowekwa na chama kuwa uongozi ni daraja la kujineemesha, wanachofanya wengi wanaotaka madaraka, ni kupata fursa nzuri zaidi ya ufisadi, sio fursa nzuri ya kutetea maslahi ya Tanzania, watanzania na CCM

Ukianza kuangalia kuna harufu ya rushwa na ufisadi kila mahali, ukivaa nguo ya kijani siku hizi upende usipende utaasikia kaharufu ka rushwa. Hata kama Kikwete leo angeamua kupambana na ufusadi ataanzia wapi? Inawezakna mawaziri waliingia bungeni kwa rushwa, wakuu wa idara mbalimbali za chama na serikali wameingia huko kwa njia hizo hizo. Kwa hiyo kimsingi ni kuwa sisi watanzania tunatakiwa tuwe na katiba yenye nguvu na Civil society yenye nguvu na isiyokuwa corrupted ili kuwe na anayeweza kumonitor ufisadi. Lakini hayo kwa sasa hayawezekani kwa kuwa CCM ambayo ndio imejaa ufisadi imehodhi mchakato mzima wa kubadilisha katiba na kuzipa uhuru civil society.
 
Mkuu Lukolo tunatakiwa tukumbuke kwanza kuwa CCM iliamua kuacha rasmi kuchukia rushwa na ufisadi baada ya kupitisha azimio la Zanzibar. Misingi yote inayozuia ufisadi na mazingira ya kupokea rushwa ilivuinjwa kwa makusudi, baada ya kuvunja azimio la Arusha. Kutokana na sababu hiyo, hata kama kiongozi wa juu wa chama tawala na nchi hatakuwa fisadi, system ya sasa imebariki ufisadi.

Kuna mahali mchambuzi alianzisha uzi mmoja akiuliza ni kwanini vijana wanagombea uongozi ndani ya CCM. Si vijana tu, walio wengi madarakani hakuna anayejali watanzania, Tanzania au CCM, wanajali maslahi yao tu. Kutokana na mazingira yaliyowekwa na chama kuwa uongozi ni daraja la kujineemesha, wanachofanya wengi wanaotaka madaraka, ni kupata fursa nzuri zaidi ya ufisadi, sio fursa nzuri ya kutetea maslahi ya Tanzania, watanzania na CCM

Ukianza kuangalia kuna harufu ya rushwa na ufisadi kila mahali, ukivaa nguo ya kijani siku hizi upende usipende utaasikia kaharufu ka rushwa. Hata kama Kikwete leo angeamua kupambana na ufusadi ataanzia wapi? Inawezakna mawaziri waliingia bungeni kwa rushwa, wakuu wa idara mbalimbali za chama na serikali wameingia huko kwa njia hizo hizo. Kwa hiyo kimsingi ni kuwa sisi watanzania tunatakiwa tuwe na katiba yenye nguvu na Civil society yenye nguvu na isiyokuwa corrupted ili kuwe na anayeweza kumonitor ufisadi. Lakini hayo kwa sasa hayawezekani kwa kuwa CCM ambayo ndio imejaa ufisadi imehodhi mchakato mzima wa kubadilisha katiba na kuzipa uhuru civil society.
Well said Mkuu! Ni lazima tutatambue zao la Azimio la Zanzibar ni ccm hii ya leo, lakini tusiishie hapo tu kwa CCM pekee, pia ni CHADEMA, CUF, n.k ni watoto wa Azimio la Zanzibar, hakuna chema kitokacho kwa mzoga kipaswacho kuliwa na binadamu, siku zote iko hivyo! Mzoga wake Uvundo tu mara zote!

Hakuna apingae kama Azimio la Zanzibar limechangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili na uwajibikaji pamoja na miiko yetu katika nyanja zote, sasa nani unafikiri anastahili kupewa dhamana hali wengi wamelelewa na kuendelea kulelewa na AZ? Ni BURE!

Ilishasemwa mara nyingi, lakini bado watu mmeng'ang'ana na ushabiki wenu wa vyama...KAMA TUNA NIA KWELI YA DHATI YA KUIKOMBOA TANZANIA, BASI HATUNA BUDI KUPATA KIZAZI KIPYA CHA FIKRA, yaani kiwe NJE YA HUU UVUNDO WA AZIMIO LA ZANZIBAR! Zaidi ya hapo ni kupigiana kelele na kupotezeana muda tu! Kamwe huwezi kulina asali halikuwa umefuga manyigu, usishangae manundu itakuwa ndio hekima yako!

TUNAHITAJI AZIMIO JIPYA, KUTOKA KIZAZI KIPYA CHA FIKRA! Msidanganyike na maneno ya kipumbavu eti "Ndio Uhalisia wa Dunia" ukishaamini hivyo wewe ni MTUMWA TAYARI!

Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU. Tukiamua TUNAWEZA!

Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani.
Anaita sasa!
 
Mkuu Lukolo tunatakiwa tukumbuke kwanza kuwa CCM iliamua kuacha rasmi kuchukia rushwa na ufisadi baada ya kupitisha azimio la Zanzibar. Misingi yote inayozuia ufisadi na mazingira ya kupokea rushwa ilivuinjwa kwa makusudi, baada ya kuvunja azimio la Arusha. Kutokana na sababu hiyo, hata kama kiongozi wa juu wa chama tawala na nchi hatakuwa fisadi, system ya sasa imebariki ufisadi.

Kuna mahali mchambuzi alianzisha uzi mmoja akiuliza ni kwanini vijana wanagombea uongozi ndani ya CCM. Si vijana tu, walio wengi madarakani hakuna anayejali watanzania, Tanzania au CCM, wanajali maslahi yao tu. Kutokana na mazingira yaliyowekwa na chama kuwa uongozi ni daraja la kujineemesha, wanachofanya wengi wanaotaka madaraka, ni kupata fursa nzuri zaidi ya ufisadi, sio fursa nzuri ya kutetea maslahi ya Tanzania, watanzania na CCM

Ukianza kuangalia kuna harufu ya rushwa na ufisadi kila mahali, ukivaa nguo ya kijani siku hizi upende usipende utaasikia kaharufu ka rushwa. Hata kama Kikwete leo angeamua kupambana na ufusadi ataanzia wapi? Inawezakna mawaziri waliingia bungeni kwa rushwa, wakuu wa idara mbalimbali za chama na serikali wameingia huko kwa njia hizo hizo. Kwa hiyo kimsingi ni kuwa sisi watanzania tunatakiwa tuwe na katiba yenye nguvu na Civil society yenye nguvu na isiyokuwa corrupted ili kuwe na anayeweza kumonitor ufisadi. Lakini hayo kwa sasa hayawezekani kwa kuwa CCM ambayo ndio imejaa ufisadi imehodhi mchakato mzima wa kubadilisha katiba na kuzipa uhuru civil society.
We are sailing in the same boat. Rushwa imepandwa ikapaliliwa na kuwekewa mbolea na viongozi wa CCM. Ndiyo maana nadiriki kusema hakuna kiongozi hata mmoja wa kutoka CCM awe ni Magufuli au ni Mwakyembe wanaowaona kuwa ni lulu, atakayeweza kuikabili rushwa. Kwa kuwa kila mtu ndani ya CCM ni muumini wa rushwa kwa namna moja au nyingine. Ninakushukuru sana kwa kunikumbusha namna ambavyo Mwinyi aliamua kwa makusudi kuihalalisha rushwa kwenye azimio lake la Zanzibar. Kwa hiyo hivi sasa kwa CCM rushwa ni kama moja ya sera zake na si adui wa haki tena.
Ndiyo maana nasema ni kiongozi wa upinzani tu atakayeweza kuwa na uthubutu wa kuikataa na kuisimamia rushwa kwa dhati. Si kwa kuwaondoa wafanyakazi wote maidarani bali kwa kuanza kumshughulikia mmoja baada ya mwingine na kwa uwazi. Hakuna anayependa kupoteza kazi yake bwana. Ni nani atakayekubali kupokea hata kama ni mabilioni ya fedha halafu aishie jela na kudhalilishwa kwenye vyombo vya habari? Kwanini wenzetu wachina hawaijadili rushwa kama tatizo? Tunahitaji strategic reasoning tu hapa.
 
Well said Mkuu! Ni lazima tutatambue zao la Azimio la Zanzibar ni ccm hii ya leo, lakini tusiishie hapo tu kwa CCM pekee, pia ni CHADEMA, CUF, n.k ni watoto wa Azimio la Zanzibar, hakuna chema kitokacho kwa mzoga kipaswacho kuliwa na binadamu, siku zote iko hivyo! Mzoga wake Uvundo tu mara zote!

Hakuna apingae kama Azimio la Zanzibar limechangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili na uwajibikaji pamoja na miiko yetu katika nyanja zote, sasa nani unafikiri anastahili kupewa dhamana hali wengi wamelelewa na kuendelea kulelewa na AZ? Ni BURE!

Ilishasemwa mara nyingi, lakini bado watu mmeng'ang'ana na ushabiki wenu wa vyama...KAMA TUNA NIA KWELI YA DHATI YA KUIKOMBOA TANZANIA, BASI HATUNA BUDI KUPATA KIZAZI KIPYA CHA FIKRA, yaani kiwe NJE YA HUU UVUNDO WA AZIMIO LA ZANZIBAR! Zaidi ya hapo ni kupigiana kelele na kupotezeana muda tu! Kamwe huwezi kulina asali halikuwa umefuga manyigu, usishangae manundu itakuwa ndio hekima yako!

TUNAHITAJI AZIMIO JIPYA, KUTOKA KIZAZI KIPYA CHA FIKRA! Msidanganyike na maneno ya kipumbavu eti "Ndio Uhalisia wa Dunia" ukishaamini hivyo wewe ni MTUMWA TAYARI!

Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU. Tukiamua TUNAWEZA!

Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani.
Anaita sasa!
Tunahitaji fikra mpya! You are very right! Tunahitaji pia msimamizi mwenye commitment anayetekeleza kwa vitendo kiapo chake cha kuilinda katiba. Lakini hatuhitaji kizazi kipya. Kwa kuwa hakuna kizazi kitakachoshushwa kutoka angani? Watoto wetu na wajukuu zetu wataendelea kuzaliwa katika mfumo huu huu wa kirushwa.

Tunachohitaji hapa ni uongozi mpya wenye fikra mpya na unaoichukia rushwa kwa dhati kabisa. Hili si suala la chama, bali ni suala la individual leader. Kwamba tufanikiwe kumpata rais ambaye ana serious commitment ya kuliondoa tatizo la rushwa. Awe ni kiongozi ambaye hayupo tayari kumfumbia macho hata waziri wake aliyempigia kampeni mwanzo mwisho. Na hawa watu si kwamba hawapo, tunao sana. Kwani Nyerere alishushwa kutoka mbinguni? Si alizaliwa katika kizazi cha kikoloni ambacho pia kilikuwa na rushwa? Lakini wakati ule, mtu alilipwa mshahara senti tano na bado alifanya kazi kama mtumishi mwaminifu wa umma na si mtawala! Mimi naamini hiki kitu kinawezekana, ni seriousness tu katika kuchukua hatua.

Tulikuwa na mjadala na watu fulani kule facebook, tukaongelea juu ya uwajibikaji wa TISS, TAKUKURU, police na mamlaka nyingine za serikali katika suala zima la kutoa taarifa za rushwa (kwa mfano wizi wa TANESCO, mabilioni ya Uswis, RICHMOND na kadhalika). Kuna watu walieleza wazi kabisa kwamba mkuu wa nchi ni mzito kufanya maamuzi. Anapelekewa taarifa zote lakini nyingi anazizima na nyingine anachukuwa mda mrefu kuzifanyia maamuzi! Kwanini anafanya hivyo? Niambieni kama angekuwa ni rais anayefanya maamuzi kwa wakati bila kujali ni nani anahusika na rushwa, tungekuwa wapi?

Trend ya kumaliza rushwa inaweza kwenda hivi: Rais akimwajibisha waziri ipasavyo bila kumuonea haya, waziri atafanya hivyo hivyo kwa wakurugenzi, wakurugenzi hali kadhalika kwa mameneja nao vivyo hivyo kwa walio chini yao. Mwisho wa siku kila mtu atakuwa anamwogopa hata rafiki yake wa karibu linapokuja suala la rushwa. Na hivi ndivyo Nyerere alivyofanikiwa. Sasa rais mwenyewe mla rushwa, nani atajali kuhusu suala la rushwa?
 
Lukolo,

…japo mimi bado naamini kwa kuzingatia rushwa ya individuals na public (kimfumo), viongozi wa juu wakiamua kuwa serious kuikataa, hakuna atakayeiendekeza. Kwa mfano hii rushwa ya individual, umeielezea vema kwamba inatokana na uwajibikaji mdogo, kutofuata sheria na taratibu kwa mjibu wa katiba. Je ni nani aliyeapa kuisimamia katiba? Kwanini katiba inapovunjwa hachukui hatua?

Ni kweli lakini unajua pia suala la Katiba na usimamiaji wake is a two way process; Kwa upande mmoja, ni muhimu kwa viongozi kuwajibika, lakini kwa upande mwingine, pia ni muhimu kwa wananchi kuwajibika; Kuna mchangaji mmoja hapa alisema kwamba suluhisho juu ya suala la rushwa na ufisadi ni lazima lianzie na wananchi wenyewe; Nakubaliana na hoja hii – tunaweza kutatua au angalau kupunguza makali ya tatizo hili kwa kufuata mchakato ambao ni bottom – up – wananchi influencing the top, not top – bottom – viongozi influencing the bottom; Na kaam Mwalimu alivyosema, Rushwa katika jamii haina budi kuwa treated kama uhaini/treason; Katiba mpya haitoshi kutekeleza hili, inahitaji Political Will ya viongozi, lakini such a Political Will itakuja iwapo viongozi wataona kwamba kweli jamii inataka kubadilika; Binafsi naona ni jamii ndio itatuangusha kwani inafaidika sana na rushwa katika mazingira ya economy of affection kama nilivyojadili;

Kobello amekazania sana kuuliza swali la atafanyeje? Napenda niamini kwamba Kobello aliwahi kuwa kiongozi katika taasisi ndogo japo shule. Fanya utafiti mdogo kwa kuangalia namna ambavyo walimu na wanafunzi wanaweza kuwa na tabia zinazoendana na mkuu wa shule. Kama mkuu wa shule ataweka sheria na taratibu za uendeshaji wa shule na akazisimamia kwa kuanza kuwawajibisha watendaji wake, nakuhakikishia watendaji wake hawatamfumbia macho yeyote watakayegundua kwamba amekiuka sheria na taratibu za aina yoyote. Ndiyo maana shule inayofanya vibaya hubadilishwa mwalimu mkuu na si walimu wote.

Mfano wa shule ni mzuri kwani shule is a formal institutions with rules, procedures n.k, na yeyoye ambae anakiuka haya, anashughulikiwa accordingly; Lakini nje ya shule, jamii hii inatawaliwa na informal rules, procedures etc; all formalities remain at the institutional level – the school;

Iwapo unakumbuka mjadala wangu Sehemu ya PILI, nilizungumzia tofauti baina ya Collectivity na Community; Shule ni mfano wa Collectvity na ndio maana it works, lakini scope yake ipo very limited kwani shule hiyo hiyo imezungukwa na Community ambayo literary ndio inayoendesha shule husika;

Weak penetration of capitalism hasa hinterland ni kikwazo cha formalization and modernization of the State, hasa kupitia uimarishaji wa civic institutions ili ziwe na prominent role katika maisha ya watu ya kila siku; Mfano wako wa shule ni mzuri, lakini una limitations zake, ila kama una ideas on how we can use this model to formalize jamii yetu kwa ujumla kama njia moja wapo ya kutatua tatizo la rushwa na ufisadi katika jamii yetu, utakuwa umefanya jambo kubwa sana kwa nchi yako;

Hoja yako kuhusu rushwa na uchaguzi ni nzuri lakini kwa kweli it is just a romantic folly; Wewe unatazama rushwa kama vile ni kitendo cha hiyari cha wagombea; UKipata muda naomba upitie bandiko langu namba 26, paragraph kama nane za mwisho ambapo naongelea suala la Economy of Affection; Ningependa kusikia mawazo yako juu ya jinsi gani Chama nje ya CCM kitataua tatizo husika i.e. Economy of Affection, kwa kupitisha to sheria kali kali kama unavyoshauri;
 
Kwa hiyo kimsingi ni kuwa sisi watanzania tunatakiwa tuwe na katiba yenye nguvu na Civil society yenye nguvu na isiyokuwa corrupted ili kuwe na anayeweza kumonitor ufisadi. Lakini hayo kwa sasa hayawezekani kwa kuwa CCM ambayo ndio imejaa ufisadi imehodhi mchakato mzima wa kubadilisha katiba na kuzipa uhuru civil society.

Civil Society maana yake civic institutions of the state kuwa na nguvu over and above community based institutions ambazo zinaendeshwa zaidi na informal rules, procedures etc; Hizi zipo zaidi vijijini lakini pia mijini, na zina sura ya udini, ukabila, ukanda n.k; Kama nilivyojadili hapo awali, majority of Tanzanians live and depend on informal institutions kuliko formal institutions; Katiba mpya haitaweza kubadili sana hili, lazima tuanze kwa kujenga a sense of 'STATE' miongoni mwa jamii, na kwamba its institutions (civic institutions) ni muhimu zaidi kuliko community institutions; Kwa maana nyingine, tuanze kuishi collectively na sio in communities sijui za waislamu, wakristo, kanda ya kaskazini, pwani, kusini, ziwa n.k; National integration ni muhimu towards this end kwa maana ya kwamba we should have a Unity in Diversity - na hapa unity refers to political and emotional unity and diversity refers to the socio - cultural plurality; Hii itatusaidia kufanikisha formation of the state and later consolidation;

Kwa sasa we dont have a state that we formed wenyewe bali iliyo rithiwa kutoka kwa mkoloni; It is the very same state ambayo wakati wa harakati za uhuru, ilikuwa ni adui, na ilichukua efforts za wattu weusi ambao walikusanywa na mkoloni chini ya State ya Tanganyika, kuiangusha State hii ya mkoloni together with its civic institutions; Watanganyika walifanya hivyo kwa kuaminishwa kwamba the state and its civic institutions ni adui, na sio rafiki; inakuwaje leo kienyeji enyeji hoja hii igeuzwe kwamba sasa the state and its civic institutions ni rafiki yao? Why? Just because viongozi wa nchi sio wazungu tena? Viongozi hao hao wanaendelea kutokana na community zile zile (e.g. wabunge), na kwa vile sehemu kubwa ya jamii yetu haijafikiwa na state and its civic institutions, jamii hii inategemea viongozi hawa wachume kwa whatever methods necessary from the STATE na kupeleka maendeleo huko kwenye jamii husika; Wanatarajiwa kufanya hivyo, na hii ndio huzaa ufisadi kama nilivyojadili kwenye hoja yangu juu ya Economy of Affection;

Kuhusu CCM kujaa ufisadi, ni kweli lakini ingekuwa hivyo kwa chama kingine chochote iwapo utakubaliana na mimi kwamba Utamaduni plays a big role katika hili; The problem with our STATE under CCM ni kwamba - in its interaction with the society, kuna tatizo in terms of its capacity to exercise control of groups mbalimbali ndani ya jamii; Hii ni kutokana na ukweli kwamba, wakati the colonial State put priority in controlling the Territory of Tanganyika, TANU ilipopokea started by controlling the People (not territory), na tabia hii inaendelea hadi leo kwani CCM na sera zake za maendeleo zinajali maeneo yenye watu wengi kuliko yasio na watu wengi bila ya kujali iwapo yale yenye watu wachache yana ukubwa gani in terms of territory; Nje ye territory in terms of mipaka ya nchi na ulinzi wake, hakuna lingine la maana CCM inafanya; ushahidi wa hili upo kupitia observation ya jinsi gani huduma za jamii zinavyotolewa na serikali, na pia jinsi gani baadhi ya jamii, licha ya kuishi kwenye eneo kubwa sana, lakini kwa vile ni jamii ya wachache, civic institutions hazigusi maisha yao ya kila siku;

Another problem with our state ni kwamba - it can easily be penetrated by groups ndani ya jamii kupitia informal means to acquire influence, kama nilivyojadili elsewhere; Hapa ndio hoja yako inaingia kuhusu CCM na ufisadi kwani kwa bahati mbaya, ndio chama kilichopo madarakani na kuwa victim wa forces zote hizi; Ikumbukwe kwamba wakati wa mfumo wa chama kimoja, viongozi wa CCM walikuwa notorious kukiuka katiba ya nchi kwa kupinda pinda mambo ili mambo yaende; Hii ni kutokana na ukweli kwamba civic institutions of the state alone haziwezi kufanya kazi, na nimelijadili hili kwwa kina kwenye hoja yangu juu ya problematic state na economy of affection;

Kwa kifupi, our STATE is so deeply embedded in societal relations that largely remain locally specific and inadequately integrated into a system of rules; Na hili litaendelea kuwepo hata CCM ikiondoka madarakani; We need to start a true formation of the state - our own state, na kurekebisha mapungufu ambayo tuliyarithi kutoka kwa colonial state; Baada ya hatua hii, tuingie katika state consolidation phase; Vinginevyo Tanzania as a State itaendelea kuwa dhaifu, fragile and it might end up becoming a failed state kama Somalia na nyinginezo kama hatutakuwa makini;
 
Lukolo,



Ni kweli lakini unajua pia suala la Katiba na usimamiaji wake is a two way process; Kwa upande mmoja, ni muhimu kwa viongozi kuwajibika, lakini kwa upande mwingine, pia ni muhimu kwa wananchi kuwajibika; Kuna mchangaji mmoja hapa alisema kwamba suluhisho juu ya suala la rushwa na ufisadi ni lazima lianzie na wananchi wenyewe; Nakubaliana na hoja hii – tunaweza kutatua au angalau kupunguza makali ya tatizo hili kwa kufuata mchakato ambao ni bottom – up – wananchi influencing the top, not top – bottom – viongozi influencing the bottom; Na kaam Mwalimu alivyosema, Rushwa katika jamii haina budi kuwa treated kama uhaini/treason; Katiba mpya haitoshi kutekeleza hili, inahitaji Political Will ya viongozi, lakini such a Political Will itakuja iwapo viongozi wataona kwamba kweli jamii inataka kubadilika; Binafsi naona ni jamii ndio itatuangusha kwani inafaidika sana na rushwa katika mazingira ya economy of affection kama nilivyojadili;



Mfano wa shule ni mzuri kwani shule is a formal institutions with rules, procedures n.k, na yeyoye ambae anakiuka haya, anashughulikiwa accordingly; Lakini nje ya shule, jamii hii inatawaliwa na informal rules, procedures etc; all formalities remain at the institutional level – the school;

Iwapo unakumbuka mjadala wangu Sehemu ya PILI, nilizungumzia tofauti baina ya Collectivity na Community; Shule ni mfano wa Collectvity na ndio maana it works, lakini scope yake ipo very limited kwani shule hiyo hiyo imezungukwa na Community ambayo literary ndio inayoendesha shule husika;

Weak penetration of capitalism hasa hinterland ni kikwazo cha formalization and modernization of the State, hasa kupitia uimarishaji wa civic institutions ili ziwe na prominent role katika maisha ya watu ya kila siku; Mfano wako wa shule ni mzuri, lakini una limitations zake, ila kama una ideas on how we can use this model to formalize jamii yetu kwa ujumla kama njia moja wapo ya kutatua tatizo la rushwa na ufisadi katika jamii yetu, utakuwa umefanya jambo kubwa sana kwa nchi yako;

Hoja yako kuhusu rushwa na uchaguzi ni nzuri lakini kwa kweli it is just a romantic folly; Wewe unatazama rushwa kama vile ni kitendo cha hiyari cha wagombea; UKipata muda naomba upitie bandiko langu namba 26, paragraph kama nane za mwisho ambapo naongelea suala la Economy of Affection; Ningependa kusikia mawazo yako juu ya jinsi gani Chama nje ya CCM kitataua tatizo husika i.e. Economy of Affection, kwa kupitisha to sheria kali kali kama unavyoshauri;
Naikubali sana approach ya bottom-up. Revolutions nyingi sana duniani zimetokea kutokana na approach hiyo. Lakini Tanzania ni nchi ya tofauti kabisa na nchi zilizo nyingi duniani. Watanzania ni waoga na wenye unyenyekevu wa kinafiki. Si rahisi kwa watanzania kusimama na kukipinga hata kile ambacho kwa hakika kinawaumiza. Watabaki kunong'ona tu huko pembeni bila kukipeleka mahali husika.

Lakini sababu kubwa ya kuwa na tabia ya aina hii ni kutokana na aina ya viongozi waliopo madarakani. There are too many irresponsible leaders. Ambao wanaweza kupewa taarifa na wakaikalia tu. Kwa mfano unaweza kumreport mtu fulani kutokana na vitendo vyake, kumbe huyo mtu anakula pamoja na director wa shirika au taasisi, na mwisho wa siku ukajikuta wewe ndo unafukuzwa kazi. Lakini zaidi ya yote, mfumo wa inteligensia ya Tanzania ni wa kishenzi pia. Ndiyo maana kuna mahali nimesema wala rushwa wakubwa nchini ni pamoja na usalama wa Taifa. Maana mtu wa kawaida ukireport rushwa ya viongozi wa serikali, unakuwa umeyaweka maisha yako hatarini. Kama akina Mwakyembe pamoja na kuwa viongozi bado maisha yao yalitishiwa, je jiulize kwa mtu baki kama mimi. Wananinyonga na hakuna popote nitakaporepotiwa kwamba nilinyongwa. Inabaki kuwa ni hasara ya ndugu zangu, mke wangu na wanangu tu.

Kuna mtu mmoja hapa aliwahi kuleta uzi kwamba mke wa Rais alimlazimisha director wa TPA atoe makontena bila kuyakagua. Na kwa shingo upande huyu mkurugenzi aliyatoa. Kwanini hakureport jambo hili mahali pengine au hata kwenye vyombo vya habari? Ni wazi kwamba alijua kufanya kwake attempt ya kumreport mke wa rais kunaweza kupelekea kupoteza maisha na kuacha watoto yatima. Sasa hapa unagundua kwamba hata kama jamii ingekuwa na dhamira, bado kama viongozi watakuwa bado ni wabia wa rushwa utekelezaji wake utakuwa ni mdogo na mgumu zaidi maana wananchi wenye kimbelembele cha kuongelea habari za rushwa watajikuta wakitishiwa maisha na kuuawa kama si kupoteza nafasi zao za kazi.

Lakini linaloweza kutusaidia kama tutatumia hii bottom-up approach ni kuwa na wanasiasa aggressive, hasa wa upinzani wenye uwezo wa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya madhara ya rushwa ndogondogo hadi zile kubwa. Tukatumia nguvu ya umma. Popote inaporepotiwa rushwa kama hivi sasa mabilioni ya Uswis mara hizi bilioni 80 za TANESCO, vyama vya upinzani waandae maandamano kupinga huo ubadhirifu. Pia wanaharakati wanaweza kuwa na nafasi katika hili la kutoa elimu na kuandaa ant-corruption movements.

Pamoja na ukweli kwamba hii approach inaweza kuwa ni nzuri na yenye nguvu, lakini bado ina changamoto za ushahidi. Na itafanikiwa kumaliza rushwa ndogo ndogo za kwenye grassroot tu. Lakini zile za mawaziri kusaini mikataba mibovu hazitaweza kuisha. Ndiyo maana nafikiri top-down approach kwa sasa inaweza kufanya kazi kwa kuwa situation ipo worse. Tuwe na top-down approach ambayo itakuwa ni kwa mamlaka na amri na si kwa kuridhia, halafu baadaye hali ikiwa kwenye unafuu, tutaongea habari za maoni ya wananchi na kuwapa mamlaka wananchi kuwezo kucontrol hilo.

Tukiongelea shule kama organization ya mfano katika utendaji na usimamizi wa sheria na taratibu. Mimi nafikiri kinachoiwezesha shule si tu sheria na taratibu zake bali leadership style yake ndiyo inayomatter zaidi. Kwa maana ya kwamba tunaweza kuwa na kiongozi ambaye anaendesha mambo kwa kushirikisha subordinates wake, wanakaa pamoja kukubaliana sheria na taratibu za uendeshaji na kukubaliana aina ya adhabu kwa atakayekiuka. Uongozi shirikishi mahali pengi umekuwa na matokeo mazuri. Vivyo hivyo katika ngazi ya taifa tunaweza kuwa na huu utaratibu. Rais akakaa na mawaziri wake, wakuu wa wilaya, mikoa, wakuu wa idara na taasisi mbalimbali. Wakaweka mkakati wa pamoja wa kupambana na rushwa. Na ikawekwa wazi kwamba iwapo rushwa itarepotiwa kutoka kwenye eneo lake la kazi na ikagundulika kwamba kiongozi wa eneo husika ameshindwa kuchukua hatua, ni automatically kiongozi huyo anapoteza kazi na kushitakiwa.

Kwa mfano mimi nilisoma shule ya private. katika shule hii kulikuwa na sanduku la maoni ambalo linafunguliwa na mkuu wa shule tu. Inapotokea mwanafunzi amefanyiwa chochote iwe na mwalimu au na mwanafunzi mwenzake anaandika kimemo anakitumbukiza moja kwa moja kwenye sanduku la maoni la mkuu wa shule. Tutumie strategy hiyo pia kitaifa. Mkuu anachofanya, baada ya kupata hicho kimemo anamuita mwanafunzi kumuulizia mazingira ya tukio na pia kutafuta ushahidi mwingine. mwisho wa siku unakuta tu mwalimu kafukuzwa kazi au mwanafunzi kasimamishwa masomo.

Katika level ya nchi pia tutoe namba za simu kwa kila raia (vyombo vyote vya habari vizitangaze ili hata wale wa vijijini wazipate), kwa ajili ya kila mwananchi kureport hali ya kutokuwajibika kwa baadhi ya watendaji. Ukiambiwa njoo kesho mara mbili unatoa taarifa kupitia hiyo namba ili waleta investigators wao. Ukizungushwa kwenye kupewa huduma yoyote katika ofisi ya serikali au binafsi unatoa taarifa mara moja. Hawa wanaohudumiwa ambao kimsingi ndiyo wanaooumizwa na rushwa ndiyo wanaweza kuwa chachu mhimu ya mabadiliko kuliko hao viongozi. Katika approach hii botto up approach inaweza kuwa effective. kwa mfano ukienda kuchukua TIN namba pale TRA samora, unaambiwa njoo kesho. Lakini ukiwaona wale wamama waliokaa kihasarahasara around ukawapa 15000 unapata TIN numba ndani ya dakika tu. Sasa kama kuna mahali pa kureporti kuna mtu atashindwa kufanya hivyo. maana ni dhahiri kwamba hakuna basis ya mtu kuja kesho kuchukua TIN namba bali ni mbinu tu za kupokea rushwa. Lakini sasa ni lazima pia tuweke wazi kwamba hizo report zitapelekwa kwa nani ambaye atakuwa clean? Hilo nalo litahitaji mkakati wake.

Kwenye hoja ya economic of affection nitakupa mifano ya watu wawili ninaowafahamu kwa karibu sana ambao wamekuwa viongozi katika nchi yetu. Hawa ni Marehemu Jackson Makwetta (RIP) na Ibrahimu Kaduma. You know them very well, wamekuwa mawaziri kwa nyakati tofauti katika nchi hii. Lakini nataka kukuambia hawakumsaidia mtu kwa kuwa wanataka kuonekana. Kuna ndugu zao wa karibu kabisa: dada zao, wadogo zao mama zao ambao hadi dakika ya mwisho mimi nimewafahamu wakiwa wanaishi maisha magumu sana na hawakupata hata nafasi ya kwenda shule despite the fact kwamba hawa ndugu walikuwa na nafasi nzuri serikalini. Kama mianya ya rushwa itakuwa imezibwa, mtu ata-reason out kama apokee rushwa au aibe ili kusaidia ndugu zake na kupoteza kabisa kazi na mwisho wa siku kuishia jela au aendelee kushare kidogo alichonacho na kuendelea kujihakikishia maisha yenye nafuu kwa faida ya watoto wake?

Jackson Makwetta amefariki akiwa hana hata nyumba ya maana ya kuishi. Huyu mtu aliamua kusacrifice maisha yake. Akaacha kuishi kwa anasa, na kutumia kila kidogo alichokipata kwa ajili ya kuiendeleza jamii yake kielimu. Nimeona Jackson Makwetta akitoa hela yake ya mfukoni kwenda kununua bati za kuezekea shule. Angetaka kujinufaisha na kuishia kwenye mabangaloo na kumiliki akaunti Uswis, angeweza tu kuiba pesa za serikali na kuzipeleka huko vijijini kujenga shule na kuwasomesha ndugu zake, na hizo za kwake za mfukoni akaziwekeza kwenye maisha binafsi. Lakini Makwetta amefariki akiacha ndugu zake wakiwa kwenye umasikini mkubwa.

Kwanini hiyo economy of affection iwe ni issue kwa watu fulani na si kwa wengine? Hapo ndipo ninaposema iwekwe tu mikakati ambayo ipo serious na top leader awe na serious commitment ya kusimamia. Kwa hakika hatutakuwa na classess za maisha. Maana watoto na ndugu wa kiongozi watakuwa na equal opportunity kama wale wasio ndugu wa viongozi. Maana kuwa kiongozi hakutamgurantee mtu kuwa na pesa za ziada za kuwagawia hata ndugu zake au kuwekeza hadi kwenye benki za ulaya. To me hiyo economic of affection bado siyo excuse nzuri ya kutufanya tushindwe kuikabili rushwa. Economic of affection inaonekana ni tatizo kwa kuwa kuna loophole ya watu kuweza kuiba hizo fedha. Lakini kama mianya ingezibwa hakuna cha economif of affection wala majukumu. Tumeshindwa tu kuwa na kiongozi ambaye yupo commited.
 
Tunahitaji fikra mpya! You are very right! Tunahitaji pia msimamizi mwenye commitment anayetekeleza kwa vitendo kiapo chake cha kuilinda katiba. Lakini hatuhitaji kizazi kipya. Kwa kuwa hakuna kizazi kitakachoshushwa kutoka angani? Watoto wetu na wajukuu zetu wataendelea kuzaliwa katika mfumo huu huu wa kirushwa.

Tunachohitaji hapa ni uongozi mpya wenye fikra mpya na unaoichukia rushwa kwa dhati kabisa. Hili si suala la chama, bali ni suala la individual leader. Kwamba tufanikiwe kumpata rais ambaye ana serious commitment ya kuliondoa tatizo la rushwa. Awe ni kiongozi ambaye hayupo tayari kumfumbia macho hata waziri wake aliyempigia kampeni mwanzo mwisho. Na hawa watu si kwamba hawapo, tunao sana. Kwani Nyerere alishushwa kutoka mbinguni? Si alizaliwa katika kizazi cha kikoloni ambacho pia kilikuwa na rushwa? Lakini wakati ule, mtu alilipwa mshahara senti tano na bado alifanya kazi kama mtumishi mwaminifu wa umma na si mtawala! Mimi naamini hiki kitu kinawezekana, ni seriousness tu katika kuchukua hatua.

Tulikuwa na mjadala na watu fulani kule facebook, tukaongelea juu ya uwajibikaji wa TISS, TAKUKURU, police na mamlaka nyingine za serikali katika suala zima la kutoa taarifa za rushwa (kwa mfano wizi wa TANESCO, mabilioni ya Uswis, RICHMOND na kadhalika). Kuna watu walieleza wazi kabisa kwamba mkuu wa nchi ni mzito kufanya maamuzi. Anapelekewa taarifa zote lakini nyingi anazizima na nyingine anachukuwa mda mrefu kuzifanyia maamuzi! Kwanini anafanya hivyo? Niambieni kama angekuwa ni rais anayefanya maamuzi kwa wakati bila kujali ni nani anahusika na rushwa, tungekuwa wapi?

Trend ya kumaliza rushwa inaweza kwenda hivi: Rais akimwajibisha waziri ipasavyo bila kumuonea haya, waziri atafanya hivyo hivyo kwa wakurugenzi, wakurugenzi hali kadhalika kwa mameneja nao vivyo hivyo kwa walio chini yao. Mwisho wa siku kila mtu atakuwa anamwogopa hata rafiki yake wa karibu linapokuja suala la rushwa. Na hivi ndivyo Nyerere alivyofanikiwa. Sasa rais mwenyewe mla rushwa, nani atajali kuhusu suala la rushwa?

Kwanza TUPATE FIKRA MPYA. Msimamizi mwenye kujidhatiti utamtoa wapi kwa sasa hali kuwa Fikra Mpya hazipo? Wote ni zao la Mzoga AZ, hivi unajua kwamba kusingekuwa na Upinzani huu leo kama kusingekuwa na Azimio la Zanzibar?

Tupate msimamizi atakayejidhatiti kusimamia katiba, Katiba ipi? Je, ni hii iliyozaliwa na sera za Uvundo wa AZ?

FIKRA MPYA NDIZO ZITAKAZOLETA UONGOZI MPYA WENYE KUJIDHATITI, NA SI VINGINEVYO, Uongozi uliozaliwa na Fikra Mfu za AZ hautatusaidia bado. Sasa ni UPINZANI GANI UNAOHISI UNA HIZO FIKRA MPYA ZINAZOTOFAUTIANA NA UVUNDO WA AZ? Binafsi sioni!
Sisi wenyewe kama Wenye nchi, ndio tupaswao kuzalisha hizo FIKRA MPYA, na sisi wenyewe ndio WASIMAMIZI WA FIKRA HIZO, tutakuwa na dhamana ya kusimamia Fikra zetu!

Kuendelea kuamini na kuaminisha watu kuwa kuna Taasisi ya kuleta Ukombozi ni Ulimbukeni na dhambi kubwa!
Ninaposema Tunahitaji Kizazi kipya cha Fikra, simaanishi kizazi cha binadamu yaani watoto wetu hapana, bali ni KIZAZI KIPYA CHA FIKRA. Tuachane na hiki cha AZ!

Mkuu Mchambuzi,
Umenena vyema sana kuwa " WE NEED TO START A TRUE FORMATION OF THE STATE-OUR OWN STATE" naafikiana nawe mia kwa mia! Cha kushangaza mara zote tunaishia hapo, tunaacha mambo yaeleeelee kama maboya na kupotea, kesho yake mwingine anaanzisha mjadala unafikishwa hadi hapo unazimika, kesho yake hivyo hvyo! Je, haya si maigizo? Tunataka nani awe msimamizi wa FIKRA ZETU? Leo kuanza kuwajadili wanasisia katika dhdna ile ile ya watawala na wapinzani KUTATUFIKISHA WAPI? Ni nani wa kufanya hayo kama sio sisi wenyewe?

Hili ndio jibu la matatizo yote ya mwanaafrika wa Tanzania na kwingineko katika kauli hii " We Need to Start a True Formation of The State-Our own State" hilo ndilo JIBU!

TUANZE HAPO SASA na si kuanza kushindanisha hoja za nani ni Fisadi sana kuliko mwenzake! Hakika, HAITUSAIDII.

Mungu wetu yu hai, tayari kutupigania vitani.
Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa

Let me agree with you kwamba vyama vya upinzani havina fikra mpya. Wala hakuna taasisi yenye uwezo wa kuleta fikra mpya. Then tell us where will these new thoughts come from? What will be the source, who is going to pioneer them?
 
Last edited by a moderator:
Civil Society maana yake civic institutions of the state kuwa na nguvu over and above community based institutions ambazo zinaendeshwa zaidi na informal rules, procedures etc; Hizi zipo zaidi vijijini lakini pia mijini, na zina sura ya udini, ukabila, ukanda n.k; Kama nilivyojadili hapo awali, majority of Tanzanians live and depend on informal institutions kuliko formal institutions; Katiba mpya haitaweza kubadili sana hili, lazima tuanze kwa kujenga a sense of 'STATE' miongoni mwa jamii, na kwamba its institutions (civic institutions) ni muhimu zaidi kuliko community institutions; Kwa maana nyingine, tuanze kuishi collectively na sio in communities sijui za waislamu, wakristo, kanda ya kaskazini, pwani, kusini, ziwa n.k; National integration ni muhimu towards this end kwa maana ya kwamba we should have a Unity in Diversity - na hapa unity refers to political and emotional unity and diversity refers to the socio - cultural plurality; Hii itatusaidia kufanikisha formation of the state and later consolidation;

....

Kuhusu CCM kujaa ufisadi, ni kweli lakini ingekuwa hivyo kwa chama kingine chochote iwapo utakubaliana na mimi kwamba Utamaduni plays a big role katika hili; The problem with our STATE under CCM ni kwamba - in its interaction with the society, kuna tatizo in terms of its capacity to exercise control of groups mbalimbali ndani ya jamii; Hii ni kutokana na ukweli kwamba, wakati the colonial State put priority in controlling the Territory of Tanganyika, TANU ilipopokea started by controlling the People (not territory), na tabia hii inaendelea hadi leo kwani CCM na sera zake za maendeleo zinajali maeneo yenye watu wengi kuliko yasio na watu wengi bila ya kujali iwapo yale yenye watu wachache yana ukubwa gani in terms of territory; Nje ye territory in terms of mipaka ya nchi na ulinzi wake, hakuna lingine la maana CCM inafanya; ushahidi wa hili upo kupitia observation ya jinsi gani huduma za jamii zinavyotolewa na serikali, na pia jinsi gani baadhi ya jamii, licha ya kuishi kwenye eneo kubwa sana, lakini kwa vile ni jamii ya wachache, civic institutions hazigusi maisha yao ya kila siku

Mkuu mchambuzi ninaposema Civil society nilikuwa nakusudia kuutaja mhimili wa dola usio rasmi mbali na Executive, Legislature and judiciary, au kwa kiingereza fourth and fifth estates, yaani ule unaoweza kuwaangalia hao watatu(kwenye kapu hilo tunaweza kuweka media, NGOs, interest groups, pressure groups and alike. Tatizo ni kuwa serikali yetu imeuvunja kabisa mhimili huo. Sijui kama mwanzoni ulivunjwa kwa nia njema ya kuwa control watu na sio territory au kwa nia mbaya. Lakaini wakati wa TANU hali labda haikuwa mbaya sana kwa kuwa serikali ya Mwalimu kwa kiasi kikubwa iliweza kujidhibiti na kujikosoa ilipofanya makosa. Lakini sasa haina uwezo huo tena, chama sio tena collective entity but it is a body of people who are there for economic motives.

Kwa sasa the state of fourth and fifth estate is in mess, nyingi ni za mtindo wa kuchumia tumbo na zina survive kwa kudra ya chama na serikali, au zinatumika kama ni silaha katika mapambano ya kisiasa. Bado hazina msingi imara ya kisheria na ziko vulnerable naa kushughulikiwa, na even worse focus ni fedha za wafadhili na sio kuikemea serikali. Sasa hivi hata media zikiandika kuhusu uozo wa serikali serikali hata haishituki. Kibaya zaidi nazo tayari zimemezwa na politics...angalia TLS, TFTU, RAAWU, UDASSA, NEMC utaona kuna harufu kali ya CCM ndani yake.

Kimsingi ni vigumu sana kupambana na ufisadi wakati structures zote za state hazifunction na kudischarge duties zake kama zinavyotakiwa, na kuwa politicized kama zilivyo sasa.

Unachosema kuwa tunaelekea kuwa failed state, nadhani nakubaliana na wewe kabisa. We are very close to that, nilikuwa naangalia hotuba za Mwalimu Nyerere, aliyotoa Kilimanjaro na aliyotoa wakati wa mkutano uliompita Mkapa kuwa mgombea urais. Ukiangalia yale yote kwa sasa ndio tunayaona, udini sasa ni karata ya kisiasa, ufisadi sasa ni way of life, uhalifu unalindwa hapingwi, haki iko kwa wenye nguvu...we are already here. 2015 kama tutapata rais kwa mchezo kama wa 2010 tunaweza kuanza kuvuna tunayopanda sasa. We are no longer in unity in our diversity, we are working so hard to create divisions na chuki.

Tatizo ni kuwa sasa hivi jamii yetu yote imeharibika na hakuna anayefanya kazi ya kuifix, wenye nguvu wanafanya kazi ya kuibomoa zaidi kwa manufaa yao kisiasa. Ni kama kila mtu amepoteza hope.
 
Lukolo,

Asante sana kwa mchango wako mzuri kwa mara nyingine tena; Naomba kujibu hoja zako za bandiko namba 36 kama ifuatavyo:

Kwanza naomba nianze na hoja yako kuhusu Mzee Kaduma na Marehemu Makweta; Nakubaliana na wewe juu ya hili kwani hawa walikuwa mawaziri tokea miaka ya mwanzo ya sabini; Iwapo kuna mtu atakuja na hoja kwamba waliacha uongozi zamani sana hivyo hapakuwa na mianya ya kufisadi, hii sio sahihi kwani Makweta amekuwa waziri kuanzia miaka ya mwanzo ya sabini hadi mwaka 2000; Ukiangalia mawaziri wengine walioingia kwenye uongozi hata katika kipindi kifupi tu 1995 – 2000, hawa maisha yao ni ya juu sana kulinganisha na makweta; Kuhusu Kaduma, same applies; Licha ya kuwa waziri mambo ya nje, Kilimo n.k, pia alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mkonge Tanzania hadi miaka ya tisini; Hakuna Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umma (hata wale wa miaka ya themanini) ambae ana maisha ya kawaida kama ya mzee Kaduma;

Kwa kifupi, I can't agree with you more; Kinacho watenganisha hawa na viongozi wengine ni Uzalendo na mapenzi kwa taifa lao; Wapo wengine kina Ibrahim Mbita n.k, ambao kwa masikio yangu nimewahi kusikia siku za huko nyuma wanasiasa kadhaa ambao leo ni matajiri wakubwa wakimcheka mzee wetu huyu eti ‘amechoka na maskini.'

Hoja ya pili ya kujibu ni kuhusu shule kama mfano wa jinsi gani tunaweza kufanya formalization katika jamii yetu na kuwa na rule of law n.k; Kimsingi nakubaliana na wewe, lakini bado naona kwamba kuna changamoto nyingi sana towards that end; Ni muhimu kwanza wananchi waka hamisha loyalty yao from community institutions to state institutions (civic institutions); Lakini ili kufanikiwa, ni muhimu kwa Umma kuwa na absolute confidence kwa Serikali husika; Ni hapa ninapokubaliana na wewe, lakini pamoja na hayo, ni muhimu tukaelewa kwanini wananchi walio wengi bado wana more loyalty to community institutions than civic institutions:

Kilichotokea ni kwamba – harakati za kudai uhuru zilitumia Local Community Institutions to organize efforts and strategies, na bila ya hizi institutions kuunga mkono TANU, uhuru usingepatikana; Watu weusi waliunga mkono TANU kupitia their community institutions za kidini, kikabila n.k, kwa imani kwamba – Civic Institutions of the Colonial State was the greatest Enemy of all time;

Mimi nadhani tatizo kubwa lililojitokeza ambalo ni moja ya makosa ya Mwalimu ni kusahahu kuwafanya watanganyika wale kwanza kuwa RAIA/CITIZENS of Tanganyika, kabla ya kitu kingine chochote; Badala yake, walikusanywa kusanywa hapa na pale na kuambiwa kwamba mipaka aliyoweka mkoloni itaendelea kuwa ile ile, lakini serikali ya sasa itakuwa kwa ajili yenu; Kuwa raia wan chi ni kitu muhimu sana na kinajega sense of collectivity; ndio maana hata kwa nchi zilizoendelea, uraia hupitia michakato mingi kama vile uelewa na umuhimu juu ya Civic matters n.k; Mwalimu hakufanya haya, ingawa alijitahidi kufanikisha Utaifa na pia kujenga loyalty ya umma kwa state kupitia ideology iliyohimiza usawa, chini ya developmental state, ingawa juhudi hizi hazikwenda mbali sana;

Leo hii, watanzania wengi wapo trapped between the Market and their subsistence surroundings huku state ikiendelea to milk them through uzalishaji wa mazao ya kilimo to feed the urban elites, kilimo for exports kukidhi gharama za kuendesha serikali n.k; Ndio maana kwa kiasi fulani, the state ni adui kwa jamii nyingi, na kiungo pekee cha kuipa state its legitimacy ni viongozi wanaotoka katika hizi communities – za kidini, kikanda, kikabila, ambao ili wafanikiwe kisiasa, ni lazima waende kuchuma kwenye State na kupeleka resources kwenye communities zao; bila ya kufanya hivyo, hawawezi kupata acceptance; haushangai kwanini kuna viongozi wengi mafisadi lakini kwa vile tu they share their wealth huko wanapotoka, wanaendelea kutamba?

Vinginevyo sina maana kwamba hatuwezi kuondokana na economy of affection and its forces, maana yangu ya msingi katika hili ni kwamba ni lazima tuelewe the root – cause, why it exists and who benefits kabla hatujaja na mikakati mbadala ya kuwezesha public realm in the sense of civic institutions zianze kukumbatiwa na wananchi walio wengi kuliko community based institutions zinazoendeshwa informally, ambazo pamoja na kuwa corrupt, lakini they carry such high benefits kwa wananchi wengi in terms of social capital and economic gain;

Mwisho ni kuhusu tabia na utamaduni wetu; ningependa kulijadili kama ifiatavyo:

Watanzania wengi accept maisha yao kama yalivyo, ndio maana they don't do much to change it; kuamka kwa vijana mijini sio kigezo kwamba sasa watanzania wameamka bali ni jadi yao kama vijana kwani hata miaka ya mwisho ya hamsini na pia mwanzo ya uhuru, TANU iliona umuhimu wa kuanzisha na kuimarisha TANU Youth League to arrest the situation; Taasisi hii ikawafanya vijana kuwa occupied kidogo kwani walipewa such a militancy power mara nyingine kuliko polisi, na walikuwa wanalipwa; Pia TANU youth league ilisaidia kuweka mazingira ya recruitment ya vijana kuwa viongozi wa baadae; Ukichanganya pia na uanzishwaji wa Chipukizi, JKT n.k, seke seke la vijana na mabadiliko likafifia; Kidogo naenda nje ya mada lakini nadhani unaelewa naelekea wapi;

Nikirudi kwenye hoja yangu ya msingi juu ya suala hili la utamaduni na tabia zetu watanzania kukubali maisha kama yalivyo– our religious convictions mara nyingine work against us; The most uneducated people in Tanzania I should say wapo fatalistic; maana ya neno hili kwa mujibu wa dictionary ili nisipoteza uzito wa neno lenyewe ni kama ifuatavyo:

"A submissive mental attitude resulting from acceptance of the doctrine that everything that happens is predetermined and inevitable."

Kwa mtazamo wa wananchi wengi hawa wa vijijini, there is little that they can do to control events in their surroundings; They accept and submit, period! Hii acceptance ni on supernatural order kutokana na religious convinctions, na inachangia sana to make them less likely to challenge harsh realities katika maisha yao ya kila siku;

Kutokana na haya, acceptance of hardship is a key feature ya personality ya watanzania na inachangia kwa kiasi kikubwa sana hali ya umaskini wao; We are patient, and we are used to long term sufferings; lakini inapotokea wakaamka, mara nyingi sio kwa maslahi ya taifa bali maslahi ya kada yao (aidha vijana, maskini, dini au kabila fulani), kutokana na kundi husika to vie for control of certain resources or decision making strictures juu ya such resources; its rare kuona mchakato huu unahusisha mass movements au protest against unjust government; and when the latter happens, ni kwa kushinikizwa na political actors fulani fulani;

Njia za kurekebisha mapungufu kama haya ni kurudi pale pale – conflict between the State and its Formal and Civic Institutions vis as vis Community and Informal Institutions; Which one delivers more to the majority? Of course the latter;
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom