Mange Kimambi kuja na maandamano nje ya World Bank HQ; huu mkakati umenishtua sana

Nakubaliana na wewe Mkuu,na mimi nimechangia katika hili janga la taifa linaloitwa CCM,lakini yaliyopita yamepita tutizame wapi tunaelekea kama taifa..
Tumsaidie Rais kuleta order, haiwezekani kuachia wahalifu waendelee kuifanya tz jalala..kila mahali uozo na hao wanaoguswa ndio vinara wa kulalamika this time watanyooka tu wawe ccm cuf act whatever..
 
Dude kuwa client haimanisha una 100% za kupata mkopo kuna factors nyingine wanaangalia, mfano kama hufati demokrasia, haki za binadamu usitegemee hao WB watakupa mkopo. Kaeni mtafakari vizuri hii battle siyo ya kitoto .
Mkubwa hatishiwi nyau wewe kaa utulie rais wetu mpendwa akutengenezee Maisha yako na kizazi chako
 
Tukio dogo sana hilo baada ya 26/4 huwezi kukuta media zinajadili jambo hilo...kilichotegemewa kutokea hakikutokea thats why nasema ni jambo dogo sana.
Wewe unaona kuwa ni tukio dogo,huo ni muono wako,lakini dunia inaliangalia hili tukio ni kbwa sana kwa nchi ya amani kama Tanzania,Mkuu umefatilia magazeti ya nchi jirani na nchi rafiki zetu kama Kenya na South Afrika tyameandika nini kuhusu siku ya 26/4..,

Mange kashinda,dada hana hata kilo 60 kaishinda serikali nzima ya Magufuli na vyombo vyake vya usalama,...Aibu kubwa
 
Tumsaidie Rais kuleta order, haiwezekani kuachia wahalifu waendelee kuifanya tz jalala..kila mahali uozo na hao wanaoguswa ndio vinara wa kulalamika this time watanyooka tu wawe ccm cuf act whatever..
Mhalifu na jambazi mkubwa kwa raia wa Tanzania kwa sasa ni raisi mwenyewe..,watu wanapotea,wanapigwa risasi,watanzania hatuko salama,huo ndio ujumbe Mange kadhamiria kutuma ili dunia ipate kufahamu nini kinaendelea Tanzania,..kafanikiwa kwahilo
 
Mkuu hivi vitu ni process na mkija kujaa kwenye 18 zao hamtakuwa na namna, kwa ushauri kaeni mtafakari upya namna ya kuaddress haya mambo.
Mmebaki na matumaini hewa ya ushindi wa miujiza. Eti mkijaa kwenye 18 kwa hiyo mnavizia vizia. Mtasubiri sana, kwa taarifa yetu interchange ya ubungo itajengwa, SGR itajengwa, stiglers gorge itajengwa achilia mbali miradi mingine kibao itajengwa na kumalizika kabla ya 2025 haijalishi kwa mkopo au cash! Kwa bahati nzuri watanzania wanajivunia kuwa na Rais asiyekatishwa tamaa na changamoto za kitoto kama mnazotaja. Rais wetu jembe kweli kweli hadi wazungu wenyewe wanaweweseka ovyo!
 
..sasa hivi serikali hii inahaha kupata pahala pa kukopa pesa za miradi mikubwa wanayofanya kisiasa.....sasa hawana sehemu nyingi za kukopa Na wamebaki kuzuga kuwa watatumia pesa za ndani..ambazo hazipo....
..hivyo kwa kuwashtaki kwa world bank kwa njia ya maandamano itakua pigo angamizi la kuwashika pabaya mno....mange amejipanga....
 
Zile chaguzi ndogo hazionyeshi support ya watanzania kwa rais. Ile idadi ya wapiga kura, na mbinu zilizotumika kuhakikisha ccm inashinda zote zitawekwa wazi. wakati ule uhuni unafanyika sidhani kama mlijua madhara yake, sasa ni muda wa kuvuna kile alichopanda. Ile hamasa wananchi waliyokuwa nayo awamu yake ilipoanza sasa imetoweka rasmi, ugumu wa maisha, ajira, na sasa amepandikiza hofu ili ionekane anakubalika. Mkuu jamaa ana shida na kibaya hata wansccm hawawezi kumdhibiti tena. Hebu niambie hata jambo dogo kama sukari, nipe bei aliyokuta akiingia madarakani na iliyo sasa. Ukiweza taja kiwango cha ajira kwenye awamu yake, zaidi ya kuhadaa umma kwa kufungua miradi ya mtangulizi wake ili ionekane ni yeye ndio kaifanya. Hapo tunangoja hatima ya 1.5t
Ni uchaguzi upi hakuwahi kulalamika kuibiwa kura? Tumeshawazoea kazi kulia lia tu kama makinda ya ndege. Endelea kujipa matumaini ipo siku utashinda hata kama ni uzeeni
 
She is Pupp
Mkubali mkatae huyu DADA kuna WATU WAPO NYUMA YAKE(mostly walioguswa maslahi yao na AWAMU hii)....she is not smart at all kuyafanya haya anayo yafanya sasa kwa tunaomjua tokea TUKIWA WATOTO PAMOJA,.......na ni lazima watakuja kivingine sasa...Either kwa kukutengeneza vikundi vya KIKAGAIDI au kuanza kufanya mauaji yanayoendana na UGAIDI lengo ni kutengeneza chuki baina ya serikali na WANANCHI...ni suala la muda tu
She is a Puppet
 
Wewe unaona kuwa ni tukio dogo,huo ni muono wako,lakini dunia inaliangalia hili tukio ni kbwa sana kwa nchi ya amani kama Tanzania,Mkuu umefatilia magazeti ya nchi jirani na nchi rafiki zetu kama Kenya na South Afrika tyameandika nini kuhusu siku ya 26/4..,

Mange kashinda,dada hana hata kilo 60 kaishinda serikali nzima ya Magufuli na vyombo vyake vya usalama,...Aibu kubwa
Kashinda nn huyo mange, fafanua
 
Sijui kwa nini mtu anaweza pima upingwaji wa Rais sasa hivi lakin hawezi ona uharibifu uliokuwepo kabla Rais huyu hajaingia madarakani..nchi hii ilikuwa mzoga!! kila aina ya uchafu ilikuwa umeweka makazi hapa..makampuni makubwa hasa ya madini yalikuwa yameweka mirija kunyonya rasilimali zetu yalikuwa yamenunua viongozi ndio maana hawakuwa tena wanatetea masilah ya nchi..kumbuka ile tume ya kupitia sheria mpya za madini ambapo hata baada ya ripoti kukabidhiwa kwa muunda tume badala ya kutujulisha kile kilionekana na tume yeye aliwakimbizia rafiki zake nje na wao bila hata kuwaza na jinsi walivyokuwa wanatudharau wakaandikiana kufahamishana kuwa hakuna lolote litafanyika kubadili sheria za madini..na ndivyo ilivyokuwa, hatuwezi kuendelea kudharauliwa hivyo, wapo waliojenga empire za kikabila, kidini, kiukoo nk..yote hayo yalikuwa kama jambo la kawaida, amepatikana jasiri wa kukomesha ujinga huo LAZIMA wahanga watasimama kupinga! HAWATAWEZA! watafute mambo mengine ya kufanya..mange amejitoa akili hafikirii hata hatari anayotembea nayo ya kufanya watoto wake mwenyewe kukosa mama yao ktk umri huu sababu eti anatetea watanzania..si kweli kipo kitu amepewa chenye thamani zaidi hata ya watoto wake!
vp kuhusu bunge live na mikutano ya siasa?
 
Huyu Mange Kimambi anababaisha watu ambao wavivu kusoma. Wasomi tunajua "public choice Theory" inasemaje kwa watu kama Mange na wengineo wanaongea kwa niaba ya umma. Soma nadharia hiyo utajua ninachomaanisha. Ujinga kuivuruga nchi kwa maslahi binafsi...Kuna malengo yake binafsi anayotaka kuyafikia hiyo ni political platform anajua yeye anafanya nini lakini si kwa MANUFAA YA TANZANIA BALI KWA MANUFAA YAKE BINAFSI...
How....?
 
Back
Top Bottom