The Economist na Mauongo Yao Kuihusu Tanzania: Waidanganya Dunia Tuna Torture Wakimbizi!. Wanapata Faida Gani?. Kwanini Tunanyamazia Uongo Huu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Wanabodi,
Kila mara nasisitiza humu, uongo ukisemwa sana, na kuachwa kujirudia rudia bila kukanushwa, mwishowe uongo huo hugeuka ukweli. Na uongo ambao ni uongo mtupu, ukisemwa kuwa kitu fulani kitatokea, tusipo kanusha uongo huo, halafu hicho kitu kikaja kutokea kweli, then, kufuatia kuanuni ya matokeo, ule uongo utahesabika ndio ukweli, kwa sababu umetokea kweli. Hii ni kufuatia baadhi ya kauli, zinauwezo wa kuumba.

Mfano kuna huu uongo wa jarida hili kuhusu hili jambo la kuihusu Tanzania, ambao ulisemwa mwaka 2019. na kudaiwa kuwa litatokea Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka 2020. Hatukukanusha, tukanyama na kuwapuuza kwa hoja za uzushi huo ni upepo tuu na utapita.

Lakini kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020, hilo jambo, hawa The Economist walilolizusha, likatokea kweli!, matokeo yake, sasa itaonekana kuwa kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni kweli kilipangwa kabla, na The Economist walikisema, wakati kiukweli, kile The Economist walichokisema, ilikuwa ni uongo na uzushi, lakini kwa vile, hatukukanusha uongo huo na uzushi huo, kisha ukaja kutokea kiukweli kabisa, dunia italiamini jarida la Economist kuwa walisema kweli, hata kama matokeo ya uchaguzi mkuu huu, ni Watanzania wenyewe, kwa ridhaa yao, wamewakataa wapinzani, na kuichagua CCM kwa mapenzi yao, katika uchaguzi huru na wa haki, licha ya dosari ndogo ndogo, no one will belive its peoples will! ya Watanzania!, watauamini uongo ule kuwa kilichotokea kilipangwa, kikasemwa kimepangwa, kikatekelezwa na ndicho kilichotokea!.

Kwenye toleo la la wiki hii, Jarida la The Economist limeendeleza mauongo yao kuihusu Tanzania, waidanganya dunia kuwa Tanzania, inaendelea kufanya mahojiano kwa kutumia njia haramu za mateso makubwa ya Torture, na njia hizo zinatumika kuwatesa wakimbizi wa Burundi, ili kuwalazimisha kurejea nchini kwao. Japo mimi sio mtu wa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, kuthibitisha au kukanusha tuhuma hizi, lakini. kwa vile ni mwandishi wa habari, niliyehudumu kwenye sekta ya habari kwa takriban miongo mitatu, hivyo ninakuwa na uwezo uitwa "insight", wa kubaini kitu cha uongo kwa kisikia au kukisoma. Hiyo insight ni uwezo unaotokana na long experiance ya uzoefu wa muda mrefu kwenye jambo fulani, hivyo mtu akisema jambo fulani la uongo, huhitaji a rocket science kumbaini anasema uongo, au ukisoma andiko la uongo, huchukui hata dakika mbili kubaini bandiko hilo ni la uongo!. Swali la kujiuliza ni hawa Jarida la The Economist, wanapata faida gani kutunga uongo wa mambo mabaya kuihusu Tanzania?, lakini pia, kwa kwanini sisi Tanzania, tunazushiwa uongo na tunanyamazia tuu uongo huu, bila kuukanusha?, au kwenye mamlaka zetu, kutokana na mauonga haya kuvurumishwa kwa ngeli, kwenye majarida na vyombo vya habari vya kimataifa, hivyo hatuna watu wenye ngeli na uwezo wa kukanusha maungo hayo kwa ngeli hizo hizo?. Sisi uwezo wetu ni kukanusha tuu maungo kwenye hivi vipeperushi vyetu vya kufungia maandazi na samaki?.

Naomba nikupeleke kwenye makala yenyenyewe nzima nzima kisha nikuchambulie, upi ni mchele, na zipi ni pumba!.

No haven​

Tanzania’s police are torturing refugees from Burundi​

People fleeing repression at home also face it in refugee camps
Middle East & Africa Dec 3rd 2020 editio
20201205_MAP001 (1).jpg

Dec 3rd 2020
GOMA
Even after Tanzanian policemen had hung him from the ceiling and beaten him with sticks, Crispin (not his real name) would not confess to being a rebel leader with plans to overthrow the government of neighbouring Burundi. It was only when they injected a liquid into his testicles that he caved in and said he was plotting a coup.
He was not. Some years ago Crispin was photographed at an anti-government protest in Burundi. Thugs from the ruling party’s youth wing, the Imbonerakure (“those who see far”), painted a red cross on his door and turned up one night to threaten him. So in 2016 he fled to a refugee camp in western Tanzania. But men from the Imbonerakure also stalk the camps with lists of dissidents provided by Burundian intelligence. They target them, allegedly with help from Tanzanian police. Desperate families often pay the Imbonerakure to have their relatives freed. The spoils are shared with local cops. Most of those picked up are accused of hoarding weapons or plotting against Burundi’s government.

In December last year men from the Imbonerakure turned up at Crispin’s shelter flanked by Tanzanian policemen. They bundled him into a police car and took him to a cell where he spent three months. He was released only because his wife paid 1m Tanzanian shillings ($430) to the Imbonerakure. “They said if she paid I would not be killed or returned to Burundi” to face imprisonment, he says.
Others were not able to buy their way out. Human Rights Watch (hrw), a New York-based watchdog, interviewed 18 refugees who had been arrested in camps by Tanzanian policemen in the past year. Several had been tortured. Eight of them were forcibly returned to Burundi, where they have been locked up without charge. Another rights group, cbdh/vicar, based in Rwanda, says that about 170 Burundian refugees have disappeared from Tanzania since 2015. “There seems to be collusion between the Tanzanian and Burundian authorities,” says Mausi Segun of hrw. “Several of those tortured were told that Tanzanian officials had information on them from Burundi.”
About 300,000 Burundians have fled their country since 2015 after violence broke out when the then president, Pierre Nkurunziza, said he would stand for an unconstitutional third term. Hundreds were killed. Activists, journalists and anyone who might have been spotted at a protest rushed to neighbouring countries. Around half of them went to Tanzania.
A new president, Evariste Ndayishimiye, was elected in June in a rigged poll. His government is just as scary. Gervais Ndirakobuca, the new security minister, is nicknamed “Ndakugarika”, meaning “I will kill you” in Kirundi, the local language. He earned his reputation as a rebel commander during the civil war and has worked hard to maintain it since. As police commissioner under the former president, who has since died, he was responsible for some of the bloodiecrackdowns on protesters. Because of this the eu and America have imposed sanctions on him.

With such people in the government, few refugees seem likely to believe its assurance that the country is safe and that they should return. Officials in Tanzania and Burundi drew up a secret agreement that was leaked last year. It said all refugees should “return to their country of origin whether voluntarily or not”. Some 50,000 have gone back in the past two years. Many cite insecurity in the camps, in particular arbitrary arrests, as their reason for returning. Moreover, camp authorities have threatened Burundians, saying that if they do not sign up to go home they will lose their refugee status and risk arrest. Some of those returning say that they were threatened or detained when they crossed the border. Many have fled again, but this time into safer Uganda.
Crispin has no choice but to stay in Tanzania. He has been warned by the Imbonerakure that if he tries to leave for another neighbouring country, he will be stopped at the border and sent back to Burundi. “It is terrifying to live in a country where you can be arrested at any time. I am constantly frightened,” he said. “But there is nowhere for me to go.” ■
This article appeared in the Middle East & Africa section of the print edition under the headline "No haven"

Kwa vile hii story iko kwenye ngeli, na najua jinsi mambo ya ngeli yanavyotusumbua sisi Watanzania tulio wengi, na hadi viongozi wetu, naomba kuizungumzia kwa kifupi hii story yenyewe
Mkimbizi wa Burundi aitwea Crispin kwa jina la bandia, analituhumu jeshi letu la polisi kwa kumfunga kwa kamba na kumninginiza kwenye kennch za dari kama nyama buchani, na kumchapa sana kwa fimbo kumlazimisha kuwa yeye ni kiongozi wa waasi wa Burundi wenye mpango wa kupindua serikali ya Burundi. Hata baada ya kupigwa sana, hakukiri, lakini alipodungwa sinda ya majimaji fulani kwenye sehemu zake, kufuatia maumivu aliyopata, akakiri uongo ili asife kwa mateso.

Kabla ya kukimbilia Tanzania na kuomba ukimbizi, akiwa nchini Burundi, alionekana kwenye pichaakiongoza maandamano ya waasi kuipinga serikali ya Burundi, askari wa umoja wa vijana wa chama tawala Burundi, wajulikanao kama Imbonerakure waliuchora mlango wa nyumba yake alama ya msalaba kwa rangi nyekundu, na usiku mmoja wakamuibukia na kumtishia, hivyo mwaka 2016 akatorea Tanzania kuomba ukimbizi.

Anasema akiwa kambini, siku moja hao jamaa the Imbonerakure also kwa kusindikizwa na polisi wa Tanzania, wakamuibukia kambini wakiwa na list ya waasi wanaosakwa kurudishwa Burundi kwenda kujibu mashitaka ya uhaini. Hivyo akashikwa na kuwekwa mahabusu kwa muda wa miezi 3 bila kufikishwa mahakamani, huku polisi wakimtishia mkewe, bila kutoa milioni moja, mumewe atarudishwa Burundi kwenda kuuwawa, hivyo mkewe akahangaika kuitafuta, akawapa polisi, ndipo akaachiwa. Hizo fedha polisi wa Tanzania, wanagawana na hao jamaa the Imbonerakure

Taasisi ya Human Rights Watch ya Marekani iliwahoji wakimbizi 18 walioshikwa Tanzania, wakatiwa mahabusu, wakateswa kwa torture na kurudishwa kwa nguvu Burundi. Kikundi cha kutetea haki cbdh/vicar, based in Rwanda, kimedai tangu mwaka 2015,wakimbizi 170 wa Burundian waliokuwa Tanzania, wamepotea, Kupotea huko kumehusishwa na polisi kushirikiana na hao, mbonerakure.

Jarida linadai Tanzania na Burundi, zimeingia makubaliano ya siri, ya kuwarejesha wakimbizi wa Burundi kwa lazima, watake wasitake. Wakimbizi 50,000 wamerudishwa. Taarifa zinasema wakimbizi hao, wanalazimishwa kusaini hati ya kurejea kwao, na wanaogoma, wanatishiwa kuwa hadhi yao ya ukimbizi itafutwa hivyo kuhesabika ni wahamiaji haramu. Wengi wa wakimbizi hao wanadai Tanzania sasa sio salama kwa Wakimbizi, hivyo sasa wanakimbilia Uganda.

Huyu mkimbizi Crispin, anayedaiwa kuteswa na mkrwe kutoa milioni moja ili aachiwe, amesema ataendelea kuishi Tanzania kwasababu hana pengine pa kwenda
Uchambuzi wangu wa taarifa hii ni kama ufuatavyo
 1. Msingi wa uchambuzi wangu ni kutumia kitu kinaitwa logical progression kwa kufuata formula ya tenga la samaki, samaki mmoja akioza, wote wameoza!. Ukivua samaki asubuhi, ukawaweka kwenye tenga, ukavua wengine mchana, ukawaweka kwenye tenga lilelile, kisha ukavua wengine jioni, nao ukawaweka tenga hilo hilo, ulipofika sokoni, ile unatoa samaki mmoja, ukamuona ameanza kuoza, usijifariji kuwa huyo samaki aliyeoza ni kati ya wale samaki waliovuliwa asubuhi, hivyo akaanza kuwapekua na kuwatafuta wale waliovuliwa jioni kwa kudhani, watakuwa bado ni fresh!, huo ni kujisumbua bure, kwenye tenga la samaki, samaki mmoja akioza, wote wameoza!.
 2. Kanuni hiyo ndio nimeitumia kwenye hii story, hata kama ni kweli, kuna baadhi ya mambo mabaya haya yametokea, kama kwenye kuripoti, meripoti mambo ya ukweli, asilimia 99%, na ili kuikoleza story yako, ukaweka jambo moja tuu la uongo, ule uongo mmoja, unabatilisha kweli zote 99, na kuonekana yote ni uongo mtupu, kama yule samaki mmoja, anavyoozesha, samaki wote kwenye tenga la samaki.
 3. Ili habari yoyote iwe ni habari kamilifu na timilifu, inapaswa kuwa na sifa kuu 4.
  1. Truthfulness
  2. Objectivity
  3. Impartiality
  4. Balancing
 4. Uongo wa Kwanza: Habari hiyo haina Truthfulness, ukweli, hivyo ni habari ya uongo!. Truthfulness ndio kanuni kuu ya uandishi wa habari, duniani kote, "tell nothing but the truth", yaani kusema kweli daima, na kuandika ukweli mtupu. Katika kuripoti habari yoyote, ili pia habari hiyo iweze kuaminika, ni kuripoti with pictures, visuals, or actualities ili msomaji aone, kuona ni kuamini, hivyo kwenye reporting, ukifanikiwa kupiga picha, video, au kufanya mahojiano, halafu ukaweka picha, video na interviews, msomaji au mtazamaji, akiona hizo picha au video, ataamini zaidi, kuliko maandishi pekee. Ili kujenga picha mbaya ya Tanzania kwa wasomaji wao, na kuuhadaa ulimwengu kuhusu Tanzania, habari hiyo imeandamana na picha ya kutishia amani ya vurugu na kuchomwa matairi barabarani,
  20201205_MAP001.jpg
  japo picha hiyo ni picha ya tukio la kweli, lakini sio Tanzania!, wameiweka bila kuandika maelezo yoyote ya hiyo picha ili wasomaji waone ni Tanzania!. Hivyo uongo huu mmoja tuu, wa kutumia picha ya uongo, kutoka nchi zenye vurugu, na kuiripoti as if ni Tanzania, inatosha kubatilisha story yote nzima nzima, hata kama yote yaliyosemwa ni kweli yalitokea!, kuutumia uongo kuhalalisha kitu cha kweli, kunachachua ukweli wote na kuonekana wote ni uongo!.
 5. Uandishi unaongozwa na misingi, taratibu na kanuni, uki publish picha yoyote kwenye gazeti lolote, lazima kwanza utoe kitu kinaitwa Photo credit, ya ni nani aliyepiga hiyo, imepigwa lini, imepigwa wapi na kutoa maelezo ni kwenye tukio gani!. Sasa kwa vile story ni negative kuhusu Tanzania, wakatafuta picha mbaya kutoka huko walikotafuta, wakaipachika kwa kutoa tuu photo credits kuwa ni picha ya Reuters, lakini bila maelezo yoyote, kusema hapo ni wapi, lini au ni tukio gani, ili msomaji akisoma tuu, aone ni Tanzania!, kitu ambacho sio kweli, hiyo picha sio Tanzania!. Unaweza kuni challenge, kwa hoja kuwa maadam mimi sio ripota wa hiyo story, nimejuaje hapo sio Tanzania?, hapo sasa ndipo matumizi ya ile logical progression yanapokuja. Watanzania ni watu pisi sana!, ukiangalia huo wingi wa hayo mawe barabarani, na ukumbwa wa mawe yenyewe, na wingi wa matairi yaliyochomwa, huo ni uthibitisho, hiyo picha ni ya kutoka nchi za watu wenye vurugu. Watanzania hatuko hivyo!. Wametumia picha ya vurugu, kuchafua tuu image ya taifa letu!. Watalii ni very sensitive people, unapozungumzia Tanzania na kuweka picha kama hiyo, bila kusema hapo ni wapi na ni lini, amini usiamini, hata kama ulipanga uje Tanzania, ukishaona tuu kitu kama hicho, unaghairi, huji!.
 6. Ili mwandishi kuandika habari yoyote, kitu cha kwanza ni unapata kitu kinachoitwa "news tip", hii ni kutoka kwa mtu anayekutonya habari fulani, kwa sisi waandishi experienced, unajikuta una "nose for news" yaani pua yako ina uwezo mkubwa wa kunusa habari, baada ya tip, unatafuta news lead, uanzie wapi. Yule mtoa habari wako anaitwa "source", katika kuandika habari yoyote yenye tuhuma nzito, kwanza inamtaka mwandishi kujiridhisha na ukweli wa huyo source wake. Ukiisha kamilisha kumhoji, unatakiwa kabla hujaichapisha hiyo habari, usitegemee just a single source, lazima ufanye verification, kuzithibitisha hizo tuhuma, kwa kufanya double checking na cross checking. Hii habari ya The Economist, imemtumia source mmoja tuu mwanzo mwisho!, hivyo kama source ni muongo, anakuingiza chaka, it's very unprofession kutumia just a single source kwa tuhuma nzito kama hii, hivyo habari hii imeegemea upande mmoja, sio impartial, haina impartiality!.
 7. Baada ya kuipata habari na mwandishi kuandika, anafanya kitu kinachoitwa, objectivity consideration, kwa mwandishi unajiuliza hii habari ina malengo gani?, msomaji akisoma atapata picha gani, kwa vile hili jarida, kila siku linaripoti taarifa negative tuu kuhusu Tanzania, na hili niliwahi kulizungumzia, https://www.jamiiforums.com/threads...-hakuna-mazuri-yotote-ya-kuyaangazia.1471986/ , hivyo mwandishi ameripoti with malice aforethought kwa kutafuta negative stories tuu kuhusu Tanzania, hivyo habari hiyo kukosa objectivity.
 8. Ukipata habari yoyote ya tuhuma za upande mmoja, maadili yanatufundisha usiripoti one sided story, lazima uutafute upande wa pili na kuusikia ili kuibalance story yako. Na kwa vile hii tuhuma, inahusu mambo nyeti ya kuhusisha vyombo vya usalama, then mwandishi alipaswa kuibalance story yake kwa kupata the authoritative source, wa kwanza ni mtu wa UNHCR kuthibitisha hizo tuhuma, wa pili ni RPC wa eneo husika kuthibitisha, hilo tukio limetokea. Hili halikufanyika, hivyo hiyo sio balanced story, imekosa balance, hivyo ku justify ile hoja ya malice aforethought.

Paskali
 
sincerely

JF-Expert Member
Nov 5, 2020
297
1,000
Kama wanadanganya wewe inakuuma nini, maana siku zote ukweli hujitenga, unaweweseka nini bruh, the world already knows what you people have done to those innocent immigrants

Mashirika ya haki za binadamu yamefanya investigations yamekuja na ripoti za kuaminika nyie mnakuja na propaganda

Pascal wewe unabehave as if hukwenda shule kabisaaaa

Stand on the truth at list once hata kama unaabundu chaiperson
 
Don Nzoko

JF-Expert Member
Jan 6, 2020
226
250
una hakika gani Kama ni uongo,wanasema no research no right to speak ukiwa Kama mwandishi(ingawa sasa siyo) ungeweza kuchimbia ukaja na uhalisia bt snc sasa hv umekuwa maana halisi ya jina lako(njaa) unasaka uteuzi unaona Kama mauongo,wao walianza kuhusu habari ya msumbiji serikali ilijfanya kufunika yalipokuwa hadharani je?punguza njaa Paschal Kama teuzi ipo itakuja tu na si kwa speed hii au unataka nafasi ya dr.Abbas kabisa?
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,135
2,000
Wacha wee!!!

Sasa mbona hujatuonesha huo ukweli au kutueleza huo ukweli?!

Kwa haraka haraka tu hapo nimeona wakielezea brutality ya polisi wa Tanzania kwa Wakimbizi wa Burundi!!

Wakati the Economist wakieleza hayo ya Wakimbizi, wenye macho yao wanafahamu jinsi polisi wa Tanzania walivyo brutal hata kwa Watanzania wenyewe!!!

Sasa ikiwa wanakuwa too brutal hata kwa Watanzania wenzao, kitawazuia nini kuwa too brutal kwa wakimbizi?!

Aidha nimeona hapo The Economist wakisema suala la Polisi wa Tanzania kumchomoa 1M mtuhumiwa Mkimbizi ili atolewe!!

Wakati the Economist wakizungumzia ukwapuaji huo dhidi ya Wakimbizi, kila mwenye macho na masikio anajua hayo ndo maisha halisi ya Watanzania dhidi ya polisi wanaolipwa kwa kodi zao!! Kila mwenye kichwa kilicho hai anafahamu jinsi polisi wanavyobambikia watu kesi, na ukishatoa mkwanja tu, unaachiliwa... KUINGIA BURE KUTOKA KITU KIDOGO ni msemo unaofahamika vema!!!

Sasa ikiwa hao polisi wanafanya huo ukwapuaji hata kwa Watanzania wenzao wanaowalipa mishahara kupitia kodi zao, watashindwa nini kufanya hayo dhidi ya Wakimbizi?!

Unaweza kufafanunua uongo wenyewe ni upi hasa?! Is it some kind of joke au kabisa unaamini watu watakuwa wanasema uongo kuhusu torturing inayofanywa na polisi wetu?!
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
19,716
2,000
Hawa wakimbizi wanatokea maeneo ambayo waTz hulalamika kuibiwa mifugo na at times kushambuliwa na hao wakimbizi. Recent example ni wavuvi waTanzani kule Ziwa Victoria kushambuliwa na wakimbizi. Sikumbuki sahihi ila nafikiri kuna kifo kilitokea.

Pia kwavile wanatokea maeneo yenye vita siyo ajabu kukuta wengine wanaingia Tz wakiwa na silaha.

Ninachosema ni kwamba yawezekana askari wetu wanawatesa hao watu ila ni katika kukabiliana na hayo niliyoyasema. Tz hatuna askari wa kutosha wala wenye ujuzi wa kuhoji bila adhabu wengi hutaka kumalizana na mshukiwa na kuhamia kesi nyingine.

So kwa maoni yangu tuwekeze nguvu hapo kwenye training na new recruitments.
 
Mr Tyang

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
1,235
2,000
Nasema hivi yeyote atakaejaribu kuitikisa Tanzania hakika atatikisika kwa maana Mungu ameitua Tanzania kuwa taifa teule kwa zama hizi na ndo Maana kaiepusha na balaa la Dunia lijulikanalo Kama Corona na bado anaendelea kuikinga zidi ya maadui na wanafiki wote waliopo nje na ndani ya Tanzania na ndo maana hata kila walipangalo halitimii Wala halitatimia.

Waliombea Mizoga itapakae Tanzania, haikutapakaa.
Waliombea uchaguzi uvurugike, haukuvurugika.
Waliombea Amani ipotee baada ya Uchaguzi, haukupotea.
Waliombea tuwekewe vikwazo vya kiuchumi hatukuwekewa.
Sasahivi wamehamia kwenye kutuchonganisha na warundi lakina hawatafanikiwa..

Narudia Tena Tanzania ndo Taifa teule kwasasa duniani kote.

I love my country
 
Sizinga

JF-Expert Member
Oct 30, 2007
8,563
2,000
Pascal Mayalla huu ni uchochezi, hii ripoti ungeiacha hukohuko wala hata mi nisingeiona, kwa kuileta hapa jukwaani unafanya uchochezi maana watanzania wengi wanapita huku, ungekanusha kwenye forums zao hukohuko
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
3,521
2,000
Hii habari kuna mahala tena nimeiona, na wewe Mayalla inawezekana hizi news ukawa unazileta hapa sio kwa lengo la kukemea kama unavyojinadi, ila zaidi wengi wajue ukatili wanaofanyiwa hao wakimbizi.

Jinsi polisi wetu walivyo na njaa siwezi kubisha kama wanataka pesa toka kwa hao wakimbizi wa Burundi, na kubambia watu kesi ndio tabia yao kila mtu anawajua.

Sasa mjiulize kwanini kila siku mpigiwe kelele nyie tu?!
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
11,840
2,000

No haven​

Tanzania’s police are torturing refugees from Burundi​

People fleeing repression at home also face it in refugee camps
Middle East & AfricaDec 3rd 2020 edition

Dec 3rd 2020
GOMA
Even after Tanzanian policemen had hung him from the ceiling and beaten him with sticks, Crispin (not his real name) would not confess to being a rebel leader with plans to overthrow the government of neighbouring Burundi. It was only when they injected a liquid into his testicles that he caved in and said he was plotting a coup.
He was not. Some years ago Crispin was photographed at an anti-government protest in Burundi. Thugs from the ruling party’s youth wing, the Imbonerakure (“those who see far”), painted a red cross on his door and turned up one night to threaten him. So in 2016 he fled to a refugee camp in western Tanzania. But men from the Imbonerakure also stalk the camps with lists of dissidents provided by Burundian intelligence. They target them, allegedly with help from Tanzanian police. Desperate families often pay the Imbonerakure to have their relatives freed. The spoils are shared with local cops. Most of those picked up are accused of hoarding weapons or plotting against Burundi’s government.

In December last year men from the Imbonerakure turned up at Crispin’s shelter flanked by Tanzanian policemen. They bundled him into a police car and took him to a cell where he spent three months. He was released only because his wife paid 1m Tanzanian shillings ($430) to the Imbonerakure. “They said if she paid I would not be killed or returned to Burundi” to face imprisonment, he says.
Others were not able to buy their way out. Human Rights Watch (hrw), a New York-based watchdog, interviewed 18 refugees who had been arrested in camps by Tanzanian policemen in the past year. Several had been tortured. Eight of them were forcibly returned to Burundi, where they have been locked up without charge. Another rights group, cbdh/vicar, based in Rwanda, says that about 170 Burundian refugees have disappeared from Tanzania since 2015. “There seems to be collusion between the Tanzanian and Burundian authorities,” says Mausi Segun of hrw. “Several of those tortured were told that Tanzanian officials had information on them from Burundi.”
About 300,000 Burundians have fled their country since 2015 after violence broke out when the then president, Pierre Nkurunziza, said he would stand for an unconstitutional third term. Hundreds were killed. Activists, journalists and anyone who might have been spotted at a protest rushed to neighbouring countries. Around half of them went to Tanzania.
A new president, Evariste Ndayishimiye, was elected in June in a rigged poll. His government is just as scary. Gervais Ndirakobuca, the new security minister, is nicknamed “Ndakugarika”, meaning “I will kill you” in Kirundi, the local language. He earned his reputation as a rebel commander during the civil war and has worked hard to maintain it since. As police commissioner under the former president, who has since died, he was responsible for some of the bloodiecrackdowns on protesters. Because of this the eu and America have imposed sanctions on him.

With such people in the government, few refugees seem likely to believe its assurance that the country is safe and that they should return. Officials in Tanzania and Burundi drew up a secret agreement that was leaked last year. It said all refugees should “return to their country of origin whether voluntarily or not”. Some 50,000 have gone back in the past two years. Many cite insecurity in the camps, in particular arbitrary arrests, as their reason for returning. Moreover, camp authorities have threatened Burundians, saying that if they do not sign up to go home they will lose their refugee status and risk arrest. Some of those returning say that they were threatened or detained when they crossed the border. Many have fled again, but this time into safer Uganda.
Crispin has no choice but to stay in Tanzania. He has been warned by the Imbonerakure that if he tries to leave for another neighbouring country, he will be stopped at the border and sent back to Burundi. “It is terrifying to live in a country where you can be arrested at any time. I am constantly frightened,” he said. “But there is nowhere for me to go.” ■

This article appeared in the Middle East & Africa section of the print edition under the headline "No haven"
Wewe ni mkimbizi ili tukuamini?
Wewe ni mtumishi wa UNHCR ili tukuamini?
Wewe ni Police uliyeko kambi ya wakimbizi ili tukuamini?
Wewe ni afisa uhamiaji uliyeko kambini ili tukuamini?
Wewe uko kambini Mtendeli ili tukuamini?
Kama si mmojwapo wa hao unakanusha nini? Unatishirikisha tutetee tusichokijua na wewe ukiwa huna uhakika ila kwa vile umezoea kutetea uovu basi tuungane na wewe?
Waliosemwa ni Polisi wa Tanzania na tunawajua walivyo, kama wanawatendea unyama watanzania wenzao wasio na hatia itakuwaje kwa wageni wasio ndugu zao?
Baki ukitetea uovu kwa kisingizio cha uzalendo feki.
 
mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
1,154
2,000
Mahabusu wangapi wamezieleza mahakama za Tanzania jinsi walivyo teswa na mamlaka ili wakili makosa yasiyo yao??

Sasa kama watanzania wanaolindwa na katiba wanafanyiwa hivyo unadhani hao wakimbizi watakua na hali gani?

Au unajitoa ufahamu ili ipate cheo?
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
1,872
2,000
Wanabodi,
Kila mara nasisitiza humu, uongo ukisemwa sana, na kuachwa kujirudia rudia bila kukanushwa, mwishowe uongo huo hugeuka ukweli. Na uongo ambao ni uongo mtupu, ukisemwa kuwa kitu fulani kitatokea, tusipo kanusha uongo huo, halafu hicho kitu kikaja kutokea kweli, then, kufuatia kuanuni ya matokeo, ule uongo utahesabika ndio ukweli, kwa sababu umetokea kweli. Hii ni kufuatia baadhi ya kauli, zinauwezo wa kuumba.

Mfano kuna huu uongo wa jarida hili kuhusu hili jambo la kuihusu Tanzania, ambao ulisemwa mwaka 2019. na kudaiwa kuwa litatokea Tanzania kwenye uchaguzi wa mwaka 2020. Hatukukanusha, tukanyama na kuwapuuza kwa hoja za uzushi huo ni upepo tuu na utapita.

Lakini kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020, hilo jambo, hawa The Economist walilolizusha, likatokea kweli!, matokeo yake, sasa itaonekana kuwa kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ni kweli kilipangwa kabla, na The Economist walikisema, wakati kiukweli, kile The Economist walichokisema, ilikuwa ni uongo na uzushi, lakini kwa vile, hatukukanusha uongo huo na uzushi huo, kisha ukaja kutokea kiukweli kabisa, dunia italiamini jarida la Economist kuwa walisema kweli, hata kama matokeo ya uchaguzi mkuu huu, ni Watanzania wenyewe, kwa ridhaa yao, wamewakataa wapinzani, na kuichagua CCM kwa mapenzi yao, katika uchaguzi huru na wa haki, licha ya dosari ndogo ndogo, no one will belive its peoples will! ya Watanzania!, watauamini uongo ule kuwa kilichotokea kilipangwa, kikasemwa kimepangwa, kikatekelezwa na ndicho kilichotokea!.

Kwenye toleo la la wiki hii, Jarida la The Economist limeendeleza mauongo yao kuihusu Tanzania, waidanganya dunia kuwa Tanzania, inaendelea kufanya mahojiano kwa kutumia njia haramu za mateso makubwa ya Torture, na njia hizo zinatumika kuwatesa wakimbizi wa Burundi, ili kuwalazimisha kurejea nchini kwao. Japo mimi sio mtu wa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, kuthibitisha au kukanusha tuhuma hizi, lakini. kwa vile ni mwandishi wa habari, niliyehudumu kwenye sekta ya habari kwa takriban miongo mitatu, hivyo ninakuwa na uwezo uitwa "insight", wa kubaini kitu cha uongo kwa kisikia au kukisoma. Hiyo insight ni uwezo unaotokana na long experiance ya uzoefu wa muda mrefu kwenye jambo fulani, hivyo mtu akisema jambo fulani la uongo, huhitaji a rocket science kumbaini anasema uongo, au ukisoma andiko la uongo, huchukui hata dakika mbili kubaini bandiko hilo ni la uongo!. Swali la kujiuliza ni hawa Jarida la The Economist, wanapata faida gani kutunga uongo wa mambo mabaya kuihusu Tanzania?, lakini pia, kwa kwanini sisi Tanzania, tunazushiwa uongo na tunanyamazia tuu uongo huu, bila kuukanusha?, au kwenye mamlaka zetu, kutokana na mauonga haya kuvurumishwa kwa ngeli, kwenye majarida na vyombo vya habari vya kimataifa, hivyo hatuna watu wenye ngeli na uwezo wa kukanusha maungo hayo kwa ngeli hizo hizo?. Sisi uwezo wetu ni kukanusha tuu maungo kwenye hivi vipeperushi vyetu vya kufungia maandazi na samaki?.

Naomba nikupeleke kwenye makala yenyenyewe nzima nzima kisha nikuchambulie, upi ni mchele, na zipi ni pumba!.

No haven​

Tanzania’s police are torturing refugees from Burundi​

People fleeing repression at home also face it in refugee camps
Middle East & Africa Dec 3rd 2020 editionDec 3rd 2020
GOMA
Even after Tanzanian policemen had hung him from the ceiling and beaten him with sticks, Crispin (not his real name) would not confess to being a rebel leader with plans to overthrow the government of neighbouring Burundi. It was only when they injected a liquid into his testicles that he caved in and said he was plotting a coup.
He was not. Some years ago Crispin was photographed at an anti-government protest in Burundi. Thugs from the ruling party’s youth wing, the Imbonerakure (“those who see far”), painted a red cross on his door and turned up one night to threaten him. So in 2016 he fled to a refugee camp in western Tanzania. But men from the Imbonerakure also stalk the camps with lists of dissidents provided by Burundian intelligence. They target them, allegedly with help from Tanzanian police. Desperate families often pay the Imbonerakure to have their relatives freed. The spoils are shared with local cops. Most of those picked up are accused of hoarding weapons or plotting against Burundi’s government.

In December last year men from the Imbonerakure turned up at Crispin’s shelter flanked by Tanzanian policemen. They bundled him into a police car and took him to a cell where he spent three months. He was released only because his wife paid 1m Tanzanian shillings ($430) to the Imbonerakure. “They said if she paid I would not be killed or returned to Burundi” to face imprisonment, he says.
Others were not able to buy their way out. Human Rights Watch (hrw), a New York-based watchdog, interviewed 18 refugees who had been arrested in camps by Tanzanian policemen in the past year. Several had been tortured. Eight of them were forcibly returned to Burundi, where they have been locked up without charge. Another rights group, cbdh/vicar, based in Rwanda, says that about 170 Burundian refugees have disappeared from Tanzania since 2015. “There seems to be collusion between the Tanzanian and Burundian authorities,” says Mausi Segun of hrw. “Several of those tortured were told that Tanzanian officials had information on them from Burundi.”
About 300,000 Burundians have fled their country since 2015 after violence broke out when the then president, Pierre Nkurunziza, said he would stand for an unconstitutional third term. Hundreds were killed. Activists, journalists and anyone who might have been spotted at a protest rushed to neighbouring countries. Around half of them went to Tanzania.
A new president, Evariste Ndayishimiye, was elected in June in a rigged poll. His government is just as scary. Gervais Ndirakobuca, the new security minister, is nicknamed “Ndakugarika”, meaning “I will kill you” in Kirundi, the local language. He earned his reputation as a rebel commander during the civil war and has worked hard to maintain it since. As police commissioner under the former president, who has since died, he was responsible for some of the bloodiecrackdowns on protesters. Because of this the eu and America have imposed sanctions on him.

With such people in the government, few refugees seem likely to believe its assurance that the country is safe and that they should return. Officials in Tanzania and Burundi drew up a secret agreement that was leaked last year. It said all refugees should “return to their country of origin whether voluntarily or not”. Some 50,000 have gone back in the past two years. Many cite insecurity in the camps, in particular arbitrary arrests, as their reason for returning. Moreover, camp authorities have threatened Burundians, saying that if they do not sign up to go home they will lose their refugee status and risk arrest. Some of those returning say that they were threatened or detained when they crossed the border. Many have fled again, but this time into safer Uganda.
Crispin has no choice but to stay in Tanzania. He has been warned by the Imbonerakure that if he tries to leave for another neighbouring country, he will be stopped at the border and sent back to Burundi. “It is terrifying to live in a country where you can be arrested at any time. I am constantly frightened,” he said. “But there is nowhere for me to go.” ■
This article appeared in the Middle East & Africa section of the print edition under the headline "No haven"

Stay Tuned, Uchambuzi wangu unafuata.

Paskali
We don't need all these stories what we want 'A county of reconciliation,we are Tanzanians with our political difference, and race still we are one people.'', But CCM took WAPINZNIA as enemies.
Tunataka haki usawa na upendo kwa wote'' sio nchi ya kubagua wapinzani kisha utarajie tusizushiwe mauongo. Hivi unatarajia nini pale unapomuhasimu Ndugu yako? halafu akasikia una semwa vibaya ,unadhani atakuteteaje?

Tuweni wakweli
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
3,945
2,000
Pascal Mayalla huu ni uchochezi, hii ripoti ungeiacha hukohuko wala hata mi nisingeiona, kwa kuileta hapa jukwaani unafanya uchochezi maana watanzania wengi wanapita huku, ungekanusha kwenye forums zao hukohuko
Hapa ndipo penye watu wenye KUFIKIRI....

Paschal Mayalla kuyaongelea hapa na kukanusha UPOTOSHWAJI unaofanywa na hao WAZUSHI ni sawa na ni SAHIHI....

Kwani pumba na mchele siku zote HUTENGWA kwa kuchambuliwa na kupepetwa NYUNGONI...
Hapa ni NYUNGONI...na siku hizi HUWEZI UKAFICHA TAARIFA katika huu ulimwengu wa DIGITAL...
Unataka kusema ya kwamba hilo gazeti liko SAYARI ya MARS kusikofikika KIRAHISI?

Paschal endelea kutuchambulia Kaka....
Wapotoshaji hao na wengineo ni kuwakabili kwa HOJA kama ulizomwaga HAPA.....

Siempre siempre Tanzania.
Hasta la Victoria Tanzania.
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,273
2,000
Kama wanadanganya wewe inakuuma nini, maana siku zote ukweli hujitenga, unaweweseka nini bruh, the world already knows what you people have done to those innocent immigrants

Mashirika ya haki za binadamu yamefanya investigations yamekuja na ripoti za kuaminika nyie mnakuja na propaganda

Pascal wewe unabehave as if hukwenda shule kabisaaaa

Stand on the truth at list once hata kama unaabundu chaiperson
Sidhani kama umeelewa lengo la Pascal Mayalla kuleta andiko hili.

Ni kinyume sana na unavyofikiri wewe.
Hapo anawataka serikali ikomeshe hayo mambo na ikanushe isiache ikichafuka hivi kimataifa.
 
MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,829
2,000
Wacha wee!!!

Sasa mbona hujatuonesha huo ukweli au kutueleza huo ukweli?!

Kwa haraka haraka tu hapo nimeona wakielezea brutality ya polisi wa Tanzania kwa Wakimbizi wa Burundi!!

Wakati the Economist wakieleza hayo ya Wakimbizi, wenye macho yao wanafahamu jinsi polisi wa Tanzania walivyo brutal hata kwa Watanzania wenyewe!!!

Sasa ikiwa wanakuwa too brutal hata kwa Watanzania wenzao, kitawazuia nini kuwa too brutal kwa wakimbizi?!

Aidha nimeona hapo The Economist wakisema suala la Polisi wa Tanzania kumchomoa 1M mtuhumiwa Mkimbizi ili atolewe!!

Wakati the Economist wakizungumzia ukwapuaji huo dhidi ya Wakimbizi, kila mwenye macho na masikio anajua hayo ndo maisha halisi ya Watanzania dhidi ya polisi wanaolipwa kwa kodi zao!! Kila mwenye kichwa kilicho hai anafahamu jinsi polisi wanavyobambikia watu kesi, na ukishatoa mkwanja tu, unaachiliwa... KUINGIA BURE KUTOKA KITU KIDOGO ni msemo unaofahamika vema!!!

Sasa ikiwa hao polisi wanafanya huo ukwapuaji hata kwa Watanzania wenzao wanaowalipa mishahara kupitia kodi zao, watashindwa nini kufanya hayo dhidi ya Wakimbizi?!

Unaweza kufafanunua uongo wenyewe ni upi hasa?! Is it some kind of joke au kabisa unaamini watu watakuwa wanasema uongo kuhusu torturing inayofanywa na polisi wetu?!
Mkuu Chige, kwenye Refugee & Migration Law kuna kitu kinaitwa The Principle of Non-Refoulment, ambacho kinatakaza kwa namna yoyote ile serikali kuwarudisha kwa lazima wakimbizi ndani ya nchi ambayo wanaweza kupata mateso (Persecution) au kuuwawa. Tanzania imevunja sana hii kanuni dhidi ya wakimbizi tangu kipindi cha Mzee Mkapa.

Miaka ya 90 alikuja Raisi wa Burundi akafika hadi kwenye makambi ya wakimbizi na kuwahakikishia kwamba Burundi ni shwari na warudi. Lakini walivyorudi tu wakakutana na mtutu wa bunduki, maelfu na maelfu ya wakimbizi waliuwawa na serikali ya Tanzania ikajifanya haifahamu chochote kile.

Sasa tukija kwenye hilo lako, ni heri polisi kukutana nao ni ngumu: Wale majamaa wa Uhamiaji wamepewa nguvu kubwa ambayo wanaitumia vibaya hasa kufanya vitendo vya rushwa dhidi ya wakimbizi. Kibaya zaidi wanashindwa kufahamu tofauti kati ya Mhamiaji Haramu (Illegal Immigrant) na Mkimbizi (A Refugee/Asylum Seeker), wenyewe wakikukamata wanafanya kitu kinaitwa A Transfer of Burden of Proof ambapo wewe ndiyo unatakiwa ujitetee kwamba ni Mtanzania, Mhamiaji haramu au Mkimbizi na ukishindwa basi inakula kwako.

Sheria ya Uhamiaji imewapa hii nguvu, lakini ukishindwa kufanya hivyo wao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho kukufanya lolote. Nadhani kisheria huu ni mwanya mbaya ambao unajenga mazingira ya matumizi mabaya ya madaraka hasahasa pale ambapo yanatumika kisiasa. Kubwa ni kwamba lazima tuwe na njia mbadala ya haraka ambayo itampa mkimbizi au raia haki ya rufaa endepo atahisi kuonewa na hizi mamlaka.

Tatizo hili limesababishwa na mianya kwenye Mikataba ya Kimataifa na Kikanda inayolinda haki za wakimbizi, ambapo haizibani sana serikali husika. Wao huishia kusema "A Grant of Asylum is strictly a state's prerogative" halafu huku kwingine wanasema "A host state must take all necessary precautions to ensure protection of refugee population residing in its territory". Hapa ndipo matatizo yanaanza, Serikali zinajiamulia kufanya lolote kwasasababu The Grant of Asylum is state's prerogative.

Kuna dada moja Mjerumani nlishawahi kufanya naye kazi, yeye anafanya kwenye shirika la wakimbizi kule kwao Ujerumani. Juzi ameniambia wakimbizi wanaudhi sana hasa hawa jamaa wa kiarabu kutoka Syria, maana ukiwapa moja wao watataka mbili: wanafanya ubakaji, wanataka kuhudumiwa kwa kodi za wajerumani na baadhi wanahusishwa na mitandao ya Ugaidi. Lakini kasema pamoja ya yote haya kuna cha kujifunza kuhusu utu na ubinadamu maana hawa watu hawana pakwenda.

Kiufupi ni kwamba wajerumani (mabeberu + wakristo) wameona ni vyema kukaa na waarabu (waislamu), ambao wametoka kilomita nyingi bara jingine kwenda kuomba hifadhi nchini kwao. Lakini sisi watanganyika tunahisi ni nongwa kuwapokea majirani wenzetu ambao ni weusi kama sisi, tena ambao baadhi yao wana maelfu ya ndugu nchini Tanganyika. Ukiangalia vizuri utatambua kwamba huu ni mkakati urioratibiwa vizuri na vyombo vya ulinzi na usalama, hasa baada ya mkuu wa nchi kusema wazi kabisa kwamba "Tanzania ilishawalea sasa inatosha, mrudi kwenu mkajenge nchi".
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom