Maneno ya Rais Samia ni Maoni si Msahafu, Msingi ni Katiba

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,826
35,827
Mama akiongea jana na wana habari alikumbusha kuwa alikuwa pale kwa maongezi zaidi wala hakupenda iwe hotuba.

Mama alikuwa pale kubadilishana mawazo.

Mama ni mwana diplomasia mahiri. Anajua anachokitaka na anajua kukiwasilisha vyema. Mama anakijua kiswahili sawasawa. Mama anacheza na lugha kama anavyotaka. Ana uwezo mkubwa wa kuyafurahisha makundi yote pasipo na yeye kuvunja sheria wala katiba.

Haupo ushahidi thabiti zaidi kwenye hilo kuliko huu:

IMG_20210610_103030_594.jpg


Matendo huongea zaidi kuliko maneno.

Anaendelea na mazungumzo yake na makundi mbalimbali na hadi sasa hakuna moja lililotokea kuvunjika moyo kwa kukutana naye.

Kundi la jana si la mwisho katika mwendelezo huo, ambapo kila kundi linafahamika kuwa na maslahi yake yaliyo mbele zaidi.

Kundi la jana lilihitaji kusikia upande wa maslahi yake yakiwamo madeni yao yapatayo 6bn/-. Mustakabala wa fursa za matangazo, fursa zingine zikiwamo ruzuku, ushirikishwaji, nk. Kuwa fair mengine yalikuwa yatokanayo tu.

Vilio vya kukosekana kina Pascal Mayalla aka manjaa vinasikika.

Hili si kundi la mwisho kwenye kuonana naye.

Kauli za mama katika mazungumzo haya au popote si msahafu. Yeyote kuendelea kutoa maoni yake kufuatia maoni ya mama ni haki yake ya msingi.

Mtu hahukumiwi kwa maoni yake bali kwa vitendo.

Kama kawaida wasiotutakia mema wamepata fursa zao za kupalilia mitafaruku:


Wanatumia lolote kujaribu kutufarakanisha.

Nia na madhumuni yao bado si haba kuendelea kuwaulizia.

Ninawasilisha.
 
Nisiache kukazia:

Hitajio la uwepo wa katiba mpya, kuheshimiwa kwa haki, uhuru wa watu na utawala wa sheria kutokuwa msingi wa mazungumzo ya jana, kwa upande wa wanahabari dhidi ya hoja nyingi za maslahi binafsi mbele ya rais, ilikuwa ni fursa adhimu sana iliyopotezwa.

Au nasema uongo ndugu zangu wazalendo bila kukusahau mshirika wangu bwana Pascal Mayalla?
 
Back
Top Bottom