Maneno Ya Hekima

Maneno Ya Hekima

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,271
Reaction score
29,934
_*MANENO YA HEKIMA*_


```Kucha zinapokuwa kubwa huwa tunakata kucha, hatukati vidole... Na matatizo yanapokuwa makubwa, jukumu letu ni kukata matatizo, si kukata uhusiano wetu

Ndege hula vijidudu na ndicho chakula chake kikuu, anapokufa vijidudu humla ndege... na hayo ndio maisha, usimdharau kiumbe kwa udhaifu wake, kesho atakushinda kwa nguvu, uaibike.✍

Samaki anayefumba mdomo wake, hashikwi na ndoana ya mvuvi, jitahidi kufumba mdomo wako kwani kuna watu wengi wana hamu ya kukutia ndoana kwa makosa yako.

Kabla ya kumuhukumu mtu, msikilize kwanza, usisikilize ya kuambiwa.

Waweza Ongezea Ndugu yangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom