Maneno ya Baba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno ya Baba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Judgement, Feb 9, 2012.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Nianze kwa kumtakia RIP, kwani hatunae katika uso wa ardhi.
  Si mara moja au mbili, ni mara nyingi Baba yangu nikiwa tumekaa nae zama za uhai wake, alikua akiyarejelea maneno haya :-
  (Nikimnukuu)
  Baba > Mwanangu mimi Baba yako nimekua, na nimekutana na mengi.
  Katika dunia hii mwanangu ukitaka ufanikiwe kimaisha , ishi na watu vizuri.
  Na uweke taswira usoni kwako kua watu ndiyo mtaji wako, na wewe ni mtaji kwa watu wengine.
  Hakikisha usibweteke na mali za ndugu zako na ukazitegemea, nenda juu chini umiliki za kwako.
  Ishi na familia yako kwa mapenzi, lakini usisahau kua mkeo si ndugu yako.
  Na katika dunia hii mwanangu unapokutana na watu (binadamu) ukawasikia mtu anakwambia
  "Mimi sipendi wizi kwelikweli "
  "Mimi sipendi uongo"
  "Mimi sipendi uzinzi"
  Basi mwanangu uwasikiapo watu wakijinadi kwa kauli hizo , waangalie kwa macho mawili , kwani hua wanakua ni kinyume na kauli zao.
  Anaejinadi hapendi uzinzi basi ndiyo mzinzi nambari one !
  Mwanangu wale wenye tabia na mienendo yao mema hua hawajinadi , huvaa silka ya tabia zao kimyakimya na jamii ndiyo huwatambua.
  (mwisho wa kunukuu)
  Binafsi yangu maneno haya ya Baba yote ninayaona ukweli wake.
   
 2. G Mpoleeee

  G Mpoleeee Senior Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera ulie lelewa na baba ako.
   
 3. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mwenzangu umelelewa na nani?
   
 4. G Mpoleeee

  G Mpoleeee Senior Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  mama na baba wa kambo.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  kila rule ina exceptions.
  Ila kama unaona ni kweli kwako basi yashike yatakuongoza vizuri.
   
 6. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Asente Senior wangu ! Kwa nyongeza angalia mf. wa mtu anaekusudia kujiua, mkusudiaji wa kweli hua hajinadi !
  Mtashtukia keshajitundika !
  Na ukimuona anaejinadi kuji'kill hua ni magumashi
   
 7. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kwanza hongera kwa kupata baba aliyekuusia hayo, ni maneno mazuri sana.
  Hapo kijani, pole sana kwa kuondokewa na hazina kama hii, lakini ni kazi ya Muumba.
  Pili, hapo nyekundu, ulimfahamu alichokusudia kusema? Naomba ufafanuzi, tafadhali.
   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye Red nilivyofahamu, alikwishanipa muhtasari in advance namna alivyoishi na kutendwa na mke wake wa kwanza kabla hajamuoa mama yangu.
  Aliniambia kua mke wake wa kwanza alimfanyia mambo mengi ya kimsingi ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba wakweze na kumjengea nyumba mkewe pembeni mbali na waliokua wakiishi, mke aliipangisha. Hati akaindika jina la mkewe.
  Na ile ya wakwe Hati akaiandika jina la Ba-mkwe wake.
  Pamoja na yote hayo mke huyo akaja kumsaliti katika ndoa kwa kuwa na mwanaume nje ya ndoa.
  Na kusababisha ndoa yao kuvunjika.
  Aidha kuna wakati fulani Baba alikua aki'deal na illegal deal (meno ya Tembo) na huyo mke wameshaachana, huyo x-wife alikwenda kumchoma kwa polisi (wa kikoloni miaka hiyo 67")
  Ambapo Baba alikamatwa na baadae kufungwa.
  Ndiyo akawa akiniambia mke mfanyie mengi ya kumfanyia lakini usimwekee siri zako zote bayana (japo si wanawake wote wenye tabia hii ni baadhi)
  Kwa vile mume huwezi jua yupi atakae kusaliti hivyo ishi nae kwa tahadhari.
  Isitoshe x wife huyo wa Baba akaolewa na mgoni wa Baba na wakaishi kwenye nyumba aliyojenga Baba.
  Ndiyo likaja neno mke si nduguyo.
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  RIP baba judgement. Naruhusiwa kupita hapa?
   
 10. Da Pretty

  Da Pretty JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 3,050
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Una bahati Judgement,
  Mwenzenu mi babangu bosi tena dikteta kazini hadi nyumbani.
  Hana story yoyote,anatoa maelekezo tu bila kuruhusu mjadala.
  Hatuna uhuru nae kabisa.
   
 11. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Asante kwa pole, Husn but kwa leo na kwa furaha uliyonayo kwa result unatakiwa upumzike.
  Fanya ulale hii mida sio mizuri, ndiyo mida ya Popobawa kuamka na kuanza kuvinjari jukwaa hadi jukwaa, usije ukakumbana nae usiku huu hafai kabisa ukutanenae.
   
 12. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Pole kwa hilo ! Hata hivyo Da Pretty bado mi nakutamania pamoja na udikteta wake lakini yupo juu ya uso wa ardhi, unamuona.
  Mie wangu pamoja na mazuri yake yu'ndani mwa tumbo la ardhi .
   
 13. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  hakika mkeo si nduguyo...alinena babu yangu..baba jajiment
   
 14. sister

  sister JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  duh pole yake kwa kweli mana ni sad story yenye fundisho.
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Umenifanya nitokwe machozi!Nimemkumbuka mzazi wangu wa pekee aliyenijali sana hapa duniani!I WILL AlWAYS MIS U DADY,RIP!
   
 16. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Eiyer ! Pole my fellow ! Alafu recently nilikua nakutana nawe several tyms hapa mitaa hii (MMU) But currently imekua nadra sana kukutana nawe.
  Ni tunapishana majukwaa ? Au umepunguza kuvinjarivinjari mitaa hii ? Manaake now days there a lot of social networks .
   
 17. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Leonard ! Hakuna mtu wa karibu kwa Mume kama Mke .
  Na kwa Mke ni Mume, each other ni ritehand wa mwenzake.
  But , But, But !
  Pakijatokea ugomvi wa balaa na divorce ikawa establish !
  Na kila mmoja akashika njia yake, viumbe hawa hutokea wakawa maadui kiasi kufika hata mmojawao akisikia ex- mwenza kafa hahudhurii hata mazishi ! Ndiyo kwanza anashukuru.
  Lakini nduguyo hata mgombanaje undugu haufi wala hauna subsitute (instead of )
  Undugu ni kama kabila (tribe) haubadilishiki !.
  Mke anabadilishika !
  Dini
  inabadilishika.
  Mke sio nduguyo.
   
 18. m

  mkazamjomba Member

  #18
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na mume pia si nduguyo jamani
   
 19. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  kuna watu wawili walikutana ukubwani

  mmoja alikuwa mwanamichezo maarufu

  na akasema 'maisha ninayoishi ni baba yangu amenisaidia'
  siku zote alisema nitafanikiwa kuwa mwanamichezo maarufu....

  na mwingine alikuwa jambazi aliekubuhu......na yeye akasema....

  hata mimi baba yangu alikuwa anasema 'wewe mtoto utakuwa jambazi wewe'.......

  be careful na unayoyasema kwa watoto wako
   
 20. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  baba yangu aliniambia siku chache kabla ya ndoa yangu kwamba unapocheka na mkeo hakikisha usicheke mpaka ayaone magego yako
   
Loading...