Maneno haya ya zamani jamani yanikumbusha mbali!

kulumangia
chachacha
utanichoma saa nane
kulumangia
eva gitano
nyerere kabmbe, mwinyi mshua
kaunda suti
nyanya pensi
kiini macho
kukwida
kupiga ngwala
kusalandia
kula kwa macho
pajero pajero linanisumbua
kuzamia meli
kijastibikozi
hapendwi mtu
eva gitano
bagibagi
 
Du mmenikumbusha zamani wazee.
Haya machache mengine.
Danga chee
Demu
Kiduchu
kula mboko
Mwanasesere
Mabobish
Chai maharage
Kipira

Hilo neno Danga chee,lilikuwa linaenda na neno lingine lisemalo "Dukinaa"

Hivi yalikuwa na maana gani vile haya?
 
Jah People ana penda wadada wenye wowowo yaani sijawahiku kumdekishia akiwa na akina betina yeye ni ngongingo kwa kwenda mbele utafikiri katoka ngambo bwana. kuna siku nimemkuta pale hoteli ya Mzalendo amehifadhi Banana zake kwenye mfuko wa Rambo amegiza ubeche yupo na kishtobe aliyepiga losso chini na ukimcheki juu Shem wetu kapiga Chillimen na mkanda wa kipepeo afu juu kanyosha nyele zake na kibanio ananukia Yolanda na anagaa kwa kupiga Rays............. Zamani jamani raha tupu afu watu walikuwa sio wanyimi!!!!!

Mzee Mkanda wa Kipepeo na Marashi ya Yolanda hahahahahah
 
Hilo neno Danga chee,lilikuwa linaenda na neno lingine lisemalo "Dukinaa"

Hivi yalikuwa na maana gani vile haya?

mkuki moyoni-kiatu kilichochongoka kwa mbele, adiosamigo-kuagana, amigo-aina ya unyoaji nywele, bwenzi, chacha-aina ya viatu vya plastiki vilivyo wazi, bizbo, skuna , santana, pekosi, bugaluu, bamping, roboti .
 
Msure, Sakala, Kurudi Kishujaa, Pimbi, Kula kobis, Kurusha Air, Kicheche, Mkavirondo
 
Chakacha...Uchune...Chapa mwendo...Kalumanzira...Lala mbele...Acha KUNICHORA...Hana somo...Madoido...Fidodido!
 
Kuna Ch*pi ilikuwa inaitwa VIP, si unajua wakati ule twacheza Chandimu ukishtuka unaweza kuikuta kifuani afu upo tumbo wazi!
 
sijui kama mie ni mbongo jamani maana ya maneno haya ni nini? siyajui


WanaJF kuna maneno ni dhahiri ukiyakumbuka unaweza kucheka kama si kuhuzunika kwani yatavuta memmories na kukumbuka mengi mmo kwa wakati huo, mi nakumbuka machache ingawa mengine bado yanadumu, tukumbushane basi ingawa najua wakati ule utandawazi haukuwawepo au kama ulikuwepo basi kwa kiduchu sana, Yafuatayo ni baadhi ya hayo maneno au misemo ya enzi za mwalimu:- 1. Nyapu
2. Mnaa
3. Manga
4. Kutupia ndoano
5. Kupiga chabo
wadau tukumbushane mengine!
 
Kuna viatu vile vilikuwa na soli kama njumu, venyewe vikiitwa "gogo" mnavikumbuka? raba tukizzita ndaba, na mktu ukatinga zile mara wanasema 'za kuchumpa'
 
Back
Top Bottom