Maneno haya ni sawa, tofauti au yanakaribiana? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maneno haya ni sawa, tofauti au yanakaribiana?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by F12, Aug 28, 2011.

 1. F12

  F12 Member

  #1
  Aug 28, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa matumizi ya kawaida na ya kila siku ya maneno haya, inawezekana kuna watu huitwa kwa majina haya isivyostahiri. Maneno yenyewe ni kama;

  1. Tahila
  2. zezeta
  3. punguani
  4. hayawani
  5. chizi
  6. kichaa
  7. Mwendawazimu
  8. Chakaramu
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,051
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika kama hayawani=taahira...ngoja tuwasubili wakali kwanza
   
 3. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Swali zuri, lakini ili kupata ulinganifu na majibu mazuri rejea kwenye Kamusi ya Kiswahili ya TUKI.
   
 4. A

  Albimany JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  1)Taahira na sio Tahila. Taahira ni wale watu waliofanana dunia nzia ambao hua ni kama walemavu flani na akili zao hua haziko sawa.

  2)Zezeta ni mtu mlemavu pia lakini muili wake anakua umelegea hauwezi ni kama kuparalaiz fulani hivi.

  3)Punguani ni mtu mpungufu wa akili anakua sawa ila hazimtoshi vizuri anakua tofauti kidogo na mtu wa kawaida.

  4)Hayawani ni neno la kiarabu lenye maana ya mnyama,sasa wasuahili hulitumia pale tunapotaka kumfananisha mtu na mnyama ama kivitendo au kiakili.

  5)Chizi ni mtu ambae anaakili zake ila vitendo vyake anavyofanya ni kama mtu alio na upungufu wa akili.

  6) Kichaa ni Ugonjwa wa akili mbao ni hatari anaepata ugonjwa huu anaweza kujidhuru mwenyewe au anaweza kumdhuru mtu na hata kuuwa.

  7Mwendawazimu ni mtu ambae hukosa akili baadhi ya kipindi na kipindi fulani hutulia akawa mzima.

  8)Chakaramu ni Mtu mkamilifu wa akili ila anakosa busara wakati anapofanya mambo yake na pia anakosa utulivu wa nafsi yake,hujifanyia mambo kwa vile akili yake itakavyo mtuma tu.

  Maneno haya yote yanakaribiana maana zake ila sio sawa,kila neno lina uzito wake na yote haya yanauhusiano na upungufu wa akili.
   
 5. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 60
  <br />
  <br />
  mkuu nakubaliana na wewe koote, ila hapo kwenye neneo zezeta nakataa,,, according to dictionary ya tuki, zezeta imekua tranclated kama a fool, idiot or imbecil,, soo in other words tunaweza kusema zezeta ni mtu mjinga, sio aliyelegea viungo kama usemavyo wewe,
   
 6. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />
  Umenichanganya kabisa yani... Khaa!
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa kujazia hapo Zezeta ni pamoja na ulegevu lakini pia utamuona mdomo wake unalegea mpaka mate yanakuwa yakimtoka muda wote. Mfano wavuta madawa ya kulevya akikosa dawa hizo ndio anakuwa kama Zezeta
   
Loading...