Maneno 'HAPA KAZI TU' yaondolewe kwenye mali za nchi, yanatia aibu na wala hayana maana yoyote

Huu ni ushauri ninaoupeleka kwa wahusika wote pamoja na wenye mali ambao ni wananchi.

Kuwepo kwa maneno haya ya kijinga kwenye ndege zilizonunuliwa kwa hela za wananchi, au unaweka maneno haya kwenye meli zetu ni upuuzi usio na mfano. Haya yanafanywa na makondakta wa daladala za DSM kwa lengo la kujiliwaza kutokana na foleni za mkoa huo.

Kama tunataka kuchorachora ndege zetu au meli zetu basi tuchore maandishi ya maana, kama Timu ya Simba imeweka nembo ya 'VISIT TANZANIA', kwanini msifanye hivyo kwenye mali za Taifa badala ya kutuwekea mavitu yasiyo na maana?

Hivi ukiulizwa na wageni maana ya 'HAPA KAZI TU' utajibu nini? mbona mnatudhalilisha kirahisi namna hii? Tafadhali sana TUHESHIMIANE.
Kwenye kichwa cha habari umesema hayo maneno hayana maana yoyote,ikimaanisha hayana athari yoyote,sasa ni nini shida hadi wewe kutaka yaondolewe?
 
Kweli kabisa, hii slogani ilikuwa inanichefua kabisa na sikuwahi kuona maana ya "hapa kazi tu" mimi nilikuwa kila wakati najua kinachoendelea ni "hapa upigaji tu, hapa udikteta tu, hapa ubaguzi tu, hapa uuaji tu". Tufute kabisa slogani hii ya kishenzi.
 
Huu ni ushauri ninaoupeleka kwa wahusika wote pamoja na wenye mali ambao ni wananchi.

Kuwepo kwa maneno haya ya kijinga kwenye ndege zilizonunuliwa kwa hela za wananchi, au unaweka maneno haya kwenye meli zetu ni upuuzi usio na mfano. Haya yanafanywa na makondakta wa daladala za DSM kwa lengo la kujiliwaza kutokana na foleni za mkoa huo.

Kama tunataka kuchorachora ndege zetu au meli zetu basi tuchore maandishi ya maana, kama Timu ya Simba imeweka nembo ya 'VISIT TANZANIA', kwanini msifanye hivyo kwenye mali za Taifa badala ya kutuwekea mavitu yasiyo na maana?

Hivi ukiulizwa na wageni maana ya 'HAPA KAZI TU' utajibu nini? mbona mnatudhalilisha kirahisi namna hii? Tafadhali sana TUHESHIMIANE.
Hwbu acha maneno unajua hizo ndege zilinunuliwa kwa bei gani na kwa bajeti ipi iliyopitishwa a bunge.
 
Wewe mbona mzito mno kuelewa? Pamoja na uchache wa wanachama mtapata kura zaidi ya milioni moja ambazo nyingi ni kura za huruma. Bahati mbaya hazitawasaidia kushinda
Kivipi za huruma ilihali CCM imeshindwa Kila kitu? Hivi 2025 kwenye kampeni mtawaambia Nini wananchi? Ilihali bei ziko juu, no umeme , no Maji, no ajira, wakulima kilio n.k ni kundi Gani litawapigia kura? Mind you Mama Samia ni mzenji so Hana mtaji wa kura huku bara so bila kula za huruma hakuna mwenye akili timamu ataichagua CCM
 
Nakumbuka Helcopta iliyomuua Deo filikunjombe iliandikwa HAPA KAZI TUU
Magufuli alikuwa hajawa raisi bado
 
Kweli kabisa, hii slogani ilikuwa inanichefua kabisa na sikuwahi kuona maana ya "hapa kazi tu" mimi nilikuwa kila wakati najua kinachoendelea ni "hapa upigaji tu, hapa udikteta tu, hapa ubaguzi tu, hapa uuaji tu". Tufute kabisa slogani hii ya kishenzi.
Ndio maana nasema kunahitajika msaada wa kisaikolojia, sasa wewe huo msemo tu ulikuwa unakuchafua unashindwa kuishi kwa raha kisa msemo ambao unakiri hauna maana yeyote.

Nashukuru sana Mungu kwa kuniepusha haya mnayoyapitia wenzangu, muhimu ni msaada tu wa kisaikolojia.
 
16761965551622085051184554267076.jpg
 
Back
Top Bottom