Mimi nichukue fursa hii kuwapa pole , lakini niwe jasiri sana kusema ukweli kama ninyi waandishi hamtafanya editing ..
Kwanza kabisa niweke wazi kuwa jambo hili limesababishwa na chokochoko za udini ambazo muasisi wake ni serikali ya CCM na viongozi wake, aliyepiga bomu hapa leo sio jambazi wa kutaka mali bali ni mtu aliyeelewa na kufundishwa tofauti kwa nia mbaya kuhusu dini nyingine, haya maneno ya udini yalianzishwa na viongozi wa chama tawala lengo likiwa ni kuwagawa na kuwatawala raia lakini kwa sasa wamelikoroga, wamewachonganisha watu wa dini mbali mbali haswa waislamu na wakristo ambao ndio wengi ktk taifa hili bila kujua madhara ya mkakati huu kuwa utaligawa taifa.
Sasa basi kazi hiyo haya ndio mavuno yake kwani tukio hili lina sura zote za kiimani, na nilitake jeshi la polisi kufanya kazi ya kukamata haraka kama ambavyo walinikamata mimi nyumbani kwangu kwa mabomu na vitisho, poleni sana .
Nimejitahidi kuweka alivyosema lema
Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
CCM walianzisha vipi udini?chokochoko za udini ambazo muasisi wake ni serikali ya CCM
haya maneno ya udini yalianzishwa na viongozi wa chama tawala
CCM walianzisha vipi udini?
Subiri ushhidii kesho Bungeni!CCM walianzisha vipi udini?
Radio Maria baada ya kuona Mh. Lema anaongea pumba walimtoa hewani. Na kwa kuonyesha kwamba hawabahatishi, walimtoa hewani mara mbili.
Mh. Lema akili yake haipo sawa, kuna uwezekano mkubwa alipokuwa mtoto alisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
1. Katika kampeni za uchaguzi mkuu 2005 CUF ilikuwa na nguvu CCM katika majukwaa walijinadi kuwa wananchi wasiichague CUF sababu ni chama cha kidini na mwisho wa siku IGP O.Mahita alionyesha visu kuwa ni vya CUF kwa ajili ya kuleta vurugu siku ya uchaguzi2. katika kampeni za Uchaguzi mkuu 2010 CHADEMA ilikuwa na nguvu CCM katika majukwaa waliwaambia wananchi wasiichague CHADEMA ni chama cha kidini na mgombea ni Padri hivyo wataeneneza Ukristo.Kwa hoja hizo huoni kwamba CCM wamepandikiza haya tuyaonayo sasa? kulikuwa na ulazima gani kuzungumza maneno kama hayo kwenye kampeni.CCM walianzisha vipi udini?
Yaani Haujui? Ni kivipi Sheikh Ponda alipata fursa ya kuongea Hadharani dhidi ya Dini zingine? Bila ya Serikali kujua?
Inakuwaje Rais hajui UDINI ulianzaje wakati campaign zake za 2010 alikuwa anaongelea UDINI na UKABILA? Bila Tricks zake za DIVIDE and RULE unadhani anakuwa Rais wa NCHI hii this term?