Maneno aliyoambiwa Kandili haya!

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,223
56,875
Alipoona Kandili hajibu neno aliongeza, “Nitakuibia siri yetu wanawake. Sisi huwaweka wanaume wote katika mafungu matatu. Fungu la kwanza ni la wale wanaume ambao tunawapenda kwa dhati. Wanaume ambao tuko tayari kuishi nao kwa heri au shari.

Kundi la pili ni la wanaume wazuri wa sura ya umbo. Kundi hilo tunalipenda kwa ajili ya kujionyesha tu mbele ya wenzetu. Anapita kijana mzuri. Wenzako wote wanababaika. Wewe unajitapa: ‘Yule wangu.’ Kundi la tatu ni la akina Bon. Watu wabaya au wazee. Tunawafuata kwa ajili ya uzito wa mifuko yao. Wao …”

Haikuwa mara ya kwanza kwa Kandili kusikia falsafa biyo. Hivyo alimkatiza Maua kwa kufoka tena: “Kwa hiyo mimi niko katika kundi lipi kati ya hayo?”

“Wewe. Wewe umeziba mwanya kwa makundi yote,” alijibiwa. “Wewe ni wewe tu mpenzi. Niamini tafadhali.”...

nimecheka sana haswa hilo jibu la maua mpaka nimeamua ku share nanyi waungwana!..😂
kitabu ni "pesa zako zinanuka"
muandishi Ben Mtobwa.​
 
Alipoona Kandili hajibu neno aliongeza, “Nitakuibia siri yetu wanawake. Sisi
huwaweka wanaume wote katika mafungu matatu. Fungu la kwanza ni la wale
wanaume ambao tunawapenda kwa dhati. Wanaume ambao tuko tayari kuishi
nao kwa heri au shari. Kundi la pili ni la wanaume wazuri wa sura ya umbo.
Kundi hilo tunalipenda kwa ajili ya kujionyesha tu mbele ya wenzetu. Anapita
kijana mzuri. Wenzako wote wanababaika. Wewe unajitapa: ‘Yule wangu.’
Kundi la tatu ni la akina Bon. Watu wabaya au wazee. Tunawafuata kwa ajili ya
uzito wa mifuko yao. Wao …”

Haikuwa mara ya kwanza kwa Kandili kusikia falsafa biyo. Hivyo alimkatiza
Maua kwa kufoka tena: “Kwa hiyo mimi niko katika kundi lipi kati ya hayo?”

“Wewe. Wewe umeziba mwanya kwa makundi yote,” alijibiwa. “Wewe ni wewe
tu mpenzi. Niamini tafadhali.”...

nimecheka sana haswa hilo jibu la maua mpaka nimeamua ku share nanyi waungwana!..
kitabu ni "pesa zako zinanuka"
muandishi ben mtobwa.

umenikumbusha mbali sana Pesa zako zina nuka. Njemba alisafiri kutoka zanzibar adi mombasa kutafuta utelezi.

Kina kandili walikuwa walanguzi wa bidhaa muhimu then wanafucha wanauza bei wanazotaka wao
 
umenikumbusha mbali sana Pesa zako zina nuka. Njemba alisafiri kutoka zanzibar adi mombasa kutafuta utelezi.

Kina kandili walikuwa walanguzi wa bidhaa muhimu then wanafucha wanauza bei wanazotaka wao
ndo nipo nakisoma hapa mkuu ben anauandishi wa namna yake...😁
 
Back
Top Bottom