Mandela alipewa sifa aliyostahili Nyerere! So sad!

Nyerere heshima tuliyompa hapa nyumbani inatosha, hao wengine hatuwezi kulazimisha watambue mchango wake.
 
Mandela uliwai kuskia kaweka mtu kizuini kama walivyofanyia tutemeke sanga au Jumbe
Enzi zile Nyerere alikabiliwa na hofu nyingi. Vita Baridi, Makaburu ambao siku zote walitaka kung'ofoa Roho. Magharibi walikuwa wakimtilia Mashaka kuikaribisha Urusi na Cuba Afrika. Kumbuka ndiye yeye aliyeshinikiza kuwe na Vyama vingi 1992 na kushinikiza wawepo wagombea Binafsi. Pia alikataza Wapinzani kunyanyaswa lakini walikuwa wakimpuuza!

Nyerere alikuwa na Udictator kidogo, lakini alikuwa na excuse! Kama ambavyo Ukiwa Mkweli Madictator Kagame na Museveni kweli wana some excuse. Ingawa bado Wangaliweza Kujengea Nchi zao Mazingira ya kuchagua Viongozi wazuri kwa njia ya Amani. Hofu yao ya Wasirudi walikotoka kwa Uganda wasirudi 1972-86 na Rwanda 1994. Hofu zao kwa Bahati Mbaya zitatimizwa na Udictator wao. Wasipoacha Nchi zao zitarudi kulekule! Ila kuwa wana hofu ya kweli naamini wanayo.

Ila Nchi kama Tanzania Mshenzi yeyote leo hawezi Kusema anakisingizio cha Kuwa Dictator!
 
Na
NI kweli, Nyerere kafanya mambo makubwa sana tena sana ukilinganisha na Mandela!!

Wakati Nyerere alikuwa ni mpigania uhuru wa Afrika Mandela hakupata fursa ya kuonesha kwamba alikuwa ni mpigania uhuru wa Afrika na kwahiyo kilichopo kwenye kumbukumbu ni upiganaji wake dhidi ya nchi yake!

Hata hivyo, kwa wakati ule hakuwa na namna zaidi ya kuipigania nchi yake ambayo bado ilikuwa kwenye minyororo ya makaburu!!

Lakini pamoja na yote hayo suala la kuunda Truth & Reconciliation Commission si jambo la kupuuza hata kidogo na sina shaka hili ndilo lililompa sifa nyingi Mandella!!!

Hata kama Msumbiji walikuwa na kitu kama hicho bado Mandella hakulazimika kufuata nyayo za Msumbiji!!!

Hata kama angehubiri akuanzae mmalize bado Mandela angepata support kubwa sana kutoka kwa wananchi wa Afrika Kusini! Hawa wananchi bado walikuwa na madonda mabichi ya moyoni yaliyotokana na udhalimu wa Makaburu!!!

Ingekuwa ni rahisi sana kwa sababu suppression kubwa ya Makaburu ilikuwa mijini; tena kwa kiasi kikubwa ni kutoka jiji lile lile kubwa kuliko yote!! Hapa Mandela angepata support kubwa sana kama angeamua "akuanzae mmalize!"

Kwanza kuna tofauti kati ya Truth & Reconciliation Commission ya Msumbiji na ile ya South Africa!

Kwa kumbukumbu zangu, Tume ya Mapatano Msumbiji iliundwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya RENAMO & FRELIMO! Kwavile sina uhakika sana am ready to be corrected with evidence lakini naweza kutumia logical argument ku-support madai yangu!!!

FRELIMO hawakuwa na sababu ya kuunda Tume ya Mapatano ya kuwasuluhisha na Wareno kwa sababu Mreno Msumbiji hapakuwa kwake na alitakiwa kuondoka na yule atakayebaki abaki huku akijua Msumbiji halikuwa koloni la Wareno tena!!!

Na kweli, Wareno waliondoka na kurudi Ulaya haidhuru hata kama wapo waliokuwa wamebakia!!!

Sasa kama ni Tume ya Mapatano kati ya RENAMO na FRELIMO pamoja na wafuasi wao; katu huwezi kuilinganisha na ile tume ya Afrika Kusini!

Wakati tume ya Msumbiji ilikuwa ni kuwapatanisha ndugu... Waafrika kwa Waafrika wasahau waliyofanyiana wao kwa wao, ile ya Mandela ndani ya Afrika ya Kusini kimsingi ilikuwa ni kuwafanya Waafrika wasahau unyama wote waliofanyiwa na wageni... Makaburu kutoka Ulaya!

Si jambo dogo hili hata kidogo!!!!

Wakati pasingekuwepo ile tume ya Msumbiji basi Waafrika wangeendelea kuuana wao kwa wao!! Lakini kama isingekuwepo ile ya Afrika Kusini; ambao wangeathirika zaidi ni Makaburu kwa sababu walikuwa outnumbered kwa kiasi kikubwa.

Hata Kibaraka wao Chief Mangosuthu Buthelezi asingeweza kuwasadia kwa sababu wafuasi wa Inkatha Freedom Party
ambao walikuwa tu Durban nao walikuwa outnumbered kwa mbali sana na wafuasi wa ANC!

Lakini pamoja na yote hayo... Mandela akasema let bygone be bygone na kuamua kuunda Tume ya Mapatano ambayo kimsingi ni kwa ajili ya kupatana na wale wale waliomweka korokoroni kwa miaka 27!!!!!

Si jambo dogo hilo hata kidogo!!!!

Pamoja na yote hayo, Mandela anaamua kushirikiana serikalini na wale wale waliomweka ndani kwa miaka 27... si jambo dogo hili!!

Pamoja na yote hayo, Mandela anampa cheo cha Uwaziri wa Mambo ya Ndani (mnaweza kunisahihisha kwa sababu sikutaka ku-verify) Chief Mangosuthu Buthelezi, kiumbe wa Kiafrika ambae wazi wazi alikuwa akiihujumu ANC... si jambo dogo hili!!!

Na ile ilikuwa ni truth commission kweli kweli manake kila kitu kilikuwa wazi!

Bado nakumbuka na Kiingereza changu cha Form I nilivyokuwa namfuatilia Winnie Mandela Live wakati akihojiwa hadi akanifanya nitafute dictionary kufahamu neno "ridiculous" ambalo Winnie alikuwa akilitumia mara kwa mara wakati amekalishwa kitimoto!!!

Si jambo dogo kumwacha mke wako nae awekwe kitimoto tena mbele ya kamera za televisheni!!!

Kwahiyo alichokuwa amefanya Mandella is more than kufanya kile ambacho kilifanywa na Msumbiji bali alifanya jambo ambalo lilihitaji kitu kingine la ziada!!!!

To sum up, ingawaje nakiri Nyerere amefanya mambo makubwa kwa Afrika kuliko Mandela lakini bado Mandela nae ana-deserve heshima anayopata na wala hajapata kwa upendeleo!!

NI bahati mbaya sana dunia haifahamu mchango wa Mwalimu ingawaje kwa dunia siwezi kushangaa kwa sababu Mwalimu alikuwa anawasaidia waafrika wenzake na nje ya Afrika it's none of their business!!! Uchungu wangu ni pale ambapo hata Afrika yenyewe inapoonekana kutofahamu mchango huu wa Mwalimu!!!

Lakini ngoja niweke kumbukumbu sawa kwa manufaa ya vizazi vyetu manake wengi huwa hatulizungumzii vizuri hili jambo!!

Pamoja na kwamba tangu mwanzo Mwalimu alionesha kusaidia harakati za ukombozi, lakini mengine mengi yaliyofuata alikuwa anatekeleza kazi aliyokuwa amepewa na OAU.

Baada ya OAU kuundwa, pia ziliundwa kamati mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha na kutatua changamoto mbalimbali barani Afrika! Kwa mfano, kulikuwa na Kamati ya Viwanda (and something) ambayo Makao Makuu yake yalikuwa Gaborone, Botswana!!!

Tanzania tukatwishwa zigo la ukombozi ambapo Kamati ya Ukombozi ilikuwa na makao yake makuu Dar es salaam!!!

Main goal ya Kamati ya Ukombozi ilikuwa ni moja: kuhakikisha nchi zote zilizokuwa chini ya ukoloni nazo zinapata uhuru! By the time, nchi hizo zilikuwa Msumbiji, Angola na Guinea Bissau!!

Na kweli, Mwalimu Nyerere aliifanya kazi hiyo kwa moyo mmoja na mara kadhaa kutumia raslimali za taifa ili mradi tu kuhakikisha lengo hilo linafikiwa na kweli likafikiwa!!

Nadhani Kamati ya Ukombozi ndie kamati pekee ya OAU iliyokuwa imefanikiwa malengo yake miongoni mwa kamati zingine zote!!!

Remember, Afrika Kusini haikuwa considered kama ilikuwa inatawaliwa! Ni kama Zanzibar... Zanzibar haiwi considered kwamba ilitawaliwa na Sultan at least baada ya ujio wa wakoloni wa Ulaya!!!
No Vita vya Renamo Vilianzwa 1983 Na vilimalizika na Makubaliano ya Nkomati ya 1985. Kabla ya Kufa kwa Samora. Truth and Reconciliation ilianza tangu 1976 na hapo 1981 ilikuwa ni siku ya Kukamilisha tume. Pili ungesikiliza hiyo video iko Wazi there is nothing to do with Renamo.
 
Mwalimu Nyerere Muda Mfupi Baada ya Uhuru alipata Ugeni wa Siri, Ugeni wa Nelson Mandela. Mandela alikuwa akitaka Msaada kwa Nyerere wa Kuanzisha Jeshi la Kupigania Haki la Umkoto We Skzwe yaani Mkuki wa Bwana au Mkuki wa Mfalme.

Kulingana Na Kitabu cha Mandela cha Long Walk to Freedom, Nyerere alionyesha Kusita, alimshauri asubiri asifanye jitihada za Kijeshi mpaka Walter Sisulu aachiliwe. Wakaagana Nelson akamwambia Mwalimu atarudi Tena na Akaenda Ethiopia ambako alikutana na Haile Selassie, Haile Selassie alimwelewa Mandela Kwa haraka na Akampa Pesa nyingi sana tu. Mandela akasafiri kurudi SA. Kufika huko muda Mchache akakamatwa hivyo hakuweza Tena kuonana na Nyerere.

Baada ya Mandela Kukamatwa na Nyerere Kuona kwa Undani Uonevu wa Ukoloni Nchi za Kusini Mwa Afrika na Ubaguzi wa Rangi SA, basi akaamua Kujitwisha Mzigo wa Kusaidia Majeshi ya nchi zote zile na Pia sio tu hivyo Bali kiwazi wazi akazunguka Dunia Nzima Kupiga Kelele na Pia Kutafuta fedha za kusaidia Majeshi yale. Na mara nyingi akatumia hata Majeshi ya Tanzania kusaidi. Hii ilimhatarisha binafsi na nchi kwa ujumla!

Msumbiji ilipopata Uhuru Nyerere ndiye aliyewakalisha Akina Samora na Kuwaambia wasilipize Visasi kwa Wazungu au Collaborators (Waliokuwa wakiwasaidia wazungu) na kwa Mwongozo wa Moja kwa moja wa Nyerere Ikaanzishwa Tume ya Ukweli na Usuluhishi (Truth and Reconciliation) ambapo waliofanya uhalifu wa kinyama walikuwa wakikiri na Kuomba Msamaha.

South Afrika ilipokuwa Democratic 1994 Mandela Akafuata Mfano huo nukta kwa Nukta. Lakini Dunia Nzima ikamwenzi sana Mandela, Mandela alizikwa na Viongozi wote Wa dunia, Ila Nyerere hakupewa heshima wala shukurani anayoistahili na Dunia wakati wa Kifo chake.

Kila uendapo Duniani Unakuta Sanamu za Mandela, Ila Nyerere hata AU ilibidi Mugabe aseme ikiwa Afrika haitaki Kumkumbuka Nyerere Zimbabwe itafanya Kivyake!

Kwa hili tunaungana kifikra. Nyerere anao mchango mkubwa mno katika kuitengeneza Afrika ya sasa kuliko Mandela. Hata kuachia madaraka wakati wananchi wakiwa wanamuhitaji. Wananchi walimuhitaji kwelikweli si kinafiki.
Mapenzi ya mataifa ya nje kwa Mandela ni huruma na majuto kwa yale waliyomfanyia mzee yule. Mandela mwenyewe aliufahamu umhimu wa Mwl Nyerere kiasi cha kuona kuwa mtu wa kwanza nje ya South Afrika kuonana naye alikuwa Mwl Nyerere siku tisa baada ya kutoka gerezani.
 
No, Uasi wa Renamo chini ya Mbwa na Nyoka Alphonso Dlakama 1983 Na na ulimalizwa na Makubaliano ya Nkomati ya 1985. Kabla ya Kufa kwa Samora. Nimemwita Dlakama Mbwa Kwani Kama ilivyokuwa Savimbi Angola, Huyu Mbwa alisaidiwa na Makaburu kuivuruga Mozambique, Halafu mbinu ya mbwa hawa kupata pesa na silaha ilikuwa kuwadanganya Marekani wanapigania Ubepari dhidi ya Ukomunist. Truth and Reconciliation ilianza tangu 1976 na hapo 1981 ilikuwa ni siku ya Kukamilisha tume. Pili ungesikiliza hiyo video iko Wazi there is nothing to do with Renamo.
 
Mataifa ya Nje yanamsifu Mtu akifumbia macho au Akisamehe Unyama wao! Ila wao hawasamehe wala hawasahau. Wakifanya Uhalifu wa Kivita au Unyama wa ajabu wa makusudi wanasema ,"We did mistakes" Lakini akifanya mwingine hayo hayo wanasema ni evil, ni madness etc! Ndio Maana Nachukia sana Double Standard Ni Tabia inayonuka zaidi ya Uharo wa Kipindupindu!
 
Kuna msemo wa kiswahili unasema"Muoshwa huoshwa"Alichofanya Nyerere kwa wenzake wapigania Uhuru wa Tanganyika ndicho alichofanyiwa.Harakati za kudai Uhuru kilikuwa na watu wengi ambao walianza haraka kipindi Nyerere yupo Kijijini kwao,Alipokuja dar es salaam alishikwa mkono na watu na kumwonyesha njia Lakini cha kushangaza michango yao haitambuliki historia yote inamtaja Nyerere ndo Simba wa uhuru.Mtupa tope humrudia
 
No, Uasi wa Renamo chini ya Mbwa na Nyoka Alphonso Dlakama 1983 Na na ulimalizwa na Makubaliano ya Nkomati ya 1985. Kabla ya Kufa kwa Samora. Nimemwita Dlakama Mbwa Kwani Kama ilivyokuwa Savimbi Angola, Huyu Mbwa alisaidiwa na Makaburu kuivuruga Mozambique, Halafu mbinu ya mbwa hawa kupata pesa na silaha ilikuwa kuwadanganya Marekani wanapigania Ubepari dhidi ya Ukomunist. Truth and Reconciliation ilianza tangu 1976 na hapo 1981 ilikuwa ni siku ya Kukamilisha tume. Pili ungesikiliza hiyo video iko Wazi there is nothing to do with Renamo.

Kwani Eduardo Dos santos alikua anasaidiwa na nani na Kama Savimbi n mbwa kwanin mpaka leo Angola wanamueshimu na alizikwa kwnye makaburi ya Taifa kwa heshima Zote na UNITA n chama cha Kisiasa na kinasonga mbele acha upuuzi kasome vizur historia ya Angola 1960-1975-1992-2002 mpka sasa ..
 
Swali hilo hilo ligeuze kwa hapa nchini, mbona watu waliosimama bega kwa bega na Nyerere kudai uhuru hapa nchini hawaenziwi ipasavyo?
 
Mwalimu Nyerere Muda Mfupi Baada ya Uhuru alipata Ugeni wa Siri, Ugeni wa Nelson Mandela. Mandela alikuwa akitaka Msaada kwa Nyerere wa Kuanzisha Jeshi la Kupigania Haki la Umkoto We Skzwe yaani Mkuki wa Bwana au Mkuki wa Mfalme.

Kulingana Na Kitabu cha Mandela cha Long Walk to Freedom, Nyerere alionyesha Kusita, alimshauri asubiri asifanye jitihada za Kijeshi mpaka Walter Sisulu aachiliwe. Wakaagana Nelson akamwambia Mwalimu atarudi Tena na Akaenda Ethiopia ambako alikutana na Haile Selassie, Haile Selassie alimwelewa Mandela Kwa haraka na Akampa Pesa nyingi sana tu. Mandela akasafiri kurudi SA. Kufika huko muda Mchache akakamatwa hivyo hakuweza Tena kuonana na Nyerere.

Baada ya Mandela Kukamatwa na Nyerere Kuona kwa Undani Uonevu wa Ukoloni Nchi za Kusini Mwa Afrika na Ubaguzi wa Rangi SA, basi akaamua Kujitwisha Mzigo wa Kusaidia Majeshi ya nchi zote zile na Pia sio tu hivyo Bali kiwazi wazi akazunguka Dunia Nzima Kupiga Kelele na Pia Kutafuta fedha za kusaidia Majeshi yale. Na mara nyingi akatumia hata Majeshi ya Tanzania kusaidi. Hii ilimhatarisha binafsi na nchi kwa ujumla!

Msumbiji ilipopata Uhuru Nyerere ndiye aliyewakalisha Akina Samora na Kuwaambia wasilipize Visasi kwa Wazungu au Collaborators (Waliokuwa wakiwasaidia wazungu) na kwa Mwongozo wa Moja kwa moja wa Nyerere Ikaanzishwa Tume ya Ukweli na Usuluhishi (Truth and Reconciliation) ambapo waliofanya uhalifu wa kinyama walikuwa wakikiri na Kuomba Msamaha.

South Afrika ilipokuwa Democratic 1994 Mandela Akafuata Mfano huo nukta kwa Nukta. Lakini Dunia Nzima ikamwenzi sana Mandela, Mandela alizikwa na Viongozi wote Wa dunia, Ila Nyerere hakupewa heshima wala shukurani anayoistahili na Dunia wakati wa Kifo chake.

Kila uendapo Duniani Unakuta Sanamu za Mandela, Ila Nyerere hata AU ilibidi Mugabe aseme ikiwa Afrika haitaki Kumkumbuka Nyerere Zimbabwe itafanya Kivyake!

Mandela was far intelligent than him
 
Japo angekuwa amekaa selo ya wakolon hata miaka 20 hivi angemfikia fikia!
 
Mandela was far intelligent than him
Mandela angekuwa intelligent hivyo asingekamatwa wewe.

Sifa nyingine zinatokana na geopolitics. Naweza kusema Mandela amepewa sifa zaidi ya Nyerere kwa sababu ya dhahabu ya South Africa.

Ni hivi. Wazungu wamehamia South Africa kwa sababu ya dhahabu. Bila dhahabu South Africa ingekuwa koloni lingine tu la Muingerez ambalo lingepata uhuru miaka ya 60 na Mandela kama angekuwa rais angekuwa rais kama marais wengine tu wa Afrika.

Lakini kwa sababu South Africa ilikuwa na dhahabu nyingi sana, wazungu wakaipigania. Soma kuhusu Boers War kama hujasoma. South Africa ikawa tamu mpaka wazungu wakalowea kabisa.

Hilo likasababisha apartheid. Likasababisha utawala huu dhalimu udumu sana. Likasababisha Mandela afungwe muda mrefu sana na kuwa mfungwa mashuhuri kuliko wote duniani kwa kipindi kirefu.

Nyerere hakuweza kupata press aliyopata Mandela kwa sababu hakuwa mfungwa kwa kipindi kirefu hivyo.

Pia, Mandela alivyotoka jela alitumia diplomasia ya hali ya juu kusamehe wazungu. Wazungu wakampa kiki zaidi kama mtu wa amani.

Nyerere aliwafukuza wazungu na kwenda kuji ally na wa China.

Umaarufu wa Mandela umetokana na geopolitics zaidi ya yeye kuwa exceptional kulinganisha viongozi wengine.
 
Kuna msemo wa kiswahili unasema"Muoshwa huoshwa"Alichofanya Nyerere kwa wenzake wapigania Uhuru wa Tanganyika ndicho alichofanyiwa.Harakati za kudai Uhuru kilikuwa na watu wengi ambao walianza haraka kipindi Nyerere yupo Kijijini kwao,Alipokuja dar es salaam alishikwa mkono na watu na kumwonyesha njia Lakini cha kushangaza michango yao haitambuliki historia yote inamtaja Nyerere ndo Simba wa uhuru.Mtupa tope humrudia
Wafuasi wa Mudi mmeshakuja!
Mnapenda stori feki za uchonganishi
 
NI KAWAIDA UKISHAKUWA KIBARAKA WA WAZUNGU UTATUKUZWA SANA NAO,UTAPEWA SIFA KEDEKEDE.
KWANGU MIMI MANDELA NI KIBARAKA TU WA WAZUNGU NA NYERERE NI MKOMBOZI WA AFRIKA.MSUMBIJI,ANGOLA,SA,ZIMBABWE WANALITAMBUA HILI
 
Kuna msemo wa kiswahili unasema"Muoshwa huoshwa"Alichofanya Nyerere kwa wenzake wapigania Uhuru wa Tanganyika ndicho alichofanyiwa.Harakati za kudai Uhuru kilikuwa na watu wengi ambao walianza haraka kipindi Nyerere yupo Kijijini kwao,Alipokuja dar es salaam alishikwa mkono na watu na kumwonyesha njia Lakini cha kushangaza michango yao haitambuliki historia yote inamtaja Nyerere ndo Simba wa uhuru.Mtupa tope humrudia
Huo msemo havimuhusu Nyerere, uelewa wako tu wa kukaririshwa na kunyweshwa sumu pasi kujiuliza ndo shida.

Aliowakuta Nyerere Kwanza hata hawakuweza na wengine hata kuwaza kumpatia huru WA nchi yote ya Tanganyika, wapo walio hitaji huru WA maeneo, makundi nk. Hata Marekani anajulikana Washington, walikuwepo wengi kabla yake. SA walikuwepo akina Biko nk

Elimu zao wengi hazikuwa nzuri, hata hivyo wakipewa nafasi, waliokuwa na elimu walikwenda kinyume na itikadi Zach ujamaa, hawakupaswa kupewa nafasi.

Kuhusu Nyerere na Mandela, hili liko wazi Nyerere akienda kinyume na interest za kibepari, wasingemkubali na inawezekana walipanga hata kumuua. Mandela ingawa alikuwa na damu ys kijamaa, masharti yalimlazimu afuate ubepari, na hii ndiyo heshima yake ktk ulimwengu WA kibepari.
 
Asante sana mleta mada, MAULANA MOLA wetu ni mwaminifu sana!
 
Kwani Eduardo Dos santos alikua anasaidiwa na nani na Kama Savimbi n mbwa kwanin mpaka leo Angola wanamueshimu na alizikwa kwnye makaburi ya Taifa kwa heshima Zote na UNITA n chama cha Kisiasa na kinasonga mbele acha upuuzi kasome vizur historia ya Angola 1960-1975-1992-2002 mpka sasa ..
Upuuzi uko wapi hapo sasa? Inaelekea hata humjui Savimbi, itikadi Zake nk. Humjui.
 
Japo angekuwa amekaa selo ya wakolon hata miaka 20 hivi angemfikia fikia!
Kukaa selo ndo ukomavu na ushujaa? Kuna hadithi Kama hizi zilianza kulishwa kwa jamii miaka ile, ugangsta, utoto WA mama nk. Mazao yake wanasiasa wetu vijana wa leo nao wanapishana tu selo wakidai ndo ujanja, Mandela hakupenda hilo limtokee, kaisome hotuba yake "I am prepared to die" alivyojitetea vya kutosha asifungwe.

Na makosa aliyoyafanya ni ys kimkakati kabisa, sio yale yakuuzia jina magazetini kama ya wana rap musicians WA US.
 
Waswahili tumezoea kulalamika tu.
Mwalimu Nyerere ni wa kwetu, hivyo ni juu yetu kumtangaza na sifa zake zote katika ukombozi wa nchi husika.
Hizo sifa pia ndizo zitaweza kuifanya Tanzania ijulikane kwa walimwengu na kuhabarisha jinsi Tanzania na udogo na umasikani ilimudu kuhimili vishindo vya wakubwa mpaka kuweezesha ukombozi huo.
Watu wa Mataifa ya Magharibi wanaenda kwa propaganda za mitandao.
Tuamke sasa tuonyeshe ushujaa wetu tulivyochangia ukombozi.
Mandela alifungwa, lakini waliowezesha mageuzi ndani ya Afrika Kusini ni wengine na ndiyo maana Raisi Mugabe anakasrika sana kuona wanaenziwa wasiostahili.
 
Back
Top Bottom