Mandela alipewa sifa aliyostahili Nyerere! So sad!

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,807
Mwalimu Nyerere Muda Mfupi Baada ya Uhuru alipata Ugeni wa Siri, Ugeni wa Nelson Mandela. Mandela alikuwa akitaka Msaada kwa Nyerere wa Kuanzisha Jeshi la Kupigania Haki la Umkoto We Skzwe yaani Mkuki wa Bwana au Mkuki wa Mfalme.

Kulingana Na Kitabu cha Mandela cha Long Walk to Freedom, Nyerere alionyesha Kusita, alimshauri asubiri asifanye jitihada za Kijeshi mpaka Walter Sisulu aachiliwe. Wakaagana Nelson akamwambia Mwalimu atarudi Tena na Akaenda Ethiopia ambako alikutana na Haile Selassie, Haile Selassie alimwelewa Mandela Kwa haraka na Akampa Pesa nyingi sana tu. Mandela akasafiri kurudi SA. Kufika huko muda Mchache akakamatwa hivyo hakuweza Tena kuonana na Nyerere.

Baada ya Mandela Kukamatwa na Nyerere Kuona kwa Undani Uonevu wa Ukoloni Nchi za Kusini Mwa Afrika na Ubaguzi wa Rangi SA, basi akaamua Kujitwisha Mzigo wa Kusaidia Majeshi ya nchi zote zile na Pia sio tu hivyo Bali kiwazi wazi akazunguka Dunia Nzima Kupiga Kelele na Pia Kutafuta fedha za kusaidia Majeshi yale. Na mara nyingi akatumia hata Majeshi ya Tanzania kusaidi. Hii ilimhatarisha binafsi na nchi kwa ujumla!

Msumbiji ilipopata Uhuru Nyerere ndiye aliyewakalisha Akina Samora na Kuwaambia wasilipize Visasi kwa Wazungu au Collaborators (Waliokuwa wakiwasaidia wazungu) na kwa Mwongozo wa Moja kwa moja wa Nyerere Ikaanzishwa Tume ya Ukweli na Usuluhishi (Truth and Reconciliation) ambapo waliofanya uhalifu wa kinyama walikuwa wakikiri na Kuomba Msamaha.

South Afrika ilipokuwa Democratic 1994 Mandela Akafuata Mfano huo nukta kwa Nukta. Lakini Dunia Nzima ikamwenzi sana Mandela, Mandela alizikwa na Viongozi wote Wa dunia, Ila Nyerere hakupewa heshima wala shukurani anayoistahili na Dunia wakati wa Kifo chake.

Kila uendapo Duniani Unakuta Sanamu za Mandela, Ila Nyerere hata AU ilibidi Mugabe aseme ikiwa Afrika haitaki Kumkumbuka Nyerere Zimbabwe itafanya Kivyake!
 
Attachments

  • Samora Machel HD.mp4
    24.7 MB
  • UPITN 31 10 78 FRONT LINE SUMMIT.mp4
    20.8 MB
Nyerere hakufanya hayo yote ili aje kujengewa minara dunia mzima kama Mandela.Nyerere hakufanya ili aje asifiwe au akifa aje kuzikwa na viongozi wa dunia mzima kama Mandela la hasha.

Hata Real Madrid mfungaji magoli ni Christian Ronaldo lakini mtengenezaji ni Marcelo au Lucas Modrich

Na Barcelona mfungaji ni Messi na mpishi mkubwa Ineasta

Hawa watengenezaji Hata hawajulikani lakini ndiyo engines za hizo timu na Hata Mwl Nyerere ameplay role kubwa sana ktk ukombozi wa nchini kusini mwa Africa lakini recognition yake kimataifa iko chini Si kama Mandela.

.Si jambo la kulalamika kuhusu Nyerere kwasababu, Hata ktk jamii zetu wapo watu ni muhimu sana na wanasaidia sana lakini hawataki kabisa Hata kujulikana.
 
NI kweli, Nyerere kafanya mambo makubwa sana tena sana ukilinganisha na Mandela!!

Wakati Nyerere alikuwa ni mpigania uhuru wa Afrika Mandela hakupata fursa ya kuonesha kwamba alikuwa ni mpigania uhuru wa Afrika na kwahiyo kilichopo kwenye kumbukumbu ni upiganaji wake dhidi ya nchi yake!

Hata hivyo, kwa wakati ule hakuwa na namna zaidi ya kuipigania nchi yake ambayo bado ilikuwa kwenye minyororo ya makaburu!!

Lakini pamoja na yote hayo suala la kuunda Truth & Reconciliation Commission si jambo la kupuuza hata kidogo na sina shaka hili ndilo lililompa sifa nyingi Mandella!!!

Hata kama Msumbiji walikuwa na kitu kama hicho bado Mandella hakulazimika kufuata nyayo za Msumbiji!!!

Hata kama angehubiri akuanzae mmalize bado Mandela angepata support kubwa sana kutoka kwa wananchi wa Afrika Kusini! Hawa wananchi bado walikuwa na madonda mabichi ya moyoni yaliyotokana na udhalimu wa Makaburu!!!

Ingekuwa ni rahisi sana kwa sababu suppression kubwa ya Makaburu ilikuwa mijini; tena kwa kiasi kikubwa ni kutoka jiji lile lile kubwa kuliko yote!! Hapa Mandela angepata support kubwa sana kama angeamua "akuanzae mmalize!"

Kwanza kuna tofauti kati ya Truth & Reconciliation Commission ya Msumbiji na ile ya South Africa!

Kwa kumbukumbu zangu, Tume ya Mapatano Msumbiji iliundwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya RENAMO & FRELIMO! Kwavile sina uhakika sana am ready to be corrected with evidence lakini naweza kutumia logical argument ku-support madai yangu!!!

FRELIMO hawakuwa na sababu ya kuunda Tume ya Mapatano ya kuwasuluhisha na Wareno kwa sababu Mreno Msumbiji hapakuwa kwake na alitakiwa kuondoka na yule atakayebaki abaki huku akijua Msumbiji halikuwa koloni la Wareno tena!!!

Na kweli, Wareno waliondoka na kurudi Ulaya haidhuru hata kama wapo waliokuwa wamebakia!!!

Sasa kama ni Tume ya Mapatano kati ya RENAMO na FRELIMO pamoja na wafuasi wao; katu huwezi kuilinganisha na ile tume ya Afrika Kusini!

Wakati tume ya Msumbiji ilikuwa ni kuwapatanisha ndugu... Waafrika kwa Waafrika wasahau waliyofanyiana wao kwa wao, ile ya Mandela ndani ya Afrika ya Kusini kimsingi ilikuwa ni kuwafanya Waafrika wasahau unyama wote waliofanyiwa na wageni... Makaburu kutoka Ulaya!

Si jambo dogo hili hata kidogo!!!!

Wakati pasingekuwepo ile tume ya Msumbiji basi Waafrika wangeendelea kuuana wao kwa wao!! Lakini kama isingekuwepo ile ya Afrika Kusini; ambao wangeathirika zaidi ni Makaburu kwa sababu walikuwa outnumbered kwa kiasi kikubwa.

Hata Kibaraka wao Chief Mangosuthu Buthelezi asingeweza kuwasadia kwa sababu wafuasi wa Inkatha Freedom Party
ambao walikuwa tu Durban nao walikuwa outnumbered kwa mbali sana na wafuasi wa ANC!

Lakini pamoja na yote hayo... Mandela akasema let bygone be bygone na kuamua kuunda Tume ya Mapatano ambayo kimsingi ni kwa ajili ya kupatana na wale wale waliomweka korokoroni kwa miaka 27!!!!!

Si jambo dogo hilo hata kidogo!!!!

Pamoja na yote hayo, Mandela anaamua kushirikiana serikalini na wale wale waliomweka ndani kwa miaka 27... si jambo dogo hili!!

Pamoja na yote hayo, Mandela anampa cheo cha Uwaziri wa Mambo ya Ndani (mnaweza kunisahihisha kwa sababu sikutaka ku-verify) Chief Mangosuthu Buthelezi, kiumbe wa Kiafrika ambae wazi wazi alikuwa akiihujumu ANC... si jambo dogo hili!!!

Na ile ilikuwa ni truth commission kweli kweli manake kila kitu kilikuwa wazi!

Bado nakumbuka na Kiingereza changu cha Form I nilivyokuwa namfuatilia Winnie Mandela Live wakati akihojiwa hadi akanifanya nitafute dictionary kufahamu neno "ridiculous" ambalo Winnie alikuwa akilitumia mara kwa mara wakati amekalishwa kitimoto!!!

Si jambo dogo kumwacha mke wako nae awekwe kitimoto tena mbele ya kamera za televisheni!!!

Kwahiyo alichokuwa amefanya Mandella is more than kufanya kile ambacho kilifanywa na Msumbiji bali alifanya jambo ambalo lilihitaji kitu kingine la ziada!!!!

To sum up, ingawaje nakiri Nyerere amefanya mambo makubwa kwa Afrika kuliko Mandela lakini bado Mandela nae ana-deserve heshima anayopata na wala hajapata kwa upendeleo!!

NI bahati mbaya sana dunia haifahamu mchango wa Mwalimu ingawaje kwa dunia siwezi kushangaa kwa sababu Mwalimu alikuwa anawasaidia waafrika wenzake na nje ya Afrika it's none of their business!!! Uchungu wangu ni pale ambapo hata Afrika yenyewe inapoonekana kutofahamu mchango huu wa Mwalimu!!!

Lakini ngoja niweke kumbukumbu sawa kwa manufaa ya vizazi vyetu manake wengi huwa hatulizungumzii vizuri hili jambo!!

Pamoja na kwamba tangu mwanzo Mwalimu alionesha kusaidia harakati za ukombozi, lakini mengine mengi yaliyofuata alikuwa anatekeleza kazi aliyokuwa amepewa na OAU.

Baada ya OAU kuundwa, pia ziliundwa kamati mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha na kutatua changamoto mbalimbali barani Afrika! Kwa mfano, kulikuwa na Kamati ya Viwanda (and something) ambayo Makao Makuu yake yalikuwa Gaborone, Botswana!!!

Tanzania tukatwishwa zigo la ukombozi ambapo Kamati ya Ukombozi ilikuwa na makao yake makuu Dar es salaam!!!

Main goal ya Kamati ya Ukombozi ilikuwa ni moja: kuhakikisha nchi zote zilizokuwa chini ya ukoloni nazo zinapata uhuru! By the time, nchi hizo zilikuwa Msumbiji, Angola na Guinea Bissau!!

Na kweli, Mwalimu Nyerere aliifanya kazi hiyo kwa moyo mmoja na mara kadhaa kutumia raslimali za taifa ili mradi tu kuhakikisha lengo hilo linafikiwa na kweli likafikiwa!!

Nadhani Kamati ya Ukombozi ndie kamati pekee ya OAU iliyokuwa imefanikiwa malengo yake miongoni mwa kamati zingine zote!!!

Remember, Afrika Kusini haikuwa considered kama ilikuwa inatawaliwa! Ni kama Zanzibar... Zanzibar haiwi considered kwamba ilitawaliwa na Sultan at least baada ya ujio wa wakoloni wa Ulaya!!!
 
Asante kwa maelezo mazuri mwanahistoria mujarabu kabisa!
Ninachoshindwa kujua na ninachojiuliza ni kwamba Mandela kweli aliamua kuwasamehe kutoka moyoni kweli au alishindwa namna ya kupambana nao akajifanya kuwasamehe kwa kuwa walikita mizizi sana ndani ya SA?
NI kweli, Nyerere kafanya mambo makubwa sana tena sana ukilinganisha na Mandela!!

Wakati Nyerere alikuwa ni mpigania uhuru wa Afrika Mandela hakupata fursa ya kuonesha kwamba alikuwa ni mpigania uhuru wa Afrika na kwahiyo kilichopo kwenye kumbukumbu ni upiganaji wake dhidi ya nchi yake!

Hata hivyo, kwa wakati ule hakuwa na namna zaidi ya kuipigania nchi yake ambayo bado ilikuwa kwenye minyororo ya makaburu!!

Lakini pamoja na yote hayo suala la kuunda Truth & Reconciliation Commission si jambo la kupuuza hata kidogo na sina shaka hili ndilo lililompa sifa nyingi Mandella!!!

Hata kama Msumbiji walikuwa na kitu kama hicho bado Mandella hakulazimika kufuata nyayo za Msumbiji!!!

Hata kama angehubiri akuanzae mmalize bado Mandela angepata support kubwa sana kutoka kwa wananchi wa Afrika Kusini! Hawa wananchi bado walikuwa na madonda mabichi ya moyoni yaliyotokana na udhalimu wa Makaburu!!!

Ingekuwa ni rahisi sana kwa sababu suppression kubwa ya Makaburu ilikuwa mijini; tena kwa kiasi kikubwa ni kutoka jiji lile lile kubwa kuliko yote!! Hapa Mandela angepata support kubwa sana kama angeamua "akuanzae mmalize!"

Kwanza kuna tofauti kati ya Truth & Reconciliation Commission ya Msumbiji na ile ya South Africa!

Kwa kumbukumbu zangu, Tume ya Mapatano Msumbiji iliundwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya RENAMO & FRELIMO! Kwavile sina uhakika sana am ready to be corrected with evidence lakini naweza kutumia logical argument ku-support madai yangu!!!

FRELIMO hawakuwa na sababu ya kuunda Tume ya Mapatano ya kuwasuluhisha na Wareno kwa sababu Mreno Msumbiji hapakuwa kwake na alitakiwa kuondoka na yule atakayebaki abaki huku akijua Msumbiji halikuwa koloni la Wareno tena!!!

Na kweli, Wareno waliondoka na kurudi Ulaya haidhuru hata kama wapo waliokuwa wamebakia!!!

Sasa kama ni Tume ya Mapatano kati ya RENAMO na FRELIMO pamoja na wafuasi wao; katu huwezi kuilinganisha na ile tume ya Afrika Kusini!

Wakati tume ya Msumbiji ilikuwa ni kuwapatanisha ndugu... Waafrika kwa Waafrika wasahau waliyofanyiana wao kwa wao, ile ya Mandela ndani ya Afrika ya Kusini kimsingi ilikuwa ni kuwafanya Waafrika wasahau unyama wote waliofanyiwa na wageni... Makaburu kutoka Ulaya!

Si jambo dogo hili hata kidogo!!!!

Wakati pasingekuwepo ile tume ya Msumbiji basi Waafrika wangeendelea kuuana wao kwa wao!! Lakini kama isingekuwepo ile ya Afrika Kusini; ambao wangeathirika zaidi ni Makaburu kwa sababu walikuwa outnumbered kwa kiasi kikubwa.

Hata Kibaraka wao Chief Mangosuthu Buthelezi asingeweza kuwasadia kwa sababu wafuasi wa Inkatha Freedom Party
ambao walikuwa tu Durban nao walikuwa outnumbered kwa mbali sana na wafuasi wa ANC!

Lakini pamoja na yote hayo... Mandela akasema let bygone be bygone na kuamua kuunda Tume ya Mapatano ambayo kimsingi ni kwa ajili ya kupatana na wale wale waliomweka korokoroni kwa miaka 27!!!!!

Si jambo dogo hilo hata kidogo!!!!

Pamoja na yote hayo, Mandela anaamua kushirikiana serikalini na wale wale waliomweka ndani kwa miaka 27... si jambo dogo hili!!

Pamoja na yote hayo, Mandela anampa cheo cha Uwaziri wa Mambo ya Ndani (mnaweza kunisahihisha kwa sababu sikutaka ku-verify) Chief Mangosuthu Buthelezi, kiumbe wa Kiafrika ambae wazi wazi alikuwa akiihujumu ANC... si jambo dogo hili!!!

Na ile ilikuwa ni truth commission kweli kweli manake kila kitu kilikuwa wazi!

Bado nakumbuka na Kiingereza changu cha Form I nilivyokuwa namfuatilia Winnie Mandela Live wakati akihojiwa hadi akanifanya nitafute dictionary kufahamu neno "ridiculous" ambalo Winnie alikuwa akilitumia mara kwa mara wakati amekalishwa kitimoto!!!

Si jambo dogo kumwacha mke wako nae awekwe kitimoto tena mbele ya kamera za televisheni!!!

Kwahiyo alichokuwa amefanya Mandella is more than kufanya kile ambacho kilifanywa na Msumbiji bali alifanya jambo ambalo lilihitaji kitu kingine la ziada!!!!

To sum up, ingawaje nakiri Nyerere amefanya mambo makubwa kwa Afrika kuliko Mandela lakini bado Mandela nae ana-deserve heshima anayopata na wala hajapata kwa upendeleo!!

NI bahati mbaya sana dunia haifahamu mchango wa Mwalimu ingawaje kwa dunia siwezi kushangaa kwa sababu Mwalimu alikuwa anawasaidia waafrika wenzake na nje ya Afrika it's none of their business!!! Uchungu wangu ni pale ambapo hata Afrika yenyewe inapoonekana kutofahamu mchango huu wa Mwalimu!!!
 
Ni kosa kubwa sana kihistoria lilifanyika for me naungana na Mugabe historia ya Mandela iko SA basi... lakini Nyerere ni Africa na Globally amepambana anatakiwa atambulike kama PanAfricanist number moja barani Africa kwa philosophies zake clear kabisa zilizochochea colonial liberalization
Labda ninachodhani mimi Mandela anaonekana maarufu kuliko Nyerere kwa sababu ya hulka ya wazungu walisamehewa udhalimu na unyonyaji wao SA na bado wakaendelea kuishi south Africa kama investors ambao hadi leo naweza kusema ni moja ya sababu za migogoro ya kudumu ya nchi hiyo (haves na non-haves)
 
Nyerere hakuishi zama information na technology hivyo mchango wake SA haukumbukwi. Tulikula Unga yanga, tukachukiwa na jirani zetu wa EA kwa kuwa Magari wa Mbele Ukombozi kusini kwa Afrika. Tukatengwa Na Western Block kama vile Europe na Usa
 
Asante kwa maelezo mazuri mwanahistoria mujarabu kabisa!
Ninachoshindwa kujua na ninachojiuliza ni kwamba Mandela kweli aliamua kuwasamehe kutoka moyoni kweli au alishindwa namna ya kupambana nao akajifanya kuwasamehe kwa kuwa walikita mizizi sana ndani ya SA?
Kushindwa namna ya kupambana nao; HAPANA kwa sababu wakati haya yanatokea tayari Mandela alishakuwa Rais. Angetaka angeanza kutimua askari wote wa kizungu kutoka majeshi mbali na hivyo jeshi lote kuwa chini ya weusi; bunduki zote kuwa chini ya weusi, vifaru vyote kuwa chini ya weusi na kadhaa wa kadhaa!!!!

Kama angeamua kuwafanyia ushenzi, Makaburu wasingefurukuta!!!

Naamini alikuwa na nia dhabiti kabisa ya kusahau yaliyopita na ndio maana hakuona taabu hata kuwaingiza serikalini!!!

Lakini lingine ambalo naamini liliongeza nguvu nia yake ya kusameheana ni uchumi wa Afrika Kusini!!! Kama si Kamati ya Mapatano, na kisha zikaanza tit for tat na Makaburu; basi uchumi wa Afrika Kusini ungevurugika kwa kiasi kikubwa sana!!!!
 
siku zote anaye leta mchango huwa ajulikani ila asiye kuwa na mchango ana julikana
 
Hii ni moja ya hotuba inayoonesha "unabii" wa Mwalimu!!!

Nadhani hii ni ile hotuba ambayo alisema Ulaya wanaweza kuwa more concerned na North Africa kuliko Sub-Saharan Africa kutokana na ukaribu wao na North Africa!! Hoja yake ikawa, wazungu wasipoisaidia North Africa, itafika wakati vijana maskini wa North Africa hawatakuwa na namna zaidi ya kukimbilia Ulaya kutafuta maisha!!!

Haya ndiyo yanayotokea hivi sasa!! Vijana kutoka Kaskazini mwa Afrika hawana tena uoga wa kujitosa baharini tena hata kwa mitumbwi ili mradi tu wafike Ulaya!!!
 
Yule Mzee Mungu alimpa uwezo mkubwa sana wa kutoa hotuba zenye mambo mengi ya msingi sana kwa wakati aliokuwa hai kuhusu nchi yetu na dunia pia na hotuba zake nyingi ziko valid mpaka leo hii.

Hii ni moja ya hotuba inayoonesha "unabii" wa Mwalimu!!!

Nadhani hii ni ile hotuba ambayo alisema Ulaya wanaweza kuwa more concerned na North Africa kuliko Sub-Saharan Africa kutokana na ukaribu wao na North Africa!! Hoja yake ikawa, wazungu wasipoisaidia North Africa, itafika wakati vijana maskini wa North Africa hawatakuwa na namna zaidi ya kukimbilia Ulaya kutafuta maisha!!!

Haya ndiyo yanayotokea hivi sasa!! Vijana kutoka Kaskazini mwa Afrika hawana tena uoga wa kujitosa baharini tena hata kwa mitumbwi ili mradi tu wafike Ulaya!!!
 
Aise Historia nzuri sana.Asante mleta uzi na hasa hizo clips!Wengine tulikuwa wadogo sana
 
Nimejifunza kwamba mzizi wa neno Mfalme/ Bwana uko sawa kwa lugha nyingi.Na kuna uwezekano mkubwa umetokana na jina la Julius Caesar.

Sizwe (South Africa), Caesar (Latin), Czar(Russia), Kaiser (Germany).

Kuhusu Nyerere, Waswahili walisema "Tenda wema nenda zako, usingoje shukurani".

General George Patton alisema watu wakitumia muda wao kufanya kazi badala ya kuchunguzana nani anastahili sifa wanaweza kufanya mengi zaidi.
 
Kama Nilivyoeleza Mandela Mara tu baada ya Kuanzisha Umkoto Wesizwe alikuja Tanzania, akaenda Ethiopia aliporudi SA miezi michache akakamatwa, akahukumiwa na hakuachiwa Tena hadi 1992. Uhuru wa Afrika na Afrika Kusini na Hata kuhakikisha Kufugwa kwa Mandela !unasikika Kazi hiyo Aliifanya zaidi Nyerere na sio Mandela.

Ingekuwa sio Juhudi za Nyerere hata Mandela Unge!uta Kashauwawa Jela Tangu miaka ya 70! Nyerere ndiye aliyeendeleza Madai ya Kjachiwa Mandela UN na Kila alikokwenda ulimwenguni. Kelele hasa za Nyerere ndizo zilizomweka Mandela hai huo ndio Ukweli wa Mungu. Najua Mwisho wa Yute Mandela alilindwa na Mungu, lakini Mungu anatumia Watu, na hapa alimtumia Nyerere. Period!
 
Back
Top Bottom